RITA kuthibitisha wenyewe nakala za vyeti vya kuzaliwa ina maana cheti kikithibitishwa mahakamani/ kwa wakili hakitakubalika?

RITA kuthibitisha wenyewe nakala za vyeti vya kuzaliwa ina maana cheti kikithibitishwa mahakamani/ kwa wakili hakitakubalika?

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Naomba kuuliza kwa wenye uhakika na hili: Je nakala ya cheti cha kuzaliwa kikithibitishwa mahakamani au kwa wakili kitakubalika?

Uthibitishaji wa vyeti vya kuzaliwa unatakiwa sana hasa kwenye kuomba ajira, na kwenye uombaji wa mikopo ya elimu ya juu.

Nauliza hivi kwa sababu mchakato wa kuthibitisha cheti huko RITA kwa njia ya mtandao wakati mwingine huchukua muda mrefu sana na kusababisha mtu kuwa kwenye wasi wasi wa kukosa kuomba kazi ndani ya wakati unaokubalika. Lakini kwa njia ya mahakama au wakili ni mchakato rahisi na wa haraka ndani ya siku moja.

Kama mahakama zinaruhusiwa kisheria kuthibitisha nakala za vyeti, hali kadhalika mawakili wanaruhusiwa kuthibitisha nakala hizo, kuna sababu gani ya watu kulazimika kuthibitisha vyeti rita online wakati njia hiyo ina usumbufu mkubwa, hasa kama unahitaji huduma hiyo kwa haraka.
 
Mahakama hawana orodha ya entry namba za vyeti vyote ndio maana lazima kithibitishwe na aliye kitoa kwa sababu cheti cha kuzaliwa ni sensitive sana
 
Mfano wa mtu aliyejeruhiwa na utaratibu huu wa RITA kuthibitisha nakala za vyeti vya kuzaliwa ni huyu hapa:

Mwanangu ameliza Form Six mwaka huu na anatakiwa kujiunga na chuo, ili apate mkopo anatakiwa aombe akiambatanisha cheti cha kuzaliwa.

Alikuwa na cheti cha kuzaliwa cha zamani ambacho alikituma RITA kwa ajili ya uhakiki lakini kilikataliwa kwa kigezo kuwa ni cha zamani hivyo aombe kipya, alifanikiwa kupata kingine kipya na kukituma kwa ajili ya uhakiki toka Alhamisi tarehe 26/08/21 lakini mpaka leo hajapata majibu ya hicho cheti.

Wasiwasi wangu ni kuwa anaweza kukosa mkopo kwa kushindwa kupata majibu kutoka RITA kwa wakati, kumbuka leo 31/08/21 ndio siku ya mwisho kuomba mkopo kwenye bodi ya mikopo. Nimejaribi kuangalia mwasiliano yao ya simu kwenye website yao hakuna.

Naomba msaada kwa anayefahamu hili jambo vizuri na hatua za kuchukua ili apate hayo majibu haraka.
 
Mahakama hawana orodha ya entry namba za vyeti vyote ndio maana lazima kithibitishwe na aliye kitoa kwa sababu cheti cha kuzaliwa ni sensitive sana
Lakini kumbuka kuwa mahakama na mawakili kisheria wana dhamana ya kuthibitisha nakala hizo maana wanahusika na viapo pia. Haijawahi kutungwa sheria iliyowaondolea jukumu hilo.

Kwa hiyo ni kosa kisheria kukataa nakala ya cheti iliyothibitishwa mahakamani. Kama mtu akikosa ajira kwa mfano kwa sababu hiyo ana haki ya kudai mabilioni ya fidia kwa madhara aliyosababishiwa.
 
Mahakama hawana orodha ya entry namba za vyeti vyote ndio maana lazima kithibitishwe na aliye kitoa kwa sababu cheti cha kuzaliwa ni sensitive sana
Ukisema hivyo haupaswi kuishia kwenye vyeti vya kuzaliwa tu! Kuna nakala za vitambulisho kama NIDA nk navyo ni sensitive sana. Kuna nakala za vyeti vya kitaaluma pia ni nyeti sana. Lakini bado muhuri wa mahakama na wa mawakili bado unakubalika kuthibitisha nakala hizo japo pia hawana orodha ya entry number ya vyote hivyo.

Ili mambo yaende ni lazima kuviamini vyombo na watu wenye dhamana hiyo. Huwezi ukakataa muhuri wa mahakama kuthibitisha cheti cha kuzaliwa halafu ukaukubali kwenye vyeti vya kitaaluma na vitambulisho halafu ukajifanya kuwa umeepusha udanganyifu.

Sababu pekee ninayoiona mimi ni kulazimisha mapato kwa RITA inayotokana na hiyo ada ya 3,000/=, bila kujali usumbufu unaosababishwa!
 
RITA njoni hapa mtoe maelezo: Je hamkubaliani na uthibitisho wa nakala ya cheti cha kuzaliwa uliofanywa na mahakama au na wakili? Mjue uthibitisho huo si kwa ajili ya bodi ya mikopo tu, bali pia ni hitaji la vyuo, shule na waajiri.

Je ni kosa kwa mahakama kuthibitisha nakala ya cheti cha kuzaliwa? au nyie RITA mnathibitisha tu kwa ajili ya bodi ya mikopo, na mahakama/mawakili wanaruhusiwa kuthibitisha nakala hizo kwa matumizi mengine?
 
Kama ikafika mahala tukaona cheti cha kuzaliwa ni lazima kithibitishwe na RITA tu, basi ofisi zote za RITA ngazi ya wilaya ziruhusiwe kuthibitisha vyeti hivyo, kuliko usumbufu uliopo kwa sasa!! Kufungua tu akaunti ni mbinde, kupata control number ni mbinde! Katika dunia ya leo, huo mwendo wa kinyonga hautatuacha mahali salama!1
 
Wanataka tu hela hao hawana lolote.

Mbona vyeti vya NECTA vina SERIAL NUMBERS na vinapigwa muhuri mahakamani vizuri tuuu.

Hela za wajinga zinapigwa na RITA.
 
Back
Top Bottom