Sijui kuna nini lakini sidhani kama kuna uhusiano wowote na uchaguzi. Nionavyo soko kuu limeingiliwa na wafanya biashara wadogo wadogo ambao wanafunga barabara kwa kutandaza bidhaa zao kila mahali na hawana mpangilio. Labda wanawaondoa kwa nguvu. Hay ni maoni yangu tu sijafika eneo hilo leo.
yaani ni wamejiamulia tu kuzimimina bila sababu maalum au wana sabab yazo?...halafu sokoni jamani na vurugu zote za masoko ndio wakaona mahali pa kuyafanyia hayo, najiuliza mara mbili mbili kama nitakuja kupiga kura haki ya nani vile.
Poleni sana Preta!Takribani dakika 30 zilizopita maeneo ya soko kuu Arusha polisi wamekuwa wakirusha risasi hewani na kukamata watu hovyo....ni kitendo cha kushtua sana kwa watu tuliokuwa tukipita na shughuli zetu....je hii inahusiana na mambo ya kampeni?....mwenye habari zaidi atujuze tafadhali
kwa jinsi ninavyokupenda nakuombea usidhurike wala kupata doa lolotemy dear ilinibidi nitafute pa kuingia lakini habari nilizozisikia ni kwamba kuna vurugu za kampeni.....so sijajua bado sababu ya polisi kufanya hivyo ni nini katika sehemu yenye mkusanyiko kama ule.....
kulikuwa na ubishani wa vyama vya Chadema na CCM. Kuna bendera ya CCM imewekwa mahali na Chadema wakataka kupandisha ya kwao mahali pale pale na ndipo ugomvi ukaanzia hapo. Polisi walipigiwa simu na baada ya kufika walifyatua risasi hewani kuwatawanya watu. Hali ni shwali kwa sasa.
Yeye kazi toa wapi hizo nguvu kama siyo wewe uliempa dawa yao Tarehe 31-10-2010 ..changua CHADEMAjamani haya mambo yataisha lini, au ndiyo mwenye nguvu mpishe??
kwa jinsi ninavyokupenda nakuombea usidhurike wala kupata doa lolote
poleni wakazi wa arusha naamini hakuna casualities maana hawa polisi kutumia risasi za moto wana lao jambo
karibu ungenikosa coz gari niliyokuwa nimepanda ilikuwa inapishana na hiyo deffender mara ghafla diffender ikasimama na kuanza hayo mambo....so kitendo kilikuwa kinafanyika mbele ya macho yangu na kama siyo zilikuwa zinaelekezwa juu ndio basi tena....kama sikuwa nimejaliwa shoku abzoba za roho leo ndio ilikuwa mwisho wangu.......nahakikisha Oct 31 sifanyi kosa