Kama sikosei maadili ya uchaguzi mkuu yanavitaka vyama vya siasa kutumia lugha ya kiswahili katika kampeni na
kutumia wakalimani kutafsiri pale jamii husika inapokuwa haiielewi lugha ya kiswahili. Adhabu kwa kukiuka
yaweza kuwa faini au kubatilishwa kwa mgombea pale anapoendelea kukaidi.
Ndasa yupo jimbo la Sumve wilaya ya kwimba, mkoani mwanza, yaani huyo jamaa hafai kabisa na upinzani huwa hawaweki mtuu wa maana kule sijui kwa nini hilo jimbo ni la bure kwa upinzani.
Mod; Mwanzisha thread alitaka ku-draw an unnecessary attention kwa wana jukwaa kwa sababu anajua kuwa ni udaku, hivyo alidhani watu wata-ignore kuisoma.
Kwako totoz; Mzee una bifu naye nini? Huko usukumani hata wachagga wapo kibao lakini wanaongea kisukuma utadhani ni wasukuma. Unless mtu anabisha, lakini the fact ni kwamba mgeni yeyote akishafika usukumani baada ya wiki moja anaongea kisukuma angalau to 60% accuracy. Hivyo, usukumani hakuna mtu mwenye haki ya kupiga kura huko, lakini hajui kisukuma. Huyo siyo mgombea uraisi kwamba ameongea kisukuma akiwa tarime, au kyela. Waacheni watu watambe kwenye maeneo yao ya kujidai, na pia siasa zetu zilenge zaidi katika kuwaangalia watu na siyo chama chao. Zitto hata akihamia UDP leo, Kigoma Kaskazini lazima wampe kura, wanamwangalia yeye sana, na si chama alichonancho! Usiwe unachukia watu halafu unatoa hoja ambayo haina upeo!