Dennis Robert Shughuru
JF-Expert Member
- May 30, 2024
- 5,559
- 8,747
Vipiganie weweYule Jamaa anayewaambia Graduates waende Veta, hivi ndio vitu alipaswa kuvipigania.
Ili undelee unahitaji maamuzi magumu maendeleo hayaji kwa kupetipetiKwa Tanzania haiwezekani, hiyo ni fantasy au ndoto za mchana.
The best labda 14% na hapo ni ikiwa bunge litatunga sheria kabisa kwama walivyofanya Kenya kipindi fulani, na hapo benki kuu itabidi pia riba yake iwe ndogo sana walau 4% kitu ambacho ni kigumu kukitekeleza kwa aina ya uchumi wetu kutokana na madhara yake.
Ingalikuwa ni rahisi hivo ingeshafanyika, acha ubishi.Ili undelee unahitaji maamuzi magumu maendeleo hayaji kwa kupetipeti
Wanzania hawana tabia za kulipa madeni, hata uwape bila riba.Kama kisemavyo kichwa cha habari riba za benk za kibiashara hazitakiwi kuzidi asilimia 5 hii itachochea ukuaji wa uchumi kwa sababu mikopo itapatikana kwa bei nafuu faida za mikopo kuwa na riba ndogo
Ni vizuri serikali ikalifanyia kazi hili wazo sababu lina manufaa kwa nchi
- Kuongeza mzunguko wa fedha
- Kuondoa hofu ya kukopa ambayo wanayo watu wengi
- Kuongeza ajira
- Kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja
- Kuongeza kodi serikalini
Hakuna kitu rahisi kwenye maisha Inawezekana vizuri tuIngalikuwa ni rahisi hivo ingeshafanyika, acha ubishi.
Ni kwa sababu tu wengi wao hawatumii Bank ndo maana inakua ngumu kuwapataWanzania hawana tabia za kulipa madeni, hata uwape bila riba.
Ni mabingwa tu wa unafiki, ubinafsi na utapeli.
Halmashauri zinatoa mikopo isiyo na riba ila mtu anaona uvivu kufuatilia, anaona haifai
Hata mikopo ya halmashauri ambayo haina riba , hawarudishi.Ni kwa sababu tu wengi wao hawatumii Bank ndo maana inakua ngumu kuwapata
Kwenye maisha kila mda ukiipa nafasi excuse ni ngumu sana kufanya jambo kubwa au la maanaBank wanakopeshea biashara kutumia liability amana za wateja wao (non-transactional deposits/savings account).
Hizo savings accounts ili kila apate faida mteja na banks, kuna banks wana lipa savings accounts mpaka 10% kwa miaka ya savings.
Riba ndogo za savings za muda mfupi wanalipa interest kwa wateja wao 5%-7%.
Maana yake nini huo mkopo wa biashara wa 5% auwezekani hata siku moja.
Bank inazoweza fanya ni za serikali, kwa hela ya serikali. Lakini kila wakifungua bank zao kusaidia sector iwe biashara au kilimo wanaopewa kuziongoza wanazichota baada ya muda utasikia bank zao zimejaza non-performing loans na hawana cash flow ya kuendelea na biashara.
Baada ya hapo uoni TAKUKURU, wala sijui nani kufanya uchunguzi ila utaona waziri husika wa wizara kama ni bank ya kilimo ana ukwasi wa kujengea CCM ofisi tsh 300 million huko Nzega hiyo kwake ni hela ya chai tu.
Tanzania ina safari ndefu, tukitoka hapo tunaanza kulaumu hoo tunalima pamba halafu tunaagiza nguo, mchina kiwanda chake mkopo wake labda riba 5%-7%, umeme wake unit cost chini $0.10 per unit, machine hana import duty (na ukute ana capital allowance ya 100%).
Halafu angalia na mazingira ya kuwekeza Tanzania, kuacha kuagiza bidhaa China ni hadithi za ‘Ali Nacha’.
Kwa sehemu kubwa watanzania ni watukujitekenya na kucheka wenyewe.
Embu elezea litavyowezekana benki kukopesha kwa 5%. Nasubiri maelezoHakuna kitu rahisi kwenye maisha Inawezekana vizuri tu
Jambo likiwa rahisi hilo halina impact yeyote
Sasa excuse kwenye maandishi yangu iko wapi.Kwenye maisha kila mda ukiipa nafasi excuse ni ngumu sana kufanya jambo kubwa au la maana
Hakuna jambo rahisi kwenye maisha
Afrika na Tanzania haiwezi toka kwenye umaskini kama tukitegemea excuse
Halafu wakiambiwa ukweli wanatoa vitu tu kutoka vichwani kwao wengine wanakasirika.Embu elezea litavyowezekana benki kukopesha kwa 5%. Nasubiri maelezo
Riba ya 5% inawezekana kwenye uchumi ambao ni developed sana kama US Japan ambapo kipindi kisicho cha msukosuko wa uchumu default risk ni ndogo at the same time hapo central bank unakuta riba ni 1%. Na bado hata hiyo5% unakuta ni kwa category fulani fulani tu, ukienda kwenye indivudual loans kama credit cards riba unakuta zipo kwenye 7 to 10% na huko ni majuu.Halafu wakiambiwa ukweli wanatoa vitu tu kutoka vichwani kwao wengine wanakasirika.
Kuna vitu unasoma unabaki salalee
Ndio maana nikamuelezea hapo huko majuu uwezi kukuta kuna saving account inayolipa 5%.Riba ya 5% inawezekana kwenye uchumi ambao ni developed sana kama US Japan ambapo kipindi kisicho cha msukosuko wa uchumu default risk ni ndogo at the same time hapo central bank unakuta riba ni 1%. Na bado hata hiyo5% unakuta ni kwa category fulani fulani tu, ukienda kwenye indivudual loans kama credit cards riba unakuta zipo kwenye 7 to 10% na huko ni majuu.
Sasa Tanzania hii ambayo kukopa harusi kulipa matanga, ukiweka hiyo riba ya 5% si miaka miwili unafunga benki? Maana yake ni kwamba kwa nchi ya risk kubwa kiasi hichi, riba naturally zinekuwa juu kufidia hasara ya wateja magumashi
Katika mtu wa ajabu ni weweHalafu wakiambiwa ukweli wanatoa vitu tu kutoka vichwani kwao wengine wanakasirika.
Kuna vitu unasoma unabaki salalee