Riwaya: Bondia

Casuist mi siwezi kulala bila kumuona Roman aisee
 
Last edited by a moderator:
Deus hakumpenda Rachel bali alimtamani ila alipoonjeshwa asali akanogewa ila kuchonga mzinga ili awe anapakua asali mwenyewe bilo lilimsbinda na kuamua kumkana.
 
Afadhali umekuja casuist... haya twende kazi sasa!!... maana tumekusubiria kinoma
 
RIWAYA: BONDIA
MTUNZI: HUSSEIN TUWA


SEHEMU YA KUMI NA TISA


Roman alizidi kumkaba Deus kwa ule mkanda, pua zikimtutumka, akitweta kwa ghadhabu.
"Niue nami nakufa naye afande!" Alisema kwa hasira, kisha akamalizia, "...huyu mwanaharamu kasabaisha kifo cha mdogo wangu gaddemitt, afande!"
"Utakufa wewe kwanza, naye utamuacha akitapatapa kutafuta pumzi, lakini akiwa hai. Muachie huyo askari sasa hivi!" Fatma, wakati huo akiwa koplo, alisema kwa msisitizo, bastola yake ikiwa kichwani kwa Roman. Na hata alipokuwa akisikia maneno yale, Roman alishuhudia askari wengine watatu wakivamia mle ndani, bunduki aina ya SMG zikiwa mikononi mwao, zote zikiwa zimemuelekea yeye, huku moto ukizidi kupamba mle ndani. Alihema kwa pumzi za haraka haraka, na huku bado akizidi kumkaba Deus kwa ule mkanda, alisogeza mdomo wake sikioni kwa yule rafiki yake aliyebadilika na kuwa adui yake mkubwa, na kumnong'oneza kwa sauti nzito ya kongofya.
"Umeokolewa na askari safari hii Deus, lakini ujue kuwa bado kifo chako kiko mikononi mwangu...I will kill you one day Deus...that's a promise (nitakuua tu siku moja Deus...nakuahidi hilo)!" Kwisha kusema hivyo, alimsukuma mbele kwa nguvu, akimuacha Deus akisambaratika ovyo sakafuni, naye akijikuta akisukwasukwa kwa nguvu na wale askari, mikono yake ikivutwa nyuma na akipachikwa pingu.
"Ita gari la kuzima moto hapa...upesi!" Koplo Fatma alibwata huku akimburura Roman nje ya kile chumba kilichokuwa kikiwaka moto mtindo mmoja. Nje ya nyumba ile kundi la watu waliojaa udadisi lilikuwa limetanda, wengi kati yao wakiwa ni majirani wa Deus pale mtaani. Akiwa ndani ya gari la polisi kabla ya kuondolewa eneo lile, Roman aliiona nyumba ya Deusdelity Macha, ikiteketea kwa moto kuanzia ule upande kilipokuwa chumba chake cha kulala kuelekea nyuma ya nyumba ile.
Kate alikuwa ni miongoni mwa majirani waliojazana pale nje siku ile, wakimshuhudia Roman akiingizwa kwenye gari la polisi akiwa na pingu mikononi, na jirani yao Deus akiingizwa kwenye gari jingine la polisi huku akivujwa damu. Na wakati akimtazama yule mtu aliyempa kipigo cha haja jirani yao, Kate hakutegemea kabisa kuwa kiasi cha miaka miwili baadaye angekutana na mtu yule uso kwa uso...
***
Roman alishitakiwa kwa kosa la shambulio baya na kusababisha hasara ya mamilioni baada ya kuiteketeza nyumba ya Deus kwa moto. Aliwekwa rumande wakati Deus na jamhuri wakiandaa ushahidi wa kumtia hatiani kwa kosa lile zito alilotuhumiwa kwalo. Mark alijitahidi kumtafutia dhamana, lakini haikuwezekana. Roman alionekana ni mtu hatari sana kuachiwa huru mitaani hivyo aliwekwa ndani. Mara moja Mark Tonto alitafuta wakili wa kumtetea.
Kesi iliendeshwa kwa miezi mitatu, Koplo Fatma akiongoza upande wa upelelezi. Na ni katika miezi mitatu ile, ndipo Koplo Fatma alipopata kuufahamu kwa undani uhasama uliojengeka baina ya Roman na Deus. Lakini mambo mabaya ndio kwanza yalikuwa yanaanza kwa Roman. Kutokana na kuhusishwa na kesi ya kiraia, Roman alijikuta akisimamishwa kazi jeshini, wakuu wake wa kazi wakiweka wazi kuwa iwapo atapatikana na hatia, basi na ajira yake jeshini nayo itakuwa imekwisha.


Kesi ya Deusdelity Macha dhidi ya Roman Kogga ilivutia watu wengi hususan majirani wa Kapten Deusdelity Macha walioshuhudia siku ile Roman alipotiwa nguvuni baada ya kumporomoshea kipigo Deus na kuiteketeza nyumba yake kwa moto. Miongoni mwa wale waliokuwa wakiifuatilia kesi ile kwa karibu sana kila ilipotajwa alikuwamo Kate, jirani wa Deus. Na ni katika kuendelea kwa kesi ile, ndipo mambo yote ya jinsi Deus alivyomrubuni Rachel, mdogo wa rafikiye Roman yalipoweka hadharani, Sada akitoa ushahidi wa matukio yote hayo. Siri ya Deus ikawa wazi kwa majirani na wakuu wake wa kazi pia. Hata hivyo, upande wa mashitaka ulifanya kazi nzuri ya kuusambaratisha ushahidi wa Sada kuwa hauna vithibitisho na badala yake ulikuwa ni simulizi tu miongoni mwa masimulizi ya kubuni. Aidha, upande wa mashitaka, uliweza kutumia historia ya nyuma baina ya Roman na Deus kuonesha kuwa Roman alikuwa na chuki binafsi na Deus kwa muda mrefu, pale muendesha mashitaka wa serikali alipompandisha Deus kizimbani kutoa ushuhuda wa jinsi Roman alipompiga kwa nguvu wakati wakifanya mazoezi ya ndondi wakiwa michezoni jeshini, na kumvunja taya. Kwa jinsi Deus alivyoielezea hali ile, ilionekana kama kwamba wakati walitakiwa wapigane kimichezo, Roman aliingia ulingoni kwa lengo la makusudi la kumuumiza. Ushahidi huu ulimuweka Roman kwenye wakati mgumu sana pale ulipooanishwa na lile tukio la kumvamia Deus nyumbani kwake, kumpiga na hatimaye kumchomea moto nyumba yake.
Mwisho wa kesi, mahakama ilimtia Roman hatiani. Hukumu ikawa ni kifungo cha miaka miwili pamoja na kumfidia Deus kwa hasara aliyomsababishia alipomteketezea nyumba yake kwa moto. Hivyo alitakiwa atumikie kifungo, na baada ya kifungo, alipe fidia ya ile nyumba aliyoiteketeza. Au atekeleze yote mawili kwa pamoja, lolote litakalokuwa rahisi zaidi.
Muda wote wakati hakimu akimsomea hukumu ile, Roman alikuwa amemkazia macho Deus huku akiwa ameuma midomo yake kwa hasira. Baada ya kusomewa hukumu yake Roman alitiwa pingu pale pale mahakamani, na Koplo Fatma akisaidiwa na askari wengine watatu walimuongoza kuelekea chumba cha mahabusu pale mahakamani ili asubiri gari la kumpeleka gerezani, na wakati akiongozwa kutoka pale kwenye chumba cha mahakama, Roman alipitishwa karibu na alipokuwa amesimama Deus na muedesha mashitaka wake. Roman alisimama na kumtazama kwa muda mrefu yule adui yake, kisha kwa sauti iliyojaa utulivu mkubwa alimwambia;
"Mimi nakwenda gerezani Deus. Lakini nataka nikuhakikishie kuwa miaka miwili si mingi...nitatoka. Na nikitoka, nakuja kukuua Deus, hilo ni hakika kabisa!"
Ilikuwa ni kauli ya kuogofya kuliko zote ambazo Deus alipata kuzisikia. Na wakati akiongea maneno yale, sauti na macho yake vyote vilionesha kuwa Roman alikuwa amedhamiria kulitekeleza lile alilokuwa akilisema. Kwa muda karibu mahakama yote ilikuwa kimya kabisa. Watu walitazamana, kila mmoja aliyesikia kauli ile asijue achukue hatua gani. Deus alibaki akimtazama Roman kwa woga uliokithiri, akishindwa kusema lolote.
"Twende Roman...acha mambo hayo sasa!" Koplo Fatma alimwambia huku akimsukuma mbele. Roman alimgeukia na kumtazama kwa jicho kali sana, kisha bila ya kusema neno, aligeuka na kuelekea kule alipokuwa akiongozwa.
Kutoka kwenye kona moja ya mahakama ile, Mark Tonto na Sada walikuwa wakimtazama Roman akiondolewa eneo lile huku wakibubujikwa na machozi.
Kwa hukumu ile, Roman Kogga akawa amepoteza rasmi kazi yake jeshini...
***
Wiki mbili baada ya hukumu, wakili wa Roman alifanikiwa kufikia muafaka na wakili wa Deus, wa namna ya kumfidia hasara ya kumuunguzia nyumba yake. Ilikubaliwa kuwa nyumba ya Roman aliyoachiwa urithi na wazazi wake iuzwe kwa usimamizi wa mahakama, na pesa zitakazopatikana zilipe gharama za ukarabati wa nyumba ya Deus.
Swala likafikiwa muafaka.
Hivyo, ndani ya muda mfupi sana, Roman alipoteza mdogo wake wa damu, kazi yake iliyokuwa ikimpatia riziki hapa duniani, na nyumba yake ya urithi. Na yote ni sababu ya mtu mmoja tu...Deusdelity Macha.
***
Miezi miwili baadaye, Mark Tonto alienda kumtembelea kule gerezani.
"Mark..." Roman alimsalimu rafiki yake huku akitabasamu. Mark Tonto alifanya jitihada za hali ya juu kujizuia asiangue kilio. "Roman...vipi hali yako bwana...?" Alimuuliza kupitia kwenye dirisha la wavu lililowatenganisha. "Sio mbaya...nahesabu siku tu..." Roman alimwambia. Mark aliuma midomo na kutikisa kichwa.
"Jamaa yetu ameacha kazi...ametoa notisi ya saa ishirini na nne..." Mark alimwambia. Roman alimtazama kwa macho ya kuuliza. "Deus...amecha kazi?"
"Yap! Taarifa nilizozipata zinasema kuwa jeshi lilikuwa linajiandaa kumuachisha kazi kutokana na mazingira ya kujihusisha kwake na kifo cha Rachel...inasemekana ingawa mahakama haikumtia hatiani kwa kuwa hakushitakiwa kwa kifo kile, tayari alikuwa ameshalitia doa jeshi..."
"Kwa hiyo yeye akawahi kujitia kuacha kazi kabla hajafukuzwa?"
Mark akaafiki kwa kichwa. Roman akatikisa kichwa kwa masikitiko, uso wake ukionesha kukereka na tabia ile.
"Na sasa ameingia kwenye ngumi za kulipwa...eti ameamua kuwa professional boxer..." Mark alisema kwa dharau. Lakini Roman alikuwa akimtazama kwa makini, ilhali akionekana kuwa na mawazo mazito, akili yake ikiichambua kwa kasi sana habari ile iliyoletwa na Mark.
"Unasema kaamua kuwa bondia...wa kulipwa?" Roman alimuuliza tena kwa sauti iliyojaa udadisi. Mark alimtazama kwa mshangao kidogo. "Ndio...kwa nini?"
Roman alikaa kimya kwa muda, akiwa kwenye mawazo mazito.
"Okay, naomba kuanzia sasa unikusanyie habari zake zote.Najua atakuwa anaandikwa sana magazetini, naomba unikusanyie makala zote...nitakapotoka nitataka kuziona..." Hatimaye alisema. Mark akamtazama kwa muda.
"Kwa nini unataka habari zake...kuna kitu hujaniweka wazi Roman?"
"Usijali. Naomba unifanyie hivyo nikuombavyo Mark...na...mengine nitakueleza kadiri siku zinavyokwenda. Kuna wazo limepita kichwani mwangu, ila nahitaji kulichekecha vizuri kwanza...kisha nitakueleza..." Roman alimjibu. Mark Tonto alimtazama yule rafiki na mwanafunzi wake kwa muda, kabla ya kukubaliana naye.
"Okay, Roman...unajua nitafanya lolote kwa ajili yako..."
"Thanks buddy!"
Hiyo ilikuwa ni kiasi cha miaka miwili na miezi kadhaa iliyopita...


***HAYA YOTE YALIPITA……SASA ROMAN YU URAIANI TENA…..ANA NIA YA KULIPA KISASI….
TUUSUBIRI MPAMBANO


ROMAN
davidson689 Toplady ram BPM Sangomwile Mamamercy jonnie_vincy mbalu byb sac mlyn VAN HEIST nrango mangimezamuuza ubuyu Jullie ZIgunga Mojaculbby mugaru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…