Ripoti: Baadhi ya Vyombo vya Habari Nchini Kenya Vyabainika kutoripoti Mauaji ya Wanawake kwa Weledi

Ripoti: Baadhi ya Vyombo vya Habari Nchini Kenya Vyabainika kutoripoti Mauaji ya Wanawake kwa Weledi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Baraza la Habari la Kenya kupitia
Idara ya Utafiti, Mipango na Mikakati ilitoa Muhtasari wa Uripoti wa Mauaji ya Wanawake nchini humo ambapo Baraza hilo lilibaini kuwa baadhi ya Vyombo vya Habari vimekuwa vikiripoti mauaji ya Wanawake bila weledi, hasa kwa kutoa habari zisizo sahihi, zisizo na hisia na zenye mihemko

Utafiti huo wa kuanzia Januari 1 -31 2024 ulibaini Vituo vya Anguo FM, Taifa Leo, The Star na Kiss FM viliripoti Mauaji ya Wanawake kwa kutoa habari zisizo sahihi, zisizo na hisia na kwa mihemko kupita kiasi

Baraza la Habari limetoa wito kwa wadau wa vyombo vya Habari kurejea kwenye njia sahihi na kuzingatia kuripoti Matukio ya aina hiyo bila ushabiki na kwa kuzingatia maadili

Source: AN ANALYTICAL
OVERVIEW OF FEMICIDE REPORTING IN KENYA Report
 
Back
Top Bottom