BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
CAG alibaini gharama matumizi zinazidi mapato kwa 7% hadi 19 kuanzia mwaka 2018/19 na 2021/22 kiasi cha kuongeza nakisi kutoka Tsh. Bilioni 1.92 mwaka 2018/19 hadi Tsh. Bilioni 5.81 mwaka 2021/22.
Sababu nyingine zilizochangia kushuka mapato ni Misamaha isiyo na udhibiti, kuongezeka madai yanayokataliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya pamoja na huduma duni za Kibingwa za Kulaza Wagonjwa binafsi na wa Umma.
Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG amesema, Utendaji duni unaweza kusababisha kuzorota kwa huduma za afya hospitalini kutokana na mapato duni ambayo hayawezi kukidhi gharama za uendeshaji na ugumu wa kufikia malengo ya kimkakati kutokana na kupungua kwa mapato kulingana na gharama zinazotumika.
Ninapendekeza kuwa Hospitali ya Mloganzila (a) ihakikishe huduma za kibingwa zinaimarishwa hospitalini hapo ili kuongeza wagonjwa binafsi na wa umma, (b) ihakikishe inaendana na mwongozo wa Mfuko wa Bima ya Afya ili kupunguza idadi ya madai yanayokataliwa, na (c) kuweka misamaha kielektroniki ili kuimarisha udhibiti wa misamaha inayotolewa.