Ripu nzuri ni ipi?

Ripu nzuri ni ipi?

okai

New Member
Joined
Jun 7, 2018
Posts
3
Reaction score
1
Wataalamu nisaidieni katika hili maana mafundi wengine wanasema ripu ya mkono bao ni nzuri kuliko ya kutumia galamara nawasilisha
 
Sababu za watu wengi kuacha kupiga pasi ukuta na hatimae kupiga kibao tu.

1. Ukuta ukiupiga pasi ukiwa hauja kauka unatengeneza mabonde nahata ukikauka ukitaka kupiga pasi utatumia nguvu nyingi kupiga pasi nayo pia itatengeneza mabonde kwenye ukuta maana utakua unakandamiza pasi
2. Hii inasemekana fundi rangi akija kufanya skimming haishikani vizuri na ukuta sababu ukuta unateleza kama kioo hatimae huko mbeleni rangi pamoja na skimming hubanduka kwenye huo ukuta

Plasta nzuri ni ile inayo wekwa timanzi alafu pia uwe na lati nzuri ya aluminum epuka fundi anaefanya kazi kubwa kwa siku ili amalize haraka achukue hela aondoke atalipua hiyo kazi

Ili ukuta usiwe na mabonde mabonde baada ya kupiga kibao ukamaliza chukua lati jikague kuangalia makosa kabla ukuta hauja kauka kama kuna sehemu haiko sawa irekebishe kwa kuikwangua na lati alafu nyunyiza maji kidogo piga kibao hiyo kazi itakuwa safi
 
Ni point zinazowekwa kwenye ukuta kwa kutumia kipande cha tiles vinakuwa kama chuchu vinakua na kipimo cha kobilo au pimamaji hio timanzi ndio unakuwa muongozo wa plasta isizidi hapo wala isipungue hapo ndizo kazi zangu hizo mkuu kama vipi unaweza nipa hio kazi nikakufanyia hiyo kazi
 
Sababu za watu wengi kuacha kupiga pasi ukuta na hatimae kupiga kibao tu

Mkuu, kwa uzoefu wako,
Gharama ya ufundi kupiga plasta nje pekee nyumba ya mita 11 kwa 13 inaweza kuwa Sh. ngapi?
 
Kazi nikifika sait nikaiona kwa macho naweza nikatoa hesabu sahihi kuliko hii kwa kufikilia kichwani naweza nikataja kiasi kikubwa cha pesa kumbe kazi yenyewe ni ndogo tu
 
Ni point zinazowekwa kwenye ukuta kwa kutumia kipande cha tiles vinakuwa kama chuchu vinakua na kipimo cha kobilo au pimamaji hio timanzi ndio unakuwa muongozo wa plasta isizidi hapo wala isipungue hapo ndizo kazi zangu hizo mkuu kama vipi unaweza nipa hio kazi nikakufanyia hiyo kazi
Asante boss kwa ABC ulizonipa mm niko mwanza kuhusu kukupa kazi bado navuta nguvu ya material nikishakamilia nitakutafuta
 
Mkuu nyamwage unaposema timanzi unamaanisha nn
Timanzi maana yake una nyoosha ukuta kuwa level moja kuanzia juu mpaka chini kuna sehem ambazo fundi tofali anaweza kuwa ameibia kipimo au tofali azipo level wakati wa kujenga
 
Back
Top Bottom