Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Chris Brown alihukumiwa jumanne iliyopita kutumikia kifungo cha nje cha miaka mitano kufuatia tukio la mwezi februari mwaka huu ambapo Chris Brown alimshushia kipigo cha nguvu Rihanna na kuiharibu sura yake.
Chris Brown mwenye umri wa miaka 20, alihukumiwa pia kufanya kazi ngumu za kuitumikia jamii kama vile kufagia barabara na kukata nyasi katika jimbo la Virginia.
Mbali na adhabu hizo, Chris Brown aliamriwa asijaribu kuwasiliana na Rihanna kwa simu wala kwa kumtumia mtu mwingine katika kipindi chote cha kifungo chake cha nje cha miaka mitano.
Alitakiwa pia asimsogelee Rihanna kwa umbali usiopungua mita 90 lakini kama wote watakutana kwenye shughuli za muziki basi wanatakiwa wasikaribiane kwa umbali usiopungua mita 9.
Hata hivyo, kwa mujibu wa vyombo vya habari, Rihanna amekuwa katika jitihada za kuitaka mahakama ifute uamuzi wake wa kumkataza Chris Brown kumsogelea au kuwasiliana naye.
"Wakati Rihanna alipoambiwa na mwanasheria wake kuwa jaji amekataa kufuta uamuzi huo, alionekana mwenye huzuni sana" alisema mdau mmoja wa karibu wa Rihanna akiongea na jarida moja la Uingereza.
"Alianza kuwapigia simu rafiki zake na kusema ni uamuzi gani wa kipuuzi umechukuliwa, Chris hawezi kumpiga na kumjeruhi kwa mara nyingine, Rihanna alionekana ni mwenye hasira sana".
http://www.nifahamishe.com/entertainment.aspx?NewsID=3004790