Riwaya: Bondia

na kwa nje inspekta fatma nae anataman nyie c mnapenda mbavu nene kama sie vimbaumbau tupa kule

Hahahaha Fatma aende huko kwa wapolisi wenzake....hahaa ujue kinachovutua kwa Roman sio mbavu tu...his character acha kabisa
 
aisee inabidi nirudi dar fasta kuchek pambano,,,, dah yani nimejenga taswira kichwani kwamba ni ukweli dah kumbe ni simulizi,,, natamani ingekua ni ukwelii.. weka nyingine mkuu.. dreams might come true.. loll

Rudi mjini mkuu, nna tiketi yako
 
Jamani, msidhani kwamba sipo, nipo nimechungulia tu hapa! Casuist!
 
Last edited by a moderator:
RIWAYA: BONDIA
MTUNZI: HUSSEIN ISSA TUWA


SEHEMU YA KUMI NA SABA


Rachel hakulazimika kuishi peke yake nyumbani kwa Roman. Pia alimfungulia akaunti na kuweka maelekezo maalum ya kukatwa sehemu ya mshahara wake kila mwezi na kuingizwa moja kwa moja kwenye akaunti ya Rachel. Siku ya safari ilipowadia, kaka na dada waliagana kwa huzuni.
“Usiwe na wasiwasi Rachel, tutakuwa tukiwasisliana kwa mtandao mara kwa mara...na kama kuna tatizo lolote litakalokuwa nje ya uwezo wako, muone kaka yako Deusdelity...atakusaidia”. Roman alimwambia mdogo wake wakiwa uwanja wa ndege.
“Sawa kaka...uende salama...” Rachel alijibu huku akibubujikwa machozi.
“Come on Rachel...sio kwamba Roman anaenda kuuawa huko bwana...anaenda kuongeza elimu kwa faida yenu nyote. Usilie namna hiyo...tumuombee mungu tu huko aendako arudi salama, au sio?” Deusdelity Macha, aliyekuwa pamoja nao pale uwanja wa ndege alimfariji Rachel.
“Najua kaka Deus...lakini...” Rachel alijitahidi kujibu lakini hakuweza kumalizia, alizidi kulia. Roman alimkumbatia mdogo wake kwa muda mrefu, kabla ya kumtazama usoni kwa muda, machozi yakimlenga-lenga, na kumbusu kwenye paji la uso. Aligeuka na kuingia ndani ya uwanja ule bila kugeuka nyuma. Akiwa ndani ya uwanja, ambapo alijua hawataweza kuona jinsi alivyokuwa akitiririkwa na machozi, aligeuka na kuwapungia mkono. Deus na Rachel walimpungia, naye akapotelea ndani ya eneo la kusubiria ndani ya uwanja ule.
Ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kumuona mdogo wake akiwa hai...


***


Ndani ya mwaka wake wa kwanza alikuwa akiwasiliana mara kwa mara na Rachel na Deus, na mara moja moja sana alikuwa akiwasiliana na Sajini Meja Makongoro Tondolo. Na katika moja ya mawasiliano yao adimu na kocha wake wa zamani wa ndondi, Mark alimfahamisha Roman kuwa alikuwa ameamua kustaafu jeshi ili aweze kusimamia miradi yake binafsi na apate muda zaidi wa kuinua mchezo wa ndondi. Roman alimtakia kila la kheri, naye akaendelea na masomo yake. Siku moja, akiwa ameanza mwaka wake wa pili wa masomo yake kule uingereza, Roman alipokea simu usiku wa manane kutoka Tanzania.
“Eh...hallo...”
“Roman...this is Mark...Mark Tondolo!”
“Mark...? Coach...? vipi za huko, kwema?”
“Huku si kwema Roman...ni Rachel...”
“Rachel...?”
“Amekunjwa sumu...ana hali mbaya sana...”
“Whaaaat? Ame...Deus yuko wapi...?” Roman alihamanika, usingizi wote ukimkauka ghafla, moyo ukimuenda mbio.
“Sijui Roman...Deus hapatikani...mi’ nimepigiwa simu na wanafunzi wenzake waliomfikisha hapa hospitali...walipewa namba na Rachel mwenyewe kabla hajaingizwa ICU...!” Mark alijibu.
Saa tano baadaye, Roman alikuwa kwenye ndege akirejea Tanzania. Akili ilikuwa ikimzunguka muda wote alipokuwa angani, machozi yakimbubujika, donge kubwa likiwa limemkaba kooni.


***


Mark Tonto alikuwa akimsubiri uwanja wa ndege. Alipomuona tu alijua kuwa kuna kitu hakikuwa sawa. Alitupa chini begi lake na kumkimbilia pale alipokuwa amesimama.
“Mark! Coach...vipi Rachel...yuko hospitali gani....? Deus je...?” Roman alimvurumishia maswali ya wahka, lakini Mark alikuwa amesimama kimya akimtazama kwa huzuni, midomo ikimtetemeka. Roman alimshika mabega na kumtazama kwa woga mkubwa. Macho ya Mark yalimthibitishia kile alichokuwa akikihofia tangu anapanda ndege kurudi nyumbani.
“No, Mark...No!” Alisema kwa maombolezo. “...usiniambie kuwa Rachel ame...ame...”
“She is dead Roman...Rachel is dead!” Mark alimjibu kwa huzuni huku akimkumbatia. Maneno yale yaliuchoma moyo wake kama kwamba yalikuwa ni msumari wa moto.
“Ah! Coach...imekuwaje? Kwa nini lakini...?” Roman aliuliza huku akilia kama mtoto.
“Twende nyumbani Roman...ni hadithi ndefu kidogo...”
“No! Nipeleke nikamuone mdogo wangu bwana! Na Deus yuko wapi lakini?” Roman alibwabwaja wakati Mark akimuongoza kwenye teksi.
“Tutamtafuta Deus baadae Roman, sasa tushughulikie msiba uliopo mbele yetu...” Mark alimjibu.
Alipouona mwili wa mdogo wake Roman alipoteza fahamu pale pale hospitali. Alipozinduka, alikuwa amelazwa kitandani pale hospitali. Mark Tonto alikuwa ameketi kwenye kiti kando yake.
“Oh, Mark...Rachel ametutoka Mark...” Roman alibwabwaja huku akiinuka na kuketi pale kitandani. Mark aliinuka na kuketi pamoja naye pale kitandani. “Ni amri ya mungu Roman...kuwa jasiri ndugu yangu...”
“Si amri ya Mungu hii Mark...ndugu yangu amekunywa sumu. Ina maana aidha amejiua, au ameuawa...sijui kipi ni kipi, lakini lolote litakalokuwa kati ya hayo mawili, jibu linabaki kuwa hii si amri ya Mungu!” Roman alisema kwa uchungu. Mark alimkumbatia rafikiye kwa kumfariji.
“Usikufuru Roman...hakuna litokealo bila mapenzi ya Mungu bwana. Wewe ni mpiganaji, pigana na hili kijasiri Roman...”
Roman alianza kulia upya.
Muda mfupi baadaye tabibu aliyempokea Rachel pale hospitali alifika kuonana na Roman.
“Pole sana Kepten Kogga...pole sana.” Yule tabibu alimwambia, na Roman alimtazama na kuitika kwa kichwa.
“Okay, sasa...nadhani unahitaji kujua mazingira ya kifo cha mdogo wako Kepten...” Tabibu alimwambia.
“Najua...amekunywa sumu...” Roman alisema taratibu.
“Yeah...ilikuwani sumu kali na nyingi, kiasi kwamba pamoja na jitihada zetu zote, hatukuweza kuokoa maisha yake wala ya kiumbe kilichokuwa tumboni kwake...”
“Whaaat?” Roman alimaka na kumtazama kwa makini yule tabibu. “...ki...kiumbe? kiumbe gani tumbon...oh, My God, yaani Rachel alikuwa mjazito?”
“Oh, hukuwa na habari...? Ndiyo, Rachel alikuwa na ujauzito wa miezi minne...”
Roman aliona kuwa dunia yote ilikuwa imeamua kumsaliti na kumzonga. Alimtazama yule tabibu kwa uchungu, kisha akamgeukia Mark.
“Ni nini hiki kinachotokea kwangu jamani, enh? Ni nini lakini...?” Aliuliza kwa uchungu huku akilia. Mark alibaki akitikisa kichwa tu.
“Sasa...sasa...huyu mwenye ujauzito huo...aliyembebesha ujauzito mdogo wangu...anafahamika? Mark, we unamfahamu?” Alimuuliza Mark kwa hamaniko kubwa kabisa. Mark aliuma midomo yake kwa uchungu. “Hata mimi hii habari imenijia kwa mshituko mkubwa Roman...”
“Oooh, Mark....!” Roman alisema kwa masikitiko, machozi yakimbubujika.


***


Mark aliandaa taratibu zote za mazishi. Msiba uliwekwa nyumbani kwake, na maziko yalifanyika siku iliyofuata, bila ya Deusdelity Macha kuhudhuria. Baada ya maziko, watu wachache walioshiriki kwenye msiba ule walibaki pale nyumbani kwa Mark, wakiwemo wananfunzi na walimu wa shule aliyokuwa akisoma marehemu.
Roman alimfuta Mark na kumwambia, “Mark, sasa nimekubali kuwa Rachel amekwenda na hatorudi tena. Ila bado nina mambo matatu yanayosumbua kichwa changu Mark, na haya sitatulia mpaka niyapatie majibu...”
Mark Tonto alimtazama tu rafiki yake bila ya kusema kitu, na Roman aliendelea, “Kwanza, ilikuwaje hata Rachel akanywa sumu...” alitulia kidogo, na kuendelea, “...pili, ni kwa nini Deus, ambaye ndiye niliyemkabidhi jukumu la kumuangalia Rachel wakati mimi sipo, hajaonekana kabisa katika msiba huu...” kisha akamalizia, “na tatu, ni nani huyu aliyempa ujauzito mdogo wangu...?”
Mark alitikisa kichwa kuafiki umuhimu wa mambo yale huku uso wake ukiwa umefanya tafakuri zito. Alikaa kimya kwa muda mrefu, kisha taratibu aliinua uso wake na kumtazama Roman.
“Majibu ya maswali hayo yapo Roman, ila ni machungu sana rafiki yangu...”
“Hayawezi kuwa machungu kuliko uchungu wa kifo cha mdogo wangu Makongoro...”
Kimya kilitawala kwa muda baina yao, kisha Mark akasema. “Basi itabidi nikukutanishe na binti aitwaye Sada, Roman, yeye ana majibu ya maswali yote hayo...”
Roman alishikwa wahka mkubwa.
“Ni nani huyu Sada, na...yuko wapi?”
“Huyu ni rafiki mkubwa wa marehemu...na yupo hapa hapa msibani.”
Maelezo ya Sada yalibadili kabisa muelekeo wa maisha ya Roman...


*******


Sada alikuwa rika moja na Rachel, na alipoonana uso kwa uso na Roman hakuweza kujizuia kuangua kilio upya. Mark na Roman walijitahidi kumtuliza, na baada ya muda, alijifuta machozi kwa upande wa khanga yake, akapenga kamasi laini kwa khanga ile ile na kuwaangalia wale watu wawili waliokuwa mbele yake.
“Sa...samahani sana...”
“Usijali, ni msiba mkubwa kwetu sote Sada.” Mark alisema kwa upole, kisha akaendelea, “Sasa naomba umueleze Kapten Roman hapa, yale uliyonieleza mimi juu ya Rachel, na mazingira ya kifo chake.” Mark alimwambia.
“Okay...kaka zangu...” Sada alisema na kupenga tena kamasi.
“Na...naweza kusema kuwa mimi ndiye nilikuwa rafiki wa karibu sana wa mar...wa Rachel. Alikuwa akikuongelea sana kaka Roman. Kwake wewe ulikuwa ni shujaa asiyeshindwa na lolote...” Roman aliuma midomo kwa uchungu, lakini alijitahidi kujizuia, alitaka kujua ukweli wa kifo cha ndugu yake. “...pia alinieleza kuhusu Deus, ya kwamba ni rafiki yako mkubwa na kwamba ndiye angekuwa anamsaidia iwapo atakutwa na tatizo lolote kubwa. Kiujumla tuliishi bila matatizo pale shuleni, na kaka Deus alikuwa akija kumtembelea Rachel mara kwa mara na mara nyingine, siku za mwisho wa wiki alikuwa akija kutuchukua na kutupeleka kula Ice Cream au sinema na kuturudisha shuleni...”
Roman alizidi kusikiliza kwa makini.
“Sa’ siku moja, tukiwa kwenye likizo ya katikati ya muhula, Rachel alienda mjini na Deus, na aliporudi aliniambia kuwa ...kuwa...kaka Deus alim...alimtaka kimapenzi!”
“Whaat??” Roman alimaka kwa kutoamini, macho yakimtoka pima. “Deus???”
“Ndio kaka Roman...nilishituka sana. Rachel alilia sana siku ile, hakuamini kuwa kaka Deus angeweza kumtamkia jambo kama lile...”
“Mwanaharamu...! Yani Deus anaweza kunifanyia hivi?” Roman alisema kwa uchungu.
“Hujasikia habari yote Roman...muache binti aendelee, kisha tutajadili kwa undani swala hili.” Mark alimwambia.
“Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa ni Deus ndiye aliyembebesha mimba Rachel?” Roman aliuliza kwa jazba, mishipa ya shingo ikiwa imemtutumka. Sada alitikisa kichwa kwa masikitiko.
“Mnhu! Dunia ina mambo kaka zangu...hali ilienda mpaka Rachel akajikuta akikubaliana na hoja za Deus...nadhani Deus alikuwa na nguvu ya kubwa ya ushawishi. Wakawa wapenzi...” Sada alisema na kuanza kulia.


“Ah!” Roman aliguna, na kubaki akitikisa kichwa, macho yake yakitoa mng’aro wa ghadhabu isiyo kifani. Sada aliendelea kueleza kuwa Rachel alimwambia kwamba Deus alimuahidi kumuoa “...alimwambia kuwa...kuwa hata wewe, kaka Roman, ungefurahia kuwa shemeji yake...”
“Ah, sasa mbona sikuambiwa juu ya uchumba huo? Uongo mtupu!” Roman alimaka.
“Walikubaliana kuwa wakusubiri mpaka urudi...Deus ndio angeongea nawe kwanza...ilionekana ni utaratibu mzuri tu kwa wakati ule...”
“Mzuri? Ni utaratibu mzuri huo? Mtu namkabidhi mdogo wangu yeye anaenda kumtongoza?”
“Namaanisha huo utaratibu wa kukusubiri urudi na Deus aongee nawe...lakini mambo yaliharibika pale Rachel aliposhika ujauzito...”
“Deus akamkana...!” Roman alidakia kwa jazba, sasa machozi yakimtiririka waziwazi. Sada alitikisa kichwa kwa simanzi. “Hapana. Akamtaka atoe ile mimba...!”
“Ama!?” Roman alimaka kwa mshangao, “Yaani...kwa nini?”
“Kuna sheria kali sana dhidi ya wanaume wanaowatia mimba wanafunzi kaka Roman. Deus alikuwa akiogopa hilo, lakini Rachel hakutaka kutoa mimba. Alimwambia akupigie simu huko uliko akueleze kila kitu...Deus hakuwa tayari, alisisitiza msimamo wake kuwa Rachel atoe mimba. Ikawa mizozo na majibizano. Rachel akaanza kukosa kuhudhuria masomo, kutwa barabarani akimtafuta Deus. Hali ilipozidi kuwa mbaya, Rachel akamtishia kumshitaki kwa wakuu zake wa kazi. Deus alikuja juu, na hapo ndipo alipomtakia kuwa haujui ule ujauzito...”


***KUMBE DEUS alifanya mambo haya mabaya kwa mdogo wa rafiki yake…….
HUENDA ROMAN anayo haki ya kulipa kisasi…


LAKINI JE? ATAFANIKIWA????
Toplady
ram BPM Sangomwile Mamamercy jonnie_vincy Khantwe mbalu byb sac mlyn VAN HEIST nrango mangimeza muuza ubuyu Jullie ZIgunga Mojaculbby mugaru
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…