Pre GE2025 Ridhiwani Kikwete atoa aina 25 ya vifaa kwa wenye ulemavu, asema serikali inaendelea kuboresha elimu kwa makundi yote

Pre GE2025 Ridhiwani Kikwete atoa aina 25 ya vifaa kwa wenye ulemavu, asema serikali inaendelea kuboresha elimu kwa makundi yote

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kupitia Serikali kuendelea kuhakikisha wanatoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.

IMG-20250216-WA0017.jpg

Kikwete ameyasema hayo Jana Februari 15, 2025 katika Ofisi za Halmashauri ya Chalinze alipokuwa akikabidhi aina 25 ya vifaa kwa watoto wenye mahitaji maalumu.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pia Mhe Ridhiwani ameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze kwa usimamizi mzuri wa fedha na kutoa elimu kwa wazazi ili kuona umuhimu wa kuwapeleka shule watoto hao na ameahidi kuwa serikali italeta fedha ili kukamilisha ujenzi wa mabweni.

IMG-20250216-WA0018.jpg

Aidha Mhe Mbunge amesema kupitia mfuko wa Jimbo wameleta jumla ya madawati 500 pia wataendelea kuhakikisha wanasaidia ili kutatua changamoto zilizopo na kuweka mazingira mazuri kwa watoto ili waweze kusoma kama wengine. Pia ametoa pongezi kwa walimu wanaofundisha watoto hao.

IMG-20250216-WA0019.jpg

Akiwasilisha taarifa kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Elimu msingi na Awali Bi Miriam S Kihiyo Afisa Elimu maalumu wa Halmashauri ya Chalinze Divisheni ya Awali na msingi Elikana M amesema bado kuna changamoto mbalimbali lakini ameishukuru Halmashauri ya Chalinze inavyojitahidi kutenga Fedha kwenye bajeti kupitia mapato ya ndani na kupunguza changamoto hizo kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wa Elimu.Aidha Lukuba ameiomba Ofisi ya Waziri Mkuu kutoa mwongozo kwa walimu waliosomea elimu maalumu ambao wanafundisha shule zisizo na wanafunzi wenye mahitaji maalumu kuwaajiri kwenye Shule zenye uhitaji huo.

Nae Mwenyekiti wa kamati ya shule ya Msingi Chalinze kitengo cha elimu maalumu ameishukuru Serikali kwa kuwapatia vifaa hivyo na kwani vitakuwa msaada mkubwa kwa watoto hao.

IMG-20250216-WA0020.jpg
 
Back
Top Bottom