Ninawaheshimu watu wachache katika taifa letu la Tanzania, kati ya ninaowaheshimu ni Ritta paulsen . Kama wewe unafutatilia kipindi cha Bongo Star search, utakubaliana na mimi juu ya maa huyu. Kwamba amekonda, hayo kwangu ni upepo uvumao! Kila mtu anaweza kukonda na kila mtu anaweza kuuugua.
Ritta, ana roho ya utu, she has a human heart! Ningepata bahati ya kukutana naye, ningemwambia neno hilo kwamba She has a human heart. Daima ninaguswa na jinsi anavyojaribu kuwatendea haki wale vijana wanaotafuta vipaji. Anaoneysha utu, upendo na kuwajali vijana wote.
Kila mtu ana uhuru wa kuishi maisha yake binafsi. Nisingependa kujiuliza anala wapi, anakula nini au anafanya nini akitoka kwenye jukwaa la BSS. La msingi ni ana mchango gani takika jamii. Mchango wake tumeuona; yule jamaa mlemavu aliyetaka kujitosa kwenye BSS na kushindwa, alimsaidia kurekodi mziki wake. Amekuwa akitoa misaa mingi na kuonyesha moyo wa mapendo kwa vijana na kusema kweli vijana wanalifahamu vizuri hili.
Tumpongeze kwa kazi, na tuachane na tabia za kuangilia sura na mambo mengi ya nje. Tuangalie roho za watu!