Riba za mabenki

Mkuu ni kweli hasa mikopo ya muda mfupi riba ni win-win fresh tu..hata hawa #Barclays wako poa kwa riba zao na taratibu zote sema waswahili tunaogopa hilo jina tunaona kuubwa[emoji23][emoji23]
 
Reducing rate inatumika kwa wanajeshi tu
Flat rate ni kwa watumishi waliobakia. So wanajeshi ndio wanafaidi mikopo
Jaribu pale PBZ utagundua kinyume cha hiki unachoamini mkuu.
NB: Sina interest kwenye hili nimewataja kama mfano wa Reducing Rate Method
 
Jamaa upo deep,hadi unaboa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Linapokuja suala la mikopo mara nying jitahidi sana muda wa kurejesha uwe mfupi. Kadri unavyoongeza muda wa marejesho ndio hivyo unavyojikuta ukirejesha fedha nyingi.
Mfano ukikopa TZS 5,000,000/- kwa riba ya 17% kwa mwaka utarejesha jumla ya TZS 5,472,285.12 kwa marejesho ya MWAKA MMOJA au TZS 7,455,772.80 iwapo utafanya marejesho kwa lipindi cha MIAKA MITANO. Hapo utaona kuna tofauti ya TZS 1,983,487.48‬. Hii ni kwa mujibu ya kanuni ya Reducing Balance Method ambayo hutumika na mabenki mengi. Makato haya hayajumishi gharama zingine zinazoambatana na mkopo.
2. Hakikisha unapata maelezo ya kutosha kuhusiana na mkopo kabla ya kufanya maamuzi. Hili utegemea na uelewa/udadisi anaokuwa nao mkopaji.

Hata hivyo viwango vya riba kaitka mabenki bado viko juu sana. Ingependeza kama vingefikia 10% (Per Annum) au single digit. Hii ingeleta ahuheni na kupanua wigo wa wakopaji.
 
Mimi ningeridhika Kama ningeongezewa na ushauri au mlinganisho wa mikopo na riba za mabenki nafuu angalau matano. Yaani msaada tutani
Haitoshi nini mkuu?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi ningeridhika Kama ningeongezewa na ushauri au mlinganisho wa mikopo na riba za mabenki nafuu angalau matano. Yaani msaada tutani
Haitoshi nini mkuu?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nimetafakari nimegundua wafanyakazi ndio wahanga wakubwa wa mikopo.
Kuna jamaa yangu kakopa 15,000,000 Atarejesha ndani ya miaka 7.
Hesabu iko hivi:
Kila mwezi atakatwa 309,000
309,000x12×7=25,956,000

HALI NI NGUMU SANA KWENYE HII MIKOPO
duh umenfumbua macho asee nlikua najiuliza how comes mtu anakopa milion 10 lakn anajikuta anatakiwa kulipa milion 16 na zaidi how comes

Sent using Jamii Forums mobile app
 
narudia tena kwa sauti kubwa ,,, hawa ni

(Authorized Bandits)
Sent using Jamii Forums mobile app
 
nlikimbia hesabu shule ila hapa nimeelewa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Asante kwa elimu hii

Mfano nimekopa mkopo wa miaka 5 na kabla miaka hiyo haijafika let say nimefanya marejesho kwa miaka 3 mfululizo,nataka kulipa cash niufute huo mkopo,je hapo naokoaje kulipa riba za miaka 2 iliyobaki?
 
Hesabu haidanganyi.
Nenda kwenye computer yako, fungua " new microsoft office document".
Baada ya hapo, fungua "loan amortization"
Fuata maelezo kwa kujaza mkopo wako uliopewa na baada ya hapo program itakuonyesha ni kiasi gani cha riba utalipa kulingana na muda wa mkopo na interest rate.
 
Ntajibu comment zote zilizoniuliza maswali kesho samahnini sana nlikua busy kidogo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…