Ridhiwani Kikwete: Tujikite kwenye kilimo cha Pamba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amewataka wananchi kujikita kwenye kilimo cha Pamba ambacho kitawakwamua kiuchumi.

Ridhiwani ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Vijiji vya Kilemela, Hondogo na Rupungwi katika Kata ya Mandera ambapo alisema ni wakati sasa wananchi kuona umuhimu wa zao hilo la biashara.

"Siwaambii mkatoe Mihogo mliyopanda shambani ili mlime Pamba, ila nawashauri kufufua kilimo cha zao hili ambacho kitawasaidia kuinuka kiuchumi kutokana na uboreshaji wa mazingira ya soko ulivyo sasa" amesema.

Kikwete amesema miaka ya nyuma zao hilo lilikuwa likilimwa kwa wingi katika Kata hiyo na maeneo mengine ya Halmashauri ya Chalinze na baadae mwamko ulipungua kutokana na soko na kwakua sasa mazingira yameboreshwa ni vyema kulima zao hilo ambalo litawainua kiuchumi.

Awali Ofisa kilimo wa Halmashauri ya Chalinze Jovin Bararata alisema mbegu ya zao hilo, pembejeo na dawa zinatolewa bure huku mbolea ikitolewa kwa ruzuku na mazingira ya soko yameboreshwa kutokana kuwepo kwa kiwanda cha uchakataji katika Kata ya Mandera.

Bararata amesema ni vema wananchi wakachangamkia fursa ya uwepo wa kiwanda hicho badala ya kuwaachia wakulima kutoka mikoa mingine.

Ofisa kilimo huyo amewashauri wakulima kuzingatia kuwatumia Maofisa ugani kwa ushauri wa kilimo ili walime kwa kufuata kanuni za kilimo na kupata mafuno mengi.

WhatsApp Image 2023-02-22 at 15.00.10(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-02-22 at 15.00.08.jpeg
WhatsApp Image 2023-02-22 at 15.00.09.jpeg

#ChalinzeYetu
#KaziInaendelea
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2023-02-22 at 15.00.10(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-22 at 15.00.10(1).jpeg
    58.4 KB · Views: 12
MHE. RIDHIWANI - TUJIKITE KWENYE KILIMO CHA PAMBA

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka wananchi kujikita kwenye kilimo cha Pamba ambacho kitawakwamua kiuchumi.

Mhe. Ridhiwani ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Vijiji vya Kilemela, Hondogo na Rupungwi katika Kata ya Mandera ambapo alisema ni wakati sasa wananchi kuona umuhimu wa zao hilo la biashara.

"Siwaambii mkatoe Mihogo mliyopanda shambani ili mlime Pamba, ila nawashauri kufufua kilimo cha zao hili ambacho kitawasaidia kuinuka kiuchumi kutokana na uboreshaji wa mazingira ya soko ulivyo sasa" amesema.

Kikwete amesema miaka ya nyuma zao hilo lilikuwa likilimwa kwa wingi katika Kata hiyo na maeneo mengine ya Halmashauri ya Chalinze na baadae mwamko ulipungua kutokana na soko na kwakua sasa mazingira yameboreshwa ni vyema kulima zao hilo ambalo litawainua kiuchumi.

Awali Ofisa kilimo wa Halmashauri ya Chalinze Jovin Bararata alisema mbegu ya zao hilo, pembejeo na dawa zinatolewa bure huku mbolea ikitolewa kwa ruzuku na mazingira ya soko yameboreshwa kutokana kuwepo kwa kiwanda cha uchakataji katika Kata ya Mandera.

Bararata amesema ni vema wananchi wakachangamkia fursa ya uwepo wa kiwanda hicho badala ya kuwaachia wakulima kutoka mikoa mingine.

Ofisa kilimo huyo amewashauri wakulima kuzingatia kuwatumia Maofisa ugani kwa ushauri wa kilimo ili walime kwa kufuata kanuni za kilimo na kupata mafuno mengi.

#ChalinzeYetu
#KaziInaendelea
Hapo naona ameanza kukomaa kwa kweli.
 
Kanda ya ziwa wanalima pamba ila bado ni maskini.
 
sijui kwanini ila hapa nimekumbuka zile tani za heroine zilizokamatwa kule kusini punde baada ya kifo cha JPM
 
Back
Top Bottom