Ripoti ya Sky News kuhusu Magufuli na COVID-19

Hili la corona, tutumie busara tuliache, in the circumstances the world found itseft entangled into, President Magufuri took a big bet, and for those of us who likes smooth landing, it was not right.
 
mimi nilipata corona nikiwa mbeya, na nina watu ninawafahamu karibia watano walipata korona!


hakuna aliyekufa
Safi!

Hata mimi niliipata mwezi wa pili mwaka huu.

Wala haikuwa ishu.
 
Nyani Ngabu, achana na hiyo habari ya Corona, huoni image ya nchi kimataifa imechafuka sana? Kuna nini cha kujivunia katika kusemwa vibaya namna hii? Kwamba nchi haina uhuru wa mawazo na habari kiasi hicho unaona ni jambo jema? Hii sio Tanzania. Tumekuwa kituko duniani! Hii sio Tanzania iliyoachwa na kina Nyerere na wengine. Inasikitisha sana tumefikia huku. Lakini inasikitisha zaidi kuona mtu mwenye uelewa na exposure kama wewe Nyani Ngabu huoni hii hali na ubashabikia. Hebu tazama picha na taswira pana ya nchi kimataifa ilivyochafuka badala ya kuangalia mambo kwa upeo finyu namna hii.
 
Safi!

Hata mimi niliipata mwezi wa pili mwaka huu.

Wala haikuwa ishu.
thats why sioni logic ya hizi hofu.....


unajua upimaji ukifanyika kwa wingi na case zinakua nyingi vile vile, kama ilivyo kenya wanavyozidi kupima ndipo wanaona maambukizi yanazidi lkn vifo vinapungua sana!


nadhan ndio shida waliyonayo pia US, ni kama wamepima zaid ya watu 40-50m, matokeo yake case ni almost 5m, na vifo ni 150k (including waliogongwa na magari [emoji23] as long as walikua na corona),....... %age wise ni kitu kidogo


......bottom line approach ya magufuli ilikua sahihi, its all politics nothing more......
 
Kaka mimi nashindwa kuwaelewa Wakenya, sijui kwanini wanaigaiga kila kitu. Au wanataka wapate pesa za kupambana na Corona. Naona wanachofanya sasa ni kwenda kukopeshwa au kupewa pesa ya msaada ili kununua bunduki na kuitumia kuua nzi. Sijui lini watafungua mipaka yao, ngoja tuoje. Labda wanadhani Corona itayeyuka.

 
Mkuu imechafuka kwa lipi? Kwa kutumia strategy yetu nyepesi kupambana na Corona? Yaani tusipofanya wenzetu wanalotaka basi image yetu inachafuka? Niambie umepoteza ndugu wangapi kwa Corona?


 
Unasema nchi [Tanzania] haina uhuru wa habari na mawazo?

Wewe ulichokifanya hapa ni nini kama siyo kutoa mawazo yako?

Au Kuna mtu alikuwa kakuwekea mtutu wa bunduki kichwani na akakulazimisha kuandika hivi ulivyoandika?
 
Hii ilikuwa ni vita tu ya kiuchumi, na Kenya wanataka kuitumia dhidi yetu
 
Wakenya wamepick side na kuwa puppets wa Western countries
 
Unasema nchi [Tanzania] haina uhuru wa habari na mawazo?

Wewe ulichokifanya hapa ni nini kama siyo kutoa mawazo yako?

Au Kuna mtu alikuwa kakuwekea mtutu wa bunduki kichwani na akakulazimisha kuandika hivi ulivyoandika?
Nini usichokijua kuhusu uminywaji wa uhuru wa kujieleza Tanzania hii? Huoni hapa tumeficha identity zetu?
 
Nini usichokijua kuhusu uminywaji wa uhuru wa kujieleza Tanzania hii? Huoni hapa tumeficha identity zetu?
Hujalazimishwa kuficha utambulisho wako.

Huo ni uamuzi wako.

Wapo wengine humu wanaotumia majina yao ya ukweli.

Uongo?
 
Tulimpa Mungu nafasi atupiganie, (maana sisi hatukuwa na uwezo wa kujipigania kwenye janga hilo) akafanyahivyo.

Sifa na utukufu ni kwake Muumba mbingu na nchi. Tuendelee kumshukuru Mungu kwa kuwa ametanda!!!!!


JESUS IS LORD!
 
Kwani vifo ndo vimeanza wakati wa korona
 
Swadakta mkuu wangu👏👏👏

Mungu Hamfichi Dhalimu....

Tumewatambua kuwa WALIKUWA ni waongo walipotutanabahisha kuwa tutakuwa MIZOGA kama kumbikumbi barabarani.

UONGO WAO wa SKY NEWS na wenzao tunashukuru Mungu Ya Kwamba UTATUSAIDIA kuwa ni REJEA ya Mambo huko TUENDAKO.....

Sijui tumedanganywa mfanowe Mara ngapi?!!!
Na Sijui Kama tulishaweka kumbukumbu ya UONGO wao MWINGI.

Kama Taifa linalokimbia kimaendeleo ni Bora Sasa kukatokea msukumo wa kuwekeza kwenye VIWANDA vya CHANJO dhidi ya Kinga ya magonjwa mbalimbali.
Tunaweza Tukaanza na HIZI wanazopewa WATOTO WETU toka KUZALIWA kwani kufikia mpaka Sasa magonjwa yanayolisumbua kundi la miaka 5 kushuka chini wataalam wetu WAMESHAYAJUA na;
Tuna wataalamu bobezi wa CHEMISTRY
Tuna Wataalamu bobezi wa BIOCHEMISTRY na NUCLEAR CHEMISTRY
Tuna wataalamu bobezi wa MICROBIOLOGY na ZOONOLOGY
Tuna wataalamu bobezi wa PARASITOLOGY
Tuna wataalamu bobezi wa PHYSIOLOGY,PATHOLOGY,INTERNAL MED na wengine wanaohusiana na tiba ya sisi makabwela.

Muhimu ni kuzidi kuwa na msukumo wa zile NONDO NZITO NA ZA MAANA alizozisema NAIBU WAZIRI WA AFYA Dr.Mollel akiwa bungeni siku chache Kabla ya mh.Rais Magufuli KUMTEUA.
(kwa kumbukumbu rejeeni alichokisema).

WAKATI ndio huu,uwepo wa Magufuli ni Mpango wa MUNGU ili kutupa NGUVU za KUTHUBUTU mengi TULIYOYAOTA na tukashindwa huko nyuma.
Tuitumie CHARISMA aliyonayo Magufuli ili TUBUNI na kutekeleza MAKUBWA.

MWISHO kabisa nasema yeyote aliye na Shari Juu ya Mama Tanzania,Mwenyezi Mungu Ampeperushie mbali Kabla ya yeye kusambaratisha Malengo na ndoto zetu adhimu,aaaamin aaaaamin.


Kijana Muuza Al Kasus Yenye Habat Mulki Na Habat Sauda Ya Kutosha.
Tandale Kwa Mtogole.
 
Bado kungekuwa na mambo ambayo yangeonesha athari za uwepo wa corona,kama wingi wa vifo tofauti na hali ya kawaida na pia hata kuona wengi kuuguwa kwa wingi tofauti na kawaida. Mfano nyumba za ibada hasa misikitini ambapo utaratibu wa ibada umerudi kama zamani watu wanakusanyana na hakuna tahadhari zozote hivyo hizo sehemu tungeona waumini wengi wakiugua hasa ukizingatia wengi wazee.
 
Kwa uhatari wa ugonjwa wenyewe watu wangeona utofauti wa vifo vya kabla ya corona na kipindi hiki cha corona.
 
Kusingekuwa na corona duniani,je hicho kifo ulichokihusisha na corona ungekihusisha na nini wakati ambapo hakuna corona? Au ungesema ni ushirikina?
 
Hoja ya kuulizana nani kafa huko na corona ni kutokana na aina ya ugonjwa wenyewe kuwa uwambukizaji wake na uhatari wa ugonjwa wenyewe,na ndio maana mwanzo ilikuwa akipatikana mtu mmoja mwenye corona basi mnabebwa nyumba nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…