Tuache ushabiki usio na maana kwenye mambo ya msingi. Rivers United sio timu ya kutisha sana kwa sababu miaka ya karibuni ligi ya Nigeria imeshuka sana viwango. Ndio sababu mwaka jana Simba waliweza kuwatoa Plateau kitu ambacho ingekuwa ni hadithi miaka sita iliyopita.
Kikubwa hapa ni kuwakumbusha Yanga kuwa wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kwenye maandalizi ya uwanjani na waache kuyapa nafasi kubwa mambo ya nje ya uwanja sijui mara jezi, mara Manara, n.k. Angalizo kwa Yanga mechi ni mbili tu moja nyumbani na nyingine ugenini basi na muda uliobaki ni mfupi mno tena umeingiliwa na ratiba ya mechi za kimataifa. Wakishindwa kupata matokeo hapa nyumbani itakuwa vigumu sana kupata matokeo ugenini.
Tatizo kubwa ninaliona mara nyingi kwa Yanga huwa ni namna wanavyoweza kukomalia mambo yasiyo ya msingi sana na kuacha mambo ya msingi. Kwa mfano ukiangalia "pre season" inayoendelea utadhani Simba ndio wanatangulia kucheza CL septemba na Yanga watacheza Oktoba wakati ukweli kinyume chake ndio sahihi.