A
Anonymous
Guest
Kuna kero ambayo inatuumiza wananchi wa kawaida wilaya ya ILEMELA MKOA WA MWANZA kwenye ofisi ya usajili hasa wa vyeti vya kuzaliwa, tunachukua form tunajaza details zote ziko sawa msajili akifika yeye wakati wa kuziingiza zile taatifa kwa ajili ya kutoa cheti anakosea sana vyeti vinakuwa na typing errors nyingi.
Ukirudisha cheti unaambiwa lipia gharama za marekebisho ambayo ni elfu 13,000 na bado anakwambia na pesa yangu kama ni elfu 10 au elfu 5 wakati huo huo kosa ni lake, kwanini anatufanyia hivyo wananchi?
Mbaya zaidi hataki zile details ulizojaza mwanzo zitafutwe anasema documents ziko nyingi hawezi hizo kazi ujaze upya forms za kuomba cheti cha kuzaliwa.
Inakatisha tamaa na ni unyanyasaji wa wazi cheti cha shilingi elfu nane (8,000) unajikuta unatumia zaidi ya elfu 50,000 ni kero ya wengi tunaomba msaada wa kupaza sauti kwa mamlaka husika tafadhali.
Wako katika ujenzi wa taifa
Wananchi wa ILEMELA
MWANZA