Ripoti ya benki ya Dunia kuhusu mazingira ya biashara nchini Tanzania

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Katika Makala haya tuifananishe nchi yetu na majirani zetu kwenye upatikanaji wa ajira na ukuzaji wa uchumi. Viko vitu vingi vya kuzunguza lakini kwa taarifa iliyopo naweza zungumzia upatikanaji wa nishati, hatua za kuanzisha biashara na upatikanaji wa mikopo.

Pia niweke nen kwenye masharti ya biashara kwa fikra zangu baada ya kutafakari sana jambo hili.
  • Masharti ya biashara yanawekwa ili kufanya watu wakuze vipato vyao, kwa kuzidiscourage vitu vya nje kama watu wa ndani wanajiweza kibiashara
  • Masharti huwekwa ili nchi kufaidika na biashara zinaowekwa kutoka nje. Hapa tuangalie masharti na sera zetu za biashara kama zinajali kuhusu nchi kupata mapato ya nje au tunaweka masharti ilimradi tu kuwe na masharti bila kuangalia nani ananufaika
Kwa wenye kukumbuka Gametheory, kwenye GAME THEORY, we are always playing game, lakini inabidi tuangalie vizuri ili kuona hasara yako isiwe kubwa when it happens you lose, the game does not give you a guarantee that you will always win. Ndipo nilipoelewa maana ya win-win situation. So kwenye games za kimataifa ni vyema kuifikia hiyo win-win situation

UANZISHAJI WA KAMPUNI YA BIASHARA

Siku si chini ya 38 hutumika Tanzania ili kusajili biashara yako wakati wenzetu wa Kenya hutumia siku 29 kukamilisha usajili wa biashara. Saudi Arabia ndio hawana shaka wao hutumia siku kumi na moja

Sisi tuna mlolongo wa hatua kumi ambao ukienda kama ulivyopangwa unaweza tumia siku hizo na ikitokea umekosea chochote basi siku zinaweza kuongezeka. Saudi arabia kwa wanaume wanakuwa na hatua nne za kufuata kuanzisha bisahara huku wanawake wakiongezewa moja, zikawa tano, hatua hiyo ni kuomba kibali kwa mumewe kabla ya kuomba kuanzisha kampuni ya biashara.

Kidunia sisi ni wa 162, Kenya ni wa 129 Saudi arabia ni 38 nchi ya kwanza kwenye kutocomplecate uanzishaji wa biashara ni New Zealand ambayo hutumia siku moja kukamilisha hatua zote za kuanzisha kampuni.

Idadi ya siku zilizopo hasa katika nchi zetu zinaongeza uwezekano mkubwa kutoa rushwa ili walau mtu kampuni yake iweze kufanya kazi ndani ya muda.

UPATIKANAJI WA MIKOPO

Pia ikumbukwe ni muhimu wajasiriamali kupata mikopo, lakini uhitaji wa mikopo mara nyingine huwa ghafla, hivyo basi upatikanaji wa mikopo utaonyesha ni kwa namna gani wananchi wanaweza kuenjoi mema ya nchi. Kibongo bongo najua mnajua baadhi ya taasisi za serikali zenye masharti nafuu zinavyoleta shida kuwa unaomba mkopo mwezi huu, unakuja kuitwa kupata mkopo wakoo mwaka mmoja baadae kama ni tatizo unakuta umeshatatua au kama ni wazo la biashara umeshaachana nalo.

Kwenye upatikanaji wa mikopo Tanzania imeshika nafasi ya 67 wakati kenya wako nafasi ya 4.

TRADING ACROSS BOARDERS

Ni kawaida kwa mfanya biashara kutarajia faida katika bisahara yake, hali hii humuhitaji mfanya bishara kuhitaji vitu kutoka nje ya nchi au kupeleka bidhaa zake nje ya nchi, ilimradi kutafuta faida kwenye ayafanyayo. Katika hii pia tunasuasua, kwa kuwa Tanzania imekuwa ya 182 katika kufanya biashara across the boarders, Kenya imekuwa ya 117

ENFORCING CONTACTS

Hapa watafiti waliangalia hatua za kufutwa tangu ufunguaji wa kesi hadi kumaliza kesi husika, ili kulinda mikataba, hapa Tanzania imekuwa ya 71 huku Kenya ikiwa ni ya 89


Taarifa na takwimu hizi zimetokana na kitabu cha World Bank – Doing Business

Bofya HAPA kusoma
 

Attachments

Makala imeenda shule, tuache siasa tuzifanyie kazi hizi changamoto.
 
Serikali imefanyia kazi haya mambo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…