Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Ripoti ya kila mwaka ya Faharasi ya demokrasia iliyopishwa na shirika la Economist imeonyesha kuwa demokrasia iliendelea kushuka katika mwaka wa 2021.
Ripoti hiyo imesema kuwa kwa mwaka uliopita asilimia 45.7 ya watu ulimwenguni waliishi katika aina fulani ya demokrasia, ikiwa ni kiasi cha kilichopungua kutoka asilimia 49.4 katika mwaka wa 2020.
Utafiti huo unasema ni asilimia 6.4 pekee ya watu wanaoishi katika mazingira ya demokrasia kamili ikiwa ni kiwango kilichoshuka kutoka asilimia 8.4 katika mwaka uliotangulia.
Norway inabaki kileleni mwa faharasi hiyo kama nchi yenye demokrasia zaidi. New Zealand ipo nafasi ya pili kutoka ya nne ikifuatiwa na Sweden, Finland, Icelend na Denmark.