BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mara nyengine ameendelea kuonyesha udhaifu mkubwa na ubadhirifu katika Fedha za Mikopo inayotolewa na Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu.
Fedha hizi ni 10% ya Mapato ya Ndani ya Mamlaka hizi za Serikali za Mitaa. Katika mwaka huu wa Ukaguzi, yaani 2021/2022, Mamlaka za Serikali za Mitaa zilikusanya mapato ya ndani ya jumla ya shilingi bilioni 892, hivyo fedha zilizopaswa kutolewa kama mikopo zilikuwa shilingi bilioni 89.2. Katika ukaguzi wa mwaka 2021/2022, CAG ameibua hoja zenye thamani ya Shilingi Bilioni 97.59 kuhusu mikopo hii. Thamani ya hoja za ukaguzi ni 109% ya fedha zote zilizopaswa kutolewa kama mikopo kwa makundi hayo ya jamii.
Hoja hizo ni kama zifutazo;
i. Kutorejeshwa Shilingi Bilioni 88.42 zilizotolewa kama mkopo kwenye vikundi ambapo takribani Mamlaka 180 za Serikali za Mitaa zimeshindwa kurejesha mikopo ya shilingi Bilioni 88.42.
ii. Vikundi 201 kwenye mamlaka nane za serikali za mitaa vilivyopewa mikopo ya shilingi milioni 774.66 havikutekeleza miradi iliyoidhinishwa. Vikundi hivi viligawana fedha na hapakuwepo ushahidi kama fedha zilitumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
iii. Kutokuwepo kwa vikundi vilivyopewa mikopo ya shilingi Milioni 895.94 ambapo CAG alishindwa kujiridhisha juu ya uwepo wa vikundi 48 vilivyopewa mikopo yenye thamani ya Milioni 895.94(Vikundi hewa)-Maafisa maendeleo ya jamii ya kata husika hawakufahamu lolote kuhusu vikundi hivyo.
iv. Mikopo inayodaiwa kwenye vikundi vilivyositisha shughuli za biashara shilingi Bilioni 2.25 ambapo Mamlaka 9 zikiwemo Halmashauri za Temeke, Monduli na Tandahimba zilitoa mikopo ambayo haikurejeshwa kwa vikundi vilivyositisha shughuli zao za biashara.
v. Mamlaka 33 za serikali za mitaa hazikuchangia jumla ya shilingi bilioni 5.06 kutoka kwenye mapato yao ya ndani kwa miaka mitatu mfululizo.
vi. Mikopo ya shilingi milioni 147.26 imetolewa kwa watu wenye ajira Rasmi, mathalani Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilitoa milioni 147.26 kwenye vikundi vitano vyenye wanachama wenye ajira rasmi kinyume na kanuni hivyo kupelekea malengo ya mikopo hii kutofikiwa.
Matumizi Mabaya ya Fedha za Mapato
Ukaguzi wa CAG katika Mfumo wa Mapato (LGRCIS) umeonesha makusanyo ya Tsh. Bilioni 11.07 kupitia Mashine za POS hayakupelekwa kwenye akaunti za Benki za Serikali za Mitaa husika
Pia, Mapato kupitia Mifumo ya Taarifa za Ukusanyaji Mapato ya Serikali za Mitaa (LGRCIS) (Tsh. Bilioni 76.59) hayakukusanywa kutoka kwenye Vizimba vya Masoko, Mauzo ya Viwanja, Mazao ya Kilimo, Leseni za Vileo, Ushuru wa Uchimbaji na Vifaa vya Ujenzi
Maeneo mengine ni Leseni za Biashara, Ushuru wa Huduma na Ushuru wa Kupangisha Maduka na Nyumba zilizopo Stendi za Mabasi na Masoko ya Halmashauri