Ripoti ya CAG kuhusu kituo cha Mabasi

Ripoti ya CAG kuhusu kituo cha Mabasi

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Waungwana,

Hivi ile ripoti ya CAG aliyokabidhiwa Pinda wiki chache zilizopita kuhusiana na kituo cha Mabasi kinachoendeshwa na Kingunge ilishatolewa hadharani au bado Pinda ameikalia?

Natanguliza shukrani.
 
Ndugu yangu BAK,
Jibu ni kuwa hadi sasa ameikalia. Swali jingine au ushauri juu ya hili?
 
Ndugu yangu BAK,
Jibu ni kuwa hadi sasa ameikalia. Swali jingine au ushauri juu ya hili?

Hapana Nono sina swali lingine wala ushauri bali nilitaka kujua tu kama imetolewa hadharani ili Wananchi tujue ufisadi unaoendelea pale.
 
Hapana Nono sina swali lingine wala ushauri bali nilitaka kujua tu kama imetolewa hadharani ili Wananchi tujue ufisadi unaoendelea pale.


Usisahau kuwa mhusika pale ni mbunge aliyeteuliwa na Mkuu w kaya, na huyo huyo akamteua Pinda wa kupindapinda. lazima aipeleke kwake kwanza, na yeye akamwambia iweke kwanza nitaongea na Mzee baadaye.
 
hivi mnategemea chochote kutoka kwa hawa mafisadi? wamelipana mamilioni kuandaa bogus report na hakuna chochote kitakacho badilika na mamilioni yataendelea kuliwa pale kituoni na huduma mbovu kila siku,ukiangalia vizuri issue kama ile ya ufujaji na uzembe kwenye kituo kidogo kama kile hata mkuu wa wilaya/council hata madiwani au mkurugenzi wa municipal wangeweza kumaliza mambo na mambo yakawa sawa lakini msitegemee chochote toka hii serikali ya majambazi & incompetent,tuna safari ndefu sana na umaskini wa kudumu kama hawa jamaa wakiendelea kushika nchi!
 
labda itakuwa inabadilishwa kabla ya kuja kuwekwa wazi kwa wananchi
 
Anaogopa kugusa keki ya kikongwe chetu kisicho na imani.
 
Back
Top Bottom