Rich Mavoko anakwama wapi?

kombaME

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
2,115
Reaction score
2,818
Kwa wapenzi wa mziki mzuri watakubaliana na mimi kwamba moja ya msanii aliyekuwa anatuburudisha vilivyo na kuyafanya masikio yetu yapate burudani ya kutosha ni huyu bwana mdogo, tulipokuwa tunasikia Mavoko anakwenda kutambulisha nyimbo mpya masikio yetu yalijawa na hamu kubwa kutaka kusikia safari hii amekujaje na alikuwa hatuangushi kwa kweli.

Ni mmoja kati ya wasanii ambao walitengeneza hit songs za kutosha enzi zake, kama vile; SILALI, ROHO YANGU, PACHA WANGU, MARRY ME n.k na pia amezipamba nyimbo nyingi na kuzifanya zisikilizike na zivutie masikioni mwa wengi kama lile song la KABWELA la bwana mdogo Stamina, Mavoko alilipambisha vilivyo na sauti yake kwenye chorus.Na nyinginezo nyingi.

Na hata alipoamua kujiunga na kijana mwenzake Diamond Platnumz katika label ya WCB, bado hakukosea sana japo wadau kadhaa wa mziki waliona kama amepoteza sana kuchukua uamuzi huo maana ni kama ameua upinzani ambao aliutengeneza na Platnumz, maana Ali kiba alianza kuonekana kupwaya na vita mpya mjini ikahamia kwa Mavoko na Platnumz. BTW pamoja na hayo yote bado Mavoko aliendelea kutuburudisha baada ya kutoa nyimbo kadhaa akiwa WCB kama vile KOKORO aliyeshirikiana na Platnumz, IMEBAKI STORI na SHOW ME aliyeimba na Harmonize msanii mwenza kutoka WCB.

Baada ya mgogoro ambao ukweli wa chanzo cha huo mgogoro anaujua vizuri mwenyewe Mavoko, akaamua kujitoa WCB na hapo ndipo ulipoanza mdororo wa huyu kijana, kuna nyimbo amezitoa toa lakini hajafikia hata robo ya uwezo aliouonesha mwanzo.

NINI TATIZO LA HUYU KIJANA WANABODI?
 
Kosa kubwa kwenda Wasafi, wamedukua nyota yake ki voodoo.
 
Duu yaani watu wamemkimbia mavoko.hadi jf ?? Hata waliokua wanampigia chapuo akimbie wasafi Wanapita tu kwenye huu uzi bila kusema chochote wakati mwenzao anapauka huko hata shoo za mtoni mtongani hazipati tena
 
hivi Kings Empire nayo imeishia wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…