Ripoti ya CAG: Kuna Tshs Milioni 892.92 zililipwa bila Serikali kupokea uthibitisho kuwa miradi imetelekezwa

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

CAG ameendelea kuibua madudu yaliyopo kwenye sekta mbalimbali hapa nchini ofisi yake imebaini kuwa miradi minne ililipa jumla ya Sh. 892.92 kwa mafundi na wakandarasi kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu bila kutumia nyaraka za vipimo, nyaraka ambazo zinathibitisha kazi zilizotekelezwa.

Miundombinu hiyo ni ya shule na vyuo vya walimu, ikiwa pamoja na madarasa, matundu ya vyoo, majengo ya utawala, mabweni, na majiko.

​

“Kasoro hii ilikotokana na upungufu wa watumishi katika idara ya ujenzi kulikosababisha kuidhinishwa kwa malipo bila kuhakikiwa kwa kina, kutathmini, na kupima kazi zilizofanyika. Maelezo ya kazi ambazo zilifanywa bila nyaraka za vipimo,”amesema.

Katika Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kipengele cha usimamizi wa fedha, matumizi na bajeti, amesema idara ya ujenzi kuidhinisha malipo bila kukagua na kupima kazi iliyokamilishwa kunaongeza hatari ya malipo ya ziada, malipo ya kazi isiyokamilika, na uwezekano wa matumizi mabaya ya fedha za umma.

“Ninapendekeza wasimamizi wa miradi wahakikishe kuwa kazi zinakaguliwa na kupimwa kabla ya kuidhinishwa,”amesema.

CAG amesema Kanuni ya 243(2) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2013 inazitaka taasisi zinazofanya ununuzi ziidhinishe malipo kwa kuzingatia vipimo vilivyoidhinishwa katika vipindi maalumu vya mkataba.

Aidha, Aya ya 25.3 ya Mwongozo wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi kwa Utaratibu wa Nguvukazi (force account) uliotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) wa Mei 2020 unaelekeza kuwa vipimo vya pamoja vya kazi zilizokamilika vifanywe na meneja wa mradi kwa kushirikiana na taasisi inayotekeleza mradi.

Source: Nipashe
 
Kuna haja gani kwa nchi za kiafrika kama Tanzania kuwa na Taasisi kama hizi za CAG zinazoteketeza pesa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…