Riwaya: Bondia

Huh!?!?! Mi wifi yako tena? WTF!

Duuuuh samahani aisee nadhan ni tatizo la kiufundi....nilidhamiria kumkoti mbalu...af sijajua comment yako imetoka wapi kwenye huu uzi
 
Last edited by a moderator:
Duuuuh samahani aisee nadhan ni tatizo la kiufundi....nilidhamiria kumkoti mbalu...af sijajua comment yako imetoka wapi kwenye huu uzi

Mai Wii usijali sana huyo Nyani Ngabu ni kaka yangu kwa hiyo kwako atakuwa shemeji.
 
Last edited by a moderator:
Huh!?!?! Mi wifi yako tena? WTF!

Kaka yangu wa Ngabu hebu nisaidie kuipata hiyo stori ya nyumba iliyoungua iko wapi? siioni ni ile ambayo yule mwalim Mage ameungua mpaka kufa?
 
Casuist
unaweza kutuletea na ile ya UTATA WA /9 DECEMBER?
nitafurahi sana kiongozi
 
Last edited by a moderator:
Hahahahaa wii hunipendi kumbe...kaka yako akikusikia si ntaachika mie...

Miye naweka mbolea tu au mlikubaliana kushia kwenye ule mlango wa kijani? hahaaa haha haaa
 
RIWAYA: BONDIA
MTUNZI: HUSSEIN ISSA TUWA


SEHEMU YA ISHIRINI


"Okay, naomba kuanzia sasa unikusanyie habari zake zote.Najua atakuwa anaandikwa sana magazetini, naomba unikusanyie makala zote...nitakapotoka nitataka kuziona..." Hatimaye alisema. Mark akamtazama kwa muda.
"Kwa nini unataka habari zake...kuna kitu hujaniweka wazi Roman?"
"Usijali. Naomba unifanyie hivyo nikuombavyo Mark...na...mengine nitakueleza kadiri siku zinavyokwenda. Kuna wazo limepita kichwani mwangu, ila nahitaji kulichekecha vizuri kwanza...kisha nitakueleza..." Roman alimjibu. Mark Tonto alimtazama yule rafiki na mwanafunzi wake kwa muda, kabla ya kukubaliana naye.
"Okay, Roman...unajua nitafanya lolote kwa ajili yako..."
"Thanks buddy!"
Hiyo ilikuwa ni kiasi cha miaka miwili na miezi kadhaa iliyopita...




******
Siku mbili baada ya ujio wa Inspekta Fatma pale nyumbani kwake Bagamoyo, Roman, alipanda ndege kuelekea visiwa vya ushelisheli kwa ajili ya maandalizi ya pambano lake na Deusdelity Macha. Pamoja naye walikuwako Kate, Mark na Dan Dihenga. Ilikuwa ni miezi mitatu ya mazoezi mazito kwa Roman kuliko wakati wowote maishani mwake tangu aanze kucheza ndondi. Wakati wote akiwa kwenye mazoezi yake kule ushelisheli, huku nyumbani matangazo ya redio, televisheni na hata magazeti, yalizidi kulinadi pambano lile lililokuwa likisubiriwa kwa hamu. Kambi za ushabiki baina ya mabondia wale wawili zilizidi kukua, watu wakiwekeana madau makubwa na madogo. Vipindi maalum vya michezo viliwasiliana naye moja kwa moja kwa simu akiwa kule ushelisheli na kumhoji juu ya maandalizi yake kwa mpambano ule wa kihistoria, kama jinsi alivyokuwa akihojiwa Deus aliyekuwa Tanzania.
Kila bondia alikuwa akijigamba kumuonesha kazi mwenzake.
Na kwa upande mwingine, wadhamini wao pia walikuwa wakiwatumia mabondia wale kushindanisha biashara zao. Picha za Roman akiwa ushelisheli akiongea kwa simu ya kampuni iliyomdhamini zilionekana kwenye matangazo ya televisheni na magazeti, na wakati huo huo, picha za Deus akizinadi huduma za simu za kampuni inayomdhamini nazo zilionekana kwenye televisheni, magazeti na mabango ya barabarani. Ndani ya miezi mitatu ile, Roman Kogga na Deusdelity Macha, walikuwa watu maarufu sana miongoni mwa watanzania na duniani kote. Lakini ukweli ulibaki kuwa mshindi wa pambano lao, ndiye ambaye angekuwa maarufu zaidi ya mwenzie.
Hatimaye siku ya pambano iliwadia. Pambano lilipangwa kufanyikia kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar.


***


Roman, Kate na Mark waliingia nchini saa nne asubuhi siku moja kabla ya pambano. Dan Dihenga alitangulia siku moja kabla yao ili kufanya maandalizi ya muhimu. Akiwa uwanja wa ndege, kundi la waandishi wa habari lilimzonga Roman kwa maswali juu ya matarajio yake katika pambano lililokuwa mbele yake.
"Kama nilivyosema kule Kairo, pambano la kesho ni la kusherehekea kukabidhiwa kwangu ule mkanda niliounyakua kule Kairo...kwa hiyo nawaomba watanzania waje kwa wingi kushuhudia nikikabidhiwa mkanda wangu hiyo kesho. Ahsanteni sana." Roman aliwajibu waandishi huku akipigwa picha za magazeti, televisheni na kurekodiwa na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya redio. Kwisha kusema hivyo, Dihenga alimuongoza Roman na msafara wake kwenye gari la kifahari alilowaandalia na kuondoka eneo lile. Siku ile Dan hakuwapeleka Bagamoyo, badala yake msafara wao uliishia kwenye hoteli ya kifahari ya Movenpick, jijini.
"Leo tutalala hapa Roman..." Dan alisema, "...na tutaondokea hapa kwenda ukumbini hiyo kesho."
"Wow! Yaani tayari mmeshaanza kunipa huduma za kibingwa? Safi sana!" Roman alisema huku akitabasamu, na wote walicheka.
"Hizo ni fadhila za wafadhili wetu Roman...kwa hiyo hatuhitaji kuwaangusha kesho, au sio?" Dan alimwambia.
"Ah, kuangushwa kesho ni lazima, hakuna ujanja..." Roman alijibu akiwa hana utani hata kidogo. Wote waliokuwemo mle ndani walimshangaa.
"Ati...?" Mark Tonto aliuliza kwa mshangao.
"Nini...?" Dan alimaka, wakati Kate akimtazama Roman kwa macho yaliyojaa maswali.
"...ila tu atakayeanguka hiyo kesho ni Deus!" Roman alimalizia kauli yake huku bado akiwa makini sana. Pumzi za ahueni ziliwashuka wenzake aliokuwa nao mle chumbani, Mark akiangua kicheko kikubwa.
"Ah, Roman ulitupa ugonjwa wa moyo kidogo pale..."
"Mwenye ugonjwa wa moyo saa hizi ni Deus tu..." Roman alimjibu.
Saa sita mchana siku ile walienda kwenye zoezi la kupima uzito kwenye ukumbi wa habari maelezo. Waandishi wa habari kutoka katika kila chombo cha habari nchini na nje ya nchi walikusanyika. Mabondia wote wawili walifika na makocha na ma-paromota wao. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili na miezi kadhaa, Roman alikutana tena uso kwa uso na hasimu wake Deusdelity Macha. Walipoonana tu, mabondia wale walisogeleana na kutunishiana vifua huku wakitazamana usoni kwa ghadhabu, wapiga picha za televisheni na magazeti wakipiga picha tukio lile kwa bashasha.
"Nilipata ujumbe wako kutoka kwa Inspekta Fatma, Roman...na nilimwambia kuwa nitakujibu ulingoni siku ya tukio...na sasa siku imewadia!" Deus alimwambia kwa sauti iliyojaa uchokozi. Roman alibaki akimtazama kwa ghadhabu, akiwa amebetua midomo yake kwa kukereka, lakini hakumjibu kitu.
"Vipi, leo huna la kusema Roman? Hakuna macho ya watu ya kukupa kiburi cha kuropoka utumbo wako?" Deus alimsaili kichokozi. Roman alizidi kumtazama kwa ghadhabu, sasa midomo ikimcheza kwa hasira, misuli ikiwa imememtutumka, mishipa ya shingo ikiwa imemsimama.


"Nilipokuwa napelekwa gerezani nilikuahidi jambo Deus..." Hatimaye Roman alimjibu kwa sauti iliyojaa ghadhabu na dhamira halisi, "...kesho nitakutimizia hiyo ahadi, kwa hiyo usiniharakishe...vumilia kidogo tu, ahadi itatimia!"
Uso wa Deus ulimbadilika, na akafunua kinywa kutaka kusema kitu, lakini muda huo huo walinda usalama wakaja kuwatenganisha.
Zoezi la kupimana uzito lilipokamilika, waandishi wa habari waliwahoji wale mabondia kwa muda, na Deus akajigamba kuwa yeye ndiye bingwa na ataendelea kuwa bingwa baada ya pambano lake na Roman.
Kwa upande wake Roman alirudia ile ile kauli yake aliyoitoa kule Kairo, na pale uwanja wa ndege wa JK Nyerere. Alikuwa anaenda ukumbini kuchukua mkanda wake alioushinda kule Kairo.
Magazeti yakaandika, redio an televisheni zikanadi, na homa ya ushabiki juu ya nani atamshinda mwenzake kati ya Roman Kogga na Deusdelity Macha ilipanda mara dufu...


***


Ulingo wa kimataifa ulitengenezwa ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini. Ukumbi ule ulibadilika kwa kupambwa kimataifa. Watazamaji na majaji walioteuliwa na shirikisho la ndondi duniani walikuwa wameshaingia ukumbini saa kumi na mbili za jioni. Mapambano kadhaa ya utangulizi,au exhibition, yalifanyika, lakini ilikuwa wazi kuwa wote waliofurika ukumbini usiku ule walikuwa wamekuja kushudia pambano kati ya bingwa wa dunia Desudelity Macha, na mpinzani wake mkubwa kabisa, Roman Kogga.
Ndipo muda ulipowadia, ukumbi ukiwa umejaa wahka, mtangazaji maarufu alipanda ulingoni na kutangaza kuwa muda wa pambano kuu la usiku ule, au main card, ulikuwa umewadia. Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi na vifijo.


Mwamuzi wa pambano lile kutoka Caracas, Venezuela, alipanda ulingoni na kuwaita mabondia. Ndipo kwa mbwembwe za hali ya juu, mtangazaji alianza kwa kumuita mpinzani, Roman Kogga ulingoni. Roman aliingia ukumbini kutokea mwenye chumba cha mapumziko akiwa kidari wazi na chini amevaa bukta yake nyeusi ikiwa na mkanda mpana kiunoni, jina lake la kwanza likiwa limeandikwa kwenye mkanda wa bukta ile kwa maadishi makubwa ya rangi nyeupe. Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi wakati alipokuwa akikimbia kibondia kuelekea ulingoni akisindikizwa na second wake, ambaye pia ndio alikuwa kocha wake, Mark Tonto. Roman alipanda ulingoni na kukimbia huku na huko, akitupa ngumi hewani kwa kasi ya ajabu kisha akajipigapiga kifuani na kuinua ngumi yake juu kwa ishara ya ushindi. Ukumbi ulipagawa kwa vifijo. Kwenye viti vya watazamaji, Dan Dihenga alimgeukia Kate kwa jazba.


"That's my boxer! Leo ndio Deus atajuta kunisaliti mwanaharamu!" Alimwambia. Kate alibaki akitazama kwa wasiwasi. "Naomba mungu amsaidie Roman ashinde Dan...naomba sana!"
"Ooh! Atashinda tu Kate...atashinda..tena kwa kishindo!"
Kule ulingoni, mtangazaji alimnadi bingwa Deus "deadly" Macha, na muda huo Deus naye alitoka chumbani kwake na kuelekea pale ulingoni, akiwa kifua wazi, na chini akiwa ameva bukta nyekundu, jina lake likiwa limeandikwa kwa maadishi makubwa meusi kwenye mkanda mpana wa bukta ile, mkanda wake wa ubingwa wa dunia akiwa ameuning'iniza begani kwake. Ukumbi ulimpokea kwa shangwe na mayowe mengi, naye akawa anatembea taratibu kuelekea ulingoni akisindikizwa na kocha wake huku akiwa ameinua juu ngumi yake.


Lakini ilionekana wazi kuwa Deus alikuwa anaenda ulingoni kama ng'ombe anayepelekwa machinjoni. Hakuonesha bashasha ambayo mashabiki wake waliitarajia.
Alipanda ulingoni, na hapo alibadilika ghafla. Alianza kurukaruka huku na huko, na kutupa ngumi za haraka haraka hewani huku ukumbi ukimshangilia kwa jazba, kisha akageuka kila upande wa ulingo akiuonesha juu ule mkanda wake aliokuwa anaushikilia.
Baada ya kila bondia kufanya majigambo yake ulingoni, mwamuzi aliwatuliza na kuwaita ili kuwapa nasaha za maadili ya pambano. Kisha kila bondia akarudi kwenye kona yake.Mwamuzi aliwaita kati ya ulingo na wale wapinzani wawili wakaziacha kona zao na kwenda kusimamiana kibondia katika ile pozi ya honour stance, wakisubiri amri ya kuanza pambano. Hatimaye kengele ya kuanza pambano ikagongwa, na mwamuzi akaruhusu pambano.
Deus alianza raundi ya kwanza kwa kasi. Akimshambulia Roman kwa ngumi za haraka haraka na zenye uzito wa kumpeleka mtu chini, lakini Roman alikuwa mtulivu, akimkwepa na kumtandika ngumi za kudokoa na mara moja moja akimtupia ngumi kali za ghafla ambazo hazikuleta madhara yoyote kwa Deus. Na sekunde chache kabla ya raundi ya kwanza kuisha, mabondia wale wawili walijikuta wakiwa wamekumbatiana.
"Umemuua mdogo wangu Deus...sasa leo ndio nami nakutimizia ahadi niliyokupa siku ile nilipokuwa napelekwa gerezani, mshenzi we!" Roman alimnong'oneza kwa hasira. Deus alifurukuta kujichomoa mikononi mwa Roman, lakini Roman alizidi kumbana mpaka refa alipokuja kuwatenganisha. Wote walirudi kwenye kona zao na kuanza kurudiana tena kwa pambano wakati kengele ya kumaliza raundi ilipogonga.
"Unamchezea Roman!" Mark alimkemea Roman wakati wa mapumziko. Roman alibaki akimkodolea macho yaliyojaa vitisho Deus, ambaye alibaki akimtupia macho huku akitweta kutokea kule kwenye kona yake.
"Nampiga taratibu...mpaka ajute kujiingiza kwenye ndondi!" Roman alimjibu kocha wake na kuinuka kurudi ulingoni baada ya kengele ya raundi ya pili kugongwa.


Raudi ya pili, Deus aliingia kwa kasi kali zaidi, sasa akionesha hasira za wazi wakati Roman alikuwa mtulivu zaidi, akimtupia makonde ya kushtukiza huku akimcheka mpinzani wake. Lilikuwa ni pambano kali, na kwa dakika moja nzima, Deus alimbana Roman kwenye kona na kumvurumishia makonde makali ya mfululizo huku ukumbi ukirindima kwa hoi hoi, lakini Roman alifanikiwa kuyakwepa masumbwi yale akiwa pale pale kwenye kona, mengine akiyakinga na machache yakimpata, ndipo akiwa pale pale kwenye kona alipojikunja na kujikunjua kwa sumbwi kali la upper cut lililojikita sawia kidevuni kwa Deus na kumyumbisha vibaya, naye akajichomoa kutoka kwenye ile kona na kurudi kati kati ya ulingo. Lakini sasa Deus alikuwa ameshapata matumaini ya kumuangusha mpinzani wake hivyo akamuendea tena kwa kasi, Roman akampisha kidogo na wakati huo huo akimzungushia ngumi ya kushoto, Deus aliiona na kujikinga haraka, na kushitukia akipokea cross nzito ya cross mkono wa kulia lililotua sawia kwenye upande wa uso wake. Deus aliyumba mpaka kwenye kamba na ukumbi ulichangamka kwa vifijo.


***MAMBO ULINGONI....MBABE KUPATIKANA HATIMAYE........
Khantwe muuza ubuyu mbalu
 
Last edited by a moderator:
RIWAYA: BONDIA
MTUNZI: ISSA TUWA


SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA


Roman alibaki akirukaruka katikati ya ulingo akimsubiri mpinzani wake, ingawa ile ilikuwa ni nafasi nzuri ya kumbana Deus pale kwenye kamba na kumsulubu atakavyo. Deus alirudi kwa hasira na kujaribu kumtupia makonde ya nguvu. Roman alimpisha tena kidogo na kumtandika konde la mbavu, na Deus alijikunja huku akimkumbatia Roman.
“Unamkumbuka Rachel Deus...?” Roman alimnong’oneza wakiwa wamekumbatiana pale ulingoni. Deus alijikurupusha kujinasua kutoka mikononi mwake, wazi kuwa yale maneno ya Roman yalikuwa yakimchanganya, na Roman alitumia nafasi hiyo kumuachia ghafla na hapo hapo akampa upper-cut nyingine ya kulia iliyotua tena kidevuni. Deus alipepesuka na kuangukia goti pale ulingoni. Ukumbi ulilipuka kwa shangwe, na Roman alikuwa anamuendea wakati kengele ya kumaliza raundi ulipogonga, na ukumbi ukaachia mguno wa fadhaa.
Pambano liliendelea kwa raundi nyingine mbili, na waliposhikana tena kwenye raundi ya tano, Roman alimnong’oneza, “Unakumbuka jinsi nilivyokuvunja taya Deus...? Unakumbuka jinsi nilivyoua mabondia wawili ulingoni...?”
Deus alipiga ukelele kwa hasira na kumsukuma nyuma kwa nguvu. Mara moja refa aliingilia kati na kuweka nidhamu pale ulingoni. Deus alibaki akimkodolea macho ya ghadhabu Roman huku akitweta, wakati Roman akimtazama huku akimcheka. Sasa Deus alionekana wazi kuwa alikuwa akipigana huku akiwa makini sana na ngumi ya kushoto ya Roman, lakini kufikia raundi ya saba, mabondia wote walionekana kama kwamba walikuwa wametoshana nguvu. Lakini ilipofikia raundi ya nane, Roman aliingia na mtindo tofauti kabisa wa upiganaji.
Badala ya kusimama kwa mtindo aliokuwa akiutumia tangu mwanzo wa pambano wa orthodox, yaani kusimamia kulia, ambao ndio ungempa nafasi nzuri zaidi ya kumpiga mpinzani wake kwa mkono wa kushoto, yeye sasa alitumia mtindo wa kusimamia kushoto, yaani southpaw.


Deus alichanganyikiwa, kwani kwa kutumia msimamo huu, Roman hangeweza kutupa konde la kushoto, hivyo akahisi Roman amejisahau, naye akaingia kwa makonde ya nguvu na ya mfululizo. Katikati ya raundi ile, ghafla bila ya Deus kutaraji, Roman alirudisha tena mtindo wa orthodox na kumtupia konde kali la kushoto lililomkosa kichwani Deus kwa umbali mdogo sana. Deus akajibu kwa konde la kulia la mtindo wa jab, lililompata Roman tumboni. Roman akayumba, Deus akaingia mzima mzima kwa sumbwi la cross, ambalo linapigwa kwa karibu huku mpigaji akienda na mwili wake wote kwa mpinzani wake. Roman alikuwa ametarajia jambo hili, hivyo alijikunja huku akilalia kulia na kumpisha na wakati huo huo akijikunjua huku akiachia right hook iliyotua upande wa kushoto wa kichwa wa Deus. Deus aliyumba, na hapo hapo Roman akalalia kushoto na kujikunjua haraka huku akiachia left hook iliyompata Deus upande wa kulia wa kichwa.
Deus akapoteza mwelekeo, sasa Roman alikuwa upande wake wa kushoto na sio mbele yake tena, ukumbi ulikuwa umepagawa kwa shangwe. Deus akageuka haraka kushoto kwake, lakini Roman akaruka hatua moja mbele na kumtupia ngumi sita za mfululizo za usoni kwa mtindo wa one-two, yaani kulia na kushoto kama mara tatu hivi, kila ngumi iliyoingia ilikuwa ikipokelewa na ukelele wa pamoja kutoka kwa watazamaji. Deus akayumba nyuma na kuangukia kwenye kamba, Roman aliingia pale pale kwenye kamba kwa upper cut ya kulia, na kwenye nukta ya mwisho kabisa akabadili mkono na kumshindilia Deus kwa upper cut ya kushoto iliyompata sawia kidevuni, na hapo Roman aliona macho ya Deus yakipinduka, weusi wa mboni ukipotelea ndani ya macho, na bila kusubiri zaidi alimmalizia na hook ya kulia iliyompata Deus kichwani na kumpeleka moja kwa moja sakafuni kama mzigo.
E bwana we!
Si shangwe hizo ukumbini! Hoi hoi,mbinja na mayowe ya kupagawishwa vilitawala. Dan Dihenga na Kate waliruka wima na kushangilia huku wakikumbatiana, Mark Tonto akifuatilia kwa makini wakati Roman akirudi kwenye kona yake na mwamuzi akianza kumhesabia Deus.
Huku nje ya ukumbi, Inspekta Fatma akiwa katika mavazi ya fulana, suruali ya jeans na kofia ya kepu kichwani alijipenyeza hadi kwa kocha wa Deus.
“Simamisha pambano hili...simamisha sasa hivi kocha uokoe maisha ya bondia wako!” Alimwambia kwa wahka huku akimvuta mkono.
Kocha wa Deus alimgeukia kwa mshangao.
“Khah, we’ mwanamke vipi...? Hebu toka hapa...!”
“No! Mimi ni afisa wa polisi na najua kinachoelekea kutokea...”
“Hebu toka hapa, ebbo!” Kocha alimkemea na kugeukia kule ulingoni, wakati askari wa usalama pale ukumbini walipokuja kumvuta kando Inspekta Fatma.
Kule ulingoni Deus aliwahi kusimama ilipofikia nne na kujiweka tayari kwa pambano. Refa alimuuliza iwapo yuko sawa, akaafiki kwa kichwa. Akamuwekea vidole viwili mbele ya uso wake na kumuuliza anaona vingapi, Deus akamjibu anaona viwili. Refa akaruhusu pambano liendelee.
Kutokea upande wa pili wa ulingo Mark Tonto, Kate na Dihenga waliona kile kilichokuwa kikitokea baina ya Inspekta Fatma na kocha wa Deus, ingawa hawakuweza kuelewa ni kwa nini kilikuwa kinaongelewa.
Sasa ukumbi ulikuwa hauna utulivu hata kidogo. Deus aliingia kwa kasi ya ajabu, akiwa na ghadhabu za kupelekwa chini na mpinzani wake wakati Roman akiwa amedhamiria kumaliza mchezo na kumuweka Deus mahala pake. Deus alikuja na ngumi ndefu-ndefu za mfululizo, na kwa muda walikuwa wakizungukana bila ya madhara kwa yeyote, lakini ghafla sana Roman alibadilika. Alimuendea kwa kasi mpinzani wake na kusita kama kwamba alikuwa amejigonga miguu na kupoteza uelekeo, akijikunja kutokea kwenye magoti kama anayetaka kuanguka. Deus aliiona nafasi ile na hakuifanyia ajizi. Alimuendea kwa left hook iliyobeba nguvu zake zote, na hapo, bila kutarajiwa, Roman aliruka mbele huku bado ameinama, na kujiinua wima akiwa moja kwa moja mbele yake.
Deus akajikuta yuko karibu sana na Roman kiasi cha kutoweza kumpiga kama alivyokusudia. Haraka alijitahidi kurudi nyuma lakini alikuwa amechelewa kwani tayari alikuwa ameshaingia kwenye mtego wa Roman kama inzi aingiavyo kwenye utando wa buibui, na wakati alipojiinua wima namna ile, Roman aliinuka na upper cut nzito ya kulia na hapo hapo akaifuatishia na upper cut nyingine ya kushoto. Yaani ilikuwa ni one-two ya upper cut! Si mabondia wengi wanaoweza kupiga namna ile, na mara lipigwapo pigo la namna ile, basi huwa ni pigo la kumaliza mchezo.
Ukumbi ulipayuka kwa mayowe, wakati kwa mara nyingine katika raundi ile, Deus alipojiona akinyong’onyezwa nguvu za magoti na mikono kwa mapigo ya Roman. Roman alimuona mpinzani wake akilegea, na ndipo kwa nguvu zake zote, alipomshushia konde la mkono wake wa kushoto kwa mtindo wa left hook. Deus aliiona ngumi ikimwendea kakini hakuwa na nguvu tena ya kuikwepa wala kujikinga. Ngumi ilimpata juu kidogo ya sikio na kumpeleka kiubavu-ubavu mpaka chini, akisambaratika sakafuni na kugaragara vibaya.
Ukumbi uliachia shangwe za ajabu...
“Kwisha kazi bloody kenges! Roman kamaliza mchezo bloody bastard!” Dihenga akamgeukia Kate na kumwambia kwa bashasha.
Lakini kwa namna ambayo haikutegemewa, Deus alijiinua haraka na kusimama. Akayumba kinyuma-nyuma na kuegemea kamba. Mashabiki wake waliamsha hoi hoi za kumtia moyo, wakitaja jina lake kwa pamoja.
Deeee-us...deadly!
Deeee-us...deadly!
Deee-us...deadly....
Inspekta Fatma alimfuata kocha wa Deus kwa mara nyingine.
“Inabidi usimamishe hili pambano sasa hivi kocha! Please...!” Alimwambia kwa jazba. Lakini kocha alikuwa makini na kile kilichokuwa kikiendelea kule ulingoni.
“No! Anaendelea na pambano bado mwanamke! Hebu tok...”
Fatma alilikwapua taulo jeupe kutoka mabegani kwa yule kocha na kurukia kamba za ule ulingo huku akilitupia ndani ya ulingo lile taulo.
“No Dan...look...!” Kate alipayuka huku akioneshea kule ulingoni, ambako Inspekta Fatma akiwa ameshikilia kamba za ulingo huku akipayuka maneno ya wahka.
Mwamuzi alishangaa kuona taulo likitupiwa ulingoni na mtu asiye kocha wa yeyote kati ya wale mabondia wawili. Ukumbi mzima uliachia mguno wa fadhaa uliofuatiwa na kelele za kuchanganyikiwa.
Roman alimtazama yule askari mtukutu kwa hasira, wakati Deus akimgeukia kwa mchanganyiko wa mshangao na kutoelewa.
“Achana na hili jambo Deus! Huwezi kushinda hili pambano...okoa maisha yako!” Inspekta Fatma alimpigia kelele yule bondia aliyeelemewa. Hapohapo Fatma akamgeukia Roman.
“Haina haja ya kuendelea na pambano Roman, tayari umeshaonesha uwezo wako...achana na visasi!”
“Toa nje huyo mwanamke!’ Mwamuzi alipiga kelele wakati askari wa jeshi la polisi waliokuwa kwenye sare rasmi za kazi wakimkamata tena Fatma na kumvuta kutoka ulingoni.
Fatma alizing’ang’ania zile kamba huku akipiga kelele.
“No, niacheni! Deus achana na pambano hili tafadhali! Kubali kushindwa tu...there is no way utashinda hili pambano! Mwenzio hakuja ulingoni kwa nia ya mchezo kama wote hapa wanavyodhani, nawe walijua hilo! Get out now wakati bado uko hai Deus...PLEASE!”
Deus alimtazama yule mwanadada akitolewa pale kwenye kingo za ulingo huku akitweta. Alimgeukia Roman aliyekuwa amesimama katika ile honour stance akisubiri uamuzi kutoka kwake huku akimtazama kwa macho ya ghadhabu iliyokithiri.
“Yuko sahihi Deus! Kubali kushindwa...huu mkanda hauna thamani ya maisha yako!” Alimwambia, na akaona Deus akikunja uso kwa ghadhabu maradufu.
Kule nje kocha wa Deus alikuwa akiruka huku na huko kwa hasira, akipinga kitendo cha yule mwanadada kurusha taulo ndani ya ukumbi bila ya ridhaa yake. Kule kwenye meza ya majaji nako kulikuwa kuna mtafaruku mkubwa, baadhi wakisema pambano liendelee wakati wengine wakishauri lisimamishwe.
Huku ulingoni, Deus alilitazama lile taulo lililokuwa mbele yake pale chini, kisha akamtazama Roman huku bado akiwa amekunja ngumi kimapambano.
“Umemuua Rachel Deus...na ukiendelea na huu mpambano mi nakuua! Acha sasa, na adhabu pekee utajkayopata ni kuukosa huo mkanda! Inua mikono juu uombe suluhu Deus...huenda Inspekta Fatma akawa sahihi!”
Deus alizidi kumtazama kwa ghadhabu za hali ya juu. Alilitazama lile taulo pale chini, na kurudisha tena macho yaliyojaa chuki kwa Roman.
“Usiwe mjinga Deus...!”
Kwa mguu wake wa kulia Deus alilisukumia nje ya ulingo lile taulo na kujizatiti katika ule msimamo wa honour stance tayari kuendelea na pambano huku akimtazama Roman kwa ghadhabu.
“Sikuja hapa kushindwa Roman! Kama unadhani maisha ni bora zaidi ya mkanda, jitoe wewe kwenye pambano!” Alimwambia kwa hasira, na Roman akaona kuwa yule jamaa alikuwa amedhamiria.
Ukumbi uliamka kwa hoi hoi mpya, wakati Inspekta Fatma akijishika kichwa na kuangukia magoni sakafuni huku akitazama kile kilichokuwa kikitokea kule ulingoni kwa fadhaa kubwa.
Kabla mwamuzi hajapitisha uamuzi, iwapo pambano liendelee au lisiendelee, Deus alijiengemeza kwenye kamba na kuziacha zimsukume mbele kwa kasi naye akaenda mzima mzima huku akiachia ukelele wa ghadhabu ilhali akimsukumia Roman konde la mkono wa kulia.
Roman alimuona Deus akimwendea na ngumi ya mkono wa kulia huku miguu ikimuishia nguvu, na ndipo aliporuka mbele haraka kumfuata yule mpinzani wake bazazi, mkono wake wa kushoto ukiwa juu kabisa hewani, kisha akaushusha na kuuzungusha kutokea chini na kumshindilia konde zito sana kwenye upande wa kichwa chake chini kidogo ya jicho lake la kulia.




**DEUS hoiiii…….lakini bado anatapatapa……
JE ATAFIA ULINGONI???
Khantwe muuza ubuyu Jullie Z ram mbalu
 
Last edited by a moderator:
hahahahhh...kama namuona vile anavyotapatapa......tehteh ...ROMAN muue taratiiiiiiiiiibu.....eti bloody kenges..tehtehteh na mimi naenda kuwa bondia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…