Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Richard Donner, mtengenezaji gwiji wa filamu na ambaye aliongoza filamu maarufu za "Superman", "The Goonies," na nyingine zilizotamba, amefariki dunia jana Jumatatu akiwa na miaka 91, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.
Kazi nyingine za Donner ni pamoja na filamu ya kutisha ya mwaka 1976 ya "The Omen," "Lethal Weapon" aliyoshirikiana na Mel Gibson na Danny Glover kuanzia mwaka 1987, "Scrooged" (1988) na filamu yake ya mwisho ya 2006 inayoitwa "16 Blocks."
Pia aliongoza baadhi ya sehemu za vipindi vya televisheni vya 20th Century kama "Get Smart," "Perry Mason," "Gilligan's Island" na "The Twilight Zone," kwa mujibu wa IMDB, na baadaye kuwa mtayarishaji wa filamu zilizotamba, zikiwemo za "X-Men" na "Free Willy."
Repota wa Hollywood alimkariri msaidizi wa Donner kuthibitisha habari za kifo chake, wakati Deadline ilisema hakuna sababu zilizotolewa mkewe ambaye pia ni mtayarishaji, Lauren Schuler Donner kuhusu kifo chake.
"Richard Donner alikuwa na sauti kubwa, pana usiyoweza kufikiria," nyota wa filamu ya "Goonies", Sean Astin aliandika katika akaunti yake ya Twitter.
Mwongozaji mwenzake, Steven Spielberg, ambaye aliandika hadithi iliyotumiwa kutengeneza filamu ya "The Goonies", alisema katika taarifa yake kuwa Donner alikuwa na nguvu kubwa katika filamu.
"Kuwa katika duru zake ilikuw ani sawa na kuwa na kocha unayemuhusudu, profesa mzuri, mhamasishaji mkubwa na rafiiki anayejali, mshirika mzuri," alisema Spielberg katika akaunti yake ya Twitter.
Filamu za Superman zimekuwa maarufu kote duniani kutokana na uwezo wa kipekee aliopewa muigizaji mkuu wa filamu anayekwenda kwa jina hilo.
Mwananchi