Ripoti: Wanawake walioko katika Jicho la Umma wanapitia zaidi Ukatili wa Mtandaoni

Ripoti: Wanawake walioko katika Jicho la Umma wanapitia zaidi Ukatili wa Mtandaoni

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Ripoti ya UNESCO "The Chilling: Global Trends in Online Violence Against Women Journalists" inaeleza kuwa wanawake wanaojulikana hadharani kama waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu, wanaharakati, na wabunge wanakumbwa na viwango vya juu vya ukatili wa mtandaoni.

Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 73 ya waandishi wa habari wanawake wamepitia ukatili huu, ambao mara nyingi unahusisha vitisho, matusi ya kijinsia, na unyanyasaji wa kihisia.

Ripoti inasisitiza kuwa wanawake katika nafasi hizi za umma wanakabiliwa na mashambulizi haya zaidi kuliko wenzao wa kiume, hali inayozuia ushiriki wao katika majadiliano ya hadhara na kuathiri uhuru wa kujieleza.

Takriban nusu (47%) ya Wanawake walioshiriki katika utafiti wa UNESCO wa Matokeo ya Ukatili wa Mtandaoni kwa Waandishi wa Wanawake (2020), walisema kuripoti au kutoa maoni kuhusu masuala ya kijinsia, kama vile usawa wa kijinsia, ukatili wa wanaume dhidi ya wanawake na haki za uzazi ni kichocheo kikubwa cha mashambulizi ya mtandaoni

Mada za siasa na uchaguzi zilifuata kwa 44%, zikionyesha jinsi mashambulizi ya kisiasa yanavyoongeza hatari kwa usalama wa waandishi Wanawake

Masuala ya haki za binadamu na sera za kijamii (31%) na uhamiaji (17%) pia yalichangia ukatili wa mtandaoni, huku upotoshaji wa taarifa (16%) na uandishi wa uchunguzi (14%) vikionyesha namna uandishi wa uchunguzi unavyochangia mashambulizi hayo.

Chanzo: UNESCO
 
Back
Top Bottom