SI KWELI RITA na NIDA wanarekebisha taarifa kwenye NIDA na cheti cha kuzaliwa kwa kutuma taarifa kwenye Whats App

SI KWELI RITA na NIDA wanarekebisha taarifa kwenye NIDA na cheti cha kuzaliwa kwa kutuma taarifa kwenye Whats App

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Nisaidie kupata hii habari kama ni kweli

SI KWELI BARUA12.jpg

 
Tunachokijua
NIDA hii ni mamlaka ya kitaifa nchini Tanzania inayohusika na kutoa Kitambulisho cha Taifa kwa raia wa Tanzania pamoja na wageni wanaoishi nchini kisheria.

RITA (Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini) inahusika na huduma mbalimbali za usajili, ufilisi, na udhamini

Kumekuwa na barua inayodaiwa kutolewa na kitengo cha Mawasiliano na hifadhi hati, utambuzi na matukio muhimu maishani chenye makao Makuu Dodoma, ambapo inaonekana Barua hiyo ilitolewa tarehe 22 Septemba 2024, barua hiyo inaelekeza wananchi wakafanye uhakiki wa Taarifa zao za kwenye kitambulisho cha NIDA iwapo ziko sahihi na iwapo haziko sahihi basi wanatakiwa kufanya marekebisho kwa kutuma taarifa kwenye namba tajwa hapo kwenye barua ikiwa kuna gharama za kufanya marekebisho hayo.

Aidha barua inabainisha kuwa NIDA pamoja na RITA wameshirikiana kutoa huduma za marekebisho ya taarifa zilizokosewa kwenye Cheti ch kuzaliwa na NIDA.

Je, ukweli ni Upi?

Kupitia utafutaji wa kimtandao kwa kutumia Google Reverse Image JamiiCheck imebaini kuwa Barua hiyo Si ya kweli kwani haijawahi kutolewa na NIDA, wala RITA aidha Tumebini kuwa hakuna Kitengo kinachoitwa "Mawasiliano na hifadhi hati, utambuzi na matukio muhimu maishani chenye makao Makuu Dodoma" Bali baada ya RITA na NIDA kuunganishwa Desemba 15 2023, na kuunda Taasisi moja inayohusika na utambuzi wa matukio muhimu maishani kuna kitengo kijulikanocho kama Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati (CDU)

Pia, barua hiyo ina makosa kadhaa ya kiuandishi: 1. Neno marekebisho kuandikwa kimakosa kama AREKEBISHO, 2. Hakuna jina la aliyesaini Barua hiyo wala cheo chake 3. Mpangilio mbaya wa kiundishi ikiwemo na ukolezaji wa maneno uliozidi kunathibitisha kuwa barua hiyo si halali kwani hakuna umakini wowote katika kuandikwa kwake

Vilevile Maelekezo ya urekebishaji wa taarifa kama ambavyo Barua hiyo inaelekeza haijafuata utaratibu wa kufuata wa urekebishaji taarifa uliowekwa na NIDA, kwa mujibu wa NIDA, utaratibu wa kurekebisha taarifa kama ulivyoanishwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA 2023 ni lazima kutuma Maombi kwa utaratibu maalumu kama unavyoonekana hapa
POSTA-MAREKEBISHO-YA-JINA-9.jpg

Aidha, Kwa nyakati tofauti barua yenye ujumbe wa kufanana na huo zimekuwa zikijirudia kutolewa kwa lengo la kupotosha na NIDA pamoja na RITA wamekanusha kutoa barua hiyo lakini baru zote zimekuwa zinawekwa na ya Simu +255 735 051 419 mbapo wananchi huelekezwa kutum Taarifa zao kwenye namba hiyo kw njia ya Mtandao wa Whats App. Tazama hapa, hapa, hapa, hapa na hapa kuona makanusho hayo

1728390301064-png.3118873
Back
Top Bottom