BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Kwa mujibu wa Ripoti ya Taasisi ya Global Financial Integrity (GFI) na Washirika wake imeonesha bado Tanzania ina tatizo sugu la Utakatishaji Fedha unaotokana na Biashara Haramu kiasi cha kupoteza zaidi ya Tsh. Trilioni 3.5 kila mwaka.
Kati ya vitendo vinavyochangia tatizo hilo ni pamoja na vitendo uhalifu ambao umekuwa ukiibuliwa katika Bandari ya Dar es Salaam hadi kusababisha Rais Samia kutangaza kuvunja Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na ile ya Shirika la Meli kwa kutoridhika na Utendaji kazi wake.
Rais Samia alichukua uamuzi wa kuivunja Bodi ya TPA akisema kuna madudu mengi yanayofanywa ndani ya Mamlaka hiyo licha ya Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuonesha ubadhirifu mkubwa lakini hakukuwa na hatua zilizochukuliwa kwa wahusika.
Uchambuzi kuhusu Kiasi cha Fedha zinazopotea zingeweza kufanya nini
Iwapo Tsh. Trilioni 3.5 zingetumika katika Ujenzi wa Vituo vya Afya, takriban vituo 7,000 byenye thamani ya Tsh. Milioni 500 kila kimoja vingejengwa.
Fedha hizo pia zingewezesha ujenzi wa Miradi ya Madaraja 4 yanayofanana na Daraja la Kigongo Busisi (Magufuli Bridge) linalojengwa mkoani Mwanza kwa gharama ya Tsh. 716,000.
Aidha kama Fedha za mkopo wa IMF Tsh. Trilioni 1.3 ziliwezesha ujenzi wa vyumba vya Madarasa 15,000, na hivyo kama Tsh. Trilioni 3.5 zinazopotea kila mwaka zingetumika ipasavyo zingejenga vyumba 45,000 vya Madarasa.
Pia, Fedha hizo zingeweza kununua Mashine 1,605 za CT-Scan na Mashine 2058 za MRI na kama zingepeleka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) zingetosha kufadhili wanafunzi 140,000 kutoka 28,000 waliopo sasa wanaopata Tsh. Bilioni 654.
Kama hiyo haitoshi, kiasi hicho cha Tsh. 3.5 kama kingetumika kwa usahihi, kingewezesha ununuzi wa Magari ya 43,750 ya Kubebea Wagonjwa (Ambulance) yenye thamani ya Tsh. Milioni 80 kila moja ambapo kila Halmashauri ingekuwa na magari 230.
Kama zingegawanywa kwa idadi ya watu nchini kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Watu 61,741,120 kila Mtanzania angepata Tsh. 56,688 ambayo ingewezesha kununua kilo 16 za Mchele wa Tsh. 3500 kwa kilo.
Kama mwananchi angepewa fedha hizo, angeweza kununua Simu mpya ya Tsh. 50,000 na kubakiwa na Tsh. 6,680 za muda wa maongezi na nauli za Daladala kwa siku 4 kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Kauli ya TRA
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Richard Kayombo amesema " Japokuwa bado sijaisoma hiyo ripoti lakini utafiti wa namna hiyo unatupatia uchambuzi wa kina wa hali halisi juu ya tatizo hili"
Kwa mujibu wa Kayombo, Biashara haramu huhusisha mambo mengi kama vile kuwa na biashara halali lakini yenye ukwepaji kodi, pia kufanya biashara isiyo halali kwa mujibu wa Sheria.
Kayombo alisisitiza "Tumebuni mbinu mbalimbali katika kukabiliana na biashara haramu hasa hizi zenye misingi ya ukwepaji kodi maana ndiyo zinaangukia kwenye uangalizi wetu. Tunashirikiana na Vyombo vya Dola kukabiliana na hili tatizo."
Pia amesema TRA inashirikiana na kwa karibu na Mamlaka nyingine za Forodha kutoka katika nchi za jirani ili kakabiliana na mtandao huo wa wafanyabiashara haramu, hata hivyo Kayombo amekiri kutokana na jiografia ya Tanzania ilivyo, imekuwa kazi ngumu kupambana na mtandao huo japo kazi kubwa imefanyika.
"Changamoto kubwa ni kwamba biashara hi inavuka mipaka ya nchi, na kwa kuwa tuna ukanda wa Bahari karibu kilomita 14000 lakini pia tuna Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa ambayo kimsingi yako mipakani tena na Bandari zisizo rasmi inakuwa ngumu kuzitambua" alisema
Undani wa Ripoti ya GFI
Kwa mujibu wa GFI, Wahusika katika biashara haramu pia hutoa stakabadhi za malipo zaidi ya moja ambazo huonesha tofauti za ujazo au wuingi wa biadha inayouzwa au kununuliwa kinyume na uhalisia wa mzigo.
Kwa mujibu wa GFI, Wahusika katika biashara haramu pia hutoa stakabadhi za malipo zaidi ya moja ambazo huonesha tofauti za ujazo au wuingi wa biadha inayouzwa au kununuliwa kinyume na uhalisia wa mzigo.
Ripoti pia inabainisha namna wafanyabiashara haramu wanavyotumia mfumo usio rasmi (informal value transfer system - IVTS) ambao hutumika kutuma miamala katika Mamlaka/nchi tofauti bila kusafisha fedha halisi kama inavyotumika katika miamala ya simu.
Inasemekana mara nyingi mbinu hizi chafu zenye lengo la kutoa taarifa za uongo kwa mamlaka husika hutumiwa kwenye utakatishaji fedha, ugaidi, na ukwepaji kodi ambapo 9% ya kesi zilizohusiana na ugaidi zilipokea ufadhaili kwa njia hii.
GFI imeshauri Mamlaka kuchukua hatua stahiki kukabiliana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa kikosi kazi maalumu ambacho ni shirikishi hasa ikizingatiwa kuwa idara mbalimbali ndani ya Serikali zinahitaji kushirikiana ili kupambana na biashara haramu.
jambo lingine ni ni utekelezaji wa mkakati wa kusajili taarifa za umiliki wa kimanufaa (national beneficial ownership regestries) kwani kumekuwa na kampuni nyingi za mfukoni ambazo hutumika katika uharamishaji huo wa fedha.
GLOBAL FINANCIAL INTEGRITY