BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Ni mkakati wa kuhakikisha Wananchi wanafikiwa kirahisi kuhudumiwa. Halmashauri ya Chalinze yatenga Bilioni 2.2 kwa Wanawake, Vijana na Walemavu.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amegawa pikipiki 14, vishikwambi 15 na spika 15 kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Kata wa Halmashauri ya Chalinze kwa lengo la kurahisisha ufanisi wa kazi za kuwafikia wananchi kwa urahisi kuwahudumia.
Shughuli hiyo imefanyika Viwanja vya Halmashauri ya Chalinze Machi 05, 2025 huku vifaa hivyo vyote vyenye thamani milioni 59,400,000 vikilenga kwenda kusaidia Maafisa Maendeleo ya Kata katika ufuatiliaji wa madawati ya maendeleo ya jamii, ufuatiliaji wa mikopo na uhamasishaji wa uundaji wa vikundi, ufuatiliaji wa masuala ya ukatili wa kijinsia na utoaji elimu kuhusu maambukizi ya UKIMWI na lishe.
Aidha Halmashauri ya Chalinze inatekeleza vyema adhima ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwezesha makundi ya Wanawake, Vijana na Walemavu kwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwenda kwa makundi hayo ambapo Chalinze kwa huu wa 2024/25 imetenga jumla ya Bilioni 2.2 kuwawezesha.
Mbele ya Waziri Kikwete, akiwakilisha taarifa ya mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa makundi ya Wanawake, Vijana na Walemavu kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu Ramadhani Abdala Mumba alisema Halmashauri ya Chalinze kwa kutekeleza adhima ya Rais Samia kuwezesha wananchi imetenga Bilioni 2.2 kuwawezesha ambapo vikundi 41 vya Wanawake, 16 vya Vijana na 5 vya Walemavu vimepata mikopo hiyo ili kwenda kuinua uchumi wao.