Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Akizungumza hivi karibuni kwenye mahojiano, aliyekuwa makamu wa Raiswa Kenya, Rigathi Gachagua amesema kuwa alishapewa Ksh Bilioni 2 na Rais Ruto ili ajiuzulu nafasi yake ya Umakamu.
"Ruto aliniomba nijiuzulu, na kuniahidi KSh2 bilioni. Aliniahidi na ulinzi wa kutosha na marupurupu mazuri. Pia alipendekeza kwamba naweza kugombea nafasi nyingine serikalini katika siku za usoni," Gachagua anasema.
Soma pia: Yanayojiri Bungeni Kenya: Wabunge 281 wapiga kura ya kumuondoa madarakani Gachagua
Gachagua pia alidokeza kuwa alihimizwa akubali ofa hiyo kutoka kwa wabunge kadhaa ili kumwepusha na mchakato wa kumng’oa madarakani na hatimaye aweze kugombea nafasi ya urais mwaka 2027.
Source: Buzzrom Kenya