Aliye wahi kuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, amesema kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 alifanikiwa kuwahamasisha watu milioni 4 kutoka eneo la Mlima Kenya kumpigia kura William Ruto, hatua iliyomsaidia kupata urais.
Hata hivyo, Gachagua amesema mambo yamebadilika, na sasa ana mpango wa kuhamasisha watu milioni 8 kutoka eneo hilo hilo katika uchaguzi ujao – lakini safari hii, kwa lengo la kumrudisha Ruto nyumbani.
"Nchini 2022, nilihamasisha watu milioni 4 kutoka eneo la Mlima Kenya kumpigia kura William Ruto, na wakamfanya kuwa rais. Katika uchaguzi ujao, nitahamasisha watu milioni 8 kutoka eneo hilo hilo ili kumrudisha nyumbani," alisema Gachagua.
Kauli hiyo imeibua hisia kali mitandaoni huku baadhi wakiona kama ishara ya mgawanyiko mkubwa ndani ya serikali ya Kenya Kwanza.