Ripoti: Ushuru kwenye 'Bando' za Intaneti' ni balaa Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
%2Fmethode%2Ftimes%2Fprod%2Fweb%2Fbin%2F1f76ddac-bcda-11e7-8bb9-94e1372175c0.jpg

Ripoti ya robo mwaka unaoishia Machi 2023 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaonyesha gharama za ushuru wa bando la intaneti zimeongezeka ikiliganishwa na kipindi kama hiko Machi 2022.

Machi 2022 kwa kila MB moja ushuru uliokuwa unakatwa ni shilingi mbili ambayo imeongezeka hadi kufikia Sh2.09 Machi 2023.

Aidha, ripoti hiyo inaonyesha gharama za ushuru wa bando la dakika na ujumbe mfupi umepungua Machi 2023 ikilinganishwa na Machi 2022.

“Gharama za ushuru wa bando la dakika za kupiga mitandao yote ni Sh6.37 kwa kila dakika Machi 2023 ikilinganishwa na shilingi tisa Machi 2022. Kupiga ndani ya mtandao mmoja Machi 2022 ilikuwa inatozwa shilingi nane kwa kila dakika imepungua hadi kufika Sh4.66,” imesema ripoti hiyo.

Aidha kwa upande wa ujumbe mfupi Machi 2022 ulikuwa unatozwa shilingi tatu kwa kila mmoja huku ikishuka hadi Sh1.34 kwa kila ujumbe mmoja.

Mbali na gharama hizo, pia ripoti hiyo inaonyesha laini za simu zinazotumika nchini zimeongezeka kutoka milioni 55.3 Machi 2022 hadi milioni 61.9 Machi 2023 sawa na ongezeko la asilimia 11.9.

TCRA
 
Ok
Kwa hiyo Ndugu Nape Nnauye waziri alikuwa anadanganya wananchi kuwa tatizo ni makampuni ya simu Kumbe tatizo ni Yeye Nape na TCRA

Nape na TCRA wanagonga ushuru kwenye MB kimya kimya tena kwa kasi ya 6g

Hii nchi viongozi wanawaona wanamchi malofa sana

Unaongeza ushuru kwenye MB 1 halafu unataka bei ishuke,What kind of crazy is this

Eeeeh ukishangaa ya Musa utayaona ya Nnape Nnauye

Nape anaongea mpaka miwani inatikisika kuwa bei za Bando kuwa juu ataongea na makampuni ya simu Kumbe nyuma ya Pazia wanayagonga tozo ya ushuru
 
%2Fmethode%2Ftimes%2Fprod%2Fweb%2Fbin%2F1f76ddac-bcda-11e7-8bb9-94e1372175c0.jpg

Ripoti ya robo mwaka unaoishia Machi 2023 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaonyesha gharama za ushuru wa bando la intaneti zimeongezeka ikiliganishwa na kipindi kama hiko Machi 2022.

Machi 2022 kwa kila MB moja ushuru uliokuwa unakatwa ni shilingi mbili ambayo imeongezeka hadi kufikia Sh2.09 Machi 2023.

Aidha, ripoti hiyo inaonyesha gharama za ushuru wa bando la dakika na ujumbe mfupi umepungua Machi 2023 ikilinganishwa na Machi 2022.

“Gharama za ushuru wa bando la dakika za kupiga mitandao yote ni Sh6.37 kwa kila dakika Machi 2023 ikilinganishwa na shilingi tisa Machi 2022. Kupiga ndani ya mtandao mmoja Machi 2022 ilikuwa inatozwa shilingi nane kwa kila dakika imepungua hadi kufika Sh4.66,” imesema ripoti hiyo.

Aidha kwa upande wa ujumbe mfupi Machi 2022 ulikuwa unatozwa shilingi tatu kwa kila mmoja huku ikishuka hadi Sh1.34 kwa kila ujumbe mmoja.

Mbali na gharama hizo, pia ripoti hiyo inaonyesha laini za simu zinazotumika nchini zimeongezeka kutoka milioni 55.3 Machi 2022 hadi milioni 61.9 Machi 2023 sawa na ongezeko la asilimia 11.9.

TCRA

FuigCVOXoAEAeqR.jpeg
 
Back
Top Bottom