Elections 2010 Risasi zarindima jijini Arusha

Elections 2010 Risasi zarindima jijini Arusha

Preta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
24,320
Reaction score
18,852
Takribani dakika 30 zilizopita maeneo ya soko kuu Arusha polisi wamekuwa wakirusha risasi hewani na kukamata watu hovyo....ni kitendo cha kushtua sana kwa watu tuliokuwa tukipita na shughuli zetu....je hii inahusiana na mambo ya kampeni?....mwenye habari zaidi atujuze tafadhali
 
yaani ni wamejiamulia tu kuzimimina bila sababu maalum au wana sabab yazo?...halafu sokoni jamani na vurugu zote za masoko ndio wakaona mahali pa kuyafanyia hayo, najiuliza mara mbili mbili kama nitakuja kupiga kura haki ya nani vile.
 
kulikuwa na ubishani wa vyama vya Chadema na CCM. Kuna bendera ya CCM imewekwa mahali na Chadema wakataka kupandisha ya kwao mahali pale pale na ndipo ugomvi ukaanzia hapo. Polisi walipigiwa simu na baada ya kufika walifyatua risasi hewani kuwatawanya watu. Hali ni shwali kwa sasa.
 
Sijui kuna nini lakini sidhani kama kuna uhusiano wowote na uchaguzi. Nionavyo soko kuu limeingiliwa na wafanya biashara wadogo wadogo ambao wanafunga barabara kwa kutandaza bidhaa zao kila mahali na hawana mpangilio. Labda wanawaondoa kwa nguvu. Hay ni maoni yangu tu sijafika eneo hilo leo.

Soko kuu siyo mahali pa kampeni kwa hiyo suala la uchaguzi sidhani hata kidogo.
 
Shimbo upo??
Halafu mnataka tuirudishe tena ccm? mbona wao wameweka yao.
 
yaani ni wamejiamulia tu kuzimimina bila sababu maalum au wana sabab yazo?...halafu sokoni jamani na vurugu zote za masoko ndio wakaona mahali pa kuyafanyia hayo, najiuliza mara mbili mbili kama nitakuja kupiga kura haki ya nani vile.

my dear ilinibidi nitafute pa kuingia lakini habari nilizozisikia ni kwamba kuna vurugu za kampeni.....so sijajua bado sababu ya polisi kufanya hivyo ni nini katika sehemu yenye mkusanyiko kama ule.....
 
ndio maana nawaomba WATANZANIA , twendemi tukapige kura, tuwang'oe mabazazi hawa, tukawazike makaburini, kisha Maralia Sugu atakua anaenda kupalilia makaburi yao, Twende Tanzania, hadhi yako inashuka mbele ya MATAIFA, usilale mwananchi, Timiza wajibu wako sasa. kataa ccm, kataa kawaida, chagua Mabadiliko.
 
ila mbona awa jamaa wababe hivi?sheria akivunja mwingine kesi ila wao haaaa kawaida!!tutafika kweli ivi?
hope watu wako salama uko
 
Takribani dakika 30 zilizopita maeneo ya soko kuu Arusha polisi wamekuwa wakirusha risasi hewani na kukamata watu hovyo....ni kitendo cha kushtua sana kwa watu tuliokuwa tukipita na shughuli zetu....je hii inahusiana na mambo ya kampeni?....mwenye habari zaidi atujuze tafadhali
Poleni sana Preta!

Kama mmepona, na kama hakuna aliyejeruhiwa tunashukuru Mungu!
Lakini kwa namna yoyote hiyo inahusiana na ubishani wa uchaguzi!
Soko kuu la Arusha pana ushindani mkubwa sana na kejeli za hapa na pale, hasa ukizingatia kuwa kuna mgombea mmoja mwanamke anapitisha t-shirt za kijani kwa wafanyabiashara wale mchana kutwa!
Kwa jinsi tunavyosogelea d-day inabidi kujihadhari sana tunapopita kwenye makundi ya watu!

Wanafanya mazoezi ya kutuliza ghasia kwa silaha za moto
 
jamani haya mambo yataisha lini, au ndiyo mwenye nguvu mpishe??
 
my dear ilinibidi nitafute pa kuingia lakini habari nilizozisikia ni kwamba kuna vurugu za kampeni.....so sijajua bado sababu ya polisi kufanya hivyo ni nini katika sehemu yenye mkusanyiko kama ule.....
kwa jinsi ninavyokupenda nakuombea usidhurike wala kupata doa lolote
poleni wakazi wa arusha naamini hakuna casualities maana hawa polisi kutumia risasi za moto wana lao jambo
 
Wakuu soko kuu sehemu watu wanapopenda kunywa kahawa zipo kambi mbili pale moja ya CHADEMA na nyingine ya CCM inaongozwa na Juma almaharufu Mnene.Watu wa CHADEMA ni wauza mitumba,karanga,wasukuma mikokoteni na bodaboda.Watu wa CCM ni waswahili wa mjini mitaa ya Bondeni na Pangani wanapenda kujiita watoto wa mjini.

Watu wa CHADEMA si wakaazi wa mjini kati wengi wanaondoka muda wa saa moja usiku,wengi wanishi maeneo ya Arumeru Magharibi si wapiga kura wa Arusha mjini lakini pia wapo wakaazi wa Mianzini na kidogo Ungalimited.

Eneo la Soko Kuu linataka kufanana na Saigon Dar ukipita pale unaweza kujikuta unaWEchelewa nyumbani.CCM wamefanikiwa kuidhibiti CHADEMA baada ya mgombea wao kubainika hana shule na alinunuliwa mwaka 2005.CHADEMA nao hawakubalia wanasema watamchagua Lema hata kama hajasoma.

Kata ya Kati inawapiga kura wasiozidi 3000 tu lakini kelele zake utadhani wao wana hatimiliki ya kumchagua ubunge.Wakati hayo yakiendelea mgombea ubunge wa TLP amejichimbia kwenye kata za Sombetini yenye wapiga kura 30,000 kata ya Sokoni1 yenye wapiga kura 25,000 na Ungalimited yenye wapiga kura zaidi 18,000.
 
Wahuni hao, CCM wanapanga kuanzisha vurugu ili waanze varangati kuhalalisha matamushi ya uasi wao.
 
kulikuwa na ubishani wa vyama vya Chadema na CCM. Kuna bendera ya CCM imewekwa mahali na Chadema wakataka kupandisha ya kwao mahali pale pale na ndipo ugomvi ukaanzia hapo. Polisi walipigiwa simu na baada ya kufika walifyatua risasi hewani kuwatawanya watu. Hali ni shwali kwa sasa.

asanteni preta na wakuu wote mlioko a-town; tulishaanza kufikiria ukimbizi ndani ya nchi yetu.
 
kwa jinsi ninavyokupenda nakuombea usidhurike wala kupata doa lolote
poleni wakazi wa arusha naamini hakuna casualities maana hawa polisi kutumia risasi za moto wana lao jambo

karibu ungenikosa coz gari niliyokuwa nimepanda ilikuwa inapishana na hiyo deffender mara ghafla diffender ikasimama na kuanza hayo mambo....so kitendo kilikuwa kinafanyika mbele ya macho yangu na kama siyo zilikuwa zinaelekezwa juu ndio basi tena....kama sikuwa nimejaliwa shoku abzoba za roho leo ndio ilikuwa mwisho wangu.......nahakikisha Oct 31 sifanyi kosa
 
Yes
 
Back
Top Bottom