RIP: Kanali (Mstaafu) Geofrey Marealle

RIP: Kanali (Mstaafu) Geofrey Marealle

John Mnyika

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2006
Posts
713
Reaction score
1,246
Tunasikitika kupokea kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini na mmoja wa waasisi wa CHADEMA Kanali (Mstaafu) Geofrey Marealle kilichotokea jana usiku. CHADEMA inatuma salamu za pole kwa familia ya marehemu na wanaCHADEMA wote duniani kutokana na msiba huo. Salamu za rambi rambi zitatolewa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe mara baada ya kutaarifiwa utaratibu mzima wa mazishi toka kwa familia ya marehemu.

Imetolewa tarehe 2 Disemba 2009 saa 11 jioni na Katibu Mkuu; Dr Wilbroad Slaa.


3/12/09: Mzee Marealle anatarajiwa kupumzishwa kwenye makazi ya milele nyumbani kwake Marangu siku ya Jumamosi tarehe 5 Disemba 2009. Apumzike kwa Amani


 
Mwenyezi mungu ampumzishe Mahali pepa peponi Mzee Marealle.Poleni sana Wana Chadema ndugu na marafiki wa Familia ya marehemu...Mwenyezi Mungu awazidishie nguvu na Faraja katika kipindi hichi kigumu cha Maombolezi.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.Ameni
 
Rest in peace Colonel. We will remember you always.
 
RIP another great Marealles tangu enzi za Mangi Mkuu, Thomas Marealle.
 
Msiba huko wapi sasa?

Mzee Marealle anatarajiwa kupumzishwa kwenye makazi ya milele nyumbani kwake Marangu siku ya Jumamosi tarehe 5 Disemba 2009. Apumzike kwa Amani (hope so!)

Bwana wa majeshi mwenye kutenda miujiza amrehemu na pole nyingi kwa familia na ndugu zetu wa CHADEMA!
 
Rest in peace my friend. Umetangulia nasi tutafuata. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
 
Salamu za pole kwa ndugu jamaa na marafiki katika kipindi kigumu cha msiba, tupo pamoja.
 
(RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA!......................
na mwanga wa milele umuangazie!....apumzike kwa amani,AMINA!)*3

atukuzwe baba na mwana na roho mtakatifuuuu!-KAMA MWANZO NA SASA NA SIKU ZOTE NA MILELE AMINA
 
Poleni Wafiwa wote. Poleni CHADEMA. Kumbe CHADEMA ina mizizi mizito Kilimanjaro.
 
Watu kama hawa watakumbuka na watu wote wapenda amani duniani kote
 
Back
Top Bottom