Ridhiwani: Waliotelekeza nyumba za NHC kunyang'anywa

Ridhiwani: Waliotelekeza nyumba za NHC kunyang'anywa

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
1653050912339.png

RIDHIWANI: WALIOTELEKEZA NYUMBA ZA NHC KUNYANG'ANYWA.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amewataka wapangaji wa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambao wametekeleza nyumba hizo pamoja na kuwa wanazilipia kodi kuondolewa mara moja na kupangishwa Watanzania wengine wanaohitaji.

Mhe. Ridhiwani ameyasema hayo katika Hoteli ya Nashera Jijini Dodoma wakati wa kuwaaga Wakurugenzi wa Bodi ya NHC waliomaliza muda wao wa miaka mitatu.

Amesema kuwa baadhi ya wapangaji wa NHC wamekuwa si waungwana kwa sababu wamepangishwa nyumba na wanazilipia kodi lakini hawaishi ndani ya nyumba hizo.

"Malengo ya kujengwa nyumba hizi hayakuwa kufuga popo, ni kwa ajili ya watu kuishi. Malengo hayajabadilika na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kusisitiza katika kusimamia misingi ya uanzishwaji wa shirika na Miradi yake." Alisema Mhe. Ridhiwani Kikwete.
 
Kuna mtu, watu wanatafutwa hapo. Kwani tatizo nini!? Serikali si mnalipwa Kodi yenu vizuri hata kama wakiwa wanaishi Popo.
 
Sasa wametelekezaje huku wanalipa Kodi hapo ukiona hivyo Kuna watu wanataka kukomolewa na dili kuvutwa upya
 
Back
Top Bottom