Riba za mabenki

MAGALEMWA

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
6,413
Reaction score
4,885
Jamani tuelimishane kuhusu hii mikopo ya mabenki maana watu tunashindwa kurejesha na dhamana zetu zinaishia kupigwa mnada.

Nahisi kuna tatizo la uelewa wa hizi riba.

Riba ya mkopo ni 17% of whatever wanavyopiga hesabu zao, lakini utakapomaliza kulipa, unakuta umelipa kiasi cha karibu 50% cha mkopo.

Ebu tuelimishane maana kwa nini wasiseme ukweli toka mwanzo kuwa riba ni 50% ya mkopo na siyo 17% wanayotangaza?

Na waziri anadiriki kutuambia riba za mabenki zimeshuka wakati kwa uelewa wa mkopaji kama mimi inaniwia vigumu kukokotoa na kuelewa uambiwe 17% uishie kulipa 50%.

Tafadhalini tuelimishane
 
Ni janga hilo , watu wengi wanaamini ma bankers, Banker hasemi ukweli
 
Si kweli mkuu, ngoja nikufafanulie kwa mifano hai.
NMB ukikopa milioni 10, kwenye account utawekewa milioni 9.6 baada ya makato. Kila mwezi utatakiwa kurejesha 932,000 ambayo kwa miezi 12 ni sawa na 11,184,000 ambayo ukitoa milioni 9.6 waliyokuwekea cash inabaki 1,584,000 ambayo ni sawa na 15% ya milioni 10 uliyoomba.

Ila unapoenda kuchukua mkopo wao wanakwambia Riba ni 21% reducing rate, so mwisho wa mwaka unajikuta ni kama umetoa 15% tu.

Hiyo case yako inawezekana kama umechukua mkopo wa muda mrefu labda kuanzia miaka 3 na kuendelea maana hiyo riba hua ni kwa kila mwaka. Kwa sisi wafanyabiashara riba ya mwaka kwetu sherehe tu ila kwa wafanyakazi wanaopewa mkopo wa miaka mingi ndo kama hivyo mnalia na kulaumu.
 
Hilo la muda mrefu linaelekea lina ukweli. Ila basi watoe maelezo yanayoeleweka.
 
Ila bado riba za benki ziko juu na siyo rafiki kwa wakopaji. Nadhani wangepungza ifikie hata 10% kwa mwaka, ingekua poa sana.

Sijajua ni kwa nini serikali haijengi mazingira rafiki ya kuzishusha hizi riba kwenye mabenki ili wakopaji wengi waweze kukopa na kurejesha kirahisi.
 
Tatizo watu huwa hawaelewi wakiambiwa 17%.Wenyewe wanajua ukikopa 10M maana yake unalipa ((10M + 17% ya 10M) kwa muda wote wa marejesho kitu ambacho sio sahihi.kumbe Utakacholipa inategemea na muda wa marejesho wa mkopo uliokopa.

anaekopa 10M kwa marejesho ya mwaka ni tofauti na anayekopa 10M kwa marejesho ya miaka mitatu.
 
Swala la mkopo benki ni muhimu ukaelewa njia wanazotumia kukadiria riba ya deni lako kwa mwaka.Ni vizuri wakopaji wawe wanapewa ushauri kwanza kabla ya kuomba mkopo ili kuepuka malalamiko ya kulimbikiza marejesho makubwa mwisho wa kulipa deni.

Mkopo wa muda mrefu humuumiza zaidi mkopaji ikiwa pia njia iliyotumika kutolea mkopo ni straight line method ambayo riba haibadiliki hadi muda wa mkopo unapoisha.

Pia reducing method ni njia sahihi inayopungua riba kadri ya muda wa deni unavyoelekea kuisha.

Hitimisho:Aliekopa kwa reducing method atalipa jumla ya rejesho dogo kuliko alietumia straight line method.
 
Mkuu wajanja tunakopa miezi 6 mwisho mwaka riba ni sawa na kumsukuma mlevi kwenye mteremko,sasa wewe kopa miaka mitano utalipa riba hadi za marehemu
 
Nimetafakari nimegundua wafanyakazi ndio wahanga wakubwa wa mikopo.
Kuna jamaa yangu kakopa 15,000,000 Atarejesha ndani ya miaka 7.
Hesabu iko hivi:
Kila mwezi atakatwa 309,000
309,000x12×7=25,956,000

HALI NI NGUMU SANA KWENYE HII MIKOPO
Huu sio mkopo
Huu ni ujambazi mkuu sema ni ujambazi ulioidhinishwa (Authorized Bandits)
Yaan wafanyakazi wanatakiwa wabadilike utaona wanafurahia kupanda madaraja wanaishia kwenda kunyonyolewa na benk
Kwa Mikopo ya namna hii umaskini kwa watumishi wa umma ni Pai yaan isipokuwa 22/7 bas 3.14.....
 


Habari yako naomba nikutoe tongotongo kidogo
Mimi ni mtaalamu ya maswala ya Financial instituation hivyo maswala ya Loan au Credit nayafahamu in and out.

1. Wakopaji wengi uingizwa kwenye mikopo mibaya kwasababu ya shida zao na uharaka wa kutatua changamoto izo ambapo huwa hawana uelewa wa undani juu ya maswala ya Mikopo na Urejeshaji.

2. Ukiwa ni mtu wa kukopa kariba yako itaendelea kuwa ivyo mpka siku unaingia kaburini hivyo tunamsemo unasema KOPA KIASI KWA FAIDA since shida au matatizo ya mwanadamu hayaishi siku moja, hivyo kama ni mkopaji kopa mikopo mifupi ( yaani ya muda mfupi maana huwa haiumizi) mfano mkopo wa miezi 3,6 au 12 mpka 24

3. Usipende sikiliza mtu anavyosema au kwakua ni rafiki yako usikubali akushauri sana kumbuka taasisi skuizi zinamawakala wengi ili wapate wateja mfano mpka kufikia mwaka jana kuna taasisi za kifedha takribani 150 ziliongezeka hawa wote wanategemea wateja wale wale hivyo kabla ya kukopa fanya reserch ya kulinganishi riba zunguka benk na microfinance zote za karibu uliza maswali makuu kwa afisa mikopo juu ya riba zao then linganisha utakua umepata pakuanzia na wapi pa kukopa.

4. Unapotaka kukopa uliza maswali haya riba yenu ni kiasi gani ? Na iyo riba ni ya mwaka au mwezi? Mfano Bank nyingi wana riba za 16% kwa mwaka hivyo ukigawa kwa 12 unapata riba ya mwezi ni 1.33% ila pia kuna Microfinance nyingi zinatoza riba kwa mwezi husika mfano kuna microfinance sitaitaja wana riba za 4% kwa mwezi hivyo kwa mwaka ni 48% ukilinganisha apo utaona.

Riba ya mwaka ( Bank) 16% Riba ya mwaka (Microfinance) 48%


Riba ya mwezi (Bank) 1.33% Riba ya mwezi (Microfinance) 4%

Unaweza pata jibu uende kopa wapi kati ya microfinance au bank

5. Muda wa mkopo unaoomba au kuchukua , tunashauri watu wachukue mkopo wa muda mfupi kwakua unakuweka huru na kama utataka mkopo wa muda mrefu hivyo tafuta taasisi yenye riba nafuu kuliko taasisi nyingine.

Mfano mtu anachukua mkopo wa milion 1 anakubali kukatwa 95,000 kila mwezi kwa muda wa mwaka 1 hivyo hapo unafanya mahesabu kua 95,000*12 =1,140,000 ila ukichukua mkopo wa muda mrefu mfano 1million kwa miaka 5 uwe unakatwa 35,000 inamaana hesabu zake zitakua
35,000* miaka 5( miezi 60)=2,100,000

Ukilinganisha hapo utaona kua
Kato la Bank 95,000/=
Marejesho ya Bank 1,140,000 Miezi 12( mwaka1)

Kato la Microfinance 35,000
Marejesho ya Microfinance 2,100,000 Miezi 60(miaka 5)

So unapoenda kwa afisa mikopo akikwambia unakatwa kiasi flani kwa muda flani wewe chukua kile unachokatwa zidisha na muda wa kurejesha yani

Marejesho= kato la mkopo* muda wa marejesho
Hivyo epuka mkopo wa muda mrefu kwakua unakatwa kidogo ni mzigo mkubwa sana kwako kwa miaka 5 kukatwa 35,000 inamaana inakunyima fursa ya wewe kukopesheka tena

6. SHERIA NA NJIA ZA MAREJESHO
Taasisi za kifedha zote zinatumia njia mbili yaani Reducing balance method au Flat rate method
Hivyo ni bora umuulize afisa mikopo kua wewe mkopo wako unarudisha kwa njia ipi kati ya izo
Sheria ya mikopo mfano kwa wafanyakazi kama waalimu na wengine inasema ni lazima 1/3 izingatiwe mfano mwalimu wa primary basic salary ni 419,000 then Takehome yake ni 250,000 ili aweze kopesheka lazima hesabu ifanywe yani

419,000/3 =139,666
Inamaana kwamba utaingia katika mikopo kwa kato lolote ila mwisho katika account yako inabidi ibaki 139,666 pasipo kuguswa.
Yaani Takehome-Answer of 1/3
250,000-139,666=110,333
Inamaana ukitaka mkopo utapata kwa kato la 110,333 kushuka chini ukizidisha juu ya apo unaingilia 1/3 ya mtumishi na sheria inakataza.

7. GHARAMA ZA MIKOPO
Taasisi nyingi za kifedha zinakua na mifumo yao mfano bank nyingi unapowekewa pesa katika akaunt ya mteja wanamakato yao kwa asilimia flani mfano wanakupa 2M unakuta katika account umepokea 1.95 M inamaana wamekata laki 3 na 50 kama gharama za mchakato wa mkopo yaani
Loan processing fee, Bima na nk
Ila pia kuna baadhi ya taasisi wao wanadai hawakati izo gharama mfano microfinance nyingi pale unapo omba 2M unapewa iyo iyo ila ukweli ni kua wanafanya kiini macho izo gharama wameziweka kwenye riba ntachanganua apo chini kiasi mtu anachopata katika account yake anapo omba pesa bank na microfinance na marejesho yake au riba za ziada

Bank 1.95 M

Microfinance 2M

Marejesho kwa mwaka baada ya kukopa

Bank ulichukua 2M gharama za mkopo laki 3 na 50 hivyo unapata 1.95 M mkononi ila marejesho yake kwa mwaka ni 2,280,000 kwa riba ya 1.4% kwa mwezi

Microfinance ulichukua 2M hakuna gharama ya mkopo hivyo ulipata 2M yote ila marejesho yake kwa mwaka ni 2,960,000 kwa riba ya 4% kwa mwezi
Kwanini unarejesha pesa nyingi sana?
Jibu ni kua zile gharama za mkopo zimewekwa katika riba na ndo maana riba za microfinance ni kubwa.

8 HAKI NA WAJIBU WA MTEJA
Mteja wa taasisi ya kifedha ana haki zake pia kulingana na mikataba aliyo ingia japo watu wengi uwa hawapati wasaha wa kusoma mikataba yao kabla ya kuingia katika makubaliano hivyo kushindwa jua wapi pakukimbilia
Mfano mteja uwa anahaki ya kusitisha mkopo wake ata kama mchakato ulishaanza, lakini pia mteja anahaki ya kufuta deni lake kwa njia atakayo yeye iwe kwa kuliuza kwa taasisi nyingine au kwa kulipa cash mwenyewe mfano unadaiwa bank 3M na wanariba za 16% unapo pata bank nyingine wanaotoza riba ya 12% inamaana unaweza kuuza deni ilo kwa taasisi yenye riba ndogo ( means deni linalipika na unauwezo wa kukopa kwenye taasisi ndogo)
Sasa baadhi ya taasisi uwa zikiskia mteja anauza deni uwa hawataki maana wanajua mteja anahama hivyo ni haki yako kisheria kulingana na mkataba hivyo kabla ya makubaliano soma kama inaruhusiwa kusettle deni lako.

Usitoe pesa au kuhaidi kutoa pesa ili ushughulikiwe kupata mkopo ile ni haki yako ,kufanya ivyo ni kutoa rushwa au kutengeneza mianya nya kuonesha unadhiki sana na pesa na kusahau kua upo katika makubaliano unatoa pesa au vitu kama dhamana ili upate pesa

9. UTOFAUTI WA HUDUMA
Bank huwa na mzunguko au utaratibu mrefu kidogo wa kuweka pesa au kumpa pesa mteja ila ni uhakika na unapata kiwango cha pesa kingi
Ila ukienda katika microfinance utapesa pesa kidunchu kwa muda mfupi hii ni kwakua wanajua bidhaa zao haziuziki ivyo uhalaka ndio tijayao kupata wateja mfano bank kwa kato la elfu 50 miezi 24 unaweza pata ata milioni 6 ila ukachukua siku 2-3 ata wiki kupata pesa zako ila microfinance kwa kato la elfu 50 miezi 24 unaweza pata Milioni 2.5 mpaka 3 kulingana na riba zao ila pesa ukachukua masaa 2-24 kuzipata

Kwangu mimi ni bora kupata kingi kwa kato ilo ilo kuliko kupata kidogo kwakua na shida ya haraka na marejesho makubwa

10. USHAURI
Epuka kukopa katika taasisi usizozijua au kuwa na taarifa za undani
Mfano epuka kukopa katika taasisi izi za kifedha Kama microfinance Kwakua nyingi zao wana riba ya 3-4 kwa mwezi ( siwezi zitaja kuhofia waseme nawaaribia biashara yao hivyo ni bora ujikite katika bank zenye mikopo na riba nafuu kama BOA bank wenye riba ya asilimia 9-10 kwa mwaka kama sijakosea, CRDB bank, NMB ndizo bank zenye riba nafuu na hauweni hapa Tz kwa sasa

Asanteni kama kunaswali jingine au mawazo mbadala naomba niulizwe hapa no PM
 
Dah! Umepita mulemule hasa suala la muda wa mkopo, wengi huwa tunaangalia unafuu wa makato ya mwezi badala ya pesa itakayorejeshwa hadi mwisho wa mkopo kwa ujumla.
 
"ni bora ujikite katika bank zenye mikopo na riba nafuu kama BOA bank wenye riba ya asilimia 9-10 kwa mwaka kama sijakosea",
Shukran sana kwa maelezo mazuri sana tena yakueleweka vizuri sana kasoro hapo tu riba ya BOA bank 9-10 % labda kama umepikia kwa ujumla marejesho kwa kiwango cha mkopo, Hivi ndivyo vinavyowachanganya wengi, Riba inapaswa kutamkwa kiwango% kinachotumika kukokotoa Riba kutoka kwenye mkopo, kwa uwelewa wangu haitakuwa chini 17% kwa mwaka mara nyingi (18% - 21%)

Naweza kurekebishwa maana lugha au uwelewa nayo ni changamoto
 

Nikisema asilimi 9-10 iyo ni ya mwaka mzima ndio walio na riba ndogo Tz kwa mabenk

Kimahesabu uwa ni Pesa unayo omba* riba kwa mfumo wa % *muda= Rina ( faida ya kampuni)

Yaani P*R*T/100

Na Jumla ya mkopo ni= Pesa unayoomba + faida ya kampuni

Yaani Loan Amount= P+ Bank profit( interest)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…