Ricardo Kaka, mcha Mungu na hasira za kibinadamu

Ricardo Kaka, mcha Mungu na hasira za kibinadamu

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
.
Nadhani wengi mnamjua Ricardo Izecson dos Santos, ni huyo huyo anaejulikana kwa jina la Ricardo Kaka, namba 10 bora sana katika kizazi chake
.
Najua nikikuuliza unamkumbuka Kaka kwa lipi, 90% kama si 95 watanikumbusha stori za usiku wa UEFA na AC MILAN
.
Basi ngoja nikurudishe nusu fainali usiku wa nusu fainali UEFA pale Old Trafford 2006-7, Man Utd anaibuka mshindi 3-2 goli la ushindi likifungwa na Wazza dakika za mwisho kabisa, ila stori kubwa ilikuwa kiwango bora kabisa cha Kaka
.
AC Milan ya mastermind Carlo Anceloti, kila mpira aliougusa uligeuka dhahabu, alifunga magoli mawili usiku ule, yote upande uleule, moja anawagonganisha Evra na Gabriel Heinze kichwa na goti
.
Ila kuna kitu kilitokea si kawaida ya mshika dini huyu. Unaweza hisi ni kipi? Hold on, usiumize kichwa, nipo kwa ajili yako nakujuza
.
Katikati ya Mechi Giggs alimchezea rafu Kaka, kulikua hamna namna, mtu wa Mungu alikua hashikiki, ila paap ghafla Kaka amemind akampiga roba moja ya kimafia Giggs
.
Giggs aliwahi kukiri, alipopigwa ile roba, alijiuliza "hivi kweli mtu alieshika dini anaweza kufanya kitendo kama hiki?"
.
Baada ya mechi kuisha, United wakiwa dressing room kwenye spika bila shaka kwa mbali inapiga Don't Matter ya Akon, ghafla mlango unafunguka akaingia Kaka na Gennaro Gattuso mtukutu, watu kimyaa
.
Ila ujio ulikuwa wa kheri, Kaka alimuomba Gattuso akawe mkarimani sababu anajua kiingereza aliwahi cheza pale Scotland klabu ya Rangers
.
Kaka aliomba msamaha kwa Giggs ya kuwa hakufanya swala la uungwana kumkwida
.
Giggs alimwambia Gattuso "mwambie Kaka ni kawaida hasira uwanjani kwa mchezaji hasa mechi yenye uzito kama hii ya nusu Fainali Uefa" Gattuso akatafsiri na kumwambia Kaka
.
Kaka alimpatia Giggs "Catholic Orthodox Icon" hii ni picha ya Yesu ambayo imechorwa kwa ustadi nia ni kutukumbusha upendo, pia aliinama kwa heshima akiomba msamaha, chumba kizima kilipiga makofi
.
Giggs anasema mpaka leo hajawahi ona mtu mpole, mwenye adabu na mkarimu kama Kaka
.
Ni hasira za kibinadamu tu [emoji16]
 
[emoji817]
images%20(10).jpg
 
Daaah huyu mwamba namkubali Sana na ac Milan nwinaipe Sana hii timu
 
Pia world cup 2010 alimpiga kiwiko mchezaji wa ivory cost akala umeme
 
sikumbuki ilikuwa ni mechi gani, jamaa aliingia kipindi cha pili hata dakika mbili akaasist goli, kizazi cha mpira Brazil kimeshaisha
 
Back
Top Bottom