Ripoti za Tume za Maprofesa wetu hazina tija

Ripoti za Tume za Maprofesa wetu hazina tija

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Amesikika Profesa Manyele na ripoti ya vinyesi vya ng'ombe.

Kama vile haitoshi inasemekana Profesa Mukandara naye yuko njiani kudai katiba mpya isubiri tu hadi baada ya 2025.

Hawa si wa mwanzo.

Wapo waliojinasibu kuokotwa walikotoka. Wapo waliotuaminisha kusubiria Noah zetu tokea kwenye makinikia.

Mifano iko mingi isiyokuwa na mwisho.

Ni wazi kuwa watu hawa kwa tamaa zao hawana nia njema. Kwa tamaa zao wako tayari kusema lolote.

Wito kwa Mama Samia ni kutowasikiliza wachumia tumbo hawa.

Nchi ni ya watanzania. Hatima ya watanzania iamuliwe na watanzania wenyewe. Si kuamriwa na vikundi vya watu kwa majina yoyote tafwadhali.

Kwanini kuruhusu katiba mpya itufarakanishe?

Katiba mpya si ndiyo inayokidhi mahitaji ya wote wakiwamo hata ambao hii iliyopo wao hawana taabu nayo?

Au kwani kuna maslahi gani binafsi kwa nani kwamba watayakosa ikiwa mchakato wa mabadiliko utaanza sasa?
 
Back
Top Bottom