rim za chuma ni ngumu mno huwezi kulinganisha na hizi sports rim ambazo nyingi ni fake, uzuri wa hizi sports rim ni kwamba tu zinapendezesha gari. Vile vile Sports rim original ni adimu na ukipata ni bei ghali sana (mfano set ya rim kwa inch 15-16 inacheza laki 900 mpaka milioni moja)
Mimi nilikuwa natumia hizi rim za chuma inch 14 (zilikuja na gari toka nje) ila kwa bahati mbaya zilikuwa ndogo sana na kwa barabara zetu hizi gari ilikuwa inagusa chini sana ikabidi nitafute inch 15 ila kuzipata ilikuwa shughuli kubwa, huwezi kuzipata dukani mpaka kwa madalali wa magari mtaani. Ukifanikiwa kupata hizi rim za chuma ni bori kuliko hizo sports rim.
Labda nikuulize unataka size gan?