Black star 2: Nemesis 47
Tariq Haji
0624065911
"Umechelewa" aliongea Fahad akiwa amesimama kwenye kingo za mlima mkubwa, mikono yakw ikiwa nyuma. Vamilion akatua pembeni yake, usoni alikuwa na ishara za sonono. Rahee na Nephira wakashuka kutika mgongo wa ndege huyo mkubwa na kusimama pembeni ya Fahad.
Upepo wa baridi ukawapitia kabla miale mekundu ya jua lichomozalo asubuhi kuwalaki. Fahad akavuta pumzi nyingi na kuitoa kisha akamuangalia Vamilion.
"Rafiki usiwe na huzunu sana, uwezo wako ndio kwanza umeingia katika daraja la Nirvana. Ukipata muda zaidi kuuzoea utaweza kwenda zaidi kuliko mimi" aliongea akimgusa katika bawa lake la kushoto.
Wanne hao ndio walikuwa wakwanza kuwasiki Vajra katika kundi lililoingia siku moja katika koridoo ya wakati. "Nguvu za asili zipo kwa wingi zaidi kuliko Sekai" aliongea Nephira, Fahad akamuangalia bibie kisha kwa kutumia jicho lake busara akaangilia mzunguko wake Qi.
"Hahaha! Tafuta sehemu ukae, nguvu zako zimefikia kiwango cha juu zaidi katika daraja lako la sasa, unatakiwa kuvuka" aliongea. Nephira akasogea pembeni na kukaa kitako, akakunja miguu na kufumba macho. Qi nyingi ikaanza kusafiri kutoka kwenye mazingira na kuingia kayika mwili wake.
Nephira akaiongoza Qi hiyo mpaka kitovuni kwake ambako dantian ndipo ilipokuwa imekaa. Kadiri muda ulivyokwenda ndivyo dantian yake ilivyozidi kujaa na kuanza kutengeza nyufa.
Zzzzzz!
Mlio kama wa waya za zenye kupitisha umeme mkali mkasikika kabla ya Nephira kufumbua macho. Mwanga mweupe ukatoka machoni na mdomoni kwake ukifuatiwa na mwanga ulioelekea juu na kutobia mawingu kama nguzo.
"Hongera malkia kwa kufika daraja la milele" aliongea Rahee akikunha ngumi ya kiganja kimoja na kukutanisha na kiganja kingine.
"Ahsante" alijibu na kutabasamu akisimama.
"Hongera" aliongea Fahad na kumuangalia, Nephira alipoyakutanisha macho yake na mwamba huwo akahisi mapigo ya moyo yakimuenda mbio.
Badum! Badum! Badum.
"Nyoika" akaita Fahad, ile fimbo yake ya chuma ikatokea. "Mimi na wewe hatuna mkataba, unaweza kuchagua bwana wako" akaendelea. Kwa kawaida mtu atadhani kwamba hiyo ilikuwa ni nafasi ya silaha hiyo kutafuta mmiliki wake. Lakini haikuwa hivyo, maneno hayo yaliyotoka mdomoni mwa Fahad yalimaanisha kuwa dimbo hiyo iingie mkataba na Nephira.
Ikapaa angaani kwa kasi, walioishuhudia kwa mbali walidhani ni kimondo. Kisha ikarudi chini kwa kasi mara mbili ya iliyoondoka nayo na kutuwa pembeni ya Nephira.
"Kuanzia leo ni yako hiyo" aliongea Fahad akimuangalia.
"Wewe utatumia nini" aliuliza.
"Nitatfuta silaha yenye kuhimili uwezo wako, hiyo haiwezi tena, itavunjika nikiendelea kuitumia" alijibu.
Nephira akatoa kisu kidogo na kukata kiganja chake, akaishika fimbo hiyo na kuingia "itika nyoika". Fimbo iliyokuwa nyeusi ikaanza kubadilika rangi na kuwa ya dhahabu, michoro ya ajabu ikaanza kujichora. Ilipokamilika ikatoa mwanga mkubwa sana na kutoweka.
"Hongera tena malkia" aliongea Rahee na kutoa heshima, Fahad akamuangalia na kuachia tabasamu laini. "Usijali ipo siku na wewe utapata silaha inayoendana na unachojifunza. Pia tukiwa huku, hakuna haja ya kuitana kwa majina ya vyeo vyetu" aliongea.
"Badi naomba nikuite kaka mkubwa na malkia nimuite dada mkubwa" aliongea Rahee, alishindwa kabisa kuwaita kwa majina yao.
"Sawa, bora hivyo" aliongea Fahad na kugeuka mbele kisha upandr ambao alikuwa Vamilion. "Rudi ndani" akaongea, "hahaha! Haiwezekani tena, kwa nilipofika sasa siwezi tena kuishi ndani ya mwili wako" alijibu kisha akapaa na kuzunguka anagani mara kadhaa kabla ya kurudi chini kwa kasi.
Taratibu mweli wake ukaanza kupungua ukubwa, akatua begani kwa Fahad akiwa katuka umbile la tai mweusi mwenye macho mekundu. "Hapa ndio yatakuwa makazi yangu" akaongea na kubetua kifua chake mbele.
"Unavyojisikia" alijibu Fahad na kugeuka upande ambao njia ilikuwa inashusha na kuanza kuondoka. Nephira akafuata upande wake wa kulia na Rahee upande wa kushoto. Baada ya saa taty wakafika katika kitako cha mkima huwo.
"Karibuni wageni kutika sayari nyingine" sauti ya kizee iliwakaribisha. Pembeni yake kulikuwa na gari la farasi.
"Ahsante" alijibu Fahad na kumgeukia Rahee, akatikisa kichwa na kusogea alipo mzee huyo.
"Tunataka taarifa kuhusu mji uliokuwa karibu na hapa" aliongea naa kutoa tael (pesa) moja ya dhahabu, mashavu ya yule mzee yakawa mekundu.
"Hehehe! Usijali umepata" aliongea akipeleka mkono wake mbele kupokea pesa hiyo.
"Mji wa karibu unaitwa Kunlun" akaanza kuongea, alitoa taarifa zote amazozijua kuhusu mji huwo. "Kama mnataka nitawapeleka" akaongezea. Rahee akamuangalia Fahad na baada ya muda akamgeukia tena yule mzee.
"Tutashukuru sana ukiwa utafanya hivyo" akaonge, yule mzee akafungua mlango na wote wakapanda na kukaa. Akaufunga kisha akapanda kwenye kiti cha mbele na kuwachapa farasi kiboko. Wakatoa sauti kisha wakaanza kuondoka.
"Tungeenda wenyewe ingetuchukuwa muda mchache sana" aliongea Nephira akikunja mdomo.
"Kwasababua wewe umezaliwa kwenye familia yenge uwezo huwezinjua mahangaiko wanayopitia watu ambao wapo katika haki duni" alijibu Vamilion akiwa ameketi kwenye mapaja ya mwanamke huyo.
"Mpaka umuone mtu asubuhi yote hii yuko kijiweni, basi tambua kuwa anatafuta chakula cha familia yake" aliongezea Fahad.
"Kumbuka hata uwe na nguvu kiasi gani, usipoteze asili yako. Sisi binadamu tunatakiwa kufikiria kuhusu wengine pia, unafika sehemu kuna mtu anauza chakula, hata kama sisi wana martial art hatuhitaji kula kwasababu tunapata kila kitu tunachokitaka kutoka nguvu asili. Nunua chakula hapo na ule, kwanza itakusaidia kukumbuka faida ya kuwa na ulimi na pili utatengeza tabasamu kwa muuzaji" aliendele.
"Faida ya watu kama sisi ni kuhakikisha ambao hawakujaalia kuwa na uwezo kama wetu wanaishi maisha bila shida".
"Kwanini umefunga safari hii" alishindwa kuzuia dukuduku lake Nephira, akaamua kuuliza.
"Matarajio ya wengi ni kutafuta nafasi ya kuwa na uwezo mkubwa, kwangu mimi sio hivyo japo kuwa na nguvu ni muhimu sana katika njia ya martial art. Mimi ninefunga safari hii kutafuta ukweli kwasababu ukweli ndio utakaomuweka mtu huru" alijibu Fahad.
Yule mzee muendesha farasi alikuwa akiyasikia mazungumzo hayo vyema kabida. Michirizi ya machozi ikajichora katika mashavu yake, "bado watu wenye utu wapo" alijisemea.
Baada ya safari ya saa nne, gari ya farasi ikasimama kisha yule mzee akagonga mlango. Rahee akaufungua na kushuka, "samahanini tutapumzika hapa kabla ya kuendelea na safari. Farasu wangu wote ni wazee, wanahitaji kupumzika" aliongea.
Rahee akazifikisha taarifa hizo kwa Fahad, wakashuka. Karibu na eneo hiko kulikuwa na mgahawa uliochakaa. Pembeni ya mgahawa huwo kuliko na mto mkubwa uliokuwa ukisafiri taratibu.
Wakati wanaelekea kwenye mgahawa, Fahad akasimama na kuwaangalia wale farasi wawili. Walikuwa weusi tii, weusi ambao si wa kawaida. Kwa kutumia jicho lake la tatu akawaangalia vizuri na kuthibitisha mashaka yake. "Hawa si farasi wa kawaida" alijisemea na kuungana na wengine.