Riwaya: Bondia

kapingili

Senior Member
Joined
Jul 4, 2012
Posts
155
Reaction score
192
IMEANDIKWA NA : HUSSEIN ISSA TUWA

*********************************************************************************

Simulizi : Bondia

Sehemu Ya Kwanza (1)

Lango kuu la gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam lilifunguliwa na mtu mmoja mrefu alitoka nje ya lango lile kwa hatua za kujiamini na kusimama kiasi cha hatua zipatazo tano nje gereza lile. Nyuma yake, lile lango lilifungwa, na hivyo kufungia historia ya miaka miwili ya taabu, mateso, kazi ngumu na uchungu mwingi ambayo mtu huyu alipitia alipokuwa upande wa pili wa lango lile. Ilikuwa ni saa tatu na robo asubuhi siku ya jumatano.Jamaa aliangaza kulia na kushoto pale nje huku akivuta pumzi ndefu zilizoingiza hewa nyingi mapafuni mwake, kisha akashusha pumzi zile zikiambatana na mguno wa faraja, iliyotokana na kuvuta hewa ile ya ulimwengu huru, akiwa mtu huru. Hili ni jambo alilokuwa akilisubiri kwa hamu katika muda wote ule aliokuwa akitumikia kile kifungo chake cha miaka miwili.

Pamoja na kimo chake kirefu, mtu huyu alikuwa na mwili ulioshiba pamoja na kuwa alikuwa kifungoni. Hii ni kutokana na mazoezi mazito aliyokuwa akijilazimisha kufanya akiwa kule gerezani kwa lengo maalum. Misuli yake ya mikono iliyojaa vizuri ilijidhihirisha wazi kwa kututumka na kufanya mikono ya fulana yake ya mikono mifupi ionekane kumbana. Vivyo hivyo, misuli yake ya mapaja ilionekana kututumka na kuifanya ile suruali yake ya jeans nayo ionekane kuwa inambana.
Bila kugeuka nyuma, jamaa alianza kutembea kwa hatua moja moja zilizokuwa zikivutwa bila ya haraka yoyote kuelekea barabara kuu iliyokuwa mbele yake, akiliacha lile jengo la gereza nyuma yake akiwa na azma ya kutorejea tena ndani ya kuta za jengo lile maishani mwake.Bora kufa, kuliko kurudi tena gerezani.

Alishaazimia hivyo muda mrefu, na bado alibaki na azma hiyo.
Kwake yeye mji aliuona ukiwa umebadilika sana ndani ya miaka ile miwili, lakini hilo halikuwa na maana yoyote kwake, kwani alijua kitambo kuwa pindi atakapotoka gerezani angekuta mabadiliko mengi sana jijini. Alikuwa akitembea huku akijaribu kutazama mambo yote yaliyokuwa mbele yake kwa jicho la kudadisi. Aliona kuwa magari ya usafirishaji wa abiria yalikuwa yamechorwa mistari ya rangi, tofauti na hali aliyoiacha wakati anaingia gerezani. Kidogo hili lilimpa taabu, kwani alianza kujiuliza ni jinsi gani ataweza kujua ni rangi ipi ndio ilikuwa ikiwakilisha basi la kuelekea sehemu ambayo alikuwa ameazimia kwenda baada ya kutoka gerezani.

Aliweka sawa mkoba wake mdogo alioupitisha begani kwake na kuuacha ukining'inia mgongoni na kuzidi kuikurubia ile barabara ambayo juu yake, magari yalikuwa yakipita kwa kasi sana kiasi cha kumkosesha amani.

Jamaa alikuwa na sura ya kuvutia ambayo baada ya miaka miwili gerezani, ilikuwa imeingia ukomavu fulani ambao haukuwepo hapo kabla, na ambao kwa namna yake uliongezea mvuto kwenye sura ile.

Lakini wakati akitembea taratibu kwa mwendo wake wa hatua moja moja kukiendea kituo cha mabasi yaelekeayo katikati ya jiji kilichokuwa upande wa pili wa barabara, uso wake ule wenye mvuto ulionekana wazi kuwa ulikuwa una dhamira thabiti juu ya nini alikuwa anataka kufanya baada ya kutoka gerezani, kwani baada ya miaka miwili ya kupanga na kupangua akiwa kule gerezani, hakika alikuwa anajua ni nini haswa alichotakiwa kukifanya.

Kwenye kituo cha mabasi yaliyokuwa yakielekea maeneo ya Kariakoo na katikati ya jiji kilichokuwa upande wa pili wa ile barabara kuu, mmoja wa watu waliokuwa wakisubiri mabasi pale kituoni alikuwa akifuatilia kila hatua ya yule mtu mrefu aliyetoka kule gerezani, ambaye sasa alikuwa akisubiri nafasi muafaka ya kuvuka barabara ili naye aende pale kituoni.
Alikuwa ni mwanamke aliyejitanda khanga mwili mzima hadi kichwani, kama jinsi wanawake wengi wa pwani wapendavyo kujitanda, na usoni alikuwa amevaa miwani myeusi iliyoficha kabisa sura yake. Ingawa alionekana kuwa ni msafiri miongoni mwa wale wasafiri wengi waliokuwa wakisubiri daladala pale kituoni, ukweli ni kwamba mwanadada yule aliyejitanda khanga, alikuwa akimsubiri yule mtu mrefu aliyetoka gerezani asubuhi ile!

Jamaa alivuka barabara na alikuwa akikiendea kile kituo cha mabasi, wakati mlango wa mbele wa gari dogo aina ya Hyundai nyeupe yenye namba za serikali ulipofunguka na msichana mmoja mwenye kimo cha kawaida alipoteremka na kusimama nje ya lile gari huku mkono mmoja bado ukiwa umeshikilia mlango wa gari lake.

Huyu naye alikuwa amevaa miwani ya jua, ingawa yeye alikuwa amevaa gauni refu la kitambaa laini chenye maua madogo madogo lililokuwa na mpasuo mpana upande mmoja. Kichwani alikuwa amebana nywele zake ndefu zilizotiwa dawa za kulainisha na kupendezesha nywele katika ile staili ya Pony Tail , ambapo kile kimkia cha nywele kilichokuwa kikining'inia kisogoni mwake kilikuwa kimechomoza kutokea kwenye sehemu ya nyuma ya kofia aina ya kapelo aliyokuwa ameivaa. Aliweka mkono wale wa pili juu ya paa la gari na kumtazama yule jamaa akipita upande wa pili wa lile gari akielekea kule kituoni.
"Roman!" Aliita.

Jamaa alisimama katikati ya hatua na kugeuka taratibu ule upande ilipotokea sauti iliyoita jina lake. Alimtazama yule dada mwenye kapelo na miwani ya jua huku akikunja uso kujaribu kumtambua. Yule dada aliendelea kumtazama bila ya kusema neno zaidi, akimpa muda yule mtu aliyemwita kwa jina la Roman amtambue.

Kule kituoni yule mwanamke aliyejitanda khanga naye alianza kupata waiswasi baada ya kuona yule jamaa aliyekuwa akimvizia akisimama na kumgeukia yule dada aliyetoka kwenye lile gari lenye namba za serikali.
Ni nini tena pale?

Jamaa alimtazama kwa makini zaidi yule dada na alihisi kuwa alishapata kuiona ile sura wakati fulani huko nyuma, ingawa bado hakuweza kuioanisha sura ile na kumbukumbu zake za miaka miwili iliyopita.

"Miaka miwili ni mingi kiasi cha kukufanya unisahau Roman?" Hatimaye yule dada alimuuliza yule jamaa huku akitoa miwani usoni kwake, na hapo jamaa akaachia mdomo kwa mshangao."Afande Fatma...?" Yule dada alirudisha tena miwani yake usoni. "Sasa nimekuwa Inspekta...Inspekta Fatma."

Jamaa alikunja uso, safari hii ikiwa ni kwa kukereka, na kubetua midomo kwa namna ambayo ilionesha kuwa hakufurahishwa na hali ile."Unataka nini Inspekta?" Roman aliuliza, huku akitilia mkazo wa kebehi lile neno "Inspekta."
"We need to talk Roman...you and me! (Tunahitaji kuzungumza Roman...mimi na wewe!)" Inspekta Fatma alimwambia yule jamaa bila ya kujali kebehi na kukereka kwake kwa wazi. Roman alitikisa kichwa kwa masikitiko.

"Yaani siku yangu ya kwanza nikiwa mtu huru! Halafu mtu wa kwanza kukutana na kuongea naye ni askari! What's this (Nini maana yake hii)?" Roman alisema kwa hasira."We need to talk Roman, and we need to talk now!(Tunahitaji kuzungumza Roman, na tunahitaji kuzunguza wakati huu!)"

"About what (Kuhusu nini)? Nimetumikia kifungo changu, nimemaliza. Sasa mimi ni raia huru..."
"Ingia kwenye gari Roman!" Inspekta Fatma alimkatisha. Na sauti yake ilikuwa imebeba mamlaka yote aliyokabidhiwa na jamhuri kama afisa wa jeshi la polisi mwenye jukumu juu ya usalama wa raia wote wa Tanzania.

Kule kituoni yule mwanamke aliyejitanda khanga alizidi kujichanganya katikati ya kundi la watu waliokuwepo pale kituoni huku akizidi kufuatilia kwa makini kila kilichokuwa kikiendelea kule kwenye lile gari dogo lenye namba za serikali. Na kwa kadiri ilivyokuwa, ni wazi kuwa kile kitendo cha yule mtu aliyeitwa Roman kusimama na kuongea na yule dada aliyetoka kwenye lile gari lenye namba za serikali kilimchanganya sana.

Ni nini kinaendelea pale? Roman alibetua mabega na kuuliza kwa kukereka kwa hali ya juu. "Ili iweje afande? Ni lazima niingie kwenye hilo g-" "Sio lazima. Lakini ni muhimu tuongee. Nataka kukupa lifti..."

Mtu aliyeitwa Roman alimtazama yule askari wa kike kwa muda, na yule askari aliendelea kumtazama bila ya kutetereka. Kisha, bila ya kusema neno zaidi, Roman alipiga hatua moja kubwa na kufungua mlango wa upande wa abiria wa lile gari na kuingia. Inspekta Fatma aliingia nyuma ya usukani na kuliondoa lile gari kutoka eneo lile kwa ustadi mkubwa.

Huku kituoni, mwanamke aliyejitanda khanga alichanganyikiwa vibaya sana. Alilitazama lile gari likiondoka kutoka eneo lile kwa fadhaa iliyochanganyika na hasira.

***

"Unaelekea wapi?" Inspekta Fatma aliuliza huku akiwa amekaza macho yake barabarani. Roman alikuwa amegeuzia uso wake nje ya dirisha akiangalia mandhari ya jiji alilolikosa kwa muda wa miaka miwili. Hakufanya juhudi yoyote kuficha jinsi alivyokereka na hali ya kuwa na yule askari ndani ya lile gari.

"Umesema unataka kuongea. Ongea nami nakusikiliza.
Unaweza kuzunguka jiji lote hili wakati tunaongea...sio lazima ujue niendako!" Alimjibu kwa hasira huku bado akitazama nje ya dirisha. "Nimesema tunahitaji kuongea...mimi na wewe. Hivyo natarajia na wewe uwe unaongea. Na ndio maana nimekuuliza swali ambalo naomba unijibu. Unaelekea wapi Roman?""Hiyo inakuhusu nini? Wewe si ndugu yangu, si jamaa yangu, na wala si mke wangu! Sasa sioni swala la mimi ninaelekea wapi linaingiaje kwako.

Mimi ni mtu huru bwana!" Roman alimjibu kwa jazba. Inspekta Fatma alimtupia jicho la pembeni halafu akabaki kimya kwa muda, akijishughulisha na kuendesha gari, ingawa uso wake ulionesha kuwa na mawazo mazito. Roman alifumbata mikono yake kifuani na kuendelea kutazama nje ya dirisha la lile gari.

Safari iliendelea katika hali ile kwa muda mrefu, na katika muda ule walikuwa wameanza kuingia katikati ya jiji.
Walipita uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam, na mwendo mfupi baadaye, Inspekta Fatma alipunguza mwendo wa gari na kuingia kulia ambapo aliliegesha kwa ufundi mkubwa nje ya mgahawa maarufu wa Best Bite katika lile tawi lake lililopo barabara ya Nyerere, zamani Pugu Road.

"Okay, Roman, nadhani hapa tunaweza kuongea kwa kituo zaidi."
Inspekta Fatma alimwambia yule mtu mrefu mwenye mwili ulioshiba huku akiteremka kutoka kwenye gari. Bila ya kuongea neno, lakini akionesha wazi kuwa alikuwa amechukia, Roman aliteremka na mkoba wake kutoka kwenye lile gari na kumfuata yule afisa wa polisi mrembo ndani ya ule mgahawa mzuri.

Baada ya kuagiza soda aina ya Coca Cola kwa ajili yake na bilauri ya juisi ya nanasi kwa ajili ya Roman kwa mujibu wa utashi wake, Inspekta Fatma alianzisha tena maongezi. "Roman, najua kuwa utakuwa unanichukia sana hivi sasa kwa kufanya haya niyafanyayo, lakini naomba uelewe kuwa hii ni kwa faida yako na si vinginevyo..."

Roman alimtazama yule binti bila ya kusema neno, na Fatma aliendelea."...najua kuwa baada ya kumaliza kifungo chako utakuwa tayari una mipango uliyojipangia katika maisha yako mapya. Basi na iwe ya kheri Roman, vinginevyo itakuwa mbaya sana kwako."

Roman alizidi kumtazama tu yule dada bila ya kusema neno. "Mimi nimeamua kuja kukusubiri pale Ukonga leo hii kwa sababu najali maisha yako, na kwa jinsi ninavyohisi, naona una hatari ya kurudi tena gerezani kama hutaamua kusahau yaliyopita na kutazama mbele."

Inspekta Fatma alizidi kumueleza kwa upole na msisitizo wa hali ya juu. Bado Roman alikuwa akimtazama kwa macho makavu bila ya kusema neno lolote wala kupitisha hisia yoyote usoni mwake ambayo ingeweza kusomwa na macho makini ya yule askari wa kike. Lakini Inspekta Fatma alikuwa anajua ni nini alichokuwa anataka Roman aelewe, hivyo hali ile haikumkatisha tamaa hata kidogo.

"Sahau yaliyopita Roman, na uanze maisha mapya sasa. Kama utahitaji msaada mimi niko tayari kukusaidia kwa kadiri nitakavyoweza, lakini achana kabisa na mawazo uliyonayo Roman, hayatakusaidia kitu..."
Hapo Roman hakuweza kuendelea kubaki kimya.

"Mnhu! Yaani we' unataka kuniambia kuwa unajua mi' n'na mawazo gani? Achana na mimi kabisa afande!"

Inspekta Fatma alitikisa kichwa taratibu.

"Huwezi kunidanganya Roman. Nimekuwa nikikutazama tangu unasubiri kuvuka ile barabara pale nje ya gereza hadi ulipokuwa ukipita mbele ya gari langu pale jirani na kituo cha basi. Katika sura yako kulikuwa kuna kusudio la wazi kabisa ambalo lilithibitisha hofu yangu juu ya mambo utakayotaka kuyafanya muda huu ukiwa umemaliza kifungo chako. Achana na mawazo hayo kabisa Roman..."

"Hujui usemalo Fatma...na kama huna la zaidi naomba niende zangu!" Roman alimjibu kwa hasira. Lakini Inspekta Fatma alikuwa na msimamo.
"Mimi najua, Roman. Na usidhani utanilaghai na huo ukimya wako au utanipoteza lengo kwa hayo maneno yako ya hasira. Najua! Na ndio maana nimekuja kukuasa mapema Roman. Acha yaliyopita yawe yamepita. Angalia mbele...!"
Roman alitikisa kichwa kwa kustaajabia upotofu wa mawazo ya yule askari. Lakini Fatma hakuwa mjinga.
"I am telling you Roman, let it go!(Nakuambia Roman, achana nayo kabisa!)"

"Let what go, Fatma?(Niachane na nini, Fatma?)" Roman alimuuliza kwa kukereka huku akimkunjia uso.
Fatma alitomasa hewa mbele ya uso wa Roman kwa kidole chake cha shahada kutilia msisitizo maneno yake.
"You know what!(Unajua!). Mi' najua miaka miwili uliyokaa gerezani ulikuwa ukisubiri tu siku hii ya leo ifike...na sasa imefika, unataka kutimiza yote yale uliyodhamiria wakati ukiwa kifungoni. Niamini mimi Roman, asilimia tisini ya mambo watu wanayodhamiria kufanya baada ya kutoka huko ulikotoka wewe leo hii huwa ni juu ya uovu, udhalimu zaidi na visasi! You can't be any different! (Wewe huwezi kuwa tofauti na hao)"
Roman aliguna na kutikisa kichwa.

"Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa jela haisaidii kurekebisha tabia? Sasa kwa nini basi huwa mnatupeleka huko?" Alimuuliza kwa kejeli ya wazi. Sasa ilikuwa zamu ya Inspekta Fatma kutikisa kichwa.
"You are a good guy Roman...(U-mtu mzuri Roman...)"

"Good guys do not get sent to prison, do they? (Watu wazuri huwa hawapelekwi gerezani, au sivyo?)" Roman alidakia kwa jazba na huku akipiga meza waliyokuwa wamekalia kwa kiganja cha mkono wake. Baadhi ya watu waliokuwamo mle ndani waliwageukia na kuwakodolea macho na mhudumu mmoja alisogea na kuuliza iwapo kulikuwa kuna tatizo lolote. Ilibidi Inspekta Fatma afanye kazi ya ziada kumhakikishia kuwa hakukuwa na tatizo lolote wakati Roman akibaki akiwa amekunja uso kwa ghadhabu. Inspekta Fatma alimtazama kwa upole uliochanganyika na simanzi yule jamaa.
"You used to be a good guy Roman!(Kabla ya kupelekwa gerezani ulikuwa mtu mzuri Roman!). Nataka uendelee kuwa hivyo sasa baada ya kutoka gerezani. Usiiache hii hali...haya mambo yaliyotokea, yakuharibu. Let it go!(Achana nayo!)" Inspekta Fatma alimjibu kwa hisia kali. Kidogo macho yalimtembea Roman na alitazama pembeni. Hakutaka kabisa kumtazama yule dada usoni.

"Lakini bado hiyo haikutosha kunifanya nisipelekwe gerezani Inspekta!" Roman alisema kwa uchungu.
"Ndio, lakini...You don't belong there Roman! (gerezani si mahala pako Roman!) Ndio maana sitaki ufanye kosa litakalosababisha urudi tena gerezani, kwani ikitokea hivyo Roman, ujue huko ndiko kutakuwa makazi yako for good (milele)! Yaani hukutakiwa kabisa kwenda huko..."

Roman alitikisa kichwa taratibu na kumuuliza.
"Una maana sheria ilikosea iliponipeleka gerezani?"
"No! Lakini mazingira yaliiwezesha sheria ikupeleke gerezani. Ndio maana nakuasa usifanye jambo litakalokufanya uje ujute maisha yako yote Roman!"

"Aanhaa! Kwa hiyo na wewe unakubali kuwa hii tunayoiita sheria ina upungufu? Kwamba inaweza ikatengenezewa mazingira fulani, kisha ikatumika kuwaadhibu wasio na kosa na kuweka huru waliokosa?"
Inspekta Fatma alipepesa macho kidogo. Ilikuwa ni hoja ngumu kwake kuiafiki.
"Aa...sometimes, but...(mara nyingine, lakini...)

"Kwa hiyo unakubaliana na mimi?"
Inspekta Fatma alimtazama Roman kwa macho makali.
"This does not apply to your case Roman, and you know it!(Hali hiyo haipo kwenye swala lako Roman, nawe walijua hilo!)"

Roman alibetua mabega.
"Sawa. So what do you want from me now?(Kwa hiyo sasa unataka nini kutoka kwangu?).
Inspekta Fatma alijibu moja kwa moja bila kusita. "Achana na yote yaliyopita Roman. Just Forget it! (Yaani sahau tu!)"
Roman hakumjibu na badala yake alitazama pembeni. Inspekta Fatma alimtazama kwa makini, na kwa muda mrefu.
"Hunipi ushirikiano mzuri Roman." Hatimaye alimwambia.

"Kwa sababu sitaki kushirikiana nawe afande!" Alimjibu huku akiendelea kutazama pembeni, kisha akaongezea; "...na nisingependa kuendelea kukuona maishani mwangu, if you don't mind (kama hutajali)"
Jibu hili lilionekana wazi kuwa lilimuumiza sana Inspekta Fatma.

"Naamini kama utafuata ushauri wangu hutaniona tena maishani mwako Roman. Lakini ukipuuzia na kufuata mambo ambayo nadhani ndio unataka kuyafanya..." Afande Fatma alimjibu kwa upole, huku akiiachia ile sentesi yake ielee hewani bila kuimalizia. Roman alisoma kitisho kilichokuwa ndani ya kauli ile, na alimkazia macho ghafla.
"Nikipuuzia...then what?(kisha nini?) Alimuuliza kwa jazba huku akimtolea macho ya ghadhabu ambayo yangeweza kumtisha mtu mwingine yeyote, lakini sio Inspekta Fatma.

Inspekta Fatma hakufanya haraka kumjibu, badala yake alimtazama kwa muda, kisha huku bado akimtazama moja kwa moja machoni, alimjibu kwa sauti ya upole lakini iliyojaa yale mamlaka yake yote iliyokabidhiwa na jamhuri.
"Basi nasikitika kuwa itakubidi uwe unaendelea kuniona tu kwa muda wote utakaohitajika ili kukutupa tena jela rafiki yangu!"

Jibu hili lilikuwa nje kabisa ya matarajio ya Roman na alifinya macho yake kumtazama vizuri yule askari wa kike mwenye msimamo. Walitazamana kwa muda na katika muda ule hakuna mmoja kati yao aliyekubali kushusha chini macho yake.
"Unanitishia afande?" Hatimaye Roman alimuuliza kwa sauti kavu huku akiendelea kumtazama kwa makini yule askari. Badala ya kumjibu, Inspekta Fatma alimuita mhudumu kwa ishara ya vidole vyake, na kulipia vile vinywaji walivyoagiza. Alibandika miwani yake ya jua usoni na kuinuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia.

"Good Luck in your new life Roman!(Kila la kheri katika maisha yako mapya Roman!)"
Aligeuka na kuondoka eneo lile kwa mwendo wa madaha ya kike lakini ukionesha kuwa alikuwa akijiamini na asiyetishika na lolote hapa duniani.

Kwa muda mrefu Roman alibaki akiwa amekaa pale kwenye ule mgahawa nadhifu huku uso wake ukionekana kuwa na mawazo mazito. Hatimaye aliinuka na kutoka nje ya mgahawa ule kuendelea na safari yake aliyokuwa ameidhamiria wakati alipotoka kule gerezani, akiiacha ile bilauri ya juisi aliyonunuliwa na Inspekta Fatma pale juu ya meza ikiwa haijaguswa hata kidogo.

******

Kate aliingia ndani ya sebule ghali na kuubamiza mlango nyuma yake kwa ghadhabu. Alirusha funguo za gari alilokuwa akiendesha aina ya Toyota Prado Metallic, Short Chasis, juu ya meza ndogo na nzuri sana iliyokuwa ndani ya ile sebule iliyojitosheleza kwa kila kitu. Alirusha miguu yake mbele mmoja baada ya mwingine huku akisonya na kuviacha viatu vyake vizuri vya kuchomeka vikiruka kila kimoja upande wake na kubaki vikigaa gaa juu ya zulia zito lililotandikwa pale sebuleni.

Alisonya tena na kutupa pembeni zile khanga aliyokuwa amejitanda kichwani na sehemu ya juu ya kiwiliwili chake, na hivyo kuachia nywele zake nzuri zilizokuwa zimewekwa katika ule mtindo wa ‘utajiju', na kudhihirisha fulana nyeupe kubwa iliyoonesha mwinuko mdogo wa matiti yake mazuri ambayo yalionekana wazi kuwa hayakuwa yamebanwa na sidiria na wala hayakuonesha kuwa yalikuwa yanahitaji kubanwa na sidiria yoyote.

Alitoa na ile khanga nyingine aliyokuwa amejitanda kiunoni na kuitupia juu ya sofa jingine lililokuwa karibu yake na kudhihirisha suruali ya jeans iliyoukamata mwili wake kwa namna ya kutamanisha haswa, ikionyesha jinsi makalio yake yalivyochongwa kwa mvuto wa kipekee.

Aliinua uso wake na kutoa ile miwani yake ya jua aliyokuwa ameivaa na kuiweka taratibu juu ya meza ya Runinga kubwa aina ya Sony Plasma. Aliliendea jokofu lililokuwa kwenye kona moja ya sebule ile na kulifungua huku akiinama na kuchungulia ndani ya jokofu lile ambalo nalo lilikuwa la bei mbaya na ambalo daima lilikuwa halikauki mahitaji muhimu ndani yake.

Kwenye sofa lililokuwa kwenye kona moja ya sebule ile, mtu mmoja wa makamu aliyepata umri wa miaka ipatayo arobaini na minane hivi ambaye muda wote huo alikuwa akitazama nyendo zote za yule binti kwa utulivu mkubwa tangu aingie mle ndani, aliitazama ile sehemu ya nyuma ya yule binti mrembo akiwa ameinama namna ile kwa macho yaliyoonesha kuwa yalikuwa yanavutiwa na yalichokuwa yakikiona.

Kate aliinuka akiwa na juisi ya boksi aina ya Ceres mkononi na kugeuka huku akiinua lile boksi ambalo lilikuwa limeshafunguliwa na kulipeleka kinywani. Wakati huo huo yule mwanaume aliyekuwa akimtazama kwa utulivu tangu aingie mle ndani alionesha umakini na kumtupia swali.

"Kwani imekuwaje huko...?"
Alikuwa ni mtu aliyevaa mavazi ghali na shingoni alikuwa amening'iniza cheni moja ya dhahabu kinyume na jinsi ambavyo wengi wangetarajia kutoka kwa mtu wa umri wake. Alionekana wazi kuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa pesa na yule binti angeweza kabisa kuwa mwanawe wa kumzaa.

Kate alibugia ile juisi kwa mfululizo huku akiwa ameinua juu kichwa chake ili ile juisi ishuke vizuri kooni mwake huku akimtupia jicho la pembeni yule mwanaume mtu mzima mwenye mwili mnene wa wastani na mvi chache kila upande wa kichwa chake. Alishusha lile boksi la juisi kutoka kinywani mwake.

"Sikuweza kuongea naye chochote bwana!" (Akasonya). Kisha aliinua tena lile boksi la juisi na kupiga funda jingine dogo la kile kinywaji alichokipenda sana huku akiliendea sofa lililokuwa karibu yake kwa mwendo wa pozi.
"Lakini umemuona? Ni yeye hasa? Ametoka leo?" Yule mzee aliuliza kwa bashasha. Kate aliafiki kwa kichwa kabla ya kumthibitishia kwa maneno.

"Yep! Ndiye haswa!"
Jibu hili lilionesha kumfurahisha yule bwana, lakini alitaka kujua vije amuone mtu aliyemkusudia halafu asiongee naye.
"Ah!(Aliguna) Kwa taarifa yako sio mimi peke yangu niliyekuwa nikimsubiri Roman pale nje ya gereza leo hii..." Kate alimjibu kwa kushutumu huku akiwa amembetulia midomo na yule bwana alionekana kushitushwa na habari ile huku akijisogeza mbele kwenye lile kochi alilokuwa amekalia kwa kiherehere.
"Eti Whaat?" Aliuliza kwa kutoamini.

"Kabisaaa!" Kate alimjibu na kuendelea kumuelezea mambo yote jinsi yalivyotokea hadi pale yule mtu aliyeitwa Roman alipoondoka na lile gari lenye namba za serikali. Yule bwana alibaki mdomo wazi huku akiwa amekunja uso wake katika jitihada ya kujaribu kuelewa undani wa maelezo ya Kate.

"Yaani yule mwanamke ameniboa! Laiti angejua kuwa kuna wanawake wanaoendesha gari za bei mbaya kuliko kile kimkebe chake cha serikali wala asingejitia kumchukua yule jamaa pale. Yaani nimepoteza muda wangu bure...!" Kate aliponda kwa hasira huku akiwa amekunja uso. Lakini yule mwenzake alikuwa na wasiwasi na mambo mengine kabisa kutoka katika yale maelezo yake

"Umesema Roman amechukuliwa na gari yenye namba za serikali...?" Yule mzee aliuliza tena, na kwa mara nyingine Kate alimthibitishia kuwa hivyo ndivyo. Jamaa aliguna na kutikisa kichwa.

"Sasa hii itakuwa nini...?" Aliuliza kwa sauti ya chini, ni kama alikuwa anajisemea mwenyewe tu.
"Sa' mi' n'tajuaje, Master D? Labda yule ni demu wake...." Kate alimjibu huku akijilaza kwenye lile sofa alilokuwa amekalia. Yule mtu alimtupia jicho la pembeni kisha akaendelea kutazama ukutani alipokuwa akitazama hapo awali.
"Hapana, Kate. Demu wake aje na gari la serikali? Sivyo. Hii ni issue kubwa kuliko unavyodhani..."

"Aaah, kwani si kuna mademu wengi tu humu mjini wanaofanya kazi serikalini na kupewa magari ya kutembelea? Kwa nini asiwe demu wake? Jamaa anaonekana handsome kwa kiasi chake, ingawa nilimuona kwa mbali..." Kate alimbishia.
Yule bwana aliinuka na kwenda kusimama nyuma ya dirisha na kutazama nje ya sebule ile. "Hapana. Nadhani hao ni askari...itabidi kuwa makini sana katika hili jambo."

Kate aliinua macho na kumtazama yule bwana mtu mzima kwa muda, lakini hakusema kitu zaidi. Aliamua kuziweka safi kucha zake kwa kuzichokoa-chokoa kwa kijiti cha kuchokolea meno alichokiokota sehemu fulani ndani ya sebule ile.Muda mrefu ulipita bila yeyote kati yao kusema lolote, yule mtu mzima akiwa kwenye dimbwi la mawazo, wakati yule mrembo mwenye deko aliyeitwa Kate akiendelea kucheza na kucha zake.

"Sasa tutampataje tena huyu mtu..." Yule jamaa wa makamu aliyeitwa Dan alijisemea mwenyewe. Dan Dihenga ndilo jina lake halisi, ingawa marafiki zake wa karibu walizoea kumkatisha na kumuita Master D. Kate alimtazama yule bwana kwa muda, kisha akamjibu huku akiendelea kucheza na kucha zake.

"Mi' kazi yangu nilishaifanya ila nd'o hivyo imeingiliwa na huyo mwanamke. We' ndiye unayejua...toa maelekezo, mi' n'tafuata."

Sasa ilikuwa zamu ya Master D kumtazama yule binti mrembo aliyekuwa akiendelea kuchezea kucha zake, ila sasa alikuwa ameziingilia za miguuni. Muda mrefu ulipita bila yeyote kati yao kusema neno, hatimaye Master D alirudi kwenye sofa alilokuwa amekalia hapo mwanzo na kukunja nne.

"Nadhani sasa kuna sehemu moja tu ambayo tunaweza kubahatisha kumpata. Na nadhani itatubidi tuelekee huko haraka."

Roman aliusogelea ule mwinuko mdogo wa udongo kwa hatua za pole pole mno, na kadiri alivyozidi kuusogelea ndivyo miguu ilivyozidi kumuwia mizito, na moyo ulivyozidi kumuuma. Ingawa alijua fika tangu alipotoka gerezani asubuhi ile kuwa mahala pale ndipo alipokuwa amedhamiria kuja kabla ya kwenda mahala pengine popote, lakini baada ya kufika alitamani kuwa asingekuja kabisa.

Lakini isingewezekana kuwa vinginevyo. Kwa vyovyote ilimbidi afike mahala pale. Na kama si yule askari wa kike kuingilia utaratibu wake, muda huu angekuwa ameshahudhuria eneo hili na kuwa mahala pengine kabisa.
Alisimama mbele ya ule mwinuko na kumbukumbu ya mara ya mwisho aliposimama mbele ya sehemu hii kabla haijawa na mwinuko kama ilivyo sasa ilimrudia na hapo alitoa sauti ya uchungu na macho yakamchonyota kwa machozi huku donge kubwa likamkaba kooni.

Wakati aliposimama mbele ya sehemu hii kwa mara ya mwisho palikuwa na shimo badala ya mwinuko…
Roman alipiga goti moja mbele ya ule mwinuko uliokuwa mithili ya tuta na kuinamisha uso wake kwa uchungu, paji la uso wake likiwa limelalia juu ya mkono wake uliolazwa juu ya goti lake. Machozi yalimbubujika na uchungu mwingi uliutawala moyo wake. Alijaribu kumuomba Mungu lakini hakuna neno takatifu hata moja lililomjia akilini mwake wakati ule. Kichwa kilimrindima kwa ghadhabu na moyo ulimtetema kwa uchungu.

Aliinua uso wake na kuuangalia msalaba uliochomekwa mbele ya lile kaburi, na moyo wake uliingia mlipuko mpya wa simanzi iliyochanganyika na uchungu pale aliposoma jina lililoandikwa kwenye ule msalaba.

Rachel Koga.

Ilimuwia vigumu kuamini kuwa alikuwa akilisoma jina lile kwenye msalaba...hakika hakuwa ametegemea kabisa kitu kama hicho maishani mwake.

Chini ya jina lile la marehemu aliyelala chini ya ule mwinuko wa udongo kulikuwa kuna tarehe yake ya kuzaliwa na ile aliyoaga dunia, tarehe ya kuaga kwake dunia ikiwa ni miaka miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa zile tarehe zilizoandikwa kwenye msalaba ule, ilionesha kuwa yule marehemu aliyekuwa akiitwa Rachel, aliiaga dunia hii akiwa na umri wa miaka kumi na tisa.

Miaka kumi na tisa tu!
Roman alilia!

Alilia akiwa amepiga goti pale mbele ya lile kaburi bila ya kujizuia. Alilia kwa uchungu na hasira na majonzi. Hatimaye alipata maneno ya kuongea na Mungu wake akiwa pale mbele ya lile kaburi, hivyo huku machozi yakimbubujika kwa wingi, Roman aliinua uso wake na kutazama mbinguni na maneno yakamtoka kinywani mwake huku bado kilio kikiwa kimemkabili.

"Mungu wangu! Natumai utanisamehe kwa nitakalolifanya. Ni wewe pekee ndiye mwenye uwezo wa kusamehe hata wale waliokukosea kwa namna kubwa kabisa…lakini mimi ni mwanadamu tu Mungu wangu, na ni kiumbe dhaifu sana. Sina uwezo wa kusamehe kama ulio nao wewe…na sina namna ya kutofanya makosa kwani hiyo ni ada yangu kama mja wako. Sina ninalotumainia isipokuwa msamaha wako, kwa hiyo naomba msamaha kabisa mola wangu kwa sababu jambo nililodhamiria kulifanya kwa hakika linahitaji msamaha wako…"
Hakuweza kuendelea.

Aliinamisha kichwa kwa simanzi huku machozi yakimtiririka kwa wingi na sauti ndogo za uchungu zikimtoka ilhali mabega yakimpanda na kumshuka kwa kila kwikwi ya kilio iliyomtoka.
Kwa hakika alikuwa ni mtu mwenye uchungu wa hali ya juu.

Alilia mpaka akaishiwa machozi, ndipo alipoinuka kutoka pale alipokuwa amepiga goti na kuanza kujishughulisha na kuling'olea majani lile kaburi na kuuweka sawa ule msalaba ambao kidogo ulilalia upande mmoja kutokana na kumong'onyoka kwa udongo upande mmoja wa lile kaburi.

Alijazia udongo sehemu zilizokuwa zimemong'onyoka kwa mikono yake bila kujali kujichafua. Alipomaliza alijipangusia mikono yake kwenye suruali yake ya jeans na kurudi nyuma hatua chache na kutazama kazi yake.
Ilimridhisha.

Alilitazama lile kaburi kwa muda mrefu, kisha aligeuka na kuondoka eneo lile la makaburi kwa unyonge mkubwa.
Bila ya yeye kujua, watu wawilli waliokuwa ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa hatua kadhaa kutoka kwenye yale makaburi ambayo hayakuwa yamejengewa uzio, walikuwa wakishuhudia mambo yote aliyokuwa akiyafanya pale kaburini kwa utulivu mkubwa. Alipotoka na kuanza kuelekea kituo cha basi kilichokuwa karibu kabisa na makaburi yale, alipita karibu na lile gari bila hata ya kuliangalia. Muda huo Kate alianza kufungua mlango ili amfuate, lakini Master D alimzuia huku akiendelea kumtazama yule mtu mwenye majonzi akijikongoja kutoka eneo lile.

Kate alimgeukia Master D kwa mshangao huku akitoa sauti ya kukereka na kumuuliza kulikoni anamzuia asimwendee yule mtu ambaye walikuwa wanamhitaji sana na hawajui kuwa wakimkosa wakati ule wangempata wapi tena.
"Huu sio muda muafaka Kate…" Dan alimjibu kwa sauti ya upole huku uso wake ukionesha mawazo mazito wakati akimtazama yule mtu aliyetoka gerezani asubuhi ile.

"Sasa tutampata vipi tena Master D?" Kate aliuliza wakati akimshuhudia Roman akipanda daladala mbele yao.
Bila ya kujibu, Dan aliingiza ile Prado Short Chasis barabarani na kuanza kulifuata lile daladala aina ya kipanya."Kazi yako ni kuangalia Roman anateremka kituo gani baby…mengine niachie mimi!" Alimwambia yule binti. Badala ya kumjibu Kate alijiegemeza vizuri kwenye kiti chake na kuikazia macho ile daladala iliyokuwa mbele yao.

Safari ya Roman iliishia maeneo ya Kawe ambako alienda moja kwa moja hadi kwenye eneo kubwa kidogo la biashara ambalo lilikuwa limezungukwa na milango mingi ya maduka ya biashara mbali mbali, zikiwamo saluni za kike na za kiume, maduka ya bidhaa mbalimbali za rejareja, maduka ya mavazi, simu za mikononi, huduma za kupigisha simu na mauzo ya vocha za simu mbalimbali na vitu kama hivyo. Nje ya eneo lile alimuulizia mtu aliyekuwa akimtaka na alielekezwa kwenye mlango mdogo wa chuma ambao alipoingia ndani yake alitokezea nyuma ya maduka yale ambako kulikuwa kuna baa iliyojificha. Kwa muda ule ile baa haikuwa na wateja isipokuwa walevi wachache sana waliobobea. Pale aliulizia tena na kijana aliyekuwa akifanya usafi pale baa alimuelekeza kwa kidole upande mmoja wa ile baa ambako kulikuwa kuna ukuta uliokuwa na mlango mpana wa chuma.

Roman aliusukuma ule mlango na kuingia ndani. Alitokea kwenye eneo pana lililozungukwa na mabenchi na viti vya namna mbali mbali katika kila kona ya eneo lile, ilhali eneo la katikati ya ukumbi ule kukiwa kuna ulingo wa ndondi uliokamilika.

Roman alitembeza macho mle ndani na kushuhudia vijana wengi wakiwa katika harakati za mazoezi mbali mbali ya viungo na kujenga miili yao kama mabondia wanavyotakiwa kufanya, na ile taswira ilimrejeshea kumbukumbu za siku nyingi za nyuma na akahisi mwili ukimsisimka na moyo ukimlipuka kwa matarajio na kuanza kumuenda mbio. Alibaki akiwa amesimama pembeni ndani ya ukumbi ule kwa muda akitazama zile harakati zilizokuwa zikiendelea mle ndani kwa namna ya kuvutiwa sana. Kwenye ukuta uliokuwa mbele yake upande wa pilli wa ukumbi ule kulikuwa kuna maadishi makubwa yaliyosomeka KAWE BOXING CLUB.

Hapo alijua kuwa hakuwa amepotea, kwani ndipo haswa mahala alipokuwa amekusudia kufika baada ya kutoka kule makaburini.

Wale vijana waliendelea na harakati zao bila ya kumtilia maanani, naye alilisogelea benchi moja lililokuwa kwenye kona moja ya ukumbi ule na kuketi akitazama zile harakati huku akijaribu kuangaza huku na huko mle ndani akimtafuta mtu aliyekuwa amemkusudia, lakini ilikuwa wazi kuwa hakuwepo.

Hilo halikumtia wasiwasi wowote.
Alijua kuwa angetokea tu, naye aliamua kusubiri huku akiwatazama wale vijana wakitokwa jasho kwa harakati zao za kujiweka sawa kimazoezi.

Muda mfupi baadaye mtu mmoja mfupi mwenye upara na aliyeonekana kuwa na umri wa kati miaka arobaini na saba na hamsini aliingia mle ndani kwa mwendo wa haraka akitokea kwenye mlango mwingine mdogo uliokuwa upande wa pili wa eneo lile, kando ya yale maandishi yaliyosomeka "Kawe Boxing Club".

"Alright! Alrght! Alright….! Hey!" Yule mtu alisema kwa sauti ya juu huku akipiga makofi na wale vijana waliacha mazoezi yao na kujipanga pamoja kumsikiliza.

Roman aliachia tabasamu kubwa baada ya kumuona yule mtu ambaye haikuwa na shaka kabisa kuwa ndiye mkufunzi au kocha wa wale vijana. Alikuwa amevaa suti ya mazoezi (Track Suit) iliyomkaa vizuri sana, na viatu vya raba aina ya Reebok. Alipendeza sana, na Roman alikumbuka nyakati za siku za nyuma alipokuwa pamoja na mtu yule mzee mwenye roho ya kipekee.

Yeye na mwenzake mwingine…

Alijitikisa kichwa kwa namna ya kuyafuta mawazo yale kichwani mwake na kurejesha akili yake kule kwa bwana mwenye upara na vijana wake.

"Okay! Tuna mechi ya kugombea ubingwa wa wilaya kesho kutwa na wote tunawajua wapinzani wetu tulionao hapa wilayani ni akina nani. Lengo letu ni kuchukua ubingwa wa taifa, lakini hatuwezi kufanya hivyo kama hatujashinda ngazi ya wilaya na mkoa. Mko tayari?"

"Ndiyoooo!" Wale vijana walijibu kwa sauti ya juu huku wengine wakipiga mbinja na kurukaruka huku na huko, wakitupa mgumi hewani kiufundi kwa jazba na kujijaza hamasa. Roman alizidi kuachia tabasamu kufurahishwa na hali ile.
"Okay! Dulla!"

Bondia aliyeitwa Dulla alichomoka mbele kwa mbwembwe kali za kibondia, akitupa ngumi nyingi za mfululizo hewani kwa nguvu na kasi ya kuvutia, huku akibonyea mara kwa mara kama anayekwepa masumbwi ya mpinzani na kujiinua tena na kutupa ngumi nyingine kwa mitindo ya hook na upper cut, kisha akatulia mbele ya kocha wake akiwa ameinua ngumi zake usoni mwake kama jinsi mabondia wanavyosimama wakiwa wanasubiri amri ya mwamuzi kabla ya kuanza kwa pambano.

Yule kocha alimtazama mpiganaji wake kwa namna ya kuridhishwa na makeke yake, kisha akamueleza.
"Utapanda ulingoni na Chumbi wa timu ya Wandava Boxing katika uzito wa Bantam! Chumbi ni moto wa kuotea mbali na sina haja ya kukumbusha juu ya hilo, tatizo lako kubwa ni kujiamini kuliko kawaida Dulla, na usipoangalia, hilo ndilo litakuwa kaburi lako katika ndondi…" Hapo macho ya yule mtu mwenye upara yalimuona Roman akiwa ameketi kwenye benchi kando kabisa ya ukumbi ule na hapo hapo alikatisha maelezo yake. Badala yake uso wake ulijaa mshangao huku akifinya macho kumtazama vizuri yule mtu aliyetoka gerezani asubuhi ile. Wale vijana wote nao wakafuata macho ya kocha wao na kumgeukia Roman.

"Roman…!?" Yule mzee alisema kwa sauti ya chini iliyojaa mshangao na maswali ya kutoamini.
Taratibu yule bwana aliyejengeka kimazoezi aliwasogeza pembeni wale vijana waliokuwa mbele yake na kumuendea Roman kwa mwendo wa taratibu. Roman aliinuka kutoka kwenye lile benchi alilokuwa amekalia na kuanza kumsogelea yule mzee. Walitazamana kwa muda huku wakisogeleana, na hatimaye yule mzee alijihakikishia kuwa ni kweli macho yake yalichokuwa yakimuonesha, kwamba kwa hakika yule aliyekuwa akimuona alikuwa ni mtu aliyemtambua kwa jina la Roman.

"Roman! Roman…! Umetoka…?"
Walikimbiliana na kukumbatiana kwa nguvu na upendo wa hali ya juu kwa muda mrefu. Hatimaye yule mzee alimsukuma nyuma kidogo Roman na kumtazama usoni huku akiwa amemshika mabega.
"Ah! Roman! Umetoka lini? Mbona sikuwa na taarifa…? Unaonekana uko fiti sana!" Aliuliza.
"Leo, Kocha! Nimetoka leo…asubuhi hii hii…" Roman alimjibu yule mzee ambaye kufikia pale hakuweza kuyazuia machozi yasimtiririke.

"Ah, Roman my boy! Miaka miwili sio mingi kumbe afterall eenh?" Alisema huku akiachia machozi yamtiririke bila ya kufanya bidii yoyote ya kuyafuta.
"Yeah, Coach…sio mingi kama ilivyoonekana hapo mwanzo." Roman alimjibu huku akimpangusa machozi yule mzee aliyemwita ‘Coach' kwa kiganja cha mkono wake. Wale vijana waliokuwa wakifanya mazoezi pale ukumbini walikuwa wakitazama tukio lile kwa udadisi wa hali ya juu. Yule bwana mwenye upara alimshika mkono Roman na kumuongoza kuelekea kule kwenye mlango aliotokea hapo awali na kuwakuta wale vijana wake wakifanya mazoezi pale ukumbini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Come on! Twende tukaongee ofisini kwangu!' Alimwambia bila kujali mshangao ulioonekana wazi kwenye nyuso za wale wanafunzi wake. Waliingia ndani ya ile ofisi na yule bwana alifunga mlango na kumuelekeza Roman aketi kwenye kiti kilichokuwa mbele ya meza yake mle ofisini naye akaketi juu ya meza, akikiacha kiti chake kilichokuwa nyuma ya ile meza.

Walitazamana kwa muda, kisha Roman aliongea kwa upole. "I am out now Mark (Nimetoka sasa Mark). Umeniwekea vitu vyote nilivyokuagiza?"

Makongoro "Mark Tonto" Tondolo, kocha wa ndondi wa muda mrefu, na bingwa wa zamani wa taifa wa ngumi za ridhaa katika uzito wa juu (Heavy Weight) alimtazama Roman kwa muda bila ya kusema neno. Kisha aliinuka na kuzunguka nyuma ya ile meza aliyokuwa ameikalia na kutoa faili jembamba kutoka kwenye droo ya meza ile na kumkabidhi.
"Kila kitu kimo humo ndani Roman, kama jinsi ulivyoagiza!" Alimwambia.

ITAENDELEA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi : Bondia
Sehemu Ya Tatu (3)

Baada ya lile pambano lake na mzungu kutoka Hungary, Macha alipambana na bondia kutoka Afrika ya Kusini mjini Johannesburg, ambako alimtawanya taya msauzi huyo na kuondoka mshindi. Sifa za bondia “Deus-deadly” Macha sasa zilikuwa zimeenea duniani kote, na Tanzania ikawa moja ya nchi za kutazamika katika ulimwengu wa ndondi.
Kwenye faili kulikuwa kuna habari juu ya mzozo baina ya Deus na promota wake, mzozo ambao kwa mujibu habari za magazeti, ulitokana na Deus kutoridhika na mapambano anayoandaliwa na promota wake huyo. Mwisho wa habari ile ilielezwa kuwa Deus alivunja mkataba na promota huyo na kujiunga na promota mwingine ambaye alionekana kuwa na mtazamao wa maendeleo zaidi kwa Deus kuliko yule promota wake wa awali aliyemtoa jeshini. (Roman alitikisa kichwa tena kwa masikitko, kisha akendelea kusoma).

Ndipo, miezi sita baada ya lile tukio la kutishiana baina yake na yule bingwa wa dunia wa wakati ule, promota mpya wa Deus alipokubali pambano baina ya bondia wake na bingwa yule, pambano likiwa ni la kugombea mkanda ule wa dunia. Kufikia hapa Roman alikuwa anasoma kwa hamasa, akiwa amejawa udadisi wa kujua kilichojiri kwenye pambano lile baina ya Bondia Deusdelity Macha na yule bingwa wa dunia wa wakati ule...

Lilikuwa ni pambano lililotangazwa na kunadiwa sana, na siku ya tukio ukumbi ulifurika kuliko ilivyowahi kutokea. Kengele ya kuanza pambano ilipogongwa, wapinzani wale waliendeana kwa bashasha na azma ya pambano la kukata na shoka. Na hapa ndipo Deus alipoonesha kuwa kweli yeye alikuwa muuaji kwani kufikia raundi ya kumi na moja bingwa wa dunia aliyekuwa akitetea ubingwa wake alikuwa ameshavunjwa mwamba wa pua na akitokwa damu kama maji.
Refa alilazimika kusimamisha pambano na Deus akatawazwa ubingwa wa dunia katika uzito wa Super Middle kwa Technical Knock Out.

Picha ya mwisho ndani ya faili lile ilimuonesha Deus akimvugumizia konde la kulia katikati ya uso mpinzani wake, ngumi ambayo ndiyo iliyomvunja mwamba wa pua na kumvua ubingwa. Hii ilikuwa ni miezi sita iliyopita...
Roman alishusha pumzi ndefu huku akilifunika lile faili. Aliketi kwa muda mrefu pale kwenye kiti akiwa amejawa na tafakuri nzito, kisha akainuka na kutoka nje. Alienda kuketi kwenye kona moja ndani ya ile baa iliyokuwa nje ya ile klabu na kuagiza kinywaji. Uso wake ulikuwa umekunjamana kwa mawazo mazito. Muda mfupi baadaye, Makongoro “Mark Tonto” Tondolo aliingia eneo lile na kuanza kuelekea kule kwenye klabu yake ya ndondi. Roman alimpigia mbinja, na Mark alipogeuka, alimpungua mkono.

“Haya niambie nini kilitokea jana Roman...Inspekta Fatma alikuibukia hadi huku?” Mark alisema huku akiketi kwenye kiti mbele ya Roman. Roman aliita muhudumu na Mark akaagiza kinywaji.
“Bora ingekua Inspekta Fatma Mark, angalau yeye najua ni nini kinachomsumbua”
“Ama! Ni nani kumbe?”

Roman akamsimulia juu ya tukio baina yake na yule mwanadada aliyejitambulisha kwa jina la Kate. Mark alichanganyikiwa.
“Mnh!Kate? Kate huyu wa wapi? Na alikuwa anataka nini hasa?” Alijikuta akiuliza maswali ambayo tayari Roman alishajiuliza. Roman alimbetulia mabega na kubaki akimtazama tu. Kimya kilichukua nafasi baina yao kwa muda, kisha Mark akaongea.
“Okay, sasa unadhani tufanyaje juu ya hii hali?”
“Tusifanye kitu...tuendelee na mipango yetu kama tulivyopanga.”
“Khah! Sasa na huyu Kate...?”

“Kate hatuzuii kufanya lolote. Yeye atakuja tena tu, na safari hiyo hatonitoka kirahisi...” Roman alisema kwa utulivu. Lakini Mark hakuwa na utulivu hata kidogo katika swala lile.

“Hii ni mbaya sana Roman...mbaya sana!” Alisema kwa hamasa. Roman alibaki akimtazama akiwa kimya. “Sasa unajuaje iwapo huyu...huyu...Kate, si askari aliyetumwa na Inspekta Fatma Roman? Unajua huyu Fatma mi’ hanipi amani kabisa?” Alizidi kusema kwa wasiwasi. Roman alimtazama yule rafiki yake wa makamu na kumpiga ngumi ya maskhara begani.
“Relax kocha, okay? Haitusaidii kuumiza kichwa kwa jambo ambalo hatuna hakika nalo kwa sasa bwana. Lolote ambalo yule dada alikuwa analitaka kwangu, hakulipata, hivyo lazima atarudi tena, na hapo ndipo tutajua. Kwa sasa tunaendelea na mambo yetu kama kawaida.” Alimwambia kwa kirefu. Mark alimtazama kwa muda, kisha huku bado uso wake ukiwa makini, alimwambia; “Tutaendelea na mipango yetu kama kawaida, lakini hatutakiwi ku-relax hata kidogo juu ya swala la huyu Kate, Roman...mpaka tujue ni nini hasa anataka kutoka kwako, okay?”
“Okay, kocha wangu...”

Kimya kilichukua nafasi kwa muda wakati watu wale wawili wakiendelea kunywa vinywaji vyao, kila mmoja akiwa na mawazo yake.

“Kesho ndio mnaanza mechi za kugombea ubingwa wa wilaya, sio?” Hatimaye Roman aliuliza.
“Yeah Roman. Naona vijana wako katika hali na ari nzuri, natumai tutashinda tu...”
Kimya kilitawala tena.

“Jina langu limo kwenye orodha ya mabondia waliosajiliwa kwenye timu yako?” Roman aliuliza tena.

“Kama tulivyopanga Roman. Nilikusajili tangu wakati uko gerezani, na kama bado una nia ya kuendelea na azma uliyoweka, basi nawe utapanda ulingoni pindi ukiwa tayari...”
“Azma iko pale pale Makongoro. Ila itabidi vijana wako wafanye kazi ya kuvuka katika ngazi hii ya wilaya, mimi nitaingia kwenye ngazi ya mkoa...nahitaji mazoezi zaidi...” Roman alimjibu, kisha akaendelea, “...unadhani wanaweza kutuvusha?”
“Ninajua kuwa wanaweza kutuvusha...” Mark alijibu kwa kujiamini.

****

Kwa wiki mbili mfululizo baada ya siku ile, Roman alijishughulisha katika mazoezi mazito sana ya ndondi. Akikimbia umbali mrefu kila alfajiri na kurudi kwenye ile klabu yao ya ndondi kwa ajili ya mazoezi zaidi ya viungo na ya ulingoni chini ya usimamizi makini wa kocha wake wa muda mrefu, Mark Tonto. Timu yao ya ndondi haikufanikiwa kuchukua ubingwa wa wilaya, lakini ilifanikiwa kusonga hadi ngazi ya mkoa kwa kutoka washindi wa pili katika ngazi ile ya wilaya.

Na katika wiki mbili zile, pamoja na kuweka umakini wa hali ya juu kila alipokuwa, Roman hakuonana tena na Kate wala Inspekta Fatma. Mazoezi yaliendelea kwa nguvu, na kadiri alivyokuwa akiendelea na mazoezi, ndivyo alivyozidi kujihisi akirudia kwenye uwezo wake wa ngumi aliokuwa nao hapo awali...kabla hajapigwa marufuku kushiriki katika mchezo ule aliokuwa akiupenda sana, na kujikuta akikaa nje na ulingo kwa miaka mingi, miwili kati ya hiyo akiwa gerezani.

Kadiri siku zilivyosogea, ndivyo alivyozidi kuhisi msisimko wa ajabu wakati utashi wa mchezo ule ukimtambaa ndani ya mishipa yake ya damu. Mchezo wa ngumi...ndondi...mchezo wa mabondia. Naye sasa alikuwa anajiandaa kuingia tena ulingoni kushiriki mchezo ule.

Wengi walikuwa wakishiriki mchezo ule kwa ajili ya kutaka sifa na umaarufu, wakati wengine walikuwa wakishiriki kwa ajili ya pesa tu, ilhali wengine ilikuwa ni kwa ajili ya pesa na umaarufu na sifa. Na wachache miongoni mwa mabondia walikuwa wakishiriki mchezo ule kwa upenzi tu wa michezo kama ilivyokuwa kwake kabla hajapigwa marufuku... na kabla ya kifungo chake.

Lakini safari hii Roman alikuwa anarudi ulingoni kwa ajili ya kutimiza azma. Azma ya hatari. Azma iliyokuwa ikifumfukuta moyoni kwa miaka miwili. Azma iliyogubikwa usiri mkubwa.
***

Roman alikuwa akikimbia huku akitupa ngumi mbele yake na kuruka huku na huko kibondia kando ya barabara. Alikuwa amevaa suruali ya mazoezi na fulana nchinjo ya mazoezi ambayo ilikuwa na kofia iliyofunika kichwa chake. Usoni alikuwa amevaa miwani maalum ya kumkinga na upepo na vumbi. Mark Tonto alikuwa akimfuta nyuma taratibu akiwa kwenye baiskeli. Walikuwa kwenye mazoezi makali, ikiwa ni siku tatu tu kabla ya kuanza kwa mashindano ya ndondi za ridhaa kugombea ubingwa wa mkoa, safari hii Roman naye akiwa miongoni mwa mabondia wa Kawe Boxing Club watakaopanda ulingoni.

Wakiwa katika harakati zao zile za mazoezi, hawakuitilia maanani kabisa Toyota Prado short chasis yenye rangi ya metallic iliyokuwa imeegeshwa kando ya barabara ile waliyozoea kuitumia kila asubuhi kwa ajili ya mazoezi yao makali.
Ndani ya ile gari, Master D na Kate walikuwa wakiwatazama kwa utulivu wawili wale wakiendelea na mazoezi yao. Kate alimtazama yule jamaa aliyetoka gerezani siku kadhaa zilizopita jinsi akitupa masumbwi hewani namna ile huku akiranda kulia na kushoto kistadi wakati akikimbia kando ya ile barabara, na uso wake ukafanya tabasamu dogo.

“Enhe? Nini kinafuata sasa Master D?” Alimuuliza yule mtu mzima aliyekuwa naye ndani ile gari huku bado akiwaangalia akina Roman. Ilikuwa ni zamu ya Dan kuachia tabasamu dogo, kisha akaliondoa gari kando ya barabara, akawapita akina Roman na kuondoka eneo lile.

“Kinachofuata ni kukabiliana na Roman sasa...nadhani mambo yanaenda kama tutakavyo...” Master D alimjibu.
“Okay...lini sasa?” Kate alihoji.
“Soon...very soon...(muda mfupi sana ujao) mrembo wangu!”

***
Mashindano ya ndondi kugombea ubingwa wa mkoa wa Dar es Salaam yalichukua muda wa wiki tatu. Katika wiki ya kwanza Kawe boxing club ilipandisha mabondia wanne ulingoni, watatu wakishinda na mmoja akipoteza pambano. Roman alikuwa miongoni mwa watatu walioshinda kwa kumuangusha mpinzani wake katika raundi pili tu ya pambano, na hapo hapo kujipatia mashabiki kwa jinsi alivyokuwa akipigana.

Wakiwa mazoezini ndani ya ile klabu yao mwisho wa ile wiki ya kwanza,Roman alipata ugeni asioutarajia. Siku hiyo alikuwa ulingoni akipigana na bondia mwenzake ikiwa ni sehemu ya mazoezi, mkufunzi wao Mark Tonto akiwa kama muamuzi na wakati huo huo akitoa mafunzo. Mabondia wengine wa timu ile ya ndondi walikuwa nje ya ulingo wakifuatilia pambano lile la mazoezi kwa makini, wote sasa wakiwa wamemkubali Roman kama mwenzao na kama bondia mwenye uwezo mkubwa miongoni mwao.

Yule bondia alikuwa akimjia kwa ngumi kali za mfululizo, na Roman alikuwa akiruka huku na kule, akitupatupa miguu yake mbele na nyuma kiufundi huku akimsogezea uso mpinzani wake na kuurudisha nyuma kila jamaa alipojaribu kumtupia konde, hoi hoi na vifijo vikirindima kutoka kwa mabondia wenzao waliokuwa nje ya ulingo. Jamaa alikuwa akimjia kwa kasi, Roman aliyumba kushoto na kubonyea kidogo huku akimsogelea, wakati jamaa alipotupa konde kali la kushoto lililopita hewani, na Roman aliibuka na upper cut iliyotua sawia kidevuni kwa mpinzani wake na kumpeleka chini kama mzigo.

Shangwe ziliibuka kutoka kwa mabondia wenzao, wakati Roman akimsaidia bondia mwenzake kuinuka kutoka pale chini.
“Pole partner...sikuipa nguvu zangu zote hata hivyo...kwa hiyo hutadhurika sana!” Alimwambia yule bondia huku akimsaidia kusimama.

“Sasa huo ndio upiganaji Roman!” Mark alisema kwa hamasa huku akiwasogelea wale wapiganaji wake, na kumgeukia yule kijana aliyepelekwa chini kwa konde la Roman, “...na ule si upiganaji! We’ umenaswa kwenye mtego wa Roman, Chumbi... anakuchezeshea uso nawe unautamani uso, unasahau kujikinga...” Mark alikuwa akisema, lakini hapo macho yake yaliangukia nje ya ulingo, na kutulia huko kwa muda, sentensi yake ikibaki ikielea hewani. Alimtupia jicho la haraka Roman, na kuyarudisha tena macho yake kule nje ya ulingo. Roman aligeuka kufuata ulelekeo wa macho ya Mark, kama jinsi ambavyo na wale mabondia wengine walikuwepo pale walivyofanya.

azoezi, akiwa amevaa mavazi yake ya kiaskari, kofia yake akiwa ameikumbatia chini ya kwapa lake la kushoto. Kwa mkono wake wa kulia alikuwa ameshika fimbo yake ya kiaskari ambayo alikuwa akiipiga-piga taratibu kwenye tumbo la kiganja chake cha kushoto. Uso wake uliokuwa umefunikwa kwa miwani myeusi ulikuwa ukimtazama Roman moja kwa moja kule ulingoni.

“Sasa huyu anataka nini tena hapa?” Mark Tonto alisema kwa sauti ya chini huku akimtazama yule askari wa kike. Roman alimuacha Chumbi na kuusogelea ukingo wa ule ulingo na kusimama akiwa ameshika kamba ya ulingo ule huku akimtazama Inspekta Fatma. Walibaki wakitazamana kwa muda, kisha Inspekta Fatma aliweka kofia yake kichwani taratibu, na bila ya kusema neno lolote, aligeuka na kuondoka.Hivyo tu! Roman na Mark walitazamana, lakini hakuna yeyote kati yao aliyesema neno, kisha Mark akawageukia wale mabondia wake.

“Alrigh, alright, alright, Hey! Haya tunaendelea, tumeshaona jinsi Roman na Chumbi walivyojifua...sasa nataka niwaone Dulla na Kibwe ulingoni...” Alisema huku akipiga makofi kuwahamasisha wachezaji wake. Roman aliteremka ulingoni, na taratibu aliondoka eneo lile kuelekea ofisini kwa Mark, ambako ndiko kilikuwa chumba chake cha kulala. Uso wake ulikuwa umekunjamana kwa tafakuri nzito.

“Sasa ndio nini vile?” Mark Tonto alimuuliza Roman saa moja baadaye wakiwa wamekaa kwenye ile baa iliyokuwa nje ya klabu yao ya ndondi pale Kawe, kisha akaendelea, “...yule askari ana maana gani kuja hapa na kuondoka bila kusema neno?”

Roman aliuma mdomo wake kwa hasira. “Alikuwa anajaribu kunipa ujumbe Mark...”
“Ujumbe gani sasa?”
“Kwamba bado ananifuatilia na kwamba nisisahau onyo alilonipa siku ile nilipotoka gerezani.”
Mark alitikisa kichwa kwa mastaajabu. “Ama hakika huyu mwanamke majinuni...sasa tufanyaje Roman?”
“Sisi tunaendelea na harakati zetu kama kawaida, hakuna kinachobadilika.Hii mikwara ya Inspekta Fatma hainitishi hata kidogo mimi.”

Wiki ya pili ya mashindano ya ubingwa wa mkoa wa ndondi za ridhaa, Kawe boxing club ilipoteza bondia mmoja, na Roman na Chumbi wakasonga mbele kwenye fainali, safari hii Roman akimuangusha mpinzani wake katika dakika ya kwanza tu ya raundi ya nne na ya mwisho. Lilikuwa ni pambano lililojaa hoi hoi na nderemo kwa jinsi Roman alivyokuwa akimchezea yule mpinzani wake, na hatimaye kumuangusha kwenye ile raundi ya mwisho. Sasa Roman alikuwa ni miongoni mwa mabondia wenye mashabiki wengi kabisa katika mashindano yale.

Jioni ile Mark aliandaa sherehe fupi pamoja na mabondia wake kuwapongeza Roman na Chumbi kwa kufikia fainali ambayo ingefanyika katika wiki ifuatayo. Wakiwa katikati ya sherehe zao pale kwenye ile baa iliyokuwa nje ya klabu yao, Mark alinunua gazeti la jioni lililokuwa likipitishwa na mchuuzi pale baa na kumuonesha Roman habari iliyokuwa kwenye ukurasa wa michezo wa gazeti lile.
Deus wa mauaji kukabiliana na Mswazi.

Kichwa cha habari ile kilinadi, na mara moja Roman akawa makini na habari ile, ambayo ilieleza kuwa bingwa wa dunia wa uzito wa Super Middle Deus “deadly” Macha alikuwa akitarajia kuzipiga na bondia kutoka Swaziland katika pambano la kimataifa kutetea ubingwa wake alioupata miezi sita iliyopita. Pambano lile lilipangwa kufanyika mwisho wa wiki ile, siku ya jumamosi katika ukumbi wa PTA jijini.

Habari ile ilileta mjadala baina ya wale mabondia wa ile timu ya Kawe, baadhi ya wale mabondia wakimsifia Deus jinsi alivyo mahiri katika masumbwi, na jinsi alivyokuwa akiwaangusha wapinzani wake, wengine wakitamani siku moja kuwa kama yeye.

Roman na Mark Tonto walitulia kimya akiwasikiliza wale vijana wakimjadili Deus.
“Okay boys, mnaonaje sote tukienda kushuhudia pambano hilo jumamosi hii, eenh?” Hatimaye Mark aliuliza.
Mayowe na shangwe vililipuka kutoka kwa vijana wale, wakiiafiki hoja ile ya Mark kwa mbinja na hoi hoi, wengine wakirukaruka huku wakitupa ngumi hewani na kucheza kibondia kufurahia swala lile.

“Aaah, acheni fujo sasa, ebbo!” Mark aliwaasa wale vijana wake kwa ukali huku akiona wateja wengine pale baa wakionekana kuwashangaa na kukereka kwa mayowe yale.

Roman aliinuka na kuondoka na lile gazeti kuelekea chumbani kwake bila ya kuaga. Mwili ulikuwa ukimtetemeka kwa mchanganyiko wa hamasa na jazba.

***

Siku ya pambano ukumbi wa PTA ulifurika mashabiki wa kitaifa na kimataifa. Baada ya mapambano ya utangulizi hatimaye ulifika wakati ambao hasa watu wote waliofurika pale walikuwa wakiusubiri. Bondia kutoka Swaziland alipanda ulingoni akisindikizwa na kocha na wapambe wake wachache, shangwe kidogo zilisikika,lakini zaidi ilikuwa ni sauti za kuzomea kutoka kwa mashabiki wa Deus. Kisha akaingia Deus mwenyewe akiongozana na kocha na promota wake pamoja na msururu wa wapambe, muziki wa bongo flava maalum wa kumsindikiza ukirindima kutoka kwenye maspika makubwa yaliyotandazwa kila kona ya ukumbi ule, mayowe, vifijo na mbinja vilirindima kila upande, na kadiri zile shangwe zilivyozidi, ndivyo Roman, akiwa miongoni mwa watazamaji waliohudhuria pambano lile pamoja na mabondia wenzake wa Kawe Boxing Club na kocha wao Mark Tonto, alivyoweza kusikia muitiko wa pamoja kutoka pale ukumbini.
“Deus...Deadly...Deus...Deadly...Deus...Deadly...!”

Roman alitulia kimya akitazama kila tukio kwa makini, na kengele ya kuanza pambano ilipogongwa, alishuhudia jinsi Deus akimsulubu mpinzani wake kutoka uswazi kwa namna ambayo ilimfanya aelewe ni kwa nini alifikia hatua ya kuitwa “Deus wa mauaji”. Mswazi alienda chini mara mbili, kwenye raudi ya nne na ya tisa, na alipoenda chini kwa mara ya tatu kwenye raundi ya kumi hakuinuka tena. Kwisha kazi. Deus alikuwa amefanya “mauaji’ kwa mara nyingine.

Ukumbi ulipagawa kwa vifijo. Mashabiki walijaribu kuvamia ulingo, kabla ya kutulizwa na Deus akatangazwa mshindi rasmi. Hapo ukumbi ulilipuka upya, Deus aliinuliwa juu huku akizungusha ngumi hewani kushangalia ushindi wake. Roman alisimama na kuanza kusogea karibu na ule ulingo, Mark Tonto akiwa sambamba naye.
“Vipi Roman...” Mark aliuliza.

“Nataka nimuone vizuri...” Roman alijibu huku akijisukuma mbele na kusimama hatua chache kando ya ule ulingo, akiwa amefumbata mikono kifuani kwake akimtazama yule bingwa wa dunia mtanzania akifurahia ushindi wake. Na ndipo ghafla, katika kuzunguka kwake huku na huko akishangilia ushindi wake ilhali uso wake ukiwa na tabasamu pana, macho ya “Deusdeadly” Macha yalipoangukia kwa Roman akiwa amesimama kando ya ule ulingo akimtazama.

Walionana...uso kwa uso.Ghafla uso wa bingwa wa dunia Deus ulibadilika, na lile tabasamu likafutika, nafasi yake ikichukuliwa na mshangao, kisha kitu kama woga mkubwa, na haraka ule woga ukachukuliwa na ghadhabu. Alijikurupusha na kuteremka kutoka mabegani kwa yule shabiki aliyekuwa amembeba. Katika kufanya hivyo,aliinamisha kichwa chake kuangalia asianguke, na wakati alivyofanya vile, Roman aliweza kumuona Inspekta Fatma akiwa upande wa pili wa ule ulingo.

Yule askari hakuwa akiangalia yale yaliyokuwa yakitendeka ndani ya ule ulingo, bali alikuwa akimtazama Roman kutokea kule alipokuwa amesimama!
“Shit! Inspekta Fatma!” Roman alinong’ona kwa hasira na kujirudisha nyuma akijichanganya kwenye umati wa mashabiki waliokuwepo pale.

“Wapi...wapi?” Mark Tonto alinong’ona kwa wahka, lakini Roman alimshika mkono na kumvutia kule alipokuwa akitowekea, akizidi kujichanganya katikati ya kundi la watu.
“Deusdeadly” Macha, bingwa anayeendelea kutamba na mkanda wake wa dunia katika uzito wa Super Middle, alitoka mbio hadi kwenye ukingo wa ulingo katika ule upande ambao alimuona Roman akiwa amesimama hapo awali, na kuangaza macho yake yaliyojaa wahka eneo lile.
Patupu! Roman hakuwepo!

Badala yake aliona kundi la mashabiki tu wakimshagilia na kumpungia mikono huku nyuso zao zikiwa zimejawa tabasamu. Deus hakuwatilia maanani. Alikuwa akimtafuta Roman katika kundi lile lakini hakumuona tena. Aligeukia upande wa pili wa ulingo ule hali ikawa vilevile, aliranda huku na huko ndani ya ulingo ule akijaribu kumtafuta tena Roman, lakini Roman hakuonekana kabisa machoni mwake. Ilikuwa kama kwamba yule aliyemuona hakuwa Roman bali ni taswira tu iliyojijenga kichwani mwake!

Kwenye kona moja ya ukumbi ule, Master D alimgeukia Kate na kumwambia huku akiinuka kutoka kwenye kiti chake.
“Okay, tunaweza kwenda sasa mrembo wangu...tumeona mengi kwa leo au sivyo?”
“Sana anko...sana tu. Si umeona jinsi uso wake ulivyohamanika alipomuaona Roman? E bwana we! Leo mbona tumeona mambo!” Kate alisema huku naye akiinuka.

*****

Roman alikuwa akikimbia kando ya barabara asubuhi huku akitupa-tupa ngumi hewani mbele yake kama kawaida yake. Asubuhi hii alikuwa peke yake. Ilikuwa ni asubuhi ya siku ya pili baada ya lile pambano la Deus na mswazi. Yeye pambano lake lilikuwa siku ile jioni, ambapo angepanda ulingoni na bondia kutoka timu ya wilaya ya Ilala, kugombea ubingwa wa mkoa katika ndondi za ridhaa. Alikuwa akikimbia katika upande wa barabara ambao ulimuwezesha kuona magari yaliyokuwa yakimjia mbele yake.

Hata hivyo alfajiri ile barabara ile haikuwa na magari mengi, na ndio maana alipenda kukimbia alfajiri. Mbele yake, kiasi cha mita ishirini hivi, gari aina ya Toyota Prado Short Chasis Metallic lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara likiwa limeelekea kule alipokuwa akielekea yeye, lakini upande wa pili wa barabara. Kutokea nyuma yake alisikia mvumo wa gari likielekea kule alipokuwa akikimbilia yeye, lakini hakutilia maanani, alikuwa akiendelea na mazoezi yake tu kama kawaida.

Mvumo wa lile gari lililokuwa likitokea nyuma yake uliongezeka na akahisi kama lile gari lilikuwa likiongeza kasi, na hata wakati wazo lile lilipokuwa likipita kichwani mwake, aliona mlango wa ile Prado iliyokuwa imeegeshwa mbele yake, ambayo sasa ilikuwa umbali wa kama mita tano tu kutoka pale alipokuwa, ukifunguka ghafla na mtu mmoja aliyekuwa amevaa suruali na fulana ya mazoezi akiruka nje na kumpungia mikono kwa wahka huku akipiga kelele, na hapo hapo alilisikia lile gari liliyokuwa nyuma yake likimkaribia huku likizidisha kasi.
Oh, my God! Nagongwa...!

Bila ya kugeuka nyuma, Roman alizidisha kasi ya mbio na hapo hapo alijirusha kwa nguvu kulia kwake na kuangukia kwenye kichaka kilichokuwa kando ya ile barabara. Muda huo huo aliliona gari ndogo likimpita kwa kasi sana usawa wa pale alipokuwa akikimbilia sekunde moja tu iliyopita, alijibiringisha na kusimama wima akilitazama lile gari likiyumba kidogo baada ya kumkosa na kurudi barabarani, likimkosakosa na yule mtu aliyeruka kutoka kwenye ile Prado, ambaye alijirusha upande wa pili wa gari lake lile gari lililomkosa kumgonga likitokomea kwa kasi eneo lile. Yaani lile gari ilihama kutoka upande wake na kumfuata kule alipokuwapo!

Tusi zito lilimtoka Roman, na kutimua mbio kukimbilia pale kwenye ile Prado na kuzunguka upande wa pili huku akitweta. Moyo ulimlipuka na kujikuta akibwata huku akiwa amekodoa macho.
“Wewe!!”

Kate alikuwa amekaa chini kando ya lile gari huku akiwa amejishika mguu wake.
“Unajua kwenye pochi yangu kulikuwa kuna hela mle?” Kate alimwambia huku akitabasamu, ingawa alionekana kama kwamba alikuwa kwenye maumivu makali.

“Ama?” Roman alimshangaa yule binti na kubaki akimkodolea macho, kisha akamtupia swali, “Unasemaje wewe?”
“Jamaa zako walikuwa wanataka kukugonga wale! Na kwa kasi ile wangekuua tu!” Kate alisema tena, akipuuzia lile swali la Roman. Roman alizidi kuchanganyikiwa.
“Jamaa zangu? We’ umewaona waliokuwa kwenye lile gari?”
“Kulikuwa kuna watu wawili, ila sijawaona sura...walikuwa wamekudhamiria wewe haswa!”
“Sasa we’ ulikuwa unafanya nini huku. Na usiniambie kuwa ulikuwa unanitafuta mimi tena!” Roman alimwambia kwa jazba.

“Ndio haswa. Nilikuwa nakuvizia wewe. Na ni bora nilivyofanya hivyo kwani nimekuokoa, kwani kama si mimi kukupigia kelele za kukutahadharisha jamaa wangekugonga wale!”
“Mnh! Kweli...ahsante sana. Lakini...kwa nini ulikuwa unanivizia huku saa hizi?”
“Si nikudai pesa zangu!” Kate alimjibu kwa maskhara huku bado akiwa amefinya uso kwa maumivu. Roman alibaki akimtazama kwa mastaajabu. “We’ unafanya maskhara kwenye kila kitu, eenh?Hebu inuka hapo unieleze vizuri ni nini kinachoendelea hapa?”

“Siwezi...nadhani nimetegua mguu! Nisaidie tafadhali...!” Kate alimwambia huku uso wake ukionesha kuwa alikuwa kwenye maumivu makali. Roman alimsaidia kuinuka, na alipojaribu kutembea tu yule msichana aliachia kiyowe kidogo cha maumivu na kuanza kuanguka tena chini, lakini Roman aliwahi kumdaka kiuno.
“Dah! Nimeumia sana...naomba unisaidie kuingia kwenye gari...” Kate alisema kwa uchungu. Roman alimsaidia na kumuweka nyuma ya usukani.

“Oh, Roman samahani, lakini itabidi uniendeshe, mimi sitaweza, kwani mguu niutumiao kuendeshea ndio ulioumia...” Kate alisema akiwa kwenye maumivu makali. Roman alimtazama yule dada kwa muda na akaona kuwa hakuwa akifanya maskhara.
“Sasa unajuaje kama mi’ naweza kuendesha?” Alimuuliza.
“Oh, come on Roman, mi najua mengi juu yako bwana, kwa hiyo najua kwamba unaweza kuendesha gari...hebu nisaidie tafdhali, nipeleke nyumbani!”

“Nikikusaidia utanieleza kinachokufanya unifuate-fuate namna hii?”
“Of course nitakueleza...leo nd’o nilikuwa nataka tupange siku ya kuonana, lakini ndio yametokea haya...twende tafadhali!” Kate alimjibu huku akijisukumia kwenye kiti cha abiria kule mbele. Roman aliangaza huku na huko, kisha akaingia nyuma ya usukani na kuliondoa lile gari kutoka eneo lile. Njiani Roman alijaribu kuwaza juu ya tukio lile la kukoswa kugongwa, lakini hakuweza kuwaza kitu cha msingi juu ya tukio lile kwani Kate alikuwa akimuongelesha.

“Inaelekea una maadui wengi Roman...mpaka wengine wanataka kukugonga na magari!”
“Hilo halinipi taabu.Linalonipa taabu ni wewe uko upande gani Kate, na unataka nini kwangu?”
“Mnhu! Kuhusu mimi usiwe na taabu. Mi’ niko upande wako, na nd’o maana nikakupigia kelele nilipoona kuwa lile gari lilikuwa linaelekea kukugonga...”Deusdedit Mahunda

“Na ndo maana siku ile ukaja kupekua ofisini kwetu na kunitoroka?” Roman alidakia. Kate alicheka.
“Siku ile ulinishtukiza Roman, sikuwa na namna zaidi ya kukutoroka...I am so sorry...” Kate alimjibu, na kuendelea, “...lakini pesa zangu nazitaka ujue, nilijua siku tukikutana n’takudai tu!”
“Pesa zako zipo na wala sijazitumia, ila sinazo hapa. Sasa je unaweza kuniambia ni nini unachotaka kwangu Kate...kama hilo ni jina lako kweli?”

“Okay...kwanza Kate ni jina langu kweli...kama jinsi Roman lilivyo jina lako la kweli. Na pili...ninachotaka kutoka kwako ni muda wako tu...kuna mtu nataka nikukutanishe naye Roman. Ni muhimu sana kwako na kwake pia!” Kate alimjibu, safari hii uso wake ukiwa umepoteza kabisa maskhara.

“Ni nani huyo unayetaka nikutane naye? Na ana nini ambacho ni muhimu kwangu na kwake?”
“Mimi kazi yangu ni kukutanisha naye tu Roman. Najua leo una pambano la ngumi jioni, unaonaje tukija kuonana nawe baada ya pambano leo usiku pale kwenye ile baa ya pale kwenye klabu yenu?” Kate alisema. Roman alitikisa kichwa kwa mastaajabu.

“Inaelekea unajua mambo mengi juu yangu Kate...why?”
“Labda leo usiku utajua, nikimleta huyo mtu anayetaka kukutana nawe.” Kate alimjibu.
Baada ya hapo Roman hakuongea tena. Aliendesha kimya mpaka alipomfikisha Kate nyumbani kwake. Kate alipomkaribisha ndani hakukubali.

“Sasa utarudi vipi? Ngoja basi nikupe pesa ya teksi...” Kate alimwambia.
“Usijali...n’tarudi kwa mbio tu...si unajua bado nilikua mazoezini?” Roman alimjibu. Kate alichanganyikiwa kidogo, lakini Roman hakumpa muda wa kuongea zaidi. Aliruka nyuma hatua mbili, akageuka, na kuanza kukimbia kimazoezi kurejea kwenye klabu yake ya ndondi.
“Basi sisi tutakuja huko leo usiku, okay?” Kate alimpigia kelele. Roman alimpungia mkono bila ya kugeuka wala kupunguza kasi...

***

Jioni le Roman alipanda ulingoni akiwa na ghadhabu kubwa, ghadhabu ambayo alikuwa ameielekeza kwa yule mtu asiye sura aliyetaka kumgonga makusudi asubuhi ile.
“Nakupa asilimia tisini na tisa Deus anahusika na tukio hilo Roman!” Mark alisema baada ya Roman kumsimulia tukio lile asubuhi ya siku ile.
“Kwa nini unasema hivyo Mark...? Angeweza kuwa mtu mwingine yoyote...” Roman aliuliza, ingawa hata yeye alikuwa na hisia kama alizokuwa nazo Mark.

“Acha hizo Roman! Huyu ni yeye tu! Kwanza jiulize...iweje siku zote jambo hili lisitokee lije kutokea leo baada ya yeye kukuona kwa mara ya kwanza tangu urudi uraiani? Ni yeye bloody swine...ni yeye!” Mark alimjibu kwa jazba.
Ghadhabu zake zilimuishia mpinzani wake pale ulingoni jioni ile, kwani kwa mara ya kwanza tangu arudi tena kwenye ngumi za ridhaa, Roman alitupa makonde mazito kabisa yaliyosukumwa na ghadhabu iliyokuwa ikimchemka mwili mzima. Alisukuma makonde ya nguvu na hasira kiasi kwamba katika raundi ya kwanza tu alishamdondosha chini mpinzani wake mara mbili, na alipomdondosha mara ya tatu katika raundi ile, muamuzi akatangaza Technical Knock-Out, na Roman akaipatia timu yake ya Kawe Boxing Club ubingwa wa wilaya!
Ndani ya dakika tatu tu!

Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi na vifijo, mabondia wenzake walivamia ulingo kwa furaha, naye akajikuta akiinuliwa juu juu, akiwa ameinua juu ngumi kuashiria ushindi wake ilhali sura yake bado ikiwa imefura kwa hasira...

***

“Hongera kwa kunyakua ubingwa Roman...hakika leo umepigana kwa namna tofauti kabisa na mapambano yako yaliyopita...” Dan Dihenga alimwambia mara baada ya kutambulishana na kusalimiana jioni ile.
“Oh, ahsante...kwani ni mapambano yangu gani mengine uliyowahi kuyaona?” Roman alimjibu na kumuuliza huku akimtupia jicho Mark Tonto aliyekuwa pamoja nao pale kwenye meza iliyokuwa kweye kona kabisa ya ile baa iliyokuwa nje ya klabu yao ya ndondi.

“Oh, tumekuwa tukihudhuria mapambano yako yote Roman...” . Master D alimjibu huku akitabsamu, na kuendelea, “...na nd’o maana nakwambia leo umepigana kwa namna tofauti kabisa na mapambano yako yote hayo niliyowahi kuyashuhudia.”

“Mnhu! Ukiniuliza mimi n’takwambia kuwa leo amepigana kwa ghadhabu zaidi kuliko vinginevyo!” Kate alisema huku akimtazama Roman kwa macho ya uchokozi. Muda ulikuwa ni saa mbili za usiku. Kate na Master D walifika pale klabuni kiasi cha saa moja na nusu za jioni na kutulia pale kwenye baa kwa muda, wakisikia shangwe na hoi hoi zilizokuwa zikirindima pale kwenye ile klabu ya ndondi ya akina Roman mpaka wale mabondia wengne walipoondoka na kuwaacha Roman na Mark Tonto pale klabuni. Ndipo Kate, huku akichechemea,alipokwenda kuwabishia hodi na kuwaarifu kuwa walikuwa wameshafika. Ndipo wapojumuika nao pale kwenye ile meza waliyokuwa wamekalia.
“Okay, mnaonaje mkitueleza dhamira ya ujio wenu?” Mark Tonto aliuliza huku akiielekeza kauli yake kwa Master D. Roman alitikisa kichwa kuafiki kauli ya Mark.

“Sawa kabisa...” Dan alisema na kujiweka sawa, kisha akaendelea, “...kama nilivyojitambulisha hapo awali, mi’ naitwa Dan Dihenga...na huyu ni mpwa wangu Kate...”“Na kama nilivyosema hapo awali, jina lako si geni masikioni mwangu Mr. Dihenga...” Mark alisema.
“Yeah, na kama ungekumbuka ni katika mazingira gani ulipata kulisikia jina langu, moja kwa moja ungejua dhima ya ujio wetu huu...”

“Sasa unaonaje ukituweka wazi Mr. Dihenga, maana mi’ nahitaji kujipumzisha...” Roman, bingwa mpya wa ngumi za ridhaa wa uzito wa Super Middle kwa mkoa wa Dar es Salaam, alisema.
“Very well Roman. Nitaenda moja kwa moja kwenye swala lililo kichwani mwangu...” Master D alisema na kumtazama Roman kwa muda, kisha akamgeukia Mark Tonto, na kumrudia tena Roman, “...nataka nikuingize kwenye ndondi za kulipwa Roman...nataka niwe promota wako...”

Moyo ulimpasuka Roman kwa kauli ile, na akafinya macho kidogo kwa umakini huku akimtazama yule mtu aliyeketi mbele yake, kisha akamtupia jicho Mark, moyo ukimwenda mbio. Hapo hapo Dan akamgeukia Mark haraka.
“Eenh, sina nia ya kukuvua nafasi yako kwa Roman Mark...la hasha, najua wewe ndiye umekuwa promota na kocha wake, lakini...”
“Nimeshakukumbuka sasa!” Mark alisema kwa hamasa, akimwangalia kwa mtazamo mpya yule mtu huku akimuoneshea kidole. Dan Dihenga alimuinulia nyusi na kutamtazama kama kwamba akimwambia “alaa?”
“Wewe ni Dan Dihenga!” Mark alisema huku bado akiwa na hali ya mshangao. Roman aliachia mguno huku akimtazama Dan kwa makini.

“Hilo hata mimi nalijua Mr. Tondolo...” Master D alimjibu huku akitabasamu, lakini Mark alikuwa kama kwamba hajamsikia, akaendelea,“Wewe ni promota mkubwa wa ndondi nchini...!”
Master D alibetua mabega yake tu bila ya kusema neno. Bado Mark alikuwa akimtazama kwa ule ung’amuzi mpya uliomshukia baada ya kumkumbuka yule mtu.

acha!” Mark alimalizia, na hata pale alipomalizia kauli ile, Roman alitoa mguno mkubwa wa mshangao na kumtumbulia macho yule jamaa aliye mbele yao, na kumtupia jicho Kate, ambaye alimtawanyia tabasamu pana ambalo kama kwamba lilikuwa likimwambia “...sasa ulikuwa unatarajia nini?”
“There you are!” Dan Dihenga alisema huku akitupa mikono hewani kumaanisha kuwa sasa Mark alikuwa amesema hasa kilichokuwa ndicho.

Kimya kilichukua nafasi wakati wale watu wakitazamana, kila mmoja akiuweka sawa akilini mwake ufahamu ule mpya uliotokana na ung’amuzi wa uhalisia wa Dan Dihenga.
“Kwa nini?” Hatimaye Roman aliuliza taratibu.
“Ndio kazi yangu Roman!” Dan alimjibu, na kuendelea, “Mimi kama promota wa ndondi, ni kazi yangu kutafuta mabondia wazuri na kuwapromoti katika mchezo huu mpaka wafikie mafanikio yanayohitajika kwao, kwangu na kwa mchezo huu wa ndondi hapa nchini na duniani kote. Hiyo ndio azma yangu kubwa katika ku-promoti ndondi...”

“Kwa nini umtake Roman...?” Mark aliuliza. Dan alimtazama kama kwamba alikuwa ameuliza swali la kijinga.
“Roman ni bondia mzuri! Promota yeyote ajuaye kazi yake akimuona tu Roman apiganavyo, hatosita kum-promoti. Nami ni promota nijuaye kazi yangu Mr. Tondolo...naijua vizuri sana!” Alimjibu. Muda wote huu Kate alikuwa kimya tu akifuatilia mazungumzo yale.

“Come on Mr. Dihenga! Kuna mabondia wengi tu wazuri hapa nchini ambao wana uwezo wa kufanya makubwa kama watapata promota kama wewe. Unataka kuniambia kuwa hao wote hukuwaona ila Roman tu?” Mark alimuuliza kwa hamasa. Dihenga alimtazama, kisha akamtupia macho Roman.
“Jibu swali bwana Dihenga...why me...and why now?” Roman alimsisitizia swali la Mark, akimaanisha kwa nini amteue yeye na kwa nini amteue wakati ule. Dan aliachia cheko hafifu na kutikisa kichwa kwa mastaajabu.

“Mbona napata picha kama kwamba mnaniona adui ndugu zangu?” Hatimaye aliuliza.
“Nadhani hapo mwanzo ulisema kuwa utaenda moja kwa moja kwenye swala lililo kichwani mwako Mr. Dihenga, sasa mbona tena unaaza kusua-sua? Nimesema mapema kuwa mi’ nataka kwenda kujipumzisha. Kwa hiyo kama mtaniwia radhi ndugu zangu, mi’ naenda kulala!” Roman alisema na kuanza kuinuka. Haraka sana Kate ulimdaka mkono na kumzuia.

“Hatuendi hivyo mzee!” Alimwambia huku akimtazama usoni. Roman alibaki akimtazama yule binti kwa mshangao, na kabla hajauliza Kate akamwambia, “Hapa huondoki mpaka unirejeshee pesa zangu!”
“Ati nini wewe?” Roman alimaka huku akiuchomoa mkono wake kwa nguvu kutoka kwenye himaya ya yule binti.
“Achana na Kate Roman, tuongee mambo ya maana. Kaa kitini tafadhali!” Dan alimwambia kwa utulivu. Roman alimtazama Kate kwa muda, kisha akamgeukia Dan.

“Nimekuuliza swali jepesi sana Mr. Dihenga...why me? Umeshindwa kujibu kwa hiyo mi’ naona...”
“Kwa sababu ni wewe pekee ndiye unayeweza kumvua ubingwa Deusdelity Macha, Roman!” Dan Dihenga alimkatisha kwa kumjibu kwa utulivu ilhali bado akimtazama moja kwa moja usoni.

“Atii???” Mark Tonto alimaka huku akiinuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia, wakati huo huo, Roman akajikuta akiketi kitini huku akiacha kinywa wazi na akimtazama yule mtu kama kwamba ndio kwanza alikuwa anamuona.
“Ndio!” Dihenga alithibitisha jibu lake huku akimtulizia macho Mark kwa muda kkabla ya kuyarudisha tena kwa Roman.
“Ni kweli kuwa kuna mabondia wengi wazuri hapa nchini. Lakini nakuhakikishia kuwa hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kumuangusha Deus...” Dihenga aliendelea kutetea hoja yake. Mark na Roman walitazamana. Wazi hili halikuwa kabisa miongoni mwa matarajio yao.

“Isipokuwa wewe Roman!” Dan alimalizia huku akimuoneshea kidole Roman.
Kimya kilichukua nafasi kwenye ile meza.
“Kwa nini unataka Deus aangushwe Mr. Dihenga?” Hatimaye Mark alimuuliza, ingawa tayari jibu alikuwa nalo. Dan Dihenga alibadilika kidogo, uso wake ukionesha ghadhabu yenye kufukuta.
“Mimi ndiye niliyemfikisha mahala pa kutambulika kimataifa kwenye ndondi mshenzi yule...lakini akathubutu kunigeuka na kunitolea kebehi na kashfa. Nataka nimuoneshe kuwa kama mimi ndiye niliyemfikisha hapo alipo mpaka hao anaowaona ndio mapromota wanaomfaa wakamuona, basi mimi ndiye nitakayemporomosha!” Dan Dihenga alisema.
“Na unataka kunitumia mimi katika hicho kisasi chako binafsi?” Roman alimuuliza.

“Hapana Roman. Mimi na wewe tunahitajiana katika kumfikisha Deus mahala panapomstahili...”
“Nini kinachokufanya uamini kuwa mi’ nataka kushirikiana nawe katika hilo?” Roman aliuliza. Dan alitabasamu kidogo.
“Najua mengi juu yako na Deus, Roman...mengi. Hivyo najua kuwa kwa namna moja au nyingine nawe unahitaji kumfikisha Deus mahala panapomsatahili...na pale alipo sasa sipo panapomstahili. Sote twalijua hilo!”
Duh! Roman na Mark walichoka.

“Unaelewa nini juu yangu na Deus wewe?” Roman alikuja juu. Dan hakufanya haraka kumjibu. Badala yake alimuita mhudumu na kumuomba bili ya vinywaji waliyoagiza pale mezani. Alipewa bili naye akalipa.
“Najua kiasi cha kutosha kunihakikishia kuwa mimi na wewe hivi sasa tuna lengo moja kuhusu Deus, nalo ni kumtia adabu. Sababu zetu za kutaka kufanya hivyo zinaweza kuwa tofauti, lakini hakika lengo letu laweza kuwa moja...na...naamini sote tunahitajiana katika hili!” Dan alimjibu baada ya yule mhudumu kuondoka.
“Si kweli. Sikuhitaji...hatuhitaji mtu yeyote. Tunajitosheleza kama tulivyo. Naona mkutano huu umekwisha!” Roman alisema.

“Kwa hiyo hukatai kuwa nawe una kisasi na Deus?”
“Sijui unaongelea nini...” Roman alianza, lakini Dan Dihenga alimkatisha.
“Wazee, hilo ndilo nililokuja nalo kwenu. Kitu ninachosema ni kwamba iwapo tutakubaliana, mimi nataka niwe promota wako katika ngumi za kulipwa. Nitakulipa pesa nzuri, nitakupatia vifaa vyote na mahitaji yote muhimu kwa professional boxer, nitakupatia nyumba nzuri ya kuishi, na nitakupa nafasi ya kuuchukua ubingwa ulio mikononi mwa Deus mbabaishaji hivi sasa...” akamgeukia Mark Tonto, “...na kwako, nitakuajiri kama kocha wa bondia wangu Roman, na nitakulipa kwa kadiri ya makubaliano tutakayoafikiana...ambayo nakuhakikishia kuwa yatakuwa ni makubaliano mazuri sana Mark. Wewe ni kocha mzuri, na najua kuwa unajua upiganaji wa mabondia wote wawili hawa.”

Alimalizia na kubaki akiwatazama wale watu wawili wenye azma ya siri. Si Roman wala Mark aliyeongea, hivyo Dan akamalizia, “Hiyo ndiyo kete yangu kwenu. Naomba muifikirie kwa makini sana, na baada ya siku tatu nitamtuma mpwa wangu kuja kupata jibu lenu la mwisho. Kama bado hamtakubaliana nami basi nitawaacha na hamsini zenu nami nitaendelea na hamsini zangu. Usiku mwema!”

Dan na Kate waliinuka kwa pamoja na kuanza kuondoka, wakiwaacha Roman na Mark wakiwa vinywa wazi.
“Kate!” Roman aliita. Kate na Dan walisimama na kugeuka. Roman alitoa ile pochi ya yule dada ambayo ilikuwa mfukoni mwake muda wote, na kuiweka juu ya meza huku akimtazama kwa hasira. Kwisha kufanya hivyo alimuashiria Mark na kwa pamoja waliinuka na kuondoka, ile pochi ikibaki pale mezani. Kate aliirudia pochi yake kwa mwendo wa kuchechemea...

***
Usiku ule Roman na Mark walichelewa sana kulala. Walibaki pale ofisini wakijadili juu ya ule ujio wa promota Dan Dihenga kwa undani. Hofu kubwa ya Roman ilikuwa ni iwapo Dan alikuwa ametumwa na Deus aje kumchimba undani wake, au iwapo atakuwa ametumwa na Inspekta Fatma.

“Kwa hayo yote mawili mimi nakataa Roman. Ni kweli kuwa Dan Dihenga ni promota wa ndondi, na ni kweli kuwa alikuwa promota wa Deus...na ni kweli kuwa Deus alimsaliti...hivyo ana kila sababu ya kuwa na kinyongo naye.” Mark alisema.
“Kwa hiyo...?”

“Kwa hiyo hawezi kuwa kibaraka wa Deus...yule mtu ana kinyongo kikubwa na Deus...si umesoma makala nilizokukusanyia kwenye lile faili? Walifikia hadi hatua ya kutaka kupelekana mahakamani bwana!”
“Ni kweli...na sasa nakumbuka kuwa hata jina lake nililisoma kwenye lile faili...” Roman aliafiki, kisha hapo hapo akauliza, “...na vipi kuhusu Inspekta Fatma...hawezi kumtumia?”

“Kwa lengo gani? Hali ilivyo, Dihenga ndiye ambaye anaweza kuwa kwenye nafasi ya kumtumia Inspekta Fatma na si vinginevyo. Nadhani nia ya Dihenga ni hiyo hiyo aliyotueleza...anataka akupromoti wewe ili umnyang’anye Deus ubingwa...hiyo ni njia yake ya kumlipizia kisasi. Swala ni je, sisi...wewe...uko tayari kushirikiana naye?”
Kimya kilitawala, kisha Roman akarudia tena kauli ambayo tayari alikuwa ameshaitumia zaidi ya mara tatu mle ndani tangu akina Kate waondoke.

“Lakini...inaelekea hawa akina Kate wanajua sana habari zangu...hii mimi hainipi amani kabisa Mark!”
“Sasa basi ni bora tuwe nao sambamba Roman...!” Mark alisema.
“Ili?”
“Ili tuweze kujua ni nini hasa wajuacho kuhusu wewe... na sisi tuweze kuwajua wao zaidi...nadhani tukubaliane na wazo la Mr. Dihenga Roman. Kwani sisi hatutapoteza lolote zaidi ya kunufaika...kwanza tutaweza kutimiza azma yetu, pili tutaweza kuitimiza azma hiyo katika mazingira yaliyo bora zaidi...sasa hivi Roman huna kipato chochote, kujiunga na Dihenga kutakupatia makazi bora, vifaa bora zaidi vya mazoezi, na pesa nzuri...nami pia nitanufaika kama kocha wako. Hii ni nafasi nzuri kwetu Roman...ni sawa na nyota ya jaha!” Mark alisema na kubaki akimtazama Roman kwa muda, kisha akamalizia kwa sauti ya chini, “Hiyo ni kama bado una nia ya kuendelea na ile azma yako Roman.”

“Azma iko pale pale Mark...iko pale pale!” Roman alimjibu haraka bila hata ya kusita.
“Basi na tukubaliane na ofa ya Dihenga...we have nothing to lose (hatuna cha kupoteza) kwa hii ofa Roman!” Mark alimwambia. Siku tatu baadaye, Kate alifuata jibu.
“Mwambie Dihenga tumekubali...no problem!” Roman alimwambia bila kupoteza muda. Hii ilikuwa ni taarifa tamu sana kwa Kate na Dan Dihenga.

*****

Maisha ya Roman yalibadilika ghafla. Dan alitimiza kila aliloahidi. Kwa kuhofia jaribio jingine la kumuua Roman, Dan alimhamishia Roman Bagamoyo, ambako alimpangia nyumba ndogo lakini nzuri na yenye kujitosheleza. Mark Tonto kama kocha wake alilazimika awe anaishi baina ya Bagamoyo na Dar. Kila siku akifanya safari za Bagamoyo asubuhi na kurudi jioni, baadhi ya siku akilala huko huko. Huko kazi ilikuwa ni moja tu, nayo ilikuwa ni mazoezi makali. Dan alimpatia Roman vifaa vyote muhimu vya mazoezi, na pale kwenye nyumba aliyompangia alimtengea chumba maalum cha mazoezi (Gym) ambacho kilikuwa na kila kitu.
Kwa miezi mitatu mfululizo Roman alijichimbia Bagamoyo akijijenga kibondia. Mark Tonto alikuwa naye muda wote huo ingawa siku nyingine alikuwa akirejea Dar kuwa na familia yake. Kate na Dan nao walikuwa wakimtembelea na kumtazama akifanya mazoezi, wakitumia sehemu ya muda wao kutazama mapambano ya Deusdelity Macha kwenye mikanda ya video. Na katika miezi mitatu ile, Roman na Kate waliondokea kujenga ukaribu, na hata siku nyingine Kate alikuwa akienda kule Bagamoyo peke yake na kukutana na Roman, wakitembea pwani na kuongea mambo mengi na kujuana zaidi.
Ndani ya miezi mitatu ile, hakuonana kabisa na Inspekta Fatma, isipokuwa siku moja tu alipoletewa salamu na Mark kuwa Inspekta Fatma alifika pale kwenye klabu yao ya Kawe na kumuulizia. Kwa kuwa hata wale mabondia wa Mark pale klabuni hawakujua Roman alipo, hawakuwa na msaada wowote kwake.
Roman aliendelea na mazoezi yake, na Dan hakuishia hapo katika kumjenga zaidi. Pamoja na kuwa na Mark kama kocha, pia alimletea makocha kutoka nje ya nchi ambao walikuja kumuongezea mbinu zaidi za ndondi, ikiwa ni pamoja na namna ya kubadili namna ya upiganaji akiwa ulingoni kutokana na aina ya upiganaji wa mpinzani wake.
Na baada ya miezi hii mitatu ya mazoezi makali na ya nguvu, Roman alikuwa tayari kuingia katika ulingo wa ndondi za kulipwa, kama professional boxer.

***

Dan Dihenga alimuandalia Roman pambano lake la kwanza kama bondia wa kulipwa mwezi mmoja baada ya Roman kujinadi kuwa yuko tayari kuingia rasmi ulingoni, ambapo alimpatia mpinzani kutoka afrika kusini. Katika pambano hili Roman alikuwa na nafasi ya kujivunia milioni tano za kitanzania akishinda, na milioni mbili akishindwa. Dan hakutaka kulinadi sana pambano hili kwenye vyombo vya habari, na waliondoka kimya kimya kwenda Afrika Kusini, msafara wao ukimjumuisha Dan, Roman, Mark, Kate na tabibu mmoja. Pamoja nao alikuwamo mwandishi wa habari mmoja. Mark alimuuliza Dan sababu ya kutolinadi ipasavyo pambano lile la kwanza la Roman.
“Roman hahitaji kunadiwa Mark...Roman atajinadi mwenyewe baada ya kufanya mauaji huko sauzi...we’ subiri tu, utaona!” Dan alimjibu wakiwa angani kuelekea Johannesburg. Usiku wa pambano jijini Johannesburg, Roman alitoa kipigo cha mbwa mwizi kwa mwenyeji wake, na mnamo raundi ya nane, kocha wa mpinzani wake alilazimika kutupa taulo ulingoni kumnusuru bondia wake!
Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi kutoka kwa watanzania wachache waishio Afrika Kusini waliokuwapo pale ukumbini, Roman akiinuliwa juu juu na watanzania wale. Ilikuwa ni furaha isiyo kifani kwa kambi ya Roman kule ugenini. Mara moja habari zilirudi nyumbani, mwandishi wa habari aliyesafiri na akina Roman akituma habari nyumbani usiku ule ule kwa simu, na akituma picha kadhaa za jinsi Roman alivyokuwa akimsulubu mwenyeji wake kwa mtandao wa intaneti. Usiku ule ulikuwa ni usiku wa tafrija kwa kambi ya Roman jijini Johannesburg. Walirejea Tanzania siku iliyofuata, na kukuta habari za pambano la Roman nchini Afrika kusini zikiwa zimetapakaa jijini,na waandishi zaidi wa habari wakiwasubiri uwanja wa ndege. Na ndipo hapa ambapo Dan Dihenga alimpomnadi Roman kuwa ndiye bondia wake mpya. Waandishi walimtupia maswali kadhaa naye kama promota mzoefu alitumia nafasi hiyo kumnadi vizuri sana bondia wake. Alipohojiwa na waandishi juu ya ushindi wake ule, Roman alisema kwa utulivu kabisa kuwa ushindi ule haukuwa ajabu kwake, kwani alijua kuwa atashinda. Ndipo mwandishi mmoja alipomtupia swali Dan.“Bwana Dihenga, je ndio unataka kutuambia kuwa Roman amekuja kuchukua nafasi ya Deusdelity Macha, bondia wako wa zamani na ambaye ndiye bingwa wa dunia hivi sasa?”
Bila ya kusita, Dan Dihenga alimjibu yule muandishi, “Nijuavyo mimi Roman ni bondia bora kuliko bondia mwingine yeyote hapa nchini katika uzito wake...hivyo siwezi kusema kuwa kaja kuchukua nafasi ya mtu yeyote hapa, labda tu niseme kuwa amekuja kuchukua nafasi yake inayomstahili!”
“Una maana gani kwa kauli hiyo bwana Dihenga?” Waandishi kadhaa walimrukia kwa swali hilo. Dan hakujibu kitu zaidi ya hapo. Alimuongoza bondia wake kwenye gari na kuondoka eneo lile, akiwaacha wale waandishi wakijijazia majibu yao wenyewe. Habari ya pambano lake la afrika kusini ilimfanya Roman awe gumzo kwa wengi nchini.
Lakini pia ilimrejesha tena Inspekta Fatma katika maisha yake.

ITAENDELEA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi : Bondia
Sehemu Ya Tatu (3)

Baada ya lile pambano lake na mzungu kutoka Hungary, Macha alipambana na bondia kutoka Afrika ya Kusini mjini Johannesburg, ambako alimtawanya taya msauzi huyo na kuondoka mshindi. Sifa za bondia “Deus-deadly” Macha sasa zilikuwa zimeenea duniani kote, na Tanzania ikawa moja ya nchi za kutazamika katika ulimwengu wa ndondi.
Kwenye faili kulikuwa kuna habari juu ya mzozo baina ya Deus na promota wake, mzozo ambao kwa mujibu habari za magazeti, ulitokana na Deus kutoridhika na mapambano anayoandaliwa na promota wake huyo. Mwisho wa habari ile ilielezwa kuwa Deus alivunja mkataba na promota huyo na kujiunga na promota mwingine ambaye alionekana kuwa na mtazamao wa maendeleo zaidi kwa Deus kuliko yule promota wake wa awali aliyemtoa jeshini. (Roman alitikisa kichwa tena kwa masikitko, kisha akendelea kusoma).

Ndipo, miezi sita baada ya lile tukio la kutishiana baina yake na yule bingwa wa dunia wa wakati ule, promota mpya wa Deus alipokubali pambano baina ya bondia wake na bingwa yule, pambano likiwa ni la kugombea mkanda ule wa dunia. Kufikia hapa Roman alikuwa anasoma kwa hamasa, akiwa amejawa udadisi wa kujua kilichojiri kwenye pambano lile baina ya Bondia Deusdelity Macha na yule bingwa wa dunia wa wakati ule...

Lilikuwa ni pambano lililotangazwa na kunadiwa sana, na siku ya tukio ukumbi ulifurika kuliko ilivyowahi kutokea. Kengele ya kuanza pambano ilipogongwa, wapinzani wale waliendeana kwa bashasha na azma ya pambano la kukata na shoka. Na hapa ndipo Deus alipoonesha kuwa kweli yeye alikuwa muuaji kwani kufikia raundi ya kumi na moja bingwa wa dunia aliyekuwa akitetea ubingwa wake alikuwa ameshavunjwa mwamba wa pua na akitokwa damu kama maji.
Refa alilazimika kusimamisha pambano na Deus akatawazwa ubingwa wa dunia katika uzito wa Super Middle kwa Technical Knock Out.

Picha ya mwisho ndani ya faili lile ilimuonesha Deus akimvugumizia konde la kulia katikati ya uso mpinzani wake, ngumi ambayo ndiyo iliyomvunja mwamba wa pua na kumvua ubingwa. Hii ilikuwa ni miezi sita iliyopita...

Roman alishusha pumzi ndefu huku akilifunika lile faili. Aliketi kwa muda mrefu pale kwenye kiti akiwa amejawa na tafakuri nzito, kisha akainuka na kutoka nje. Alienda kuketi kwenye kona moja ndani ya ile baa iliyokuwa nje ya ile klabu na kuagiza kinywaji. Uso wake ulikuwa umekunjamana kwa mawazo mazito. Muda mfupi baadaye, Makongoro “Mark Tonto” Tondolo aliingia eneo lile na kuanza kuelekea kule kwenye klabu yake ya ndondi. Roman alimpigia mbinja, na Mark alipogeuka, alimpungua mkono.

“Haya niambie nini kilitokea jana Roman...Inspekta Fatma alikuibukia hadi huku?” Mark alisema huku akiketi kwenye kiti mbele ya Roman. Roman aliita muhudumu na Mark akaagiza kinywaji.
“Bora ingekua Inspekta Fatma Mark, angalau yeye najua ni nini kinachomsumbua”
“Ama! Ni nani kumbe?”

Roman akamsimulia juu ya tukio baina yake na yule mwanadada aliyejitambulisha kwa jina la Kate. Mark alichanganyikiwa.
“Mnh!Kate? Kate huyu wa wapi? Na alikuwa anataka nini hasa?” Alijikuta akiuliza maswali ambayo tayari Roman alishajiuliza. Roman alimbetulia mabega na kubaki akimtazama tu. Kimya kilichukua nafasi baina yao kwa muda, kisha Mark akaongea.
“Okay, sasa unadhani tufanyaje juu ya hii hali?”
“Tusifanye kitu...tuendelee na mipango yetu kama tulivyopanga.”
“Khah! Sasa na huyu Kate...?”

“Kate hatuzuii kufanya lolote. Yeye atakuja tena tu, na safari hiyo hatonitoka kirahisi...” Roman alisema kwa utulivu. Lakini Mark hakuwa na utulivu hata kidogo katika swala lile.

“Hii ni mbaya sana Roman...mbaya sana!” Alisema kwa hamasa. Roman alibaki akimtazama akiwa kimya. “Sasa unajuaje iwapo huyu...huyu...Kate, si askari aliyetumwa na Inspekta Fatma Roman? Unajua huyu Fatma mi’ hanipi amani kabisa?” Alizidi kusema kwa wasiwasi. Roman alimtazama yule rafiki yake wa makamu na kumpiga ngumi ya maskhara begani.
“Relax kocha, okay? Haitusaidii kuumiza kichwa kwa jambo ambalo hatuna hakika nalo kwa sasa bwana. Lolote ambalo yule dada alikuwa analitaka kwangu, hakulipata, hivyo lazima atarudi tena, na hapo ndipo tutajua. Kwa sasa tunaendelea na mambo yetu kama kawaida.” Alimwambia kwa kirefu. Mark alimtazama kwa muda, kisha huku bado uso wake ukiwa makini, alimwambia; “Tutaendelea na mipango yetu kama kawaida, lakini hatutakiwi ku-relax hata kidogo juu ya swala la huyu Kate, Roman...mpaka tujue ni nini hasa anataka kutoka kwako, okay?”
“Okay, kocha wangu...”

Kimya kilichukua nafasi kwa muda wakati watu wale wawili wakiendelea kunywa vinywaji vyao, kila mmoja akiwa na mawazo yake.
“Kesho ndio mnaanza mechi za kugombea ubingwa wa wilaya, sio?” Hatimaye Roman aliuliza.
“Yeah Roman. Naona vijana wako katika hali na ari nzuri, natumai tutashinda tu...”
Kimya kilitawala tena.
“Jina langu limo kwenye orodha ya mabondia waliosajiliwa kwenye timu yako?” Roman aliuliza tena.

“Kama tulivyopanga Roman. Nilikusajili tangu wakati uko gerezani, na kama bado una nia ya kuendelea na azma uliyoweka, basi nawe utapanda ulingoni pindi ukiwa tayari...”
“Azma iko pale pale Makongoro. Ila itabidi vijana wako wafanye kazi ya kuvuka katika ngazi hii ya wilaya, mimi nitaingia kwenye ngazi ya mkoa...nahitaji mazoezi zaidi...” Roman alimjibu, kisha akaendelea, “...unadhani wanaweza kutuvusha?”
“Ninajua kuwa wanaweza kutuvusha...” Mark alijibu kwa kujiamini.

****

Kwa wiki mbili mfululizo baada ya siku ile, Roman alijishughulisha katika mazoezi mazito sana ya ndondi. Akikimbia umbali mrefu kila alfajiri na kurudi kwenye ile klabu yao ya ndondi kwa ajili ya mazoezi zaidi ya viungo na ya ulingoni chini ya usimamizi makini wa kocha wake wa muda mrefu, Mark Tonto. Timu yao ya ndondi haikufanikiwa kuchukua ubingwa wa wilaya, lakini ilifanikiwa kusonga hadi ngazi ya mkoa kwa kutoka washindi wa pili katika ngazi ile ya wilaya.

Na katika wiki mbili zile, pamoja na kuweka umakini wa hali ya juu kila alipokuwa, Roman hakuonana tena na Kate wala Inspekta Fatma. Mazoezi yaliendelea kwa nguvu, na kadiri alivyokuwa akiendelea na mazoezi, ndivyo alivyozidi kujihisi akirudia kwenye uwezo wake wa ngumi aliokuwa nao hapo awali...kabla hajapigwa marufuku kushiriki katika mchezo ule aliokuwa akiupenda sana, na kujikuta akikaa nje na ulingo kwa miaka mingi, miwili kati ya hiyo akiwa gerezani.
Kadiri siku zilivyosogea, ndivyo alivyozidi kuhisi msisimko wa ajabu wakati utashi wa mchezo ule ukimtambaa ndani ya mishipa yake ya damu. Mchezo wa ngumi...ndondi...mchezo wa mabondia. Naye sasa alikuwa anajiandaa kuingia tena ulingoni kushiriki mchezo ule.

Wengi walikuwa wakishiriki mchezo ule kwa ajili ya kutaka sifa na umaarufu, wakati wengine walikuwa wakishiriki kwa ajili ya pesa tu, ilhali wengine ilikuwa ni kwa ajili ya pesa na umaarufu na sifa. Na wachache miongoni mwa mabondia walikuwa wakishiriki mchezo ule kwa upenzi tu wa michezo kama ilivyokuwa kwake kabla hajapigwa marufuku... na kabla ya kifungo chake.

Lakini safari hii Roman alikuwa anarudi ulingoni kwa ajili ya kutimiza azma. Azma ya hatari. Azma iliyokuwa ikifumfukuta moyoni kwa miaka miwili. Azma iliyogubikwa usiri mkubwa.
***

Roman alikuwa akikimbia huku akitupa ngumi mbele yake na kuruka huku na huko kibondia kando ya barabara. Alikuwa amevaa suruali ya mazoezi na fulana nchinjo ya mazoezi ambayo ilikuwa na kofia iliyofunika kichwa chake. Usoni alikuwa amevaa miwani maalum ya kumkinga na upepo na vumbi. Mark Tonto alikuwa akimfuta nyuma taratibu akiwa kwenye baiskeli. Walikuwa kwenye mazoezi makali, ikiwa ni siku tatu tu kabla ya kuanza kwa mashindano ya ndondi za ridhaa kugombea ubingwa wa mkoa, safari hii Roman naye akiwa miongoni mwa mabondia wa Kawe Boxing Club watakaopanda ulingoni.

Wakiwa katika harakati zao zile za mazoezi, hawakuitilia maanani kabisa Toyota Prado short chasis yenye rangi ya metallic iliyokuwa imeegeshwa kando ya barabara ile waliyozoea kuitumia kila asubuhi kwa ajili ya mazoezi yao makali.
Ndani ya ile gari, Master D na Kate walikuwa wakiwatazama kwa utulivu wawili wale wakiendelea na mazoezi yao. Kate alimtazama yule jamaa aliyetoka gerezani siku kadhaa zilizopita jinsi akitupa masumbwi hewani namna ile huku akiranda kulia na kushoto kistadi wakati akikimbia kando ya ile barabara, na uso wake ukafanya tabasamu dogo.

“Enhe? Nini kinafuata sasa Master D?” Alimuuliza yule mtu mzima aliyekuwa naye ndani ile gari huku bado akiwaangalia akina Roman. Ilikuwa ni zamu ya Dan kuachia tabasamu dogo, kisha akaliondoa gari kando ya barabara, akawapita akina Roman na kuondoka eneo lile.
“Kinachofuata ni kukabiliana na Roman sasa...nadhani mambo yanaenda kama tutakavyo...” Master D alimjibu.
“Okay...lini sasa?” Kate alihoji.
“Soon...very soon...(muda mfupi sana ujao) mrembo wangu!”

***
Mashindano ya ndondi kugombea ubingwa wa mkoa wa Dar es Salaam yalichukua muda wa wiki tatu. Katika wiki ya kwanza Kawe boxing club ilipandisha mabondia wanne ulingoni, watatu wakishinda na mmoja akipoteza pambano. Roman alikuwa miongoni mwa watatu walioshinda kwa kumuangusha mpinzani wake katika raundi pili tu ya pambano, na hapo hapo kujipatia mashabiki kwa jinsi alivyokuwa akipigana.

Wakiwa mazoezini ndani ya ile klabu yao mwisho wa ile wiki ya kwanza,Roman alipata ugeni asioutarajia. Siku hiyo alikuwa ulingoni akipigana na bondia mwenzake ikiwa ni sehemu ya mazoezi, mkufunzi wao Mark Tonto akiwa kama muamuzi na wakati huo huo akitoa mafunzo. Mabondia wengine wa timu ile ya ndondi walikuwa nje ya ulingo wakifuatilia pambano lile la mazoezi kwa makini, wote sasa wakiwa wamemkubali Roman kama mwenzao na kama bondia mwenye uwezo mkubwa miongoni mwao.

Yule bondia alikuwa akimjia kwa ngumi kali za mfululizo, na Roman alikuwa akiruka huku na kule, akitupatupa miguu yake mbele na nyuma kiufundi huku akimsogezea uso mpinzani wake na kuurudisha nyuma kila jamaa alipojaribu kumtupia konde, hoi hoi na vifijo vikirindima kutoka kwa mabondia wenzao waliokuwa nje ya ulingo. Jamaa alikuwa akimjia kwa kasi, Roman aliyumba kushoto na kubonyea kidogo huku akimsogelea, wakati jamaa alipotupa konde kali la kushoto lililopita hewani, na Roman aliibuka na upper cut iliyotua sawia kidevuni kwa mpinzani wake na kumpeleka chini kama mzigo.

Shangwe ziliibuka kutoka kwa mabondia wenzao, wakati Roman akimsaidia bondia mwenzake kuinuka kutoka pale chini.
“Pole partner...sikuipa nguvu zangu zote hata hivyo...kwa hiyo hutadhurika sana!” Alimwambia yule bondia huku akimsaidia kusimama.

“Sasa huo ndio upiganaji Roman!” Mark alisema kwa hamasa huku akiwasogelea wale wapiganaji wake, na kumgeukia yule kijana aliyepelekwa chini kwa konde la Roman, “...na ule si upiganaji! We’ umenaswa kwenye mtego wa Roman, Chumbi... anakuchezeshea uso nawe unautamani uso, unasahau kujikinga...” Mark alikuwa akisema, lakini hapo macho yake yaliangukia nje ya ulingo, na kutulia huko kwa muda, sentensi yake ikibaki ikielea hewani. Alimtupia jicho la haraka Roman, na kuyarudisha tena macho yake kule nje ya ulingo. Roman aligeuka kufuata ulelekeo wa macho ya Mark, kama jinsi ambavyo na wale mabondia wengine walikuwepo pale walivyofanya.

Inspekta Fatma alikuwa amesimama nyuma kabisa ya ule ukmbi wao wa mazoezi, akiwa amevaa mavazi yake ya kiaskari, kofia yake akiwa ameikumbatia chini ya kwapa lake la kushoto. Kwa mkono wake wa kulia alikuwa ameshika fimbo yake ya kiaskari ambayo alikuwa akiipiga-piga taratibu kwenye tumbo la kiganja chake cha kushoto. Uso wake uliokuwa umefunikwa kwa miwani myeusi ulikuwa ukimtazama Roman moja kwa moja kule ulingoni.

“Sasa huyu anataka nini tena hapa?” Mark Tonto alisema kwa sauti ya chini huku akimtazama yule askari wa kike. Roman alimuacha Chumbi na kuusogelea ukingo wa ule ulingo na kusimama akiwa ameshika kamba ya ulingo ule huku akimtazama Inspekta Fatma. Walibaki wakitazamana kwa muda, kisha Inspekta Fatma aliweka kofia yake kichwani taratibu, na bila ya kusema neno lolote, aligeuka na kuondoka.Hivyo tu!

Roman na Mark walitazamana, lakini hakuna yeyote kati yao aliyesema neno, kisha Mark akawageukia wale mabondia wake.
“Alrigh, alright, alright, Hey! Haya tunaendelea, tumeshaona jinsi Roman na Chumbi walivyojifua...sasa nataka niwaone Dulla na Kibwe ulingoni...” Alisema huku akipiga makofi kuwahamasisha wachezaji wake.
Roman aliteremka ulingoni, na taratibu aliondoka eneo lile kuelekea ofisini kwa Mark, ambako ndiko kilikuwa chumba chake cha kulala. Uso wake ulikuwa umekunjamana kwa tafakuri nzito.

“Sasa ndio nini vile?” Mark Tonto alimuuliza Roman saa moja baadaye wakiwa wamekaa kwenye ile baa iliyokuwa nje ya klabu yao ya ndondi pale Kawe, kisha akaendelea, “...yule askari ana maana gani kuja hapa na kuondoka bila kusema neno?”
Roman aliuma mdomo wake kwa hasira. “Alikuwa anajaribu kunipa ujumbe Mark...”
“Ujumbe gani sasa?”
“Kwamba bado ananifuatilia na kwamba nisisahau onyo alilonipa siku ile nilipotoka gerezani.”
Mark alitikisa kichwa kwa mastaajabu. “Ama hakika huyu mwanamke majinuni...sasa tufanyaje Roman?”
“Sisi tunaendelea na harakati zetu kama kawaida, hakuna kinachobadilika.Hii mikwara ya Inspekta Fatma hainitishi hata kidogo mimi.”

Wiki ya pili ya mashindano ya ubingwa wa mkoa wa ndondi za ridhaa, Kawe boxing club ilipoteza bondia mmoja, na Roman na Chumbi wakasonga mbele kwenye fainali, safari hii Roman akimuangusha mpinzani wake katika dakika ya kwanza tu ya raundi ya nne na ya mwisho. Lilikuwa ni pambano lililojaa hoi hoi na nderemo kwa jinsi Roman alivyokuwa akimchezea yule mpinzani wake, na hatimaye kumuangusha kwenye ile raundi ya mwisho.

Sasa Roman alikuwa ni miongoni mwa mabondia wenye mashabiki wengi kabisa katika mashindano yale. Jioni ile Mark aliandaa sherehe fupi pamoja na mabondia wake kuwapongeza Roman na Chumbi kwa kufikia fainali ambayo ingefanyika katika wiki ifuatayo. Wakiwa katikati ya sherehe zao pale kwenye ile baa iliyokuwa nje ya klabu yao, Mark alinunua gazeti la jioni lililokuwa likipitishwa na mchuuzi pale baa na kumuonesha Roman habari iliyokuwa kwenye ukurasa wa michezo wa gazeti lile.
Deus wa mauaji kukabiliana na Mswazi.

Kichwa cha habari ile kilinadi, na mara moja Roman akawa makini na habari ile, ambayo ilieleza kuwa bingwa wa dunia wa uzito wa Super Middle Deus “deadly” Macha alikuwa akitarajia kuzipiga na bondia kutoka Swaziland katika pambano la kimataifa kutetea ubingwa wake alioupata miezi sita iliyopita. Pambano lile lilipangwa kufanyika mwisho wa wiki ile, siku ya jumamosi katika ukumbi wa PTA jijini.

Habari ile ilileta mjadala baina ya wale mabondia wa ile timu ya Kawe, baadhi ya wale mabondia wakimsifia Deus jinsi alivyo mahiri katika masumbwi, na jinsi alivyokuwa akiwaangusha wapinzani wake, wengine wakitamani siku moja kuwa kama yeye.

Roman na Mark Tonto walitulia kimya akiwasikiliza wale vijana wakimjadili Deus.
“Okay boys, mnaonaje sote tukienda kushuhudia pambano hilo jumamosi hii, eenh?” Hatimaye Mark aliuliza.
Mayowe na shangwe vililipuka kutoka kwa vijana wale, wakiiafiki hoja ile ya Mark kwa mbinja na hoi hoi, wengine wakirukaruka huku wakitupa ngumi hewani na kucheza kibondia kufurahia swala lile.

“Aaah, acheni fujo sasa, ebbo!” Mark aliwaasa wale vijana wake kwa ukali huku akiona wateja wengine pale baa wakionekana kuwashangaa na kukereka kwa mayowe yale.

Roman aliinuka na kuondoka na lile gazeti kuelekea chumbani kwake bila ya kuaga. Mwili ulikuwa ukimtetemeka kwa mchanganyiko wa hamasa na jazba.

***

Siku ya pambano ukumbi wa PTA ulifurika mashabiki wa kitaifa na kimataifa. Baada ya mapambano ya utangulizi hatimaye ulifika wakati ambao hasa watu wote waliofurika pale walikuwa wakiusubiri. Bondia kutoka Swaziland alipanda ulingoni akisindikizwa na kocha na wapambe wake wachache, shangwe kidogo zilisikika,lakini zaidi ilikuwa ni sauti za kuzomea kutoka kwa mashabiki wa Deus.

Kisha akaingia Deus mwenyewe akiongozana na kocha na promota wake pamoja na msururu wa wapambe, muziki wa bongo flava maalum wa kumsindikiza ukirindima kutoka kwenye maspika makubwa yaliyotandazwa kila kona ya ukumbi ule, mayowe, vifijo na mbinja vilirindima kila upande, na kadiri zile shangwe zilivyozidi, ndivyo Roman, akiwa miongoni mwa watazamaji waliohudhuria pambano lile pamoja na mabondia wenzake wa Kawe Boxing Club na kocha wao Mark Tonto, alivyoweza kusikia muitiko wa pamoja kutoka pale ukumbini.
“Deus...Deadly...Deus...Deadly...Deus...Deadly...!”

Roman alitulia kimya akitazama kila tukio kwa makini, na kengele ya kuanza pambano ilipogongwa, alishuhudia jinsi Deus akimsulubu mpinzani wake kutoka uswazi kwa namna ambayo ilimfanya aelewe ni kwa nini alifikia hatua ya kuitwa “Deus wa mauaji”. Mswazi alienda chini mara mbili, kwenye raudi ya nne na ya tisa, na alipoenda chini kwa mara ya tatu kwenye raundi ya kumi hakuinuka tena. Kwisha kazi. Deus alikuwa amefanya “mauaji’ kwa mara nyingine.

Ukumbi ulipagawa kwa vifijo. Mashabiki walijaribu kuvamia ulingo, kabla ya kutulizwa na Deus akatangazwa mshindi rasmi. Hapo ukumbi ulilipuka upya, Deus aliinuliwa juu huku akizungusha ngumi hewani kushangalia ushindi wake. Roman alisimama na kuanza kusogea karibu na ule ulingo, Mark Tonto akiwa sambamba naye.
“Vipi Roman...” Mark aliuliza.

“Nataka nimuone vizuri...” Roman alijibu huku akijisukuma mbele na kusimama hatua chache kando ya ule ulingo, akiwa amefumbata mikono kifuani kwake akimtazama yule bingwa wa dunia mtanzania akifurahia ushindi wake. Na ndipo ghafla, katika kuzunguka kwake huku na huko akishangilia ushindi wake ilhali uso wake ukiwa na tabasamu pana, macho ya “Deusdeadly” Macha yalipoangukia kwa Roman akiwa amesimama kando ya ule ulingo akimtazama.

Walionana...uso kwa uso.Ghafla uso wa bingwa wa dunia Deus ulibadilika, na lile tabasamu likafutika, nafasi yake ikichukuliwa na mshangao, kisha kitu kama woga mkubwa, na haraka ule woga ukachukuliwa na ghadhabu. Alijikurupusha na kuteremka kutoka mabegani kwa yule shabiki aliyekuwa amembeba. Katika kufanya hivyo,aliinamisha kichwa chake kuangalia asianguke, na wakati alivyofanya vile, Roman aliweza kumuona Inspekta Fatma akiwa upande wa pili wa ule ulingo.

Yule askari hakuwa akiangalia yale yaliyokuwa yakitendeka ndani ya ule ulingo, bali alikuwa akimtazama Roman kutokea kule alipokuwa amesimama!
“Shit! Inspekta Fatma!” Roman alinong’ona kwa hasira na kujirudisha nyuma akijichanganya kwenye umati wa mashabiki waliokuwepo pale.

“Wapi...wapi?” Mark Tonto alinong’ona kwa wahka, lakini Roman alimshika mkono na kumvutia kule alipokuwa akitowekea, akizidi kujichanganya katikati ya kundi la watu.
“Deusdeadly” Macha, bingwa anayeendelea kutamba na mkanda wake wa dunia katika uzito wa Super Middle, alitoka mbio hadi kwenye ukingo wa ulingo katika ule upande ambao alimuona Roman akiwa amesimama hapo awali, na kuangaza macho yake yaliyojaa wahka eneo lile.
Patupu! Roman hakuwepo!

Badala yake aliona kundi la mashabiki tu wakimshagilia na kumpungia mikono huku nyuso zao zikiwa zimejawa tabasamu. Deus hakuwatilia maanani. Alikuwa akimtafuta Roman katika kundi lile lakini hakumuona tena. Aligeukia upande wa pili wa ulingo ule hali ikawa vilevile, aliranda huku na huko ndani ya ulingo ule akijaribu kumtafuta tena Roman, lakini Roman hakuonekana kabisa machoni mwake. Ilikuwa kama kwamba yule aliyemuona hakuwa Roman bali ni taswira tu iliyojijenga kichwani mwake!

Kwenye kona moja ya ukumbi ule, Master D alimgeukia Kate na kumwambia huku akiinuka kutoka kwenye kiti chake.
“Okay, tunaweza kwenda sasa mrembo wangu...tumeona mengi kwa leo au sivyo?”
“Sana anko...sana tu. Si umeona jinsi uso wake ulivyohamanika alipomuaona Roman? E bwana we! Leo mbona tumeona mambo!” Kate alisema huku naye akiinuka.

*****

Roman alikuwa akikimbia kando ya barabara asubuhi huku akitupa-tupa ngumi hewani mbele yake kama kawaida yake. Asubuhi hii alikuwa peke yake. Ilikuwa ni asubuhi ya siku ya pili baada ya lile pambano la Deus na mswazi. Yeye pambano lake lilikuwa siku ile jioni, ambapo angepanda ulingoni na bondia kutoka timu ya wilaya ya Ilala, kugombea ubingwa wa mkoa katika ndondi za ridhaa. Alikuwa akikimbia katika upande wa barabara ambao ulimuwezesha kuona magari yaliyokuwa yakimjia mbele yake. Hata hivyo alfajiri ile barabara ile haikuwa na magari mengi, na ndio maana alipenda kukimbia alfajiri. Mbele yake, kiasi cha mita ishirini hivi, gari aina ya Toyota Prado Short Chasis Metallic lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara likiwa limeelekea kule alipokuwa akielekea yeye, lakini upande wa pili wa barabara. Kutokea nyuma yake alisikia mvumo wa gari likielekea kule alipokuwa akikimbilia yeye, lakini hakutilia maanani, alikuwa akiendelea na mazoezi yake tu kama kawaida.

Mvumo wa lile gari lililokuwa likitokea nyuma yake uliongezeka na akahisi kama lile gari lilikuwa likiongeza kasi, na hata wakati wazo lile lilipokuwa likipita kichwani mwake, aliona mlango wa ile Prado iliyokuwa imeegeshwa mbele yake, ambayo sasa ilikuwa umbali wa kama mita tano tu kutoka pale alipokuwa, ukifunguka ghafla na mtu mmoja aliyekuwa amevaa suruali na fulana ya mazoezi akiruka nje na kumpungia mikono kwa wahka huku akipiga kelele, na hapo hapo alilisikia lile gari liliyokuwa nyuma yake likimkaribia huku likizidisha kasi.
Oh, my God! Nagongwa...!

Bila ya kugeuka nyuma, Roman alizidisha kasi ya mbio na hapo hapo alijirusha kwa nguvu kulia kwake na kuangukia kwenye kichaka kilichokuwa kando ya ile barabara. Muda huo huo aliliona gari ndogo likimpita kwa kasi sana usawa wa pale alipokuwa akikimbilia sekunde moja tu iliyopita, alijibiringisha na kusimama wima akilitazama lile gari likiyumba kidogo baada ya kumkosa na kurudi barabarani, likimkosakosa na yule mtu aliyeruka kutoka kwenye ile Prado, ambaye alijirusha upande wa pili wa gari lake lile gari lililomkosa kumgonga likitokomea kwa kasi eneo lile. Yaani lile gari ilihama kutoka upande wake na kumfuata kule alipokuwapo!

Tusi zito lilimtoka Roman, na kutimua mbio kukimbilia pale kwenye ile Prado na kuzunguka upande wa pili huku akitweta. Moyo ulimlipuka na kujikuta akibwata huku akiwa amekodoa macho.
“Wewe!!”
Kate alikuwa amekaa chini kando ya lile gari huku akiwa amejishika mguu wake.
“Unajua kwenye pochi yangu kulikuwa kuna hela mle?” Kate alimwambia huku akitabasamu, ingawa alionekana kama kwamba alikuwa kwenye maumivu makali.

“Ama?” Roman alimshangaa yule binti na kubaki akimkodolea macho, kisha akamtupia swali, “Unasemaje wewe?”
“Jamaa zako walikuwa wanataka kukugonga wale! Na kwa kasi ile wangekuua tu!” Kate alisema tena, akipuuzia lile swali la Roman. Roman alizidi kuchanganyikiwa.

“Jamaa zangu? We’ umewaona waliokuwa kwenye lile gari?”
“Kulikuwa kuna watu wawili, ila sijawaona sura...walikuwa wamekudhamiria wewe haswa!”
“Sasa we’ ulikuwa unafanya nini huku. Na usiniambie kuwa ulikuwa unanitafuta mimi tena!” Roman alimwambia kwa jazba.

“Ndio haswa. Nilikuwa nakuvizia wewe. Na ni bora nilivyofanya hivyo kwani nimekuokoa, kwani kama si mimi kukupigia kelele za kukutahadharisha jamaa wangekugonga wale!”
“Mnh! Kweli...ahsante sana. Lakini...kwa nini ulikuwa unanivizia huku saa hizi?”
“Si nikudai pesa zangu!” Kate alimjibu kwa maskhara huku bado akiwa amefinya uso kwa maumivu. Roman alibaki akimtazama kwa mastaajabu. “We’ unafanya maskhara kwenye kila kitu, eenh?Hebu inuka hapo unieleze vizuri ni nini kinachoendelea hapa?”

“Siwezi...nadhani nimetegua mguu! Nisaidie tafadhali...!” Kate alimwambia huku uso wake ukionesha kuwa alikuwa kwenye maumivu makali. Roman alimsaidia kuinuka, na alipojaribu kutembea tu yule msichana aliachia kiyowe kidogo cha maumivu na kuanza kuanguka tena chini, lakini Roman aliwahi kumdaka kiuno.
“Dah! Nimeumia sana...naomba unisaidie kuingia kwenye gari...” Kate alisema kwa uchungu. Roman alimsaidia na kumuweka nyuma ya usukani.

“Oh, Roman samahani, lakini itabidi uniendeshe, mimi sitaweza, kwani mguu niutumiao kuendeshea ndio ulioumia...” Kate alisema akiwa kwenye maumivu makali. Roman alimtazama yule dada kwa muda na akaona kuwa hakuwa akifanya maskhara.
“Sasa unajuaje kama mi’ naweza kuendesha?” Alimuuliza.
“Oh, come on Roman, mi najua mengi juu yako bwana, kwa hiyo najua kwamba unaweza kuendesha gari...hebu nisaidie tafdhali, nipeleke nyumbani!”

“Nikikusaidia utanieleza kinachokufanya unifuate-fuate namna hii?”
“Of course nitakueleza...leo nd’o nilikuwa nataka tupange siku ya kuonana, lakini ndio yametokea haya...twende tafadhali!” Kate alimjibu huku akijisukumia kwenye kiti cha abiria kule mbele. Roman aliangaza huku na huko, kisha akaingia nyuma ya usukani na kuliondoa lile gari kutoka eneo lile. Njiani Roman alijaribu kuwaza juu ya tukio lile la kukoswa kugongwa, lakini hakuweza kuwaza kitu cha msingi juu ya tukio lile kwani Kate alikuwa akimuongelesha.
“Inaelekea una maadui wengi Roman...mpaka wengine wanataka kukugonga na magari!”

“Hilo halinipi taabu.Linalonipa taabu ni wewe uko upande gani Kate, na unataka nini kwangu?”
“Mnhu! Kuhusu mimi usiwe na taabu. Mi’ niko upande wako, na nd’o maana nikakupigia kelele nilipoona kuwa lile gari lilikuwa linaelekea kukugonga...”Deusdedit Mahunda

“Na ndo maana siku ile ukaja kupekua ofisini kwetu na kunitoroka?” Roman alidakia. Kate alicheka.
“Siku ile ulinishtukiza Roman, sikuwa na namna zaidi ya kukutoroka...I am so sorry...” Kate alimjibu, na kuendelea, “...lakini pesa zangu nazitaka ujue, nilijua siku tukikutana n’takudai tu!”

“Pesa zako zipo na wala sijazitumia, ila sinazo hapa. Sasa je unaweza kuniambia ni nini unachotaka kwangu Kate...kama hilo ni jina lako kweli?”
“Okay...kwanza Kate ni jina langu kweli...kama jinsi Roman lilivyo jina lako la kweli. Na pili...ninachotaka kutoka kwako ni muda wako tu...kuna mtu nataka nikukutanishe naye Roman. Ni muhimu sana kwako na kwake pia!” Kate alimjibu, safari hii uso wake ukiwa umepoteza kabisa maskhara.

“Ni nani huyo unayetaka nikutane naye? Na ana nini ambacho ni muhimu kwangu na kwake?”
“Mimi kazi yangu ni kukutanisha naye tu Roman. Najua leo una pambano la ngumi jioni, unaonaje tukija kuonana nawe baada ya pambano leo usiku pale kwenye ile baa ya pale kwenye klabu yenu?” Kate alisema. Roman alitikisa kichwa kwa mastaajabu.

“Inaelekea unajua mambo mengi juu yangu Kate...why?”
“Labda leo usiku utajua, nikimleta huyo mtu anayetaka kukutana nawe.” Kate alimjibu.
Baada ya hapo Roman hakuongea tena. Aliendesha kimya mpaka alipomfikisha Kate nyumbani kwake. Kate alipomkaribisha ndani hakukubali.

“Sasa utarudi vipi? Ngoja basi nikupe pesa ya teksi...” Kate alimwambia.
“Usijali...n’tarudi kwa mbio tu...si unajua bado nilikua mazoezini?” Roman alimjibu. Kate alichanganyikiwa kidogo, lakini Roman hakumpa muda wa kuongea zaidi. Aliruka nyuma hatua mbili, akageuka, na kuanza kukimbia kimazoezi kurejea kwenye klabu yake ya ndondi.
“Basi sisi tutakuja huko leo usiku, okay?” Kate alimpigia kelele. Roman alimpungia mkono bila ya kugeuka wala kupunguza kasi...

***

Jioni le Roman alipanda ulingoni akiwa na ghadhabu kubwa, ghadhabu ambayo alikuwa ameielekeza kwa yule mtu asiye sura aliyetaka kumgonga makusudi asubuhi ile.
“Nakupa asilimia tisini na tisa Deus anahusika na tukio hilo Roman!” Mark alisema baada ya Roman kumsimulia tukio lile asubuhi ya siku ile.
“Kwa nini unasema hivyo Mark...? Angeweza kuwa mtu mwingine yoyote...” Roman aliuliza, ingawa hata yeye alikuwa na hisia kama alizokuwa nazo Mark.

“Acha hizo Roman! Huyu ni yeye tu! Kwanza jiulize...iweje siku zote jambo hili lisitokee lije kutokea leo baada ya yeye kukuona kwa mara ya kwanza tangu urudi uraiani? Ni yeye bloody swine...ni yeye!” Mark alimjibu kwa jazba.

Ghadhabu zake zilimuishia mpinzani wake pale ulingoni jioni ile, kwani kwa mara ya kwanza tangu arudi tena kwenye ngumi za ridhaa, Roman alitupa makonde mazito kabisa yaliyosukumwa na ghadhabu iliyokuwa ikimchemka mwili mzima. Alisukuma makonde ya nguvu na hasira kiasi kwamba katika raundi ya kwanza tu alishamdondosha chini mpinzani wake mara mbili, na alipomdondosha mara ya tatu katika raundi ile, muamuzi akatangaza Technical Knock-Out, na Roman akaipatia timu yake ya Kawe Boxing Club ubingwa wa wilaya!

Ndani ya dakika tatu tu!
Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi na vifijo, mabondia wenzake walivamia ulingo kwa furaha, naye akajikuta akiinuliwa juu juu, akiwa ameinua juu ngumi kuashiria ushindi wake ilhali sura yake bado ikiwa imefura kwa hasira...

***

“Hongera kwa kunyakua ubingwa Roman...hakika leo umepigana kwa namna tofauti kabisa na mapambano yako yaliyopita...” Dan Dihenga alimwambia mara baada ya kutambulishana na kusalimiana jioni ile.
“Oh, ahsante...kwani ni mapambano yangu gani mengine uliyowahi kuyaona?” Roman alimjibu na kumuuliza huku akimtupia jicho Mark Tonto aliyekuwa pamoja nao pale kwenye meza iliyokuwa kweye kona kabisa ya ile baa iliyokuwa nje ya klabu yao ya ndondi.

“Oh, tumekuwa tukihudhuria mapambano yako yote Roman...” . Master D alimjibu huku akitabsamu, na kuendelea, “...na nd’o maana nakwambia leo umepigana kwa namna tofauti kabisa na mapambano yako yote hayo niliyowahi kuyashuhudia.”

“Mnhu! Ukiniuliza mimi n’takwambia kuwa leo amepigana kwa ghadhabu zaidi kuliko vinginevyo!” Kate alisema huku akimtazama Roman kwa macho ya uchokozi. Muda ulikuwa ni saa mbili za usiku. Kate na Master D walifika pale klabuni kiasi cha saa moja na nusu za jioni na kutulia pale kwenye baa kwa muda, wakisikia shangwe na hoi hoi zilizokuwa zikirindima pale kwenye ile klabu ya ndondi ya akina Roman mpaka wale mabondia wengne walipoondoka na kuwaacha Roman na Mark Tonto pale klabuni. Ndipo Kate, huku akichechemea,alipokwenda kuwabishia hodi na kuwaarifu kuwa walikuwa wameshafika. Ndipo wapojumuika nao pale kwenye ile meza waliyokuwa wamekalia.

“Okay, mnaonaje mkitueleza dhamira ya ujio wenu?” Mark Tonto aliuliza huku akiielekeza kauli yake kwa Master D. Roman alitikisa kichwa kuafiki kauli ya Mark.
“Sawa kabisa...” Dan alisema na kujiweka sawa, kisha akaendelea, “...kama nilivyojitambulisha hapo awali, mi’ naitwa Dan Dihenga...na huyu ni mpwa wangu Kate...”“Na kama nilivyosema hapo awali, jina lako si geni masikioni mwangu Mr. Dihenga...” Mark alisema.

“Yeah, na kama ungekumbuka ni katika mazingira gani ulipata kulisikia jina langu, moja kwa moja ungejua dhima ya ujio wetu huu...”
“Sasa unaonaje ukituweka wazi Mr. Dihenga, maana mi’ nahitaji kujipumzisha...” Roman, bingwa mpya wa ngumi za ridhaa wa uzito wa Super Middle kwa mkoa wa Dar es Salaam, alisema.

“Very well Roman. Nitaenda moja kwa moja kwenye swala lililo kichwani mwangu...” Master D alisema na kumtazama Roman kwa muda, kisha akamgeukia Mark Tonto, na kumrudia tena Roman, “...nataka nikuingize kwenye ndondi za kulipwa Roman...nataka niwe promota wako...”

Moyo ulimpasuka Roman kwa kauli ile, na akafinya macho kidogo kwa umakini huku akimtazama yule mtu aliyeketi mbele yake, kisha akamtupia jicho Mark, moyo ukimwenda mbio. Hapo hapo Dan akamgeukia Mark haraka.
“Eenh, sina nia ya kukuvua nafasi yako kwa Roman Mark...la hasha, najua wewe ndiye umekuwa promota na kocha wake, lakini...”

“Nimeshakukumbuka sasa!” Mark alisema kwa hamasa, akimwangalia kwa mtazamo mpya yule mtu huku akimuoneshea kidole. Dan Dihenga alimuinulia nyusi na kutamtazama kama kwamba akimwambia “alaa?”
“Wewe ni Dan Dihenga!” Mark alisema huku bado akiwa na hali ya mshangao. Roman aliachia mguno huku akimtazama Dan kwa makini.

“Hilo hata mimi nalijua Mr. Tondolo...” Master D alimjibu huku akitabasamu, lakini Mark alikuwa kama kwamba hajamsikia, akaendelea,“Wewe ni promota mkubwa wa ndondi nchini...!”
Master D alibetua mabega yake tu bila ya kusema neno. Bado Mark alikuwa akimtazama kwa ule ung’amuzi mpya uliomshukia baada ya kumkumbuka yule mtu.

“Wewe...wewe...ndiye promota wa zamani wa Deusdelity Macha!” Mark alimalizia, na hata pale alipomalizia kauli ile, Roman alitoa mguno mkubwa wa mshangao na kumtumbulia macho yule jamaa aliye mbele yao, na kumtupia jicho Kate, ambaye alimtawanyia tabasamu pana ambalo kama kwamba lilikuwa likimwambia “...sasa ulikuwa unatarajia nini?”
“There you are!” Dan Dihenga alisema huku akitupa mikono hewani kumaanisha kuwa sasa Mark alikuwa amesema hasa kilichokuwa ndicho.

Kimya kilichukua nafasi wakati wale watu wakitazamana, kila mmoja akiuweka sawa akilini mwake ufahamu ule mpya uliotokana na ung’amuzi wa uhalisia wa Dan Dihenga.
“Kwa nini?” Hatimaye Roman aliuliza taratibu.

“Ndio kazi yangu Roman!” Dan alimjibu, na kuendelea, “Mimi kama promota wa ndondi, ni kazi yangu kutafuta mabondia wazuri na kuwapromoti katika mchezo huu mpaka wafikie mafanikio yanayohitajika kwao, kwangu na kwa mchezo huu wa ndondi hapa nchini na duniani kote. Hiyo ndio azma yangu kubwa katika ku-promoti ndondi...”
“Kwa nini umtake Roman...?” Mark aliuliza. Dan alimtazama kama kwamba alikuwa ameuliza swali la kijinga.
“Roman ni bondia mzuri! Promota yeyote ajuaye kazi yake akimuona tu Roman apiganavyo, hatosita kum-promoti. Nami ni promota nijuaye kazi yangu Mr. Tondolo...naijua vizuri sana!” Alimjibu. Muda wote huu Kate alikuwa kimya tu akifuatilia mazungumzo yale.

“Come on Mr. Dihenga! Kuna mabondia wengi tu wazuri hapa nchini ambao wana uwezo wa kufanya makubwa kama watapata promota kama wewe. Unataka kuniambia kuwa hao wote hukuwaona ila Roman tu?” Mark alimuuliza kwa hamasa. Dihenga alimtazama, kisha akamtupia macho Roman.
“Jibu swali bwana Dihenga...why me...and why now?” Roman alimsisitizia swali la Mark, akimaanisha kwa nini amteue yeye na kwa nini amteue wakati ule. Dan aliachia cheko hafifu na kutikisa kichwa kwa mastaajabu.

“Mbona napata picha kama kwamba mnaniona adui ndugu zangu?” Hatimaye aliuliza.
“Nadhani hapo mwanzo ulisema kuwa utaenda moja kwa moja kwenye swala lililo kichwani mwako Mr. Dihenga, sasa mbona tena unaaza kusua-sua? Nimesema mapema kuwa mi’ nataka kwenda kujipumzisha. Kwa hiyo kama mtaniwia radhi ndugu zangu, mi’ naenda kulala!” Roman alisema na kuanza kuinuka. Haraka sana Kate ulimdaka mkono na kumzuia.

“Hatuendi hivyo mzee!” Alimwambia huku akimtazama usoni. Roman alibaki akimtazama yule binti kwa mshangao, na kabla hajauliza Kate akamwambia, “Hapa huondoki mpaka unirejeshee pesa zangu!”
“Ati nini wewe?” Roman alimaka huku akiuchomoa mkono wake kwa nguvu kutoka kwenye himaya ya yule binti.
“Achana na Kate Roman, tuongee mambo ya maana. Kaa kitini tafadhali!” Dan alimwambia kwa utulivu. Roman alimtazama Kate kwa muda, kisha akamgeukia Dan.

“Nimekuuliza swali jepesi sana Mr. Dihenga...why me? Umeshindwa kujibu kwa hiyo mi’ naona...”
“Kwa sababu ni wewe pekee ndiye unayeweza kumvua ubingwa Deusdelity Macha, Roman!” Dan Dihenga alimkatisha kwa kumjibu kwa utulivu ilhali bado akimtazama moja kwa moja usoni.

“Atii???” Mark Tonto alimaka huku akiinuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia, wakati huo huo, Roman akajikuta akiketi kitini huku akiacha kinywa wazi na akimtazama yule mtu kama kwamba ndio kwanza alikuwa anamuona.
“Ndio!” Dihenga alithibitisha jibu lake huku akimtulizia macho Mark kwa muda kkabla ya kuyarudisha tena kwa Roman.
“Ni kweli kuwa kuna mabondia wengi wazuri hapa nchini. Lakini nakuhakikishia kuwa hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kumuangusha Deus...” Dihenga aliendelea kutetea hoja yake. Mark na Roman walitazamana. Wazi hili halikuwa kabisa miongoni mwa matarajio yao.

“Isipokuwa wewe Roman!” Dan alimalizia huku akimuoneshea kidole Roman.
Kimya kilichukua nafasi kwenye ile meza.
“Kwa nini unataka Deus aangushwe Mr. Dihenga?” Hatimaye Mark alimuuliza, ingawa tayari jibu alikuwa nalo. Dan Dihenga alibadilika kidogo, uso wake ukionesha ghadhabu yenye kufukuta.

“Mimi ndiye niliyemfikisha mahala pa kutambulika kimataifa kwenye ndondi mshenzi yule...lakini akathubutu kunigeuka na kunitolea kebehi na kashfa. Nataka nimuoneshe kuwa kama mimi ndiye niliyemfikisha hapo alipo mpaka hao anaowaona ndio mapromota wanaomfaa wakamuona, basi mimi ndiye nitakayemporomosha!” Dan Dihenga alisema.
“Na unataka kunitumia mimi katika hicho kisasi chako binafsi?” Roman alimuuliza.

“Hapana Roman. Mimi na wewe tunahitajiana katika kumfikisha Deus mahala panapomstahili...”
“Nini kinachokufanya uamini kuwa mi’ nataka kushirikiana nawe katika hilo?” Roman aliuliza. Dan alitabasamu kidogo.
“Najua mengi juu yako na Deus, Roman...mengi. Hivyo najua kuwa kwa namna moja au nyingine nawe unahitaji kumfikisha Deus mahala panapomsatahili...na pale alipo sasa sipo panapomstahili. Sote twalijua hilo!”
Duh! Roman na Mark walichoka.

“Unaelewa nini juu yangu na Deus wewe?” Roman alikuja juu. Dan hakufanya haraka kumjibu. Badala yake alimuita mhudumu na kumuomba bili ya vinywaji waliyoagiza pale mezani. Alipewa bili naye akalipa.
“Najua kiasi cha kutosha kunihakikishia kuwa mimi na wewe hivi sasa tuna lengo moja kuhusu Deus, nalo ni kumtia adabu. Sababu zetu za kutaka kufanya hivyo zinaweza kuwa tofauti, lakini hakika lengo letu laweza kuwa moja...na...naamini sote tunahitajiana katika hili!” Dan alimjibu baada ya yule mhudumu kuondoka.
“Si kweli. Sikuhitaji...hatuhitaji mtu yeyote. Tunajitosheleza kama tulivyo. Naona mkutano huu umekwisha!” Roman alisema.
“Kwa hiyo hukatai kuwa nawe una kisasi na Deus?”
“Sijui unaongelea nini...” Roman alianza, lakini Dan Dihenga alimkatisha.
“Wazee, hilo ndilo nililokuja nalo kwenu. Kitu ninachosema ni kwamba iwapo tutakubaliana, mimi nataka niwe promota wako katika ngumi za kulipwa. Nitakulipa pesa nzuri, nitakupatia vifaa vyote na mahitaji yote muhimu kwa professional boxer, nitakupatia nyumba nzuri ya kuishi, na nitakupa nafasi ya kuuchukua ubingwa ulio mikononi mwa Deus mbabaishaji hivi sasa...” akamgeukia Mark Tonto, “...na kwako, nitakuajiri kama kocha wa bondia wangu Roman, na nitakulipa kwa kadiri ya makubaliano tutakayoafikiana...ambayo nakuhakikishia kuwa yatakuwa ni makubaliano mazuri sana Mark. Wewe ni kocha mzuri, na najua kuwa unajua upiganaji wa mabondia wote wawili hawa.” Alimalizia na kubaki akiwatazama wale watu wawili wenye azma ya siri.

Si Roman wala Mark aliyeongea, hivyo Dan akamalizia, “Hiyo ndiyo kete yangu kwenu. Naomba muifikirie kwa makini sana, na baada ya siku tatu nitamtuma mpwa wangu kuja kupata jibu lenu la mwisho. Kama bado hamtakubaliana nami basi nitawaacha na hamsini zenu nami nitaendelea na hamsini zangu. Usiku mwema!”
Dan na Kate waliinuka kwa pamoja na kuanza kuondoka, wakiwaacha Roman na Mark wakiwa vinywa wazi.
“Kate!” Roman aliita. Kate na Dan walisimama na kugeuka. Roman alitoa ile pochi ya yule dada ambayo ilikuwa mfukoni mwake muda wote, na kuiweka juu ya meza huku akimtazama kwa hasira. Kwisha kufanya hivyo alimuashiria Mark na kwa pamoja waliinuka na kuondoka, ile pochi ikibaki pale mezani. Kate aliirudia pochi yake kwa mwendo wa kuchechemea...

***
Usiku ule Roman na Mark walichelewa sana kulala. Walibaki pale ofisini wakijadili juu ya ule ujio wa promota Dan Dihenga kwa undani. Hofu kubwa ya Roman ilikuwa ni iwapo Dan alikuwa ametumwa na Deus aje kumchimba undani wake, au iwapo atakuwa ametumwa na Inspekta Fatma.

“Kwa hayo yote mawili mimi nakataa Roman. Ni kweli kuwa Dan Dihenga ni promota wa ndondi, na ni kweli kuwa alikuwa promota wa Deus...na ni kweli kuwa Deus alimsaliti...hivyo ana kila sababu ya kuwa na kinyongo naye.” Mark alisema.
“Kwa hiyo...?”

“Kwa hiyo hawezi kuwa kibaraka wa Deus...yule mtu ana kinyongo kikubwa na Deus...si umesoma makala nilizokukusanyia kwenye lile faili? Walifikia hadi hatua ya kutaka kupelekana mahakamani bwana!”
“Ni kweli...na sasa nakumbuka kuwa hata jina lake nililisoma kwenye lile faili...” Roman aliafiki, kisha hapo hapo akauliza, “...na vipi kuhusu Inspekta Fatma...hawezi kumtumia?”

“Kwa lengo gani? Hali ilivyo, Dihenga ndiye ambaye anaweza kuwa kwenye nafasi ya kumtumia Inspekta Fatma na si vinginevyo. Nadhani nia ya Dihenga ni hiyo hiyo aliyotueleza...anataka akupromoti wewe ili umnyang’anye Deus ubingwa...hiyo ni njia yake ya kumlipizia kisasi. Swala ni je, sisi...wewe...uko tayari kushirikiana naye?”
Kimya kilitawala, kisha Roman akarudia tena kauli ambayo tayari alikuwa ameshaitumia zaidi ya mara tatu mle ndani tangu akina Kate waondoke.

“Lakini...inaelekea hawa akina Kate wanajua sana habari zangu...hii mimi hainipi amani kabisa Mark!”
“Sasa basi ni bora tuwe nao sambamba Roman...!” Mark alisema.
“Ili?”
“Ili tuweze kujua ni nini hasa wajuacho kuhusu wewe... na sisi tuweze kuwajua wao zaidi...nadhani tukubaliane na wazo la Mr. Dihenga Roman. Kwani sisi hatutapoteza lolote zaidi ya kunufaika...kwanza tutaweza kutimiza azma yetu, pili tutaweza kuitimiza azma hiyo katika mazingira yaliyo bora zaidi...sasa hivi Roman huna kipato chochote, kujiunga na Dihenga kutakupatia makazi bora, vifaa bora zaidi vya mazoezi, na pesa nzuri...nami pia nitanufaika kama kocha wako. Hii ni nafasi nzuri kwetu Roman...ni sawa na nyota ya jaha!” Mark alisema na kubaki akimtazama Roman kwa muda, kisha akamalizia kwa sauti ya chini, “Hiyo ni kama bado una nia ya kuendelea na ile azma yako Roman.”

“Azma iko pale pale Mark...iko pale pale!” Roman alimjibu haraka bila hata ya kusita.
“Basi na tukubaliane na ofa ya Dihenga...we have nothing to lose (hatuna cha kupoteza) kwa hii ofa Roman!” Mark alimwambia. Siku tatu baadaye, Kate alifuata jibu.
“Mwambie Dihenga tumekubali...no problem!” Roman alimwambia bila kupoteza muda. Hii ilikuwa ni taarifa tamu sana kwa Kate na Dan Dihenga.

*****

Maisha ya Roman yalibadilika ghafla. Dan alitimiza kila aliloahidi. Kwa kuhofia jaribio jingine la kumuua Roman, Dan alimhamishia Roman Bagamoyo, ambako alimpangia nyumba ndogo lakini nzuri na yenye kujitosheleza. Mark Tonto kama kocha wake alilazimika awe anaishi baina ya Bagamoyo na Dar. Kila siku akifanya safari za Bagamoyo asubuhi na kurudi jioni, baadhi ya siku akilala huko huko. Huko kazi ilikuwa ni moja tu, nayo ilikuwa ni mazoezi makali. Dan alimpatia Roman vifaa vyote muhimu vya mazoezi, na pale kwenye nyumba aliyompangia alimtengea chumba maalum cha mazoezi (Gym) ambacho kilikuwa na kila kitu.

Kwa miezi mitatu mfululizo Roman alijichimbia Bagamoyo akijijenga kibondia. Mark Tonto alikuwa naye muda wote huo ingawa siku nyingine alikuwa akirejea Dar kuwa na familia yake. Kate na Dan nao walikuwa wakimtembelea na kumtazama akifanya mazoezi, wakitumia sehemu ya muda wao kutazama mapambano ya Deusdelity Macha kwenye mikanda ya video. Na katika miezi mitatu ile, Roman na Kate waliondokea kujenga ukaribu, na hata siku nyingine Kate alikuwa akienda kule Bagamoyo peke yake na kukutana na Roman, wakitembea pwani na kuongea mambo mengi na kujuana zaidi.

Ndani ya miezi mitatu ile, hakuonana kabisa na Inspekta Fatma, isipokuwa siku moja tu alipoletewa salamu na Mark kuwa Inspekta Fatma alifika pale kwenye klabu yao ya Kawe na kumuulizia. Kwa kuwa hata wale mabondia wa Mark pale klabuni hawakujua Roman alipo, hawakuwa na msaada wowote kwake.

Roman aliendelea na mazoezi yake, na Dan hakuishia hapo katika kumjenga zaidi. Pamoja na kuwa na Mark kama kocha, pia alimletea makocha kutoka nje ya nchi ambao walikuja kumuongezea mbinu zaidi za ndondi, ikiwa ni pamoja na namna ya kubadili namna ya upiganaji akiwa ulingoni kutokana na aina ya upiganaji wa mpinzani wake.
Na baada ya miezi hii mitatu ya mazoezi makali na ya nguvu, Roman alikuwa tayari kuingia katika ulingo wa ndondi za kulipwa, kama professional boxer.

***

Dan Dihenga alimuandalia Roman pambano lake la kwanza kama bondia wa kulipwa mwezi mmoja baada ya Roman kujinadi kuwa yuko tayari kuingia rasmi ulingoni, ambapo alimpatia mpinzani kutoka afrika kusini. Katika pambano hili Roman alikuwa na nafasi ya kujivunia milioni tano za kitanzania akishinda, na milioni mbili akishindwa. Dan hakutaka kulinadi sana pambano hili kwenye vyombo vya habari, na waliondoka kimya kimya kwenda Afrika Kusini, msafara wao ukimjumuisha Dan, Roman, Mark, Kate na tabibu mmoja. Pamoja nao alikuwamo mwandishi wa habari mmoja. Mark alimuuliza Dan sababu ya kutolinadi ipasavyo pambano lile la kwanza la Roman.

“Roman hahitaji kunadiwa Mark...Roman atajinadi mwenyewe baada ya kufanya mauaji huko sauzi...we’ subiri tu, utaona!” Dan alimjibu wakiwa angani kuelekea Johannesburg. Usiku wa pambano jijini Johannesburg, Roman alitoa kipigo cha mbwa mwizi kwa mwenyeji wake, na mnamo raundi ya nane, kocha wa mpinzani wake alilazimika kutupa taulo ulingoni kumnusuru bondia wake!

Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi kutoka kwa watanzania wachache waishio Afrika Kusini waliokuwapo pale ukumbini, Roman akiinuliwa juu juu na watanzania wale. Ilikuwa ni furaha isiyo kifani kwa kambi ya Roman kule ugenini. Mara moja habari zilirudi nyumbani, mwandishi wa habari aliyesafiri na akina Roman akituma habari nyumbani usiku ule ule kwa simu, na akituma picha kadhaa za jinsi Roman alivyokuwa akimsulubu mwenyeji wake kwa mtandao wa intaneti. Usiku ule ulikuwa ni usiku wa tafrija kwa kambi ya Roman jijini Johannesburg.

Walirejea Tanzania siku iliyofuata, na kukuta habari za pambano la Roman nchini Afrika kusini zikiwa zimetapakaa jijini,na waandishi zaidi wa habari wakiwasubiri uwanja wa ndege. Na ndipo hapa ambapo Dan Dihenga alimpomnadi Roman kuwa ndiye bondia wake mpya. Waandishi walimtupia maswali kadhaa naye kama promota mzoefu alitumia nafasi hiyo kumnadi vizuri sana bondia wake. Alipohojiwa na waandishi juu ya ushindi wake ule, Roman alisema kwa utulivu kabisa kuwa ushindi ule haukuwa ajabu kwake, kwani alijua kuwa atashinda. Ndipo mwandishi mmoja alipomtupia swali Dan.“Bwana Dihenga, je ndio unataka kutuambia kuwa Roman amekuja kuchukua nafasi ya Deusdelity Macha, bondia wako wa zamani na ambaye ndiye bingwa wa dunia hivi sasa?”

Bila ya kusita, Dan Dihenga alimjibu yule muandishi, “Nijuavyo mimi Roman ni bondia bora kuliko bondia mwingine yeyote hapa nchini katika uzito wake...hivyo siwezi kusema kuwa kaja kuchukua nafasi ya mtu yeyote hapa, labda tu niseme kuwa amekuja kuchukua nafasi yake inayomstahili!”

“Una maana gani kwa kauli hiyo bwana Dihenga?” Waandishi kadhaa walimrukia kwa swali hilo. Dan hakujibu kitu zaidi ya hapo. Alimuongoza bondia wake kwenye gari na kuondoka eneo lile, akiwaacha wale waandishi wakijijazia majibu yao wenyewe. Habari ya pambano lake la afrika kusini ilimfanya Roman awe gumzo kwa wengi nchini.
Lakini pia ilimrejesha tena Inspekta Fatma katika maisha yake.

ITAENDELEA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BONDIA - 5

Simulizi : Bondia
Sehemu Ya Tano (5)

***
Kapten Deusdelity Macha aliteremka kutoka kwenye gari la jeshi na kutembea kiaskari kuuelekea mlango wa nyumba yake. Upande wa pili wa barabara, Roman alijiinua kutoka kwenye benchi alililokuwa amekalia lililokuwa mbele ya kibanda cha mkaanga chipsi na kumfuata taratibu. Usoni alikuwa amevaa miwani ya jua na ndani ya kifua chake alikuwa akihisi mfukuto wa ghadhabu wakati akimtazama Deus akifungua mlango wa nyumba yake na kuanza kuingia ndani.
“Hallo Deus...!” Aliita taratibu, sasa akiwa hatua si zaidi ya tano kutoka mlangoni kwa Deus. Deus aligeuka, na mara tu alipomuona uso ulimbadilika na kusajili mshituko mkubwa sana.
“Roh...Roman!” Alisema kwa kitetemeshi na kubaki akimtazama.
Walitazamana.
“Un...nataka nini...umekuja lini...?” Deus alijikuta akiuliza bila kufikiri. Roman alibaki akimtazama, chuki isiyo kifani ikijijenga moyoni mwake.
“Rachel is dead Deus.”
Deus alitazama chini.
“Na...naomba uende Roman...nasikitika kwa msiba uliotokea, lakini...”
“Sijakuona msibani hata kidogo Deus...sasa najiuliza, kwa mtu ambaye ndiye niliyekukabidhi mdogo wangu wakati naondoka nchini, kwa nini usitokee msibani?” Roman alimwambia kwa sauti ya utulivu. Deus alianza kufunga mlango, akimuacha Roman nje. Haraka sana Roman aliweka kiatu chake mlangoni na kuuzuia ule mlangokufunga. Deus aliinua uso wake na kumtazama Roman kwa mshangao.
“Toka bwana!” Alisema huku akimsukuma kwa ule mlango. Roman hakutetereka.
“Umemuua Rachel Deus....”
“No! Amejiua mwenyewe Roman, na naomba usinilaumu kwa hilo...mi’ sikuwa na nia mbaya kwake, nilimpenda kikweli kabisa, lakini...”
Hapo Roman alishindwa kuzuia ghadhabu zake. Aliukamata mlango kwa nguvu na kumsukumia ndani Deus huku naye akimfuata nyuma yake.
“Kelele wewe! Ulimpenda mdogo wangu wewe? Mi’ nilikukabidhi ili umrubuni na kumtelekeza?” Alimfokea huku akimsukuma kwa mikono yake yote miwili kifuani. Hapo hapo Deus alimtandika ngumi kali ya uso, na Roman akayumba hadi ukutani huku akiachia mguno wa maumivu. Deus aligeuka na kukimbilia ndani zaidi ya nyumba yake na kujifungia chumbani kwake, ambako alienda moja kwa moja hadi kwenye simu iliyokuwa kando ya kitanda chake.
“Hallo Polisi? Mimi ni kapteni Desudelity Macha! Nahitaji msaada haraka sana nimevamiwa nyumbani kwangu...haraka!”
Nyuma yake Roman alikuwa akibamiza mlango wa kile chumba.
“Fungua mwanaharamu, fungua!” Roman alifoka huku akiubamiza mlango ule kwa hasira.
“Ondoka Roman, ondoka! Mi’ nimeita polisi...yatakayokukuta tusilaumiane!” Deus alimpgia kelele kutokea chumbani kwake.
“Umemuua mdogo wangu Deus! Nimekukabidhi nikiamini kuwa u-binaadamu kumbe ni shetani usiye haya?”
“Sikudhamiria Roman! Hebu ondoka upesi Roman...ondoka nyumbani kwangu!”
Roman alipandwa na ghadhabu. Alirudi nyuma na kuurukia kwa nguvu ule mlango. Lakini ule mlango ulikuwa mgumu sana naye aliishia kuanguka chini kwa kishindo.
“N’takuua mwanaharamu! N’takuua kama ulivyomuua mdogo wangu shenzi wee!” Roman alipiga kelele kwa hasira. Nje ya nyumba ile majirani walisikia mayowe na wakaanza kukimbilia kwenye ile nyumba kujua kulikoni. Roman aliubamiza mlango kwa nguvu bila mafanikio. Alitoka mbio na kuingia jikoni. Akachukua chupa ya mafuta ya taa na kuitupia pale mlangoni, chupa ikapasuka na mafuta ya taa yakiilowesha pazia iliyokuwa imetundikwa mbele ya ule mlango.
Akaliwasha moto lile pazia.“Utatoka humo ndani paka we! Utatoka! Kama hutoki basi utaangamia humo humo ndani kwa moto baradhuli mkubwa we!” Alimtupia maneno ya ghadhabu. Moto ukapamba kwa kasi, mlango ukaanza kuugua, moshi ukatanda kila mahali. Kule chumbani Deus alianza kukohoa kwa taabu, moshi ukimuelemea. “Roman! Roman...acha ujinga...acha...” Alipayuka kwa taabu.
Sasa moto ulikuwa umetawala mlango wote, na bila kufikiri Roman aliurukia ule mlango na kupita nao mzima mzima mpaka ndani, huku nyuma akisikia mayowe ya majirani na ving’ora vya magari ya polisi.
Deus alimshitukia Roman akitua ndani ya chumba kile kwa kishindo. Alijitupa pembeni na kujaribu kumzunguka Roman ili akimbilie nje ya ya chumba kile, lakini Roman alimrukia na kumdaka kiuno na wote wawili wakaenda chini. Deus alimsukumia Roman teke lililomtupa pembeni. Wote waliinuka kwa wakati mmoja na Roman akamsukumia konde kali la uso, lakini Deus aliliona, akabonyea likapita hewani naye akamtandika ngumi nzito ya tumbo. Roman aliguna kwa maumivu na hasira huku akiyumba. Sasa ule moto uliokuwa mlangoni alitambaa mpaka ndani na kupamba kwenye shuka la kitanda.
Roman akamrukia Deus mzima mzima na kumshidilia kichwa cha mwamba wa pua, na Deus alipelekwa mpaka ukutani, akiachia kilio cha maumivu huku akijishika pua iliyokuwa ikibubujika damu. Roman alimuendea na kumchapa konde kali la mbavu na Deus alijipinda huku akigumia kwa uchungu. Roman akamshindilia konde jingine la ubavu wa pili, Roman akajipindia upande wa pili. Roman akampa konde jingine zito la tumbo, Deus akajipinda kwa mbele. Roman akamkamata kichwa na kumsihdilia kwa goti usoni na Deus alienda chini kama mzigo. Sasa chumba chote kilikuwa kimetanda moto, kitanda chote kilikuwa kikiwaka moto, na ndimi za moto ule zilirukia kwenye pazia za madirisha, nayo yakashika moto.
“Acha Roman...acha!” Deus alikuwa akibwabwaja huku akijitahidi kuinuka. Sasa Roman alikuwa amepandwa wazimu wa ghadhabu. Alimdaka ukosi wa gwanda lake la jeshi na kumuinua, kisha akamshindilia kichwa kingine kilichotua sawia mdomoni.
Deus alichia yowe kubwa huku akienda tena chini.
“Umemuua mdogo wangu, Deus! Umemuua mdogo wagu halafu unaniambia nitoke nyumbani kwako? Nyama we, sasa nawe utaenda kuzimu kunakokustahili!”
“Roman, I am sorry...! Nisa...me...he...brother!” Deus alibwabwaja, lakini Roman alikuwa ameshapanda mzuka wa kulipa kisasi. Huku wakiwa wamezongwa na moshi kila upande, alimkamata na kuunyofoa kwa nguvu mkanda wa gwanda la kijeshi alilokuwa amelivaa Deus na kumzingira nao shingoni.
“Roman Nooookkhhhh!” Deus alipiga kelele lakini hapo hapo Roman alianza kumkaba kwa kutumia ule mkanda, akimkata mayowe yake na kumuacha akikoroma.
“Utamfuata Rachel alipo ili ukamuombe msamaha nyau we!” Roman alisema huku akitweta na akizidi kumkaba kwa ule mkanda. Macho yalimtoka pima Deus, alianza kutupa mikono huku na huko, akijitahidi kufurukuta bila mafanikio kutoka kwenye kifo dhahiri kilichokuwa mbele yake.
“Polisi! Jisalimishe sasa hivi!” Sauti kali ya kiaskari ilifoka kutokea mlangoni. Roman aliinua macho yake yaliyowiva kwa ghadhabu na moshi uliotanda mle ndani, na aliona kivuli cha mtu akiwa amesimama pale mlangoni.
“Sijisalimishi mimi! Naua! Namuua bazazi huyu! Niacheni nimmalize halafu nanyi mkaninyonge!” Aifoka huku akizidi kumkaba. Mara hiyo mlio wa bastola ulisikika, na kabla hajatanabahi, Roman alishuhudia kiumbe kikijitupa mle ndani na kujibiringisha sakafuni, kisha akajikuta akiwa amewekewa kabali shingoni kwake na mdomo wa bastola ukiwa umekandamizwa kwenye upande wa kichwa chake.
“Uko chini ya ulinzi mwanaume! Muachie huyo mtu sasa hivi, ama si hivyo napasua bichwa lako kwa risasi!”
Ilikuwa ni sauti kali ya kike.
Roman alizidi kumkaba Deus kwa ule mkanda, pua zikimtutumka, akitweta kwa ghadhabu.
“Niue nami nakufa naye afande!” Alisema kwa hasira, kisha akamalizia, “...huyu mwanaharamu kasabaisha kifo cha mdogo wangu gaddemitt, afande!”
“Utakufa wewe kwanza, naye utamuacha akitapatapa kutafuta pumzi, lakini akiwa hai. Muachie huyo askari sasa hivi!” Fatma, wakati huo akiwa koplo, alisema kwa msisitizo, bastola yake ikiwa kichwani kwa Roman. Na hata alipokuwa akisikia maneno yale, Roman alishuhudia askari wengine watatu wakivamia mle ndani, bunduki aina ya SMG zikiwa mikononi mwao, zote zikiwa zimemuelekea yeye, huku moto ukizidi kupamba mle ndani. Alihema kwa pumzi za haraka haraka, na huku bado akizidi kumkaba Deus kwa ule mkanda, alisogeza mdomo wake sikioni kwa yule rafiki yake aliyebadilika na kuwa adui yake mkubwa, na kumnong’oneza kwa sauti nzito ya kongofya.
“Umeokolewa na askari safari hii Deus, lakini ujue kuwa bado kifo chako kiko mikononi mwangu...I will kill you one day Deus...that’s a promise (nitakuua tu siku moja Deus...nakuahidi hilo)!” Kwisha kusema hivyo, alimsukuma mbele kwa nguvu, akimuacha Deus akisambaratika ovyo sakafuni, naye akijikuta akisukwasukwa kwa nguvu na wale askari, mikono yake ikivutwa nyuma na akipachikwa pingu.
“Ita gari la kuzima moto hapa...upesi!” Koplo Fatma alibwata huku akimburura Roman nje ya kile chumba kilichokuwa kikiwaka moto mtindo mmoja. Nje ya nyumba ile kundi la watu waliojaa udadisi lilikuwa limetanda, wengi kati yao wakiwa ni majirani wa Deus pale mtaani. Akiwa ndani ya gari la polisi kabla ya kuondolewa eneo lile, Roman aliiona nyumba ya Deusdelity Macha, ikiteketea kwa moto kuanzia ule upande kilipokuwa chumba chake cha kulala kuelekea nyuma ya nyumba ile.
Kate alikuwa ni miongoni mwa majirani waliojazana pale nje siku ile, wakimshuhudia Roman akiingizwa kwenye gari la polisi akiwa na pingu mikononi, na jirani yao Deus akiingizwa kwenye gari jingine la polisi huku akivujwa damu. Na wakati akimtazama yule mtu aliyempa kipigo cha haja jirani yao, Kate hakutegemea kabisa kuwa kiasi cha miaka miwili baadaye angekutana na mtu yule uso kwa uso...

***

Roman alishitakiwa kwa kosa la shambulio baya na kusababisha hasara ya mamilioni baada ya kuiteketeza nyumba ya Deus kwa moto. Aliwekwa rumande wakati Deus na jamhuri wakiandaa ushahidi wa kumtia hatiani kwa kosa lile zito alilotuhumiwa kwalo. Mark alijitahidi kumtafutia dhamana, lakini haikuwezekana. Roman alionekana ni mtu hatari sana kuachiwa huru mitaani hivyo aliwekwa ndani. Mara moja Mark Tonto alitafuta wakili wa kumtetea.
Kesi iliendeshwa kwa miezi mitatu, Koplo Fatma akiongoza upande wa upelelezi. Na ni katika miezi mitatu ile, ndipo Koplo Fatma alipopata kuufahamu kwa undani uhasama uliojengeka baina ya Roman na Deus. Lakini mambo mabaya ndio kwanza yalikuwa yanaanza kwa Roman. Kutokana na kuhusishwa na kesi ya kiraia, Roman alijikuta akisimamishwa kazi jeshini, wakuu wake wa kazi wakiweka wazi kuwa iwapo atapatikana na hatia, basi na ajira yake jeshini nayo itakuwa imekwisha.
Kesi ya Deusdelity Macha dhidi ya Roman Kogga ilivutia watu wengi hususan majirani wa Kapten Deusdelity Macha walioshuhudia siku ile Roman alipotiwa nguvuni baada ya kumporomoshea kipigo Deus na kuiteketeza nyumba yake kwa moto. Miongoni mwa wale waliokuwa wakiifuatilia kesi ile kwa karibu sana kila ilipotajwa alikuwamo Kate, jirani wa Deus. Na ni katika kuendelea kwa kesi ile, ndipo mambo yote ya jinsi Deus alivyomrubuni Rachel, mdogo wa rafikiye Roman yalipoweka hadharani, Sada akitoa ushahidi wa matukio yote hayo. Siri ya Deus ikawa wazi kwa majirani na wakuu wake wa kazi pia. Hata hivyo, upande wa mashitaka ulifanya kazi nzuri ya kuusambaratisha ushahidi wa Sada kuwa hauna vithibitisho na badala yake ulikuwa ni simulizi tu miongoni mwa masimulizi ya kubuni. Aidha, upande wa mashitaka, uliweza kutumia historia ya nyuma baina ya Roman na Deus kuonesha kuwa Roman alikuwa na chuki binafsi na Deus kwa muda mrefu, pale muendesha mashitaka wa serikali alipompandisha Deus kizimbani kutoa ushuhuda wa jinsi Roman alipompiga kwa nguvu wakati wakifanya mazoezi ya ndondi wakiwa michezoni jeshini, na kumvunja taya. Kwa jinsi Deus alivyoielezea hali ile, ilionekana kama kwamba wakati walitakiwa wapigane kimichezo, Roman aliingia ulingoni kwa lengo la makusudi la kumuumiza. Ushahidi huu ulimuweka Roman kwenye wakati mgumu sana pale ulipooanishwa na lile tukio la kumvamia Deus nyumbani kwake, kumpiga na hatimaye kumchomea moto nyumba yake.
Mwisho wa kesi, mahakama ilimtia Roman hatiani. Hukumu ikawa ni kifungo cha miaka miwili pamoja na kumfidia Deus kwa hasara aliyomsababishia alipomteketezea nyumba yake kwa moto. Hivyo alitakiwa atumikie kifungo, na baada ya kifungo, alipe fidia ya ile nyumba aliyoiteketeza.Au atekeleze yote mawili kwa pamoja, lolote litakalokuwa rahisi zaidi.
Muda wote wakati hakimu akimsomea hukumu ile, Roman alikuwa amemkazia macho Deus huku akiwa ameuma midomo yake kwa hasira. Baada ya kusomewa hukumu yake Roman alitiwa pingu pale pale mahakamani, na Koplo Fatma akisaidiwa na askari wengine watatu walimuongoza kuelekea chumba cha mahabusu pale mahakamani ili asubiri gari la kumpeleka gerezani, na wakati akiongozwa kutoka pale kwenye chumba cha mahakama, Roman alipitishwa karibu na alipokuwa amesimama Deus na muedesha mashitaka wake. Roman alisimama na kumtazama kwa muda mrefu yule adui yake, kisha kwa sauti iliyojaa utulivu mkubwa alimwambia;
“Mimi nakwenda gerezani Deus. Lakini nataka nikuhakikishie kuwa miaka miwili si mingi...nitatoka. Na nikitoka, nakuja kukuua Deus, hilo ni hakika kabisa!”
Ilikuwa ni kauli ya kuogofya kuliko zote ambazo Deus alipata kuzisikia. Na wakati akiongea maneno yale, sauti na macho yake vyote vilionesha kuwa Roman alikuwa amedhamiria kulitekeleza lile alilokuwa akilisema. Kwa muda karibu mahakama yote ilikuwa kimya kabisa. Watu walitazamana, kila mmoja aliyesikia kauli ile asijue achukue hatua gani. Deus alibaki akimtazama Roman kwa woga uliokithiri, akishindwa kusema lolote.
“Twende Roman...acha mambo hayo sasa!” Koplo Fatma alimwambia huku akimsukuma mbele. Roman alimgeukia na kumtazama kwa jicho kali sana, kisha bila ya kusema neno, aligeuka na kuelekea kule alipokuwa akiongozwa.
Kutoka kwenye kona moja ya mahakama ile, Mark Tonto na Sada walikuwa wakimtazama Roman akiondolewa eneo lile huku wakibubujikwa na machozi.
Kwa hukumu ile, Roman Kogga akawa amepoteza rasmi kazi yake jeshini...

***

Wiki mbili baada ya hukumu, wakili wa Roman alifanikiwa kufikia muafaka na wakili wa Deus, wa namna ya kumfidia hasara ya kumuunguzia nyumba yake. Ilikubaliwa kuwa nyumba ya Roman aliyoachiwa urithi na wazazi wake iuzwe kwa usimamizi wa mahakama, na pesa zitakazopatikana zilipe gharama za ukarabati wa nyumba ya Deus.
Swala likafikiwa muafaka.
Hivyo, ndani ya muda mfupi sana, Roman alipoteza mdogo wake wa damu, kazi yake iliyokuwa ikimpatia riziki hapa duniani, na nyumba yake ya urithi. Na yote ni sababu ya mtu mmoja tu...Deusdelity Macha.

***
Miezi miwili baadaye, Mark Tonto alienda kumtembelea kule gerezani.
“Mark...” Roman alimsalimu rafiki yake huku akitabasamu. Mark Tonto alifanya jitihada za hali ya juu kujizuia asiangue kilio. “Roman...vipi hali yako bwana...?” Alimuuliza kupitia kwenye dirisha la wavu lililowatenganisha. “Sio mbaya...nahesabu siku tu...” Roman alimwambia. Mark aliuma midomo na kutikisa kichwa.
“Jamaa yetu ameacha kazi...ametoa notisi ya saa ishirini na nne...” Mark alimwambia. Roman alimtazama kwa macho ya kuuliza. “Deus...amecha kazi?”
“Yap! Taarifa nilizozipata zinasema kuwa jeshi lilikuwa linajiandaa kumuachisha kazi kutokana na mazingira ya kujihusisha kwake na kifo cha Rachel...inasemekana ingawa mahakama haikumtia hatiani kwa kuwa hakushitakiwa kwa kifo kile, tayari alikuwa ameshalitia doa jeshi...”
“Kwa hiyo yeye akawahi kujitia kuacha kazi kabla hajafukuzwa?”
Mark akaafiki kwa kichwa. Roman akatikisa kichwa kwa masikitiko, uso wake ukionesha kukereka na tabia ile.
“Na sasa ameingia kwenye ngumi za kulipwa...eti ameamua kuwa professional boxer...” Mark alisema kwa dharau. Lakini Roman alikuwa akimtazama kwa makini, ilhali akionekana kuwa na mawazo mazito, akili yake ikiichambua kwa kasi sana habari ile iliyoletwa na Mark.
“Unasema kaamua kuwa bondia...wa kulipwa?” Roman alimuuliza tena kwa sauti iliyojaa udadisi. Mark alimtazama kwa mshangao kidogo. “Ndio...kwa nini?”
Roman alikaa kimya kwa muda, akiwa kwenye mawazo mazito.
“Okay, naomba kuanzia sasa unikusanyie habari zake zote.Najua atakuwa anaandikwa sana magazetini, naomba unikusanyie makala zote...nitakapotoka nitataka kuziona...” Hatimaye alisema. Mark akamtazama kwa muda.
“Kwa nini unataka habari zake...kuna kitu hujaniweka wazi Roman?”
“Usijali. Naomba unifanyie hivyo nikuombavyo Mark...na...mengine nitakueleza kadiri siku zinavyokwenda. Kuna wazo limepita kichwani mwangu, ila nahitaji kulichekecha vizuri kwanza...kisha nitakueleza...” Roman alimjibu. Mark Tonto alimtazama yule rafiki na mwanafunzi wake kwa muda, kabla ya kukubaliana naye.
“Okay, Roman...unajua nitafanya lolote kwa ajili yako...”
“Thanks buddy!”
Hiyo ilikuwa ni kiasi cha miaka miwili na miezi kadhaa iliyopita...

******

Siku mbili baada ya ujio wa Inspekta Fatma pale nyumbani kwake Bagamoyo, Roman, alipanda ndege kuelekea visiwa vya ushelisheli kwa ajili ya maandalizi ya pambano lake na Deusdelity Macha. Pamoja naye walikuwako Kate, Mark na Dan Dihenga. Ilikuwa ni miezi mitatu ya mazoezi mazito kwa Roman kuliko wakati wowote maishani mwake tangu aanze kucheza ndondi. Wakati wote akiwa kwenye mazoezi yake kule ushelisheli, huku nyumbani matangazo ya redio, televisheni na hata magazeti, yalizidi kulinadi pambano lile lililokuwa likisubiriwa kwa hamu. Kambi za ushabiki baina ya mabondia wale wawili zilizidi kukua, watu wakiwekeana madau makubwa na madogo. Vipindi maalum vya michezo viliwasiliana naye moja kwa moja kwa simu akiwa kule ushelisheli na kumhoji juu ya maandalizi yake kwa mpambano ule wa kihistoria, kama jinsi alivyokuwa akihojiwa Deus aliyekuwa Tanzania.
Kila bondia alikuwa akijigamba kumuonesha kazi mwenzake.
Na kwa upande mwingine, wadhamini wao pia walikuwa wakiwatumia mabondia wale kushindanisha biashara zao. Picha za Roman akiwa ushelisheli akiongea kwa simu ya kampuni iliyomdhamini zilionekana kwenye matangazo ya televisheni na magazeti, na wakati huo huo, picha za Deus akizinadi huduma za simu za kampuni inayomdhamini nazo zilionekana kwenye televisheni, magazeti na mabango ya barabarani. Ndani ya miezi mitatu ile, Roman Kogga na Deusdelity Macha, walikuwa watu maarufu sana miongoni mwa watanzania na duniani kote.Lakini ukweli ulibaki kuwa mshindi wa pambano lao, ndiye ambaye angekuwa maarufu zaidi ya mwenzie.
Hatimaye siku ya pambano iliwadia. Pambano lilipangwa kufanyikia kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar.

***

Roman, Kate na Mark waliingia nchini saa nne asubuhi siku moja kabla ya pambano. Dan Dihenga alitangulia siku moja kabla yao ili kufanya maandalizi ya muhimu. Akiwa uwanja wa ndege, kundi la waandishi wa habari lilimzonga Roman kwa maswali juu ya matarajio yake katika pambano lililokuwa mbele yake.
“Kama nilivyosema kule Kairo, pambano la kesho ni la kusherehekea kukabidhiwa kwangu ule mkanda niliounyakua kule Kairo...kwa hiyo nawaomba watanzania waje kwa wingi kushuhudia nikikabidhiwa mkanda wangu hiyo kesho. Ahsanteni sana.” Roman aliwajibu waandishi huku akipigwa picha za magazeti, televisheni na kurekodiwa na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya redio. Kwisha kusema hivyo, Dihenga alimuongoza Roman na msafara wake kwenye gari la kifahari alilowaandalia na kuondoka eneo lile. Siku ile Dan hakuwapeleka Bagamoyo, badala yake msafara wao uliishia kwenye hoteli ya kifahari ya Movenpick, jijini.
“Leo tutalala hapa Roman...” Dan alisema, “...na tutaondokea hapa kwenda ukumbini hiyo kesho.”
“Wow! Yaani tayari mmeshaanza kunipa huduma za kibingwa? Safi sana!” Roman alisema huku akitabasamu, na wote walicheka.
“Hizo ni fadhila za wafadhili wetu Roman...kwa hiyo hatuhitaji kuwaangusha kesho, au sio?” Dan alimwambia.
“Ah, kuangushwa kesho ni lazima, hakuna ujanja...” Roman alijibu akiwa hana utani hata kidogo. Wote waliokuwemo mle ndani walimshangaa.
“Ati...?” Mark Tonto aliuliza kwa mshangao.
“Nini...?” Dan alimaka, wakati Kate akimtazama Roman kwa macho yaliyojaa maswali.
“...ila tu atakayeanguka hiyo kesho ni Deus!” Roman alimalizia kauli yake huku bado akiwa makini sana. Pumzi za ahueni ziliwashuka wenzake aliokuwa nao mle chumbani, Mark akiangua kicheko kikubwa.
“Ah, Roman ulitupa ugonjwa wa moyo kidogo pale...”
“Mwenye ugonjwa wa moyo saa hizi ni Deus tu...” Roman alimjibu.
Saa sita mchana siku ile walienda kwenye zoezi la kupima uzito kwenye ukumbi wa habari maelezo. Waandishi wa habari kutoka katika kila chombo cha habari nchini na nje ya nchi walikusanyika. Mabondia wote wawili walifika na makocha na ma-paromota wao. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili na miezi kadhaa, Roman alikutana tena uso kwa uso na hasimu wake Deusdelity Macha. Walipoonana tu, mabondia wale walisogeleana na kutunishiana vifua huku wakitazamana usoni kwa ghadhabu, wapiga picha za televisheni na magazeti wakipiga picha tukio lile kwa bashasha.
“Nilipata ujumbe wako kutoka kwa Inspekta Fatma, Roman...na nilimwambia kuwa nitakujibu ulingoni siku ya tukio...na sasa siku imewadia!” Deus alimwambia kwa sauti iliyojaa uchokozi. Roman alibaki akimtazama kwa ghadhabu, akiwa amebetua midomo yake kwa kukereka, lakini hakumjibu kitu.
“Vipi, leo huna la kusema Roman? Hakuna macho ya watu ya kukupa kiburi cha kuropoka utumbo wako?” Deus alimsaili kichokozi. Roman alizidi kumtazama kwa ghadhabu, sasa midomo ikimcheza kwa hasira, misuli ikiwa imememtutumka, mishipa ya shingo ikiwa imemsimama.
“Nilipokuwa napelekwa gerezani nilikuahidi jambo Deus...” Hatimaye Roman alimjibu kwa sauti iliyojaa ghadhabu na dhamira halisi, “...kesho nitakutimizia hiyo ahadi, kwa hiyo usiniharakishe...vumilia kidogo tu, ahadi itatimia!”
Uso wa Deus ulimbadilika, na akafunua kinywa kutaka kusema kitu, lakini muda huo huo walinda usalama wakaja kuwatenganisha.
Zoezi la kupimana uzito lilipokamilika, waandishi wa habari waliwahoji wale mabondia kwa muda, na Deus akajigamba kuwa yeye ndiye bingwa na ataendelea kuwa bingwa baada ya pambano lake na Roman.
Kwa upande wake Roman alirudia ile ile kauli yake aliyoitoa kule Kairo, na pale uwanja wa ndege wa JK Nyerere. Alikuwa anaenda ukumbini kuchukua mkanda wake alioushinda kule Kairo.
Magazeti yakaandika, redio an televisheni zikanadi, na homa ya ushabiki juu ya nani atamshinda mwenzake kati ya Roman Kogga na Deusdelity Macha ilipanda mara dufu...

***

***
Ulingo wa kimataifa ulitengenezwa ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini. Ukumbi ule ulibadilika kwa kupambwa kimataifa. Watazamaji na majaji walioteuliwa na shirikisho la ndondi duniani walikuwa wameshaingia ukumbini saa kumi na mbili za jioni. Mapambano kadhaa ya utangulizi,au exhibition, yalifanyika, lakini ilikuwa wazi kuwa wote waliofurika ukumbini usiku ule walikuwa wamekuja kushudia pambano kati ya bingwa wa dunia Desudelity Macha, na mpinzani wake mkubwa kabisa, Roman Kogga.
Ndipo muda ulipowadia, ukumbi ukiwa umejaa wahka, mtangazaji maarufu alipanda ulingoni na kutangaza kuwa muda wa pambano kuu la usiku ule, au main card, ulikuwa umewadia. Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi na vifijo.
Mwamuzi wa pambano lile kutoka Caracas, Venezuela, alipanda ulingoni na kuwaita mabondia. Ndipo kwa mbwembwe za hali ya juu, mtangazaji alianza kwa kumuita mpinzani, Roman Kogga ulingoni. Roman aliingia ukumbini kutokea mwenye chumba cha mapumziko akiwa kidari wazi na chini amevaa bukta yake nyeusi ikiwa na mkanda mpana kiunoni, jina lake la kwanza likiwa limeandikwa kwenye mkanda wa bukta ile kwa maadishi makubwa ya rangi nyeupe. Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi wakati alipokuwa akikimbia kibondia kuelekea ulingoni akisindikizwa na second wake, ambaye pia ndio alikuwa kocha wake, Mark Tonto. Roman alipanda ulingoni na kukimbia huku na huko, akitupa ngumi hewani kwa kasi ya ajabu kisha akajipigapiga kifuani na kuinua ngumi yake juu kwa ishara ya ushindi. Ukumbi ulipagawa kwa vifijo. Kwenye viti vya watazamaji, Dan Dihenga alimgeukia Kate kwa jazba.
“That’s my boxer! Leo ndio Deus atajuta kunisaliti mwanaharamu!” Alimwambia. Kate alibaki akitazama kwa wasiwasi. “Naomba mungu amsaidie Roman ashinde Dan...naomba sana!”
“Ooh! Atashinda tu Kate...atashinda..tena kwa kishindo!”
Kule ulingoni, mtangazaji alimnadi bingwa Deus“deadly” Macha, na muda huo Deus naye alitoka chumbani kwake na kuelekea pale ulingoni, akiwa kifua wazi, na chini akiwa ameva bukta nyekundu, jina lake likiwa limeandikwa kwa maadishi makubwa meusi kwenye mkanda mpana wa bukta ile, mkanda wake wa ubingwa wa dunia akiwa ameuning’iniza begani kwake. Ukumbi ulimpokea kwa shangwe na mayowe mengi, naye akawa anatembea taratibu kuelekea ulingoni akisindikizwa na kocha wake huku akiwa ameinua juu ngumi yake.
Lakini ilionekana wazi kuwa Deus alikuwa anaenda ulingoni kama ng’ombe anayepelekwa machinjoni. Hakuonesha bashasha ambayo mashabiki wake waliitarajia.
Alipanda ulingoni, na hapo alibadilika ghafla. Alianza kurukaruka huku na huko, na kutupa ngumi za haraka haraka hewani huku ukumbi ukimshangilia kwa jazba, kisha akageuka kila upande wa ulingo akiuonesha juu ule mkanda wake aliokuwa anaushikilia.
Baada ya kila bondia kufanya majigambo yake ulingoni, mwamuzi aliwatuliza na kuwaita ili kuwapa nasaha za maadili ya pambano. Kisha kila bondia akarudi kwenye kona yake.Mwamuzi aliwaita kati ya ulingo na wale wapinzani wawili wakaziacha kona zao na kwenda kusimamiana kibondia katika ile pozi ya honour stance, wakisubiri amri ya kuanza pambano.Hatimaye kengele ya kuanza pambano ikagongwa, na mwamuzi akaruhusu pambano.
Deus alianza raundi ya kwanza kwa kasi. Akimshambulia Roman kwa ngumi za haraka haraka na zenye uzito wa kumpeleka mtu chini, lakini Roman alikuwa mtulivu, akimkwepa na kumtandika ngumi za kudokoa na mara moja moja akimtupia ngumi kali za ghafla ambazo hazikuleta madhara yoyote kwa Deus. Na sekunde chache kabla ya raundi ya kwanza kuisha, mabondia wale wawili walijikuta wakiwa wamekumbatiana.
“Umemuua mdogo wangu Deus...sasa leo ndio nami nakutimizia ahadi niliyokupa siku ile nilipokuwa napelekwa gerezani, mshenzi we!” Roman alimnong’oneza kwa hasira. Deus alifurukuta kujichomoa mikononi mwa Roman, lakini Roman alizidi kumbana mpaka refa alipokuja kuwatenganisha. Wote walirudi kwenye kona zao na kuanza kurudiana tena kwa pambano wakati kengele ya kumaliza raundi ilipogonga.
“Unamchezea Roman!” Mark alimkemea Roman wakati wa mapumziko. Roman alibaki akimkodolea macho yaliyojaa vitisho Deus, ambaye alibaki akimtupia macho huku akitweta kutokea kule kwenye kona yake.“Nampiga taratibu...mpaka ajute kujiingiza kwenye ndondi!” Roman alimjibu kocha wake na kuinuka kurudi ulingoni baada ya kengele ya raundi ya pili kugongwa.
Raudi ya pili, Deus aliingia kwa kasi kali zaidi, sasa akionesha hasira za wazi wakati Roman alikuwa mtulivu zaidi, akimtupia makonde ya kushtukiza huku akimcheka mpinzani wake. Lilikuwa ni pambano kali, na kwa dakika moja nzima, Deus alimbana Roman kwenye kona na kumvurumishia makonde makali ya mfululizo huku ukumbi ukirindima kwa hoi hoi, lakini Roman alifanikiwa kuyakwepa masumbwi yale akiwa pale pale kwenye kona, mengine akiyakinga na machache yakimpata, ndipo akiwa pale pale kwenye kona alipojikunja na kujikunjua kwa sumbwi kali la upper cut lililojikita sawia kidevuni kwa Deus na kumyumbisha vibaya, naye akajichomoa kutoka kwenye ile kona na kurudi kati kati ya ulingo. Lakini sasa Deus alikuwa ameshapata matumaini ya kumuangusha mpinzani wake hivyo akamuendea tena kwa kasi, Roman akampisha kidogo na wakati huo huo akimzungushia ngumi ya kushoto, Deus aliiona na kujikinga haraka, na kushitukia akipokea cross nzito ya mkono wa kulia lililotua sawia kwenye upande wa uso wake. Deus aliyumba mpaka kwenye kamba na ukumbi ulichangamka kwa vifijo.
Roman alibaki akirukaruka katikati ya ulingo akimsubiri mpinzani wake, ingawa ile ilikuwa ni nafasi nzuri ya kumbana Deus pale kwenye kamba na kumsulubu atakavyo. Deus alirudi kwa hasira na kujaribu kumtupia makonde ya nguvu. Roman alimpisha tena kidogo na kumtandika konde la tumbo, na Deus alijikunja huku akimkumbatia Roman.
“Unamkumbuka Rachel Deus...?” Roman alimnong’oneza wakiwa wamekumbatiana pale ukumbini. Deus alijikurupusha kujinasua kutoka mikononi mwa Roman, wazi kuwa yale maneno ya Roman yalikuwa yakimchanganya, na Roman alitumia nafasi hiyo kumuachia ghafla na hapo hapo akampa upper-cut nyingine ya kulia iliyotua tena kidevuni. Deus alitupwa nyuma na kuangukia goti pale ulingoni. Ukumbi ulilipuka kwa shangwe, na Roman alikuwa anamuendea wakati kengele ya kumaliza raundi ulipogonga, na ukumbi ukaachia mguno wa fadhaa.
Pambano liliendelea kwa raundi nyingine mbili, na waliposhikana tena kwenye raundi ya tano, Roman alimnong’oneza, “Unakumbuka jinsi nilivyokuvunja taya Deus...? Unakumbuka jinsi nilivyoua mabondia wawili ulingoni...?” Deus alipiga ukelele za hasira na kumsukuma nyuma kwa nguvu Roman. Mara moja refa aliingilia kati na kuweka nidhamu pale ulingoni. Deus alibaki akimkodolea macho ya ghadhabu Roman huku akitweta, wakati Roman akimtazama huku akimcheka. Sasa Deus alionekana wazi kuwa alikuwa akipigana huku akiwa makini sana na ngumi ya kushoto ya Roman, lakini kufikia raundi ya saba, mabondia wote walionekana kama kwamba walikuwa wametoshana nguvu. Lakini ilipofikia raundi ya nane, Roman aliingia na mtindo tofauti kabisa wa upiganaji.
Badala ya kusimama kwa mtindo aliokuwa akiutumia tangu mwanzo wa pambano wa orthodox, yaani kusimamia kulia, ambao ndio ungempa nafasi nzuri zaidi ya kumpiga mpinzani wake kwa mkono wa kushoto, yeye sasa alitumia mtindo wa kusimamia kushoto, yaani southpaw.
Deus alichanganyikiwa, kwani kwa kutumia msimamo huu, Roman hangeweza kutupa konde la kushoto. Deus akahisi Roman amejisahau, na kuingia kwa makonde ya nguvu na ya mfululizo. Katikati ya raundi ile, ghafla bila ya Deus kutaraji, Roman alirudisha tena mtindo wa orthodox na kumtupia konde kali la kushoto lililomkosa kichwani Deus kwa umbali mdogo sana. Deus akajibu kwa konde la kulia la mtindo wa jab, lililompata Roman tumboni. Roman akayumba, Deus akaingia mzima mzima kwa sumbwi la cross, ambalo linapigwa kwa karibu huku mpigaji akienda na mwili wake wote kwa mpinzani wake. Roman alikuwa ametarajia jambo hili, hivyo alijikunja huku akilalia kulia na kumpisha na wakati huo huo akijikunjua huku akiachia right hook iliyotua upande wa kushoto wa kichwa wa Deus, Deus aliyumba, na hapo hapo Roman akalalia kushoto na kujikunjua haraka huku akiachia left hook iliyompata Deus upande wa kulia wa kichwa.
Deus akapoteza mwelekeo, sasa Roman alikuwa upande wake wa kushoto na sio mbele yake tena, ukumbi ulikuwa umepagawa kwa shangwe. Deus akageuka haraka kushoto kwake, lakini Roman akaruka hatua moja mbele na kumtupia ngumi sita za mfululizo za usoni kwa mtindo wa one-two, yaani kulia na kushoto kama mara tatu hivi, kila ngumi iliyoingia ilikuwa ikipokelewa na ukelele wa pamoja kutoka kwa watazamaji. Deus akayumba nyuma na kuangukia kwenye kamba, Roman aliingia pale pale kwenye kamba kwa upper cut ya kulia, na kwenye nukta ya mwisho kabisa akabadili mkono na kumshindilia Deus kwa upper cut ya kushoto iliyompata sawia kidevuni, na hapo Roman aliona macho ya Deus yakipinduka, weusi wa mboni ukipotelea ndani ya macho, na bila kusubiri zaidi alimmalizia na hook ya kulia iliyompata Deus kichwani na kumpeleka moja kwa moja sakafuni kama mzigo.
E bwana we!
Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi, Dan Dihenga na Kate waliruka wima na kushangilia huku wakikumbatiana, Mark Tonto akifuatilia kwa makini wakati Roman akirudi kwenye kona yake na mwamuzi akianza kumhesabia Deus.
Huku nje ya ukumbi, Inspekta Fatma akiwa katika mavazi ya fulana na suruali ya jeans na kofia yake ya kepu kichwani alijipenyeza hadi kwa kocha wa Deus.
“Simamisha pambano hili...simamisha sasa hivi kocha uokoe maisha ya bondia wako!” Alimwambia kwa wahka huku akimvuta mkono. Kocha wa Deus alimgeukia kwa mshangao.
“Khah, we’ mwanamke vipi...? Hebu toka hapa...!”
“No! Mimi ni afisa wa polisi na najua kinachoelekea kutokea...”
“Hebu toka hapa, ebbo!” Kocha alimkemea na kugeukia kule ulingoni. Wakati askari wa usalama pale ukumbini walipokuja kumvuta kando Inspekta Fatma.
Kule ulingoni Deus aliwahi kusimama ilipofikia nne na kujiweka tayari kwa pambano. Refa alimuuliza iwapo yuko sawa, akaafiki kwa kichwa, akamuwekea vidole viwili mbele ya uso wake na kumuuliza anaona vingapi, Deus akamjibu anaona viwili, refa akaruhusu pambano liendelee.Kutokea upande wa pili wa ulingo Mark Tonto, Kate na Dihenga waliona kile kilichokuwa kikitokea baina ya Inspekta Fatma na kocha wa Deus, ingawa hawakuweza kuelewa ni kwa nini kilikuwa kinaongelewa.
Sasa ukumbi ulikuwa hauna utulivu hata kidogo. Deus aliingia kwa kasi ya ajabu, akiwa na ghadhabu za kupelekwa chini na mpinzani wake wakati Roman akiwa amedhamiria kumaliza mchezo na kumuweka Deus mahala pake. Deus alikuja na ngumi ndefu-ndefu za mfululizo, na kwa muda walikuwa wakizungukana bila ya madhara kwa yeyote, wakati ghafla sana Roman alipomuendea kwa kasi mpinzani wake na kusita kama kwamba alikuwa amejigonga miguu na kupoteza uelekeo, akijikunja kutokea kwenye magoti kama anayetaka kuanguka. Deus aliiona nafasi ile na hakuifanyia ajizi. Alimuendea kwa left hook iliyobeba nguvu zake zote, na hapo, bila kutarajiwa, Roman aliruka mbele huku bado ameinama, na kujiinua wima akiwa moja kwa mojambele ya Deus.
Deus akajikuta yuko karibu sana na Roman kiasi cha kutoweza kumpiga kama alivyokusudia, haraka alijitahidi kurudi nyuma lakini alikuwa amechelewa kwani alikuwa ameingia kwenye mtego wa Roman kama inzi aingiavyo kwenye utando wa buibui, na wakati alipojiinua wima namna ile, Roman aliinuka na upper cutnzito ya kulia na hapo hapo akaifuatishia na upper cut nyingine ya kushoto. Yaani ilikuwa ni one-two ya upper cut! Si mabondia wengi wanaoweza kupiga namna ile, mara lipigwapo pigo la namna ile, basi huwa ni pigo la kumaliza mchezo.
Ukumbi ulipayuka kwa mayowe, wakati kwa mara nyingine katika raundi ile, Deus alipojiona akinyong’onyezwa nguvu za magoti na mikono kwa mapigo ya Roman. Roman alimuona mpinzani wake akilegea, na ndipo kwa nguvu zake zote, alipomshushia konde la mkono wake wa kushoto kwa mtindo wa left hook. Deus aliiona ngumi ikimwendea kakini hakuwa na nguvu tena ya kuikwepa wala kujikinga. Ngumi ilimpata Deus juu kidogo ya sikio na kumpeleka kiubavu-ubavu mpaka chini, akisambaratika sakafuni na kubiringika vibaya.
Ukumbi uliachia shangwe za ajabu...
“Kwisha kazi bloody kenges! Roman kamaliza mchezo bloody bastard!” Dihenga akamgeukia Kate na kumwambia kwa bashasha.
Lakini kwa namna ambayo haikutegemewa,Deus alijiinua haraka na kusimama, akayumba kinyuma-nyuma na kusimamia kamba. Mashabiki wake waliamsha hoi hoi za kumtia moyo, wakitaja jina lake kwa pamoja. Deeee-us...deadly! Deeee-us...deadly! Deee-us...deadly....
Inspekta Fatma alimfuata kocha wa Deus kwa mara nyingine.

“Inabidi usimamishe hili pambano sasa hivi kocha! Please...!” Alimwambia kwa jazba. Lakini kocha alikuwa makini na kile kilichokuwa kikiendelea kule ulingoni.
“No! Anaendelea na pambano bado mwanamke! Hebu tok...”
Fatma alilikwapua taulo jeupe kutoka mabegani kwa yule kocha na kurukia kamba za ule ulingo huku akilitupia ndani ya ulingo lile taulo.
“No Dan...look...!” Kate alipayuka huku akioneshea kule ulingoni, ambako Inspekta Fatma akiwa ameshikilia kamba za ulingo huku akipayuka maneno ya wahka.
Mwamuzi alishangaa kuona taulo likitupiwa ulingoni na mtu asiye kocha wa yeyote kati ya wale mabondia wawili. Ukumbi mzima uliachia mguno wa fadhaa uliofuatiwa na kelele za kuchanganyikiwa. Roman alimtazama yule askari mtukutu kwa hasira, wakati Deus akimgeukia kwa mchanganyiko wa mshangao na kutoelewa.
“Achana na hili jambo Deus! Huwezi kushinda hili pambano...okoa maisha yako!” Inspekta Fatma alimpigia kelele yule bondia aliyeelemewa. Hapohapo Fatma akamgeukia Roman.
“Haina haja ya kuendelea na pambano Roman, tayari umeshaonesha uwezo wako...achana na visasi!”
“Toa nje huyo mwanamke!’ Mwamuzi alipiga kelele wakati askari wa jeshi la polisi waliokuwa kwenye sare rasmi za kazi wakimkamata Fatma na kumvuta kutoka ulingoni Fatma alizing’ang’ania zile kamba huku akipiga kelele.
“No, niacheni! Deus achana na pambano hili tafadhali! Kubali kushindwa tu...there is no way utashinda hili pambano! Mwenzio hakuja ulingoni kwa nia ya mchezo kama wote hapa wanavyodhani, nawe walijua hilo! Get out now wakati bado uko hai Deus...PLEASE!”
Deus alimtazama yule mwanadada akitolewa pale kwenye kingo za ulingo huku akitweta. Alimgeukia Roman aliyekuwa amesimama katika ile honour stance akisubiri uamuzi kutoka kwake huku akimtazama kwa macho ya ghadhabu iliyokithiri.

“Yuko sahihi Deus! Kubali kushindwa...huu mkanda hauna thamani ya maisha yako!” Alimwambia, na akaona Deus akikunja uso kwa ghadhabu maradufu.
Kule nje kocha wa Deus alikuwa akiruka huku na huko kwa hasira, akipinga kitendo cha yule mwanadada kurusha taulo ndani ya ukumbi bila ya ridhaa yake. Kule kwenye meza ya majaji nako kulikuwa kuna mtafaruku mkubwa, baadhi wakisema pambano liendelee wakati wengine wakishauri lisimamishwe.
Huku ulingoni, Deus alilitazama lile taulo lililokuwa mbele yake pale chini, kisha kwa mguu wake wa kulia alilisukumia nje ya ulingo na kusima katika ile honour stance tayari kuendelea na pambano huku akimtazama Roman kwa ghadhabu.
“Sikuja hapa kushindwa Roman! Kama unadhani maisha ni bora zaidi ya mkanda, jitoe wewe kwenye pambano!” Alimwambia kwa hasira, na Romana akaona kuwa yule jamaa alikuwa amedhamiria.
Ukumbi uliamka kwa hoi hoi mpya, wakati Inspekta Fatma akijishika kichwa na kuangukia magoni sakafuni huku akitazama kile kilichokuwa kikitokea kule ulingoni kwa fadhaa kubwa.
Kabla mwamuzi hajapitisha uamuzi, Deus alijiengemeza kwenye kamba na kuziacha zimsukume mbele kwa kasi naye akaenda mzima mzima huku akiachia ukelele wa ghadhabu ilhali akimsukumia Roman konde la mkono wa kulia.
Roman alimuona Deus akimjia na ngumi ya mkono wa kulia huku miguu ikimuishia nguvu, na ndipo aliporuka mbele haraka kumfuata mpinzani wake yule bazazi, mkono wake wa kushoto ukiwa juu kabisa hewani, kisha akaushusha na kuuzungusha kutokea chini na kumshindilia konde zito sana kwenye upande wa kichwa chake chini kidogo ya jicho lake la kulia.
Deus alienda chini kama mzigo, kinga ya meno iliyokuwa kinywani mwake ikimtoka na kusambaratika mpaka nje ya ulingo.Roman alirudi nyuma na kusimama kwenye kona ya neutral, akiiacha kona yake, huku akimtazama mpinzani wake kwa makini. Deus alijiinua na kubaki akiwa amepiga magoti na ameshika sakafu kwa mikono yake, akajiinua wima, akayumba kulia na kushoto, kisha akaenda chini mzima mzima na kuanguka chali kwa kishindo.
Ukumbi ulilipuka kwa shangwe na hoi hoi zisizo kifani. Roman alibaki akimtazama mpinzani wake akiwa ametulia chali pale sakafuni, damu ikimtoka puani na mdomoni. Mwamuzi alimsogelea Deus na kuanza kumhesabia na ilipofika tano bila ya Deus kutikisika, watazamaji nao wakawa wanahesabu pamoja naye.
“SITA...SABA...NANE...TISA...KUMIIIIII....!”
Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi na nderemo, jina la Roman likitamkwa kila kona ya ukumbi ule. Mwamuzi ulimuinua Roman mkono juu kumtangaza mshindi, na mara baada ya kufanya hivyo alimgeukia Deus aliyelala pale chini, kisha akawaashiria wahudumu walete machela.
Roman alibaki akiwa anatweta huku ameinua juu mkono wake wa kushoto kwa ishara ya ushindi huku akimtazama adui yake aliyelala pale chini. Machozi yalikuwa yakimtiririka na alikuwa akigeuka huku na huko akiwa akiwatafuta Dan, Mark na Kate, lakini kwa namna ya ajabu alikuwa hawaoni.
Sasa ulingo ulikuwa umevamiwa na baadhi ya watu wa kambi ya Deus walioenda kumtazama mtu wao aliyelala taabani pale chini. Walimvua glovu na mikono yake ikabaki na zile bandeji mabondia wanazozifunga mikononi mwao kabla ya kuvaa glovu za kupigania.
Macho ya Roman yakaangukia kwa Inspekta Fatma aliyekuwa amepiga magoti nje ya ulingo huku akimtazama kwa fadhaa na masikitiko makubwa.
Walitazamana...
Huku nyuma Deus alijaribu kujiinua lakini alishindwa. Watu wachache walikuwa wamemzonga pale chini lakini bado akili yake iligoma kabisa kukubali kuwa alikuwa amebwagwa chini na Roman. Aligeuza uso wake uliomvimba na kumuona Roman akiranda kibabe pale ulingoni huku akiwa ameinua juu mkono wake, na ghadhabu zikamzonga. Alihisi maumivu yasiyo ya kawaida kichwani...ndani ya kichwa chake, na kwa mara ya kwanza akabaini kuwa amekuwa akisikia mvumo mzito masikioni mwake tangu alipojigundua kuwa alikuwa ameagushwa chini na Roman.
Ina maana huu ndio mwisho wangu kweli?
Alijisukuma na kuinuka kwa kujishikilia kwenye kamba za pale ulingoni na baadhi ya watu wake wakamsaidia kuinuka.
Nimevuliwa ubingwa na Roman!
“Tulia tu Deus, tulia. Pambano limeisha hili...tumeshindwa kaka!” Mmoja wa watu wa kambi yake alimwambia, bila ya kujua kuwa Deus hakuwa akisikia lolote zaidi ya ule mvumo mzito masikioni mwake.
Alijishikilia kwenye stuli iliyowekwa pale kwenye kona yake kwa ajili ya kupumzikia mwisho wa raundi, na hata pale alipojishikilia kwenye stuli ile, aliona tone la damu nzito kutoka puani kwake likiangukia pale kwenye ile stuli.
Yaani Roman ndio amenifanya hivi kweli?
Aligeuka kule alipokuwa Roman na kuona kuwa alikuwa hatua chache kutoka pale alipokuwa, akiwa amemgeuzia mgongo na amezibwa kidogo na watu. Kwa nguvu alizobakiwa nazo zilizosukumwa na ghadhabu ya hali ya juu aliikwapua ile stuli na kuwasukuma wale watu waliomkinga Roman huku akimwendea kwa hasira...
Roman alikuwa anaanza kuhamisha macho yake kutoka kwa Inspekta Fatma ili awasake akina Kate, wakati alipoona uso wa yule Inspekta ukibadilika na kuwa wa taharuki, macho yakimtumbuka na kinywa kikimtanuka bila ya sauti kumtoka. Pamoja na badiliko lile alilolishuhudia katika uso wa Inspekta Fatma alisikia sauti ya Kate ikiita kwa wahka kutoka nyuma yake.
“Roomaaaaaan!”
Wito wa Kate ulikuja nukta moja tu kabla ya ule wa Inspekta Fatma ambaye hapo naye alipiga ukelele wa hamaniko huku akimuoneshea kwa mkono wake nyuma yake.
“Angaliaaaaaaa!”
Haraka Roman aligeuka nyuma yake...
La Haula!
Alijikuta uso kwa uso na Deus aliyekuwa amefinyanga uso kwa ghadhabu huku akiwa ameinua juu ile stuli kwa mkono wake wa kulia, na aliona wazi kuwa ile stuli ilikuwa inamshukia kichwani...
Deus hakuwa akisikia mayowe ya watu waliokuwa wakipiga kelele kutahadharisha juu ya kile alichokuwa akikifanya, na aliishusha kwa nguvu sana ile stuli kichwani kwa Roman aliyekuwa ameegemea kamba pale ulingoni bila ya namna yoyote ya kujiokoa...
Kate, Dan na Mark Tonto waliokuwa upande wa pili wa ulingo waliachia vilio vya fadhaa huku wakishuhudia kiwetewete kilichokuwa kinatokea.
Bila ya kuhama hata kidogo kutoka pale alipokuwa amesimama, Roman alijipindua kutokea kiunoni kwenda juu na kulalia kulia kwake huku akiwa ameegemea kamba za ulingo, na pigo baya la Deus likakikosa kichwa chale na kumpunyua kidogo juu kidogo ya unyusi wake wa kushoto, na hapohapo, bila ya kufikiri wala kupanga, Roman akajigeuza kulalia kushoto huku sumbwi lake la kushoto likichomoka kwa nguvu yenye msukumo wa ajabu na kumshindilia Deus kwa upper cut nzito sana iliyojikita sawia chini ya kidevu na kumnyanyua hewani mzima mzima kabla ya kumbwaga tena sakafuni kama mgomba.
E Bwana we!
Ukumbi sasa ulilipuka kwa yowe moja kubwa la pamoja, ambalo halikuwa la kushangilia bali na la mshituko, au mastaajabu, au mshangao.
Kisha kimya kikatanda ukumbi mzima wakati Kate, Dan na Mark wakivamia ulingo na kwenda kumzingira Roman aliyebaki akiwa ameegemea kamba huku mikono yake ameiinua kibondia katika ile honour stance, tayari kuendelea na pambano kama lipo.
Kate alishindwa kujizuia na kumkumbatia Roman pale pale ulingoni. Roman naye akamkumbatia huku ukweli wa kile kilichotokea pale ukimfunukia wazi akilini mwake.
“Oh, Roman! Alitaka kukuua yule Roman!” Kate alibwabwaja, na Roman ahakuwa na jibu, kwani alihisi donge kubwa likimkaba kooni.
Watu wengine pamoja na watoaji huduma ya kwanza walimkibilia Deus aliyekuwa amelala chali pale kwenye sakafu ya ulingo ule huku damu ikitambaa taratibu pale sakafuni kutokea sehemu kwenye kichwa cgake. Wale wahudumu wa huduma ya kwanza waliweka machela kando ya Deus pale ulingoni na kumchunguza kwa muda, kisha mmoja akamgeukia mwamuzi kwa macho yaliyohamanika.
“Amekufa huyu refa!” Alisema kwa wahka mkubwa.
Mwamuzi alibaki akiwa amekodoa macho.
Roman aliyeisikia kauli ile alifumba macho huku akimeza funda kubwa la mate kondoa donge lililomkaa kooni.
“Nimelipiza kifo chako Rachel...sasa unaweza kutulia kwa amani huko uliko mdogo wangu...rest in peace.” Alinong’ona peke yake huku akiwa amemkumbatia Kate kwa mkono mmoja, ilhali kwa ule mwingine akiwa amenyoosha ngumi yake juu, jina lake likitajwa kwa shangwe ukumbi wote ule.
Rooman...Koooga! Rooman...Kooogga! Roooman...Kooogga!
Hatua chahe pale ulingoni, Mark Tonto alikuwa akimtazama yule rafiki yake aliyetimiza azma aliyojiwekea tangu akiwa gerezani, na hakuweza kuzuia machozi kumtiririka. Moja kwa moja alikutana na macho ya Inspekta Fatma aliyekuwa akimtazama kwa macho yenye mchanganyiko wa fadhaa na kutoamini, naye akakwepesha macho yake na kujichanganya na akina Dihenga na Kate, pamoja na kundi la mashabiki waliovamia ulingo na kumbeba Roman juu juu.
Roman aliinua juu ngumi yake huku akibubujikwa na machozi.
“Nimelipiza kifo chako Rachel...nimelipiza...kama nilivyokuahidi!” Alijisemea mwenyewe wakati akimshuhudia bingwa wa zamani Deusdelity Macha akitolewa ulingoni akiwa kwenye machela.
Saa moja baadaye dunia na umma wa watanzania walitangaziwa kuwa bondia Deusdelity Macha alifariki dunia akiwa ulingoni baada ya kupigwa na mpinzani wake wakati akitetea ubingwa wake wa dunia katika uzito wa Super Middle, dhidi ya bingwa mpya wa dunia wa uzito ule, Roman Kogga.

***
Kaburi lilikuwa limejengewa vizuri kwa marumaru ghali, na msalaba uliokuwa kwenye kichwa cha naburi lile ulikuwa umesimama wima, nao ukiwa umetengenezwa kwa marumaru. Kwenye vkichwa cha kaburi lile, kibati cha shaba kilichojengewa pale kaburini na kuwekea kioo juu yake kilimnadi wazi yule marehemu aliyelala usingizi wa milele ndani ya kaburi lile.

Rachel Kogga
Dada uliyependwa kwa dhati.
Uliishi, ukadhulumiwa, ukalipiziwa.
Pumzika kwa amani.
Chini ya maneno yale, paliandikwa tarehe ambayo marehemu Rachel Kogga alizaliwa na ile ambayo aliiaga dunia .

*
MWISHO

TOA MAONI YAKO…….

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIWAYA: BONDIA

--Riwaya hii imeboreshwa zaidi.

MTUNZI: Hussein Tuwa

KIONJO 1

LANGO KUU LA GEREZA la Ukonga jijini Dar es Salaam lilifunguliwa na mtu mmoja mrefu alitoka nje ya lango lile kwa hatua za kujiamini na kusimama kiasi cha hatua zipatazo tano nje ya gereza lile. Nyuma yake lile lango lilifungwa, na hivyo kufungia historia ya miaka miwili ya taabu, mateso, kazi ngumu na uchungu mwingi ambayo mtu huyu alipitia alipokuwa upande wa pili wa lango lile.

Ilikuwa ni saa tatu na robo asubuhi siku ya Jumatano.

Jamaa aliangaza kulia na kushoto pale nje huku akivuta pumzi ndefu zilizoingiza hewa nyingi mapafuni mwake, kisha akashusha pumzi zile zikiambatana na mguno wa faraja, iliyotokana na kuvuta hewa ile ya ulimwengu huru, akiwa mtu huru. Hili ni jambo alilokuwa akilisubiri kwa hamu katika muda wote ule aliokuwa akitumikia kile kifungo chake cha miaka miwili.

Pamoja na kimo chake kirefu, mtu huyu alikuwa na mwili ulioshiba pamoja na kuwa alikuwa kifungoni. Hii ni kutokana na mazoezi mazito aliyokuwa akijilazimisha kufanya akiwa kule gerezani kwa lengo maalum. Misuli yake ya mikono iliyojaa vizuri ilijidhihirisha wazi kwa kututumka na kufanya mikono ya fulana yake ya mikono mifupi ionekane kumbana. Vivyo hivyo, misuli yake ya mapaja ilionekana kututumka na kuifanya ile suruali yake ya jinzi nayo ionekane kuwa inambana.
Bila kugeuka nyuma, jamaa alianza kutembea kwa hatua moja moja zilizokuwa zikivutwa bila ya haraka yoyote kuelekea barabara kuu iliyokuwa mbele yake, akiliacha lile jengo la gereza nyuma yake akiwa na azma ya kutorejea tena ndani ya kuta za jengo lile maishani mwake.

Bora kufa, kuliko kurudi tena gerezani.
Alishaazimia hivyo muda mrefu, na bado alibaki na azma hiyo.
Kwake yeye mji aliuona umebadilika sana ndani ya miaka ile miwili, lakini hilo halikuwa na maana yoyote kwake, kwani alijua kitambo kuwa pindi atakapotoka gerezani angekuta mabadiliko mengi sana jijini. Alikuwa akitembea huku akijaribu kutazama mambo yote yaliyokuwa mbele yake kwa jicho la kudadisi. Aliona kuwa magari ya usafirishaji wa abiria yalikuwa yamechorwa mistari ya rangi, tofauti na hali aliyoiacha wakati anaingia gerezani. Kidogo hili lilimpa taabu, kwani alianza kujiuliza ni jinsi gani ataweza kujua ni rangi ipi ndio ilikuwa ikiwakilisha basi la kuelekea sehemu ambayo alikuwa ameazimia kwenda baada ya kutoka gerezani.

Aliweka sawa mkoba wake mdogo alioupitisha begani kwake na kuuacha ukining’inia mgongoni na kuzidi kuikurubia ile barabara ambayo juu yake, magari yalikuwa yakipita kwa kasi sana kiasi cha kumkosesha amani. Jamaa alikuwa na sura ya kuvutia ambayo baada ya miaka miwili gerezani, ilikuwa imeingia ukomavu fulani ambao haukuwepo hapo kabla, na ambao kwa namna yake uliongeza mvuto kwenye sura ile.

Lakini wakati akitembea taratibu kwa mwendo wake wa hatua moja moja kukiendea kituo cha mabasi yaelekeayo katikati ya jiji kilichokuwa upande wa pili wa barabara, uso wake ule wenye mvuto ulionekana wazi kuwa ulikuwa una dhamira thabiti juu ya nini alikuwa anataka kufanya baada ya kutoka gerezani, kwani baada ya miaka miwili ya kupanga na kupangua akiwa kule gerezani, hakika alikuwa anajua ni nini haswa alichotakiwa kukifanya.

Kwenye kituo cha mabasi yaliyokuwa yakielekea maeneo ya Kariakoo na katikati ya jiji kilichokuwa upande wa pili wa ile barabara kuu, mmoja wa watu waliokuwa wakisubiri mabasi pale kituoni alikuwa akifuatilia kila hatua ya yule mtu mrefu aliyetoka kule gerezani, ambaye sasa alikuwa akisubiri nafasi mwafaka ya kuvuka barabara ili naye aende pale kituoni.
Alikuwa ni mwanamke aliyejitanda kanga mwili mzima hadi kichwani, kama jinsi wanawake wengi wa pwani wapendavyo kujitanda, na usoni alikuwa amevaa miwani myeusi iliyoficha kabisa sura yake. Ingawa alionekana kuwa ni msafiri miongoni mwa wale wasafiri wengi waliokuwa wakisubiri daladala pale kituoni, ukweli ni kwamba mwanadada yule aliyejitanda kanga, alikuwa akimsubiri yule mtu mrefu aliyetoka gerezani asubuhi ile!

Jamaa alivuka barabara na alikuwa akikiendea kile kituo cha mabasi, wakati mlango wa mbele wa gari dogo aina ya Hyundai nyeupe yenye namba za serikali ulipofunguka na msichana mmoja mwenye kimo cha kawaida alipoteremka na kusimama nje ya lile gari huku mkono mmoja bado ukiwa umeshikilia mlango wa gari lake.

Huyu naye alikuwa amevaa miwani ya jua, ingawa yeye alikuwa amevaa gauni refu la kitambaa laini chenye maua madogo madogo lililokuwa na mpasuo mpana upande mmoja. Kichwani alikuwa amebana nywele zake ndefu zilizotiwa dawa za kulainisha na kupendezesha nywele katika ile staili ya Pony Tail, ambapo kile kimkia cha nywele kilichokuwa kikining’inia kisogoni mwake kilikuwa kimechomoza kutokea kwenye sehemu ya nyuma ya kofia aina ya kapelo aliyokuwa ameivaa. Aliweka mkono wake wa pili juu ya paa la gari na kumtazama yule jamaa akipita upande wa pili wa lile gari akielekea kule kituoni.

“Roman!” Aliita.
Jamaa alisimama katikati ya hatua na kugeuka taratibu ule upande ilipotokea sauti iliyoita jina lake. Alimtazama yule dada mwenye kapelo na miwani ya jua huku akikunja uso kujaribu kumtambua. Yule dada aliendelea kumtazama bila ya kusema neno zaidi, akimpa muda yule mtu aliyemwita kwa jina la Roman amtambue.Kule kituoni yule mwanamke aliyejitanda kanga naye alianza kupata wasiwasi baada ya kuona yule jamaa aliyekuwa akimvizia akisimama na kumgeukia yule dada aliyetoka kwenye lile gari lenye namba za serikali.

Ni nini tena pale?
Jamaa alimtazama kwa makini zaidi yule dada na alihisi kuwa alishapata kuiona ile sura wakati fulani huko nyuma, ingawa bado hakuweza kuioanisha sura ile na kumbukumbu zake za miaka miwili iliyopita.
“Miaka miwili ni mingi kiasi cha kukufanya unisahau Roman?” Hatimaye yule dada alimuuliza yule jamaa huku akitoa miwani usoni kwake, na hapo jamaa akaachia mdomo kwa mshangao.
“Afande Fatma...?”

Yule dada alirudisha tena miwani yake usoni. “Sasa nimekuwa Inspekta... Inspekta Fatma.”
Jamaa alikunja uso, safari hii ikiwa ni kwa kukereka, na kubetua midomo kwa namna ambayo ilionesha kuwa hakufurahishwa na hali ile.

“Unataka nini Inspekta?” Roman aliuliza, huku akitilia mkazo wa kebehi lile neno ‘Inspekta’.
“We need to talk Roman... you and me!” Inspekta Fatma alimwambia yule jamaa bila ya kujali kebehi na kukereka kwake kwa wazi, akimaanisha kuwa kulikuwa kuna haja ya wao kuwa na mazungumzo. Roman alitikisa kichwa kwa masikitiko.
“Yaani siku yangu ya kwanza nikiwa mtu huru! Halafu mtu wa kwanza kukutana na kuongea naye ni askari! What’s this? (Nini maana yake hii?)” Roman alisema kwa hasira.

“Tunahitaji kuzungumza Roman, na tunahitaji kuzungumza sasa hivi!”
“About what?” Jamaa alimchachamalia, akitaka kujua yule mwanadada alikuwa anataka waongee kuhusu nini, kisha hapo hapo akaendelea, “Nimetumikia kifungo changu, nimemaliza. Sasa mimi ni raia huru...”

“Ingia kwenye gari Roman!” Inspekta Fatma alimkatisha. Na sauti yake ilikuwa imebeba mamlaka yote aliyokabidhiwa na jamhuri kama afisa wa jeshi la polisi mwenye jukumu juu ya usalama wa raia wote wa Tanzania.

Kule kituoni yule mwanamke aliyejitanda kanga alizidi kujichanganya katikati ya kundi la watu waliokuwepo pale kituoni huku akizidi kufuatilia kwa makini kila kilichokuwa kikiendelea kule kwenye lile gari dogo lenye namba za serikali. Na kwa kadiri ilivyokuwa, ni wazi kuwa kile kitendo cha yule mtu aliyeitwa Roman kusimama na kuongea na yule dada aliyetoka kwenye lile gari lenye namba za serikali kilimchanganya sana.
Ni nini kinaendelea pale?
 
Ahsante sana mkuu Ila huu mzigo tayari upo humu mkuu
 
Niliisoma gazeti la Lete Raha hii stori ni hatari.

Deusdeadly Macha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…