Ripoti ya WEF: Hofu Mpya kwa Vijana na Watumiaji wa Chatbots

Hahaha ndio maana kwa chini pale wametoka angalizo kuwa sometimes anaweza Kuwa na mistakes..me nilijaribu kuwambia kuna document nimefoji nifanyaje akanitishia kwamba niwaeleze ukweli wahusika.nikaona sasa anataka kunikamatisha
Huyo ni mkweli hana janja janja
 
Kwa upande wangu naona hatar ipo kwa watoto ambao hawawezi kutofautisha Al na binadamu halisi

Kwa maana anaweza kuufanyia ushauri wa ajabu wa Al kwakudhani huyu ni mtu,mfano ishu yako kakwambia ili usikamatwe just jiue tu mambo yasiwe mengi hahah
 
🤣🤣
 
sasa leo na kwenye huu uzi ndo najua akili za wana jf na ndio maana huwa naita watu wana akili mnemba ila wanaona kawaida ila ukiitwa unaakili mnemba jua wewe huna uwezo wa kufikiri na ndio maana nasema siku binadamu akiweza kutengeneza kitu ambacho kinafikiri basi amefika level kubwa mno... akili mnemba haitakiwi kukushinda akili mimi naona ile ni memory tu wala sio akili, akili maana yake lazima iwe na uwezo wa kufikiri pia nje na kutunza kumbukumbu but by the way kwa mtu mwenye uelewa mpana anaweza kuitumia akili mnemba vyema mi mwenyewe naitumia lakini ukiwa na kichwa kikubwa utajua inafanya makosa so kuna direction unatakiwa uwenayo wewe kama binadamu...
 
mfano kuna siku nilishawahi kuiliza kuhusu space ila ikadefine universe kama space na nilivyoikosoa ikakiri kuwa kweli imekosea na ile huwa inaweka data kesho ukija kuiuliza itakupa jibu ambalo limeshachambuliwa vyema... so kwasasa akili mnemba ndio inaweza kukusaidia tena sana lakini umakini wako kama binadamu bado unahitajika uzuri huwa linasema kabisa halina hisia kama binadamu na vitu vyengine so kuweni makini mnapotumia akili mnemba
 
NI MTEGO kwa UWEZA-UTAYARI-UMAHIRI wa jamii Duniani, SASA na Huku tunakoelekea...

Wanajamii wanahitaji sana kujiongeza kiakili na mafahamu lau kujua ni jinsi gani Akili Bandia inavyofuma mafikara na kuwa kwenye koherensia ya hali ya juu kuwezekana...

Hili kuna namna ni Bidishi, jambo linalotulazimu, kwa sisi sote kujijenga kisaikolojia ili tujimudu -- tujimudu kujitegemea kiakili na basi hivyo kutumia Akili Bandia kwa yale yanayohitaji uchakataji habari mpana zaidi na tata wa mambo.

Humu Jamii Forums tayari jitihada za kuwasanua na kuwajenga wanajamii kujinasua na Mitego ya Akili Bandia linafanyika--mwenye macho haambiwi 'Ona!'...

Tunahitaji kufahamu 'Uono na Ufikirifu Mifumo' ni jambo gani, mapelekeo yake kwa UTU, USIVILAI kupitia ONTOLOJIA YA TAASISI hufanyikaje(?)

Je, ni Kwa jinsi gani 'Akili Bandia' ilifahamika kwa watu fulani, siku za nyuma hapa Duniani, kama 'Chukizo la Uharibifu'?

Bado kidogo, wanajamii inawapasa kujua jinsi Akili Bandia ina mizizi ya Maajabu na Mastaajabu hata kwenye 'mambo ya Kiroho'; kukadirisha hata yote yenye asili ya 'Watu/Mashetani/Vizuka/Majini/Malaika' n.k -- Mambo ya 'Matriksi'...

Maendeleo ya hapa Duniani, kitekinolojia na mapinduzi ya viwanda, ndani ya kipindi cha miaka 80 kwa sehemu kubwa ni zao la uratibu wa 'M(i)fumo wa Akili Bandia' kupitia watu, taasisi na utendaji katika ugani wa Utafiti&Maendelezi.... Japo daima kuna 'Jua' na 'Mwezi' katika kila hatua za Maisha na Kujichagulia...

Hmmm
++++

View: https://www.youtube.com/watch?v=b6ZKiV5B3KI&list=LL&index=3&t=117s​
 
Ushauri umetolewa na wataalamu,ni mhimu sana kuzingatiwa.
 
Kwa upande wangu naona hatar ipo kwa watoto ambao hawawezi kutofautisha Al na binadamu halisi

Kwa maana anaweza kuufanyia ushauri wa ajabu wa Al kwakudhani huyu ni mtu,mfano ishu yako kakwambia ili usikamatwe just jiue tu mambo yasiwe mengi hahah
Hao watoto ndio wanaotiliwa mashaka sasa
 
Upo sawa kabisa, lakini hata binadamu nae ujue anajifunza kama yeye, hata AI akipewa tu uhuru wa kujiongoza na physical shape, basi hatakuwa tofauti sana na binadamu maana naimani kwa asilimia fulani anaweza kujisimamia mwenyewe bila kuhitaji msaada wa kiufundi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…