Ripoti ya Tume ya Mwakyembe ni another Professorial Rubbish

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Ningali ninaisaka ripoti kamili ya Dr. Mwakyembe kuhusiana na Law School nipate kuibukua kifungu kwa kifungu. Aliye nayo tafadhali itapendeza aki I share.

Hata hivyo nimefuatilia extracts kadhaa kutoka kwenye ripoti hiyo. Ama kwa hakika ni aibu mtupu yenye arrogance za kishamba.

Izingatiwe haya yamo rasmi kwenye ripoti hiyo:

1. "Sheria ni fani yenye umuhimu wa pekee katika jamii. Siyo kila mtu anaweza kuwa mwanasheria."

Eti kwamba sheria ni fani mahsusi kwa wapakwa mafuta wachache. Kwa hakika upuusi mtupu.

Kwani kia mtu anaweza kuwa mhandisi, mwalimu, daktari, nk? Kwani huo uanasheria unaongeza chakula mezani? Uanasheria? Wasemeje rocket scientists? Bure kabisa.

2. "Kwa vile sheria ni fani nyeti sana minimum qualification kwa ajili ya kujiunga na vyuo vikuu ziwekwe juu zaidi."

Kwamba sheria ni nyeti kwa unyeti upi? Kwamba unyeti huo wa sheria waauona kina Mwakyembe peke yao ambao ni wanasheria?

Upuusi mwingine wa kiwango cha lami. Mbona Kila mtu na fani yake anaiona ni nyeti?

Kwa hakika ni upuusi uliopitiliza mtu na fani yake kujidhania ati kuwa fani yake ndiyo ya maana mno kuliko zingine.

Mashindano ya umuhimu wa aina hii kwa viungo vya binadamu yaliishia na binadamu kunyimwa nafasi ya kujisaidia na ndipo ikafahamika umuhimu na kutegemeana kwa viungo vyote mwilini kwa binadamu.

Kwanini haongelei minimum qualifications ya kada zote kupandishwa?

Inatia kichefuchefu ripoti zisizokuwa na tija kama hizi kugharimiwa na kodi za wananchi. Huu ukiwa ushahidi mwingine wa uwepo wa shehena ya wasomi uchwara wasio na tija waliojaa kwenye nchi zetu za kiafrika. Kwa hivi tutaendelea kujidhihirisha kwa uduni wetu Hadi Qatar 2022.

Kwani hata ripoti ya ajali ya ndege ya precision air Kagera, ingekuwa bayana kuwanyooshea vidole hivi hawa waliotaka kutuingiza chaka mchana kweupe?

Kwani hata tuna haja ya kuunda tume za uchunguzi kuhusu nini? Ni kwa jaribio la mauaji la Lissu au kuhusu mchakato wa katiba mpya na akina Prof. Mukandara au ya Makinikia ya kina Ossoro na Mruma?

Akiiziita jina sahihi zaidi Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu:

"Ripoti za namna hii zisizokuwa na tija yoyote tokea kwa wasomi wetu ni Professorial Rubbish!"

Ama kwa hakika hii ya Mwakyembe "is just another Mayai."
 
Baada ya yale malalamiko ukafuatia uamuzi wa kuunda tume,lakini baada ya kusikia Dr. Ndumbaro wakati wa kuunda tume tayari akija na majibu yake kuhusu sababu ya wanafunzi wengi kufeli Law School, akidai sababu ni kule walikotoka, hapo tayari nikaliona tatizo la kwanza, huyu alishatoa majibu kwa tume, na tume nayo kweli ikaja na jibu hili.

Pili, uundwaji wa tume yenyewe, jambo kama hilo, lililohusu taasisi ya serikali, kuja kuundiwa tume inayoongozwa na mwanasiasa aliyekuwa watumishi wa serikali tayari kukaliondolea uwazi, hawa jamaa kulindana ni kawaida yao, bahati mbaya zaidi, walipojiondoa wale majaji waliotaka nao kuunda tume yao, ndio kila kitu kikaharibika kabisa.

So, hayo majibu yaliyokuja kuifanya ile ripoti ionekane another professorial rubbish kwangu niliyategemea mapema, kwa kifupi majibu ya ile tume yamewaongezea viburi wale walimu wa kile chuo, imewalinda, hata kama ripoti ilisema walimu wanaolalamikiwa sana wahamishiwe taasisi nyingine za serikali.
 
Baada ya yale malalamiko ukafuatia uamuzi wa kuunda tume,lakini baada ya kusikia Dr. Ndumbaro wakati wa kuunda tume tayari akija na majibu yake kuhusu sababu ya wanafunzi wengi kufeli Law School...

Nafasi adhimu za kushauri ipasavyo kwa msukumo wowote zinapopotea kama hivi ni jambo la kusiitisha sana.

Kwa nini ni vigumu kuona utaratibu wa NECTA kuwa watunga mitihani kuwa siyo wasihihisha mitihani? Kwanini watahiniwa, watunga mitihani na wasihihisha mitihani wasiwe ni pande tatu zisisojuana kuwa ndiyo muafaka zaidi kwenye kuondoa malalamiko kama haya?

Kwanini ni vigumu kuona wizara yenye dhamana ya kushughulika na elimu iisiwe wizara ya elimu peke yake? Vipi Kila wizara kuwa na vyuo vyake vyenye kulalamikiwa kama hivi?

Au hadi tupate washauri kutokea wapi Yarabi sisi?
 
Ningali ninaisaka ripoti kamili ya Dr. Mwakyembe kuhusiana na Law School nipate kuibukua kifungu kwa kifungu. Aliye nayo tafadhali itapendeza aki I share...
Wanaoirudisha nyuma nchi yetu ni hawa wanaojiita wasomi, angalia yale yaliyokuwa yanafanyika enzi hizo wakati wasomi wachache,kuanzia ujenzi wa miundombinu na majengo,Elimu yetu ilikuwa ya kumuandaa mtu kujitegemea Sayansi kimu, Sayansi Kilimo,mtu akimaliza darasa la saba alikuwa na uwezo fulani tofauti na graduate wa miaka hii ambaye anatoka Chuo empty.

angalia taasisi za umma kuna wasomi kibao Kwa vyeti ila ubunifu sifuri......... ujinga mwingine ni wasomi kutumika na wanasiasa,hawasemi ukweli hata panapohitajika kusema hivyo Kwa maslahi ya wanasiasa au kukosa teuzi.

Msomi wa Tanganyika yupo tayari kumislead jambo Kwa manufaa ya wanasiasa,Refer wale waliochunguza uchafuzi wa mto Mara,Maprofesa wale walisema eti viumbe wanakufa mto Mara kwasababu ya kinyesi Cha ng'ombe kuzidi?

Wakati ukweli ni Chemicals kutoka Mgodi wa North Mara wamwchannel maji machafu mtoni ila kwasababu ya rushwa na kukosa weledi wanasema kuna tonnes kadhaa za kinyesi Cha wanyama.........Tunahitaji ukombozi wa fikra Kwa wasomi wetu
 
Nafasi adhimu za kushauri ipasavyo kwa msukumo wowote zinapopotea kama hivi ni jambo la kusiitisha sana.

Kwa nini ni vigumu kuona utaratibu wa NECTA kuwa watunga mitihani kuwa siyo wasihihisha mitihani? Kwanini watahiniwa, watunga mitihani na wasihihisha mitihani wasiwe ni pande tatu zisisojuana kuwa ndiyo muafaka zaidi kwenye kuondoa malalamiko kama haya?

Kwanini ni vigumu kuona wizara yenye dhamana ya kushughulika na elimu iisiwe wizara ya elimu peke yake? Vipi Kila wizara kuwa na vyuo vyake vyenye kulalamikiwa kama hivi?

Au hadi tupate washauri kutokea wapi Yarabi sisi?
Hapo Law School mitihani wanatunga wao, wanasahihisha wao, karatasi za kujibia hawarudishi, na rufaa ukikata wanasikiliza wao.

Naanza kuona patakuwepo na urafiki kati ya walimu wa law school na watendaji serikalini, hivyo ripoti kama ya Mwakyembe ni kupoteza tu muda na fedha hakuna jipya, kwenye muunganiko wa sampuli hii, nani awatetee wanafunzi?
 
Ningali ninaisaka ripoti kamili ya Dr. Mwakyembe kuhusiana na Law School nipate kuibukua kifungu kwa kifungu. Aliye nayo tafadhali itapendeza aki I share.
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Sahih Sana ,Sheria siyo kila kitu kuna wahandisi na watechnology wako vzr Zaid kuliko hao wanasheria
 
Huu unyeti wa tasnia ya sheria unakuzwa tu hamna kitu ... yaani hawa mangwini wanajipaisha saba ila hamna kitu

Kwamba unyeti huo unakuzwa na wanasheria uchwara wa aina ya Mwakyembe na washirika wake. Bure kabisa.
 
Hapo Law School mitihani wanatunga wao, wanasahihisha wao, karatasi za kujibia hawarudishi, na rufaa ukikata wanasikiliza wao.

Naanza kuona patakuwepo na urafiki kati ya walimu wa law school na watendaji serikalini, hivyo ripoti kama ya Mwakyembe ni kupoteza tu muda na fedha hakuna jipya, kwenye muunganiko wa sampuli hii, nani awatetee wanafunzi?

Kigugumizi kwenye kutoona mapungufu ya wazi kama haya ni mwendelezo ule ule unaotufukisha kwenye longo longo zote tunazoletewa ikiwamo kwenye yaliyo nyeti ya katiba mpya.
 
Tafuta kwanza ripoti nzima uichambue ndiyo uje na arguments zilizoshiba.Vinginevyo na wewe utakuwa rub.....!
 
Ningali ninaisaka ripoti kamili ya Dr. Mwakyembe kuhusiana na Law School nipate kuibukua kifungu kwa kifungu. Aliye nayo tafadhali itapendeza aki I share.

Hata hivyo nimefuatilia extracts kadhaa kutoka kwenye ripoti hiyo. Ama kwa hakika ni aibu mtupu yenye arrogance za kishamba.

Izingatiwe haya yamo rasmi kwenye ripoti hiyo:

1. "Sheria ni fani yenye umuhimu wa pekee katika jamii. Siyo kila mtu anaweza kuwa mwanasheria."

Eti kwamba sheria ni fani mahsusi kwa wapakwa mafuta wachache. Kwa hakika upuusi mtupu.

Kwani kia mtu anaweza kuwa mhandisi, mwalimu, daktari, nk? Kwani huo uanasheria unaongeza chakula mezani? Uanasheria? Wasemeje rocket scientists? Bure kabisa.

2. "Kwa vile sheria ni fani nyeti sana minimum qualification kwa ajili ya kujiunga na vyuo vikuu ziwekwe juu zaidi."

Kwamba sheria ni nyeti kwa unyeti upi? Kwamba unyeti huo wa sheria waauona kina Mwakyembe peke yao ambao ni wanasheria?

Upuusi mwingine wa kiwango cha lami. Mbona Kila mtu na fani yake anaiona ni nyeti?

Kwa hakika ni upuusi uliopitiliza mtu na fani yake kujidhania ati kuwa fani yake ndiyo ya maana mno kuliko zingine.

Mashindano ya umuhimu wa aina hii kwa viungo vya binadamu yaliishia na binadamu kunyimwa nafasi ya kujisaidia na ndipo ikafahamika umuhimu na kutegemeana kwa viungo vyote mwilini kwa binadamu.

Kwanini haongelei minimum qualifications ya kada zote kupandishwa?

Inatia kichefuchefu ripoti zisizokuwa na tija kama hizi kugharimiwa na kodi za wananchi. Huu ukiwa ushahidi mwingine wa uwepo wa shehena ya wasomi uchwara wasio na tija waliojaa kwenye nchi zetu za kiafrika. Kwa hivi tutaendelea kujidhihirisha kwa uduni wetu Hadi Qatar 2022.

Kwani hata ripoti ya ajali ya ndege ya precision air Kagera, ingekuwa bayana kuwanyooshea vidole hivi hawa waliotaka kutuingiza chaka mchana kweupe?

Kwani hata tuna haja ya kuunda tume za uchunguzi kuhusu nini? Ni kwa jaribio la mauaji la Lissu au kuhusu mchakato wa katiba mpya na akina Prof. Mukandara au ya Makinikia ya kina Ossoro na Mruma?

Akiiziita jina sahihi zaidi Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu:

"Ripoti za namna hii zisizokuwa na tija yoyote tokea kwa wasomi wetu ni Professorial Rubbish!"

Ama kwa hakika hii ya Mwakyembe "is just another Mayai."
omba sana kama ita sirvive maana nilipost kitu kama hiki report ya Mukandala wakafuta
 
Nilichoandika ndiyo ulio ukweli. Palipo ukiukwaji haki wengine kukaa kimya tulishindwa.
 
Tafuta kwanza ripoti nzima uichambue ndiyo uje na arguments zilizoshiba.Vinginevyo na wewe utakuwa rub.....!

Nimeweka scope na disclaimer ukishindwa kuelewa umuhimu wake u rubbish mbona utakuhusu?

Zingatia mada zingine si kwa kila Toma.
 
Back
Top Bottom