Zawadi Mkweru
Member
- Jan 11, 2017
- 5
- 19
Utafiti mpya uliofanywa na chuo cha Aston mjini Birmingham, Uingereza umegundua kuwa katika bidhaa 9 kati ya 10 za urembo (Makeup) ambazo zimekwisha kutumika zina bakteria hatari.
Utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la Applied Microbiology, ulichunguza bidhaa 467, ikiwemo rangi za midomo, rangi za kope, na vipodozi vya ngozi ambavyo vilitolewa kwa ajili ya uchunguzi baada ya matumizi.
Matokeo yake yalipata bakteria kama E.coli, Staphylococcus na makaazi ya kuvu/fangasi ndani ya bidhaa hizo huku mchanganyiko/losheni za ngozi zikiwa na hali mbaya zaidi.
Asilimia 92 ya vipodozi vyote vilivyochunguzwa vilikuwa na bakteria/vijidudu huku wakati asilimia 72 ya wadudu hao walikuwa na staphylococcus wenye kinga kubwa dhidi ya Antibiotiki, asilimia 25 walikuwa E.coli na asilimia 57 walikuwa na fangasi.
Bidhaa zingine zilizobainika kuwa na bakteria aina ya staphylococcus zilikuwa ni Mascaras (asilimia 69) na eyeliner (asilimia 77). Moja kati ya lipsticks 10 zilikuwa na E.coli, na asilimia 37 ya lipsticks na asilimia 28 ya eyeliner zilizopimwa zilikuwa na kuvu/fangasi.
Virusi hivi, ikiwa vitaachwa na kuzaliana, vinaweza kuumiza ngozi na macho kupitia vidonda, matongotongo machoni na kuzalisha sumu kwenye damu.
Amereen Bashir kutoka Chuo Kikuu cha Aston amesema Elimu Zaidi inahitajika kufanywa ili kusaidia kuelimisha watumiaji na tasnia ya urembo kwa jumla juu ya hitaji la kuosha vifaa vya urembo mara kwa mara na kuvikausha kabisa, pamoja na hatari ya kutumia bidhaa ambazo muda wake wa kuharibika umekaribia.
Wataalam wanapendekeza kuosha zana za urembo mara kwa mara, kutupa bidhaa zilizomaliza muda wake wa matumizi na kujiepusha na kushiriki vitu vya urembo na watu wengine haswa vifaa ambavyo unavikuta saluni na vinatumiwa na kila mteja.
Watengenezaji wa bidhaa za urembo nao pia wanahimizwa kuonyesha tarehe za kumalizika kwa matumizi ya bidhaa zao ili kulinda wateja kutokana na madhara wanayoweza kuyapata.