Ridhiwani Kikwete afungua maonyesho ya viwanda vya kuzalisha Nishati kwa kutumia Teknolojia mbalimbali

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete Jana Alhamisi Machi 24, 2022 alikuwa Mgeni rasmi kwenye Ufunguzi wa maonyesho makubwa ya Viwanda vinavyozalisha Nishati kwa kutumia Teknolojia mbalimbali.

Ufunguzi wa maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya Expo Group Limited yamefanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam na yanalenga kuwasaidia Wananchi kutumia bidhaa mbalimbali zilizopo kwenye maeneo yao kuzalisha Nishati.

Naibu Waziri Kikwete amesema maonyesho hayo ni mazuri kwa Taifa hasa kwa Vijana na yatasaidia sana kujifunza kutumia sekta mbalimbali kama za madini, gesi, nishati mbalimbali na kuzitumia kutengeneza ajira na kupata kazi.

"Nimepewa heshima ya kufungua maonyesho ya BuildExpo2022 inayofanyika Diamond Jubilee, Dar es Salaam Tanzania. Nimetumia nafasi hiyo kuwakaribisha wana maonyesho Tanzania na kuwaeleza kwa kina utayari wa Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kushirikiana nao kukuza Uchumi wa Nchi na kuimarisha Mashirikiano baina ya Nchi zetu. Nchi zaidi ya 24 zimeshiriki. Alisema Mhe. Ridhiwani Kikwete.

#SSH #MamaAnapigaMwingi













 
Kiswahili ni maonesho sio maonyesho,ukisema maonyesho maana yake unaonya
 
Mambo ya aibu sana.
Familia nyingine hazitoi watu qualified?
Desh desh Pinda
Desh desh Makamba
Desh desh Nauye
Desh desh Mwinyi
Desh desh Warioba
Desh desh Sokoine
Desh desh Kawawa
Ni Msuya, Mkapa na Salim tu ndio wenye watoto wanao fight kwa jasho lao.
 
Aliyenacho ataongezewa, asiye nacho hata...

awali ni awali, hakuna awali mbovu.
 
Halafu yule wa nishati amekwenda kuzindua viwanja
 
Matapeli bana utawajua tu, naibu waziri wa ardhi anaalikwa kufungua kongamano la viwanda!?
Hiv wazir wa ardhi yupo πŸ’β€β™‚οΈπŸ’β€β™‚οΈπŸ’β€β™‚οΈ
 
Hii nchi haitaendelea mpaka kiwete Na mizizi yake yote itakapong'olewa
 
Mleta mada nimechoka hizo teknolojia hata kutaja moja moja umeshindwa ? Kuwa ni ipi na inasaidia nini.

Akili huna wewe.Uko sifuri kichwani na ni aibu kwa taifa kuwa na mtu kama wewe mbovu kichwani kama wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…