Ripoti ya TAWA: Vifo vya Tembo vimepungua Nchini

Ripoti ya TAWA: Vifo vya Tembo vimepungua Nchini

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wananyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda amesema matukio ya vifo vya Tembo yamepungua kwa asilimia kubwa Nchini.

7b95c13f-5e6c-48dd-be99-e2181b025ae1.jpg

Mabula Misungwi Nyanda

Nyanda amesema kuimarika kwa ulinzi kulikochangiwa na kuongezeka kwa vitendea kazi, morali ya watumishi, na kuimarishwa kwa Kikosi cha Muitikio wa Haraka kumekuwa sababu ya hali hiyo.

Ameeleza kuwa vifo vya Tembo vilikuwa 18 msimu wa mwaka 2016/17, lakini katika msimu wa 2020/21 vime[ungua hadi Tembo watatu.

Aidha, amesema ujangili katika Pori la Akiba la Selous umepungua kutoka mizoga ya tembo 7 iliyoonekana mwaka 2016/2017 wakati mwaka 2018/19 hadi 2020/21 hakukuwa na mzoga wa tembo ulioonekana.

Nyanda amekumbushia majukumu ya TAWA kuwa ni kuhifadhi, kusimamia na kuendeleza rasilimali ya wanyamapori nje ya Hifadhi za Taifa na eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
 
Kazi kubwa imefanyika chini ya JPM kulinda rasilimali za nchi. Ila hajatupa takwimu za 2022 maana tunajua wameanza kuuawa tena.
 
Back
Top Bottom