Kwanini tunapenda sana kuwashinikiza watu waandike au wajibu kile tunachikitaka sisi?? Tukuue ndiyo, usile leo sawa, sema ccm chama cha mafisadi sawa, nchi hii imeharibika sawa, chadema inataka kurithi a failed state sawa, Huo si ni umbumbu kupita maelezo kwa maana nyingine ni upumbavu kukubaliana kila jambo hata kama halina msingi.
Kama unataka kupinga matokeo ya kitafiti ya mwenzio nawe fanya utafiti wako kwa misingi inayofanana ili upate jibu linalopingana. Utafiti wa kisayansi siyo utafiti ya kisiasa ndugu. Sayansi ina base kenye facts siyo political truth na ndiyo maana methodology inayotumika inawekwa wazi ili kwa wale wanoupinga utafiti huo wapinge kisayansi ili kutoa mapungufu au uongo uliofanywa na taasisi au mtu fulani na hiyo inakubalika.
Kiutaratibu report ya waangalizi wa uchaguzi kama ambayo mimi nimeshawahifanya inapelekwa kwa wadau wote Tume ya Uchaguzi ya nchi husika, mkuu wa nchi, vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi, taasisi husika na vyombo vya habari maana siyo siri.
Tuache majungu ya kisiasa kama ni maswala ya kichama peleka kwenye blog ya chama na siyo JF kama mmiliki wa JF anashadadia hayo aandike chama flani JF iwe ya jamii ya chama hicho tu na siyo wote.