Ripoti ya Takukuru kuhusu 'ujenzi holela wa vituo vya mafuta' ilibaini Kituo cha Lake Oil Kawe kipo eneo salama? mbona kinabomolewa na kujengwa upya

Ripoti ya Takukuru kuhusu 'ujenzi holela wa vituo vya mafuta' ilibaini Kituo cha Lake Oil Kawe kipo eneo salama? mbona kinabomolewa na kujengwa upya

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Miezi sita iliyopita hapa jukwaani kulikuwepo na mijadala kuhusu ujenzi holela wa vituo vya mafuta hali ambayo inadaiwa kuhatarisha usalama wa Wananchi kutokana na vituo hivyo kujengwa karibu na makazi ya watu.

Mfano wa Kituo cha mafuta kilichotajwa ni kituo cha Lake Oil kilichopo Kawe, Tanganyika Packers kikitajwa kuzungukwa na makazi ya watu jambo ambalo mdau kupitia andiko lake alidai ni hatari.

Soma Kuongezeka kwa Ujenzi wa Vituo vya Mafuta kwenye makazi ya watu Serikali inasubiri ya Morogoro yatokee ndio ichukue hatua?

IMG_3369.jpeg

Baada ya siku chache taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa mwaka 2022/2023 iliyotolewa Machi 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo CP. Salum Hamduni Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, alisema kuwa walibaini vituo vya mafuta kwenye makazi ya watu jambo linaloleta hofu ya usalama, huku taarifa hiyo ikionesha kwamba asilimia 21 ya vituo vilivyokaguliwa havikuwa na leseni huku pia akibaini ongezeko la ubadilishaji wa matumizi ya aridhi kujengwa vituo vya mafuta.

Awali nilianza kuipongeza Serikali nikijua matunda ya ripoti ya Takukuru na kilio cha wadau kimeanza kupatiwa suluhu baada ya kupita kwenye kituo cha mafuta cha Lake Oil Kawe ambacho kimepigiwa kelele mara kwa mara, nikaona zoezi la ubomoaji linaendelea.

Ilibidi nisimame pembeni kando ya kituo hicho kupata huduma ya wakala bati nzuri akaja jamaa mmoja ambaye nae alikuwa akishiriki zoezi la kubomoa, nikaanza kumuuliza kinachoendelea pale, nilishangaa sana aliponiambia kituo hicho hakiondolewi badala yake kinabomolewa na kuongezewa uwezo zaidi.

IMG_3365.jpeg
Sikuwa na jambo la kusema nikaishia kushangazwa huku nikijiuliza nani ametoa tena kibali cha kuboresha kituo hicho ambacho kipo kwenye makazi ya watu badala ya kufanya mchakato wa kukiondoa kwenye eneo hilo hatarishi au ripoti ya TAKUKURU ilibaini kituo hicho kipo eneo salama?
 
Back
Top Bottom