HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,417
- 6,149
I died to save my president
Mtunzi Patrick Ck
Simu 0764294499
Season 1
Sehemu 1
Shughuli zote zilizopangwa kufanyika katika kikao cha bunge zilikamilika na kabla ya kusitisha shughuli za bunge kwa siku hiyo hadi siku inayofuata, spika wa bunge akamuita waziri anayeshughulika na bunge mheshimiwa William Kangoga ili aweze kutoa hoja ya kutengua kanuni.
“Mheshimiwa Spika, naomba kwa ruhusa yako sasa nitoe hoja kwamba bunge lako tukufu litengue kanuni ya bunge ili kuwaruhusu vijana wetu wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne waweze kuingia bungeni hapo kesho. Mheshimiwa spika naomba kutoa hoja.”
Baada ya hoja ile kutolewa wabunge wote wakasimama na kuiunga mkono halafu spika akawahoji na wote wakakubaliana na hoja ile kwamba kanuni ya bunge itenguliwe na kuwaruhusu wanafunzi ishirini waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne waweze kuingia bungeni ili waweze kupongezwa na bunge.
“Ahsanteni sana waheshimiwa wabunge kwa kukubali watoto wetu waje bungeni tuwapongeze na kuwatia moyo ili waweze kufanya vizuri zaidi huko mbele waendako,” akasema spika wa bunge halafu akasitisha shughuli za bunge hadi siku inayofuata saa tatu za asubuhi.
*********************
Ni saa tano za usiku sasa lakini bado Patricia hakuwa na usingizi. Yeye na mama yake walikuwa katika chumba kilichoko ghorofa ya nne ndani ya hoteli hii kubwa mjini Dodoma ijulikanayo kama Dodoma View Hotel. Ni moja kati ya hoteli yenye hadhi ya juu kabisa mjini Dodoma na ambayo wabunge wengi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hupenda kufikia.
“Patricia mbona hulali? Si unajua siku ya kesho itakuwa ndefu? Jitahidi ulale ili usije ukasinzia katika ukumbi wa Bunge,” akasema Bi Doroth Mwaukala, mama mzazi wa Patricia.
“Mama, nashindwa kabisa kupata usingizi siku ya leo. Usiku nauona mrefu sana,” akasema Patricia, binti aliyejaaliwa uzuri wa kipekee mno.
“Una wasi wasi?”
“Ndiyo mama, lakini si sana. Nawaza kuhusu kesho sijui itakuaje pale nitakaposhikana mkono na mheshimiwa waziri mkuu huku nikionekana katika televisheni nchi nzima. Mama, sikuwahi kuota siku kama ya kesho itakuja kunitokea katika maisha yangu. Bado siamini hadi hapo nitakaposhikana mkono na waziri mkuu ndipo nitaamini ni kweli. Mama, kesho ni siku yangu kubwa mno,” akasema Patricia.
Mama yake aliyekuwa akimtazama mwanae akatabasamu na kusema, “Usiwe na hofu Patricia. Hii si ndoto bali ni kitu cha kweli kinachokwenda kutokea hapo kesho. Kama ingekuwa ni ndoto tusingekuwa hapa Dodoma mida hii katika hoteli kubwa na nzuri kama hii. Patricia, unapaswa kujivunia mafanikio yako haya makubwa uliyoyapata. Mwanangu, umenitoa kimasomaso mimi mama yako kwani hakuna aliyemtegemea kama mwanafunzi aliyeshika namba moja nchini Tanzania atakuwa ni kutoka katika familia masikini kama ya kwetu. Umeidhihirishia nchi na dunia kwamba hata mtoto wa masikini anaweza akafanya mambo makubwa na ya kushangaza. Umelipandisha kileleni jina la familia yetu na kwa sasa sisi si watu wa kudharaulika tena kama ilivyokuwa hapo awali. Laiti baba yako angekuwa hai kushuhudia tukio hili, sipati picha angekuwa na furaha ya namna gani,” akasema Bi Doroth.
“Mama, sifa na shukurani zimwendee mwenyezi Mungu kwa neema na baraka zake nyingi kwangu lakini sifa na shukrani za pekee pia ni kwako wewe mama. Wewe ndiye kila kitu kwangu na ndiye uliyefanikisha haya yote yakawezekana. Umenipa ushirikiano mkubwa. Maongozi na maelekezo yako yameniweka katika nafasi hii nilipo sasa. Mama, unastahili sifa za kipekee kwa kunijali na kuwa nami na kunivumilia hata katika nyakati zile ngumu kabisa. Umejinyima mambo mengi ili mwanao niweze kusoma na haya ndiyo matunda yake,” akasema Patricia halafu akainuka na kuelekea dirishani, akalifungua na kuutazama mji wa Dodoma ulivyokuwa usiku hii.
“Huu ni mwanzo wa safari yangu ndefu ya maisha. Nina ndoto nyingi sana za kutimiza maishani na ndoto ya kwanza ni kuiondoa familia yangu katika umasikini huu mkubwa tulionao. Namuonea huruma mama yangu namna anavyohangaika kunisomesha. Lazima nikiri kwamba si kazi rahisi kwake lakini amejitahidi kwa kila namna na kuhakikisha kwamba hakuna siku nimekosa shule. Huyu ni mama anayestahili sifa za pekee kabisa.” Akawaza Patricia halafu akalifunga dirisha na kurejea kitandani.
“Patricia, jitahidi ulale. Muda umekwenda sana. Kesho tunatakiwa tuamke asubuhi na mapema,” akasema Bi Doroth.
“Mhh! Mama, sijui kama nitaweza kupata usingizi. Sijazoea kulala sehemu laini kama hii,” akasema Patricia na wote wakacheka.
“Patricia, unatakiwa uanze kuzoea vitu kama hivi. Huu ni mwanzo wako wa safari ndefu ya maisha yako. Siku moja vitu kama hivi utaviona vya kawaida. Jitahidi ulale,” akasema mama yake halafu akamfunika shuka vizuri akaenda kuzima taa wakalala.
*********************
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Patricia kuingia katika viwanja vya bunge. Aliustaajabia uzuri wa eneo hili. Hakukaukiwa na tabasamu. Siku hii alikuwa amependeza mno. Alivaa gauni lenye rangi nyeupe chini na juu likiwa na rangi nyeusi. Miguuni alivaa viatu virefu vilivyoendana na gauni alilovaa. Mavazi haya ya gharama alizawadiwa na Juliana mwanamitindo maarufu hapa nchini ambaye alifurahishwa mno na matokeo ya Patricia.
Wanafunzi bora ishirini walipokewa na katibu wa bunge halafu wakakabidhiwa kwa wafanyakazi wa bunge ambao walianza kuwatembeza sehemu mbalimbali za bunge. Patricia alionekana kuwa na furaha pengine kuliko wengine wote kwa sababu hakujua kama siku moja angeweza kufika mahala pale. Kati ya wanafunzi ishirini waliofanya vizuri mtihani wa kidato cha nne wengi walionekana kutoka katika familia bora zenye kujiweza kifedha. Ni Patricia pekee ambaye alitoka katika familia iliyo masikini zaidi lakini pamoja na umasikini wa familia yake iliyokuwa ikiishi katika chumba kimoja tu cha kupangisha, aliweza kuwaongoza wanafunzi wote nchini waliofanya mtihani wa kidato cha nne na kushika nafasi ya kwanza.
Kwa siku ya leo ingekuwa vigumu kuamini kwamba Patricia anatoka katika familia duni kwa namna alivyokuwa amependeza kwa mavazi aliyopewa na mwanamitindo Juliana. Wakati amekaa na wenzake wakisubiri kuingia katika ukumbi wa bunge, mara akatokea mama yake na kumuita pembeni. “Mama kuna nini mbona umefurahi namna hiyo?” Patricia aliuliza. “Patricia, huwezi amini. Juliana amekuja.” “Juliana?!” Patricia akastuka. “Ndiyo.” “Amekuja kufanya nini?” “Amekuja kukusapoti katika siku yako kubwa.” “Kweli mama?!” akauliza Patricia huku akiruka ruka kwa furaha. “Ndiyo Patricia. Anasema kwamba hakutaka kukutaarifu mapema kwamba atakuja. Alitaka akushangaze.” “Mama yuko wapi dada Juliana? Nipeleke nikaonane naye,” akasema Patricia na kwa haraka wakatembea hadi katika maegesho ya magari ambako Juliana alikuwa garini na rafiki yake aishiye mjini Dodoma. Mara tu Patricia alipotokea, Juliana akatoka garini na kumkumbatia.
“Wow! Dada Juliana sikujua kama utakuja Dodoma,” akasema Patricia. Juliana akatabasamu na kusema, “Sikutaka kukutaarifu mapema kama nitakuja Dodoma. I wanted to surprise you. Siwezi kukosa katika siku yako kubwa na muhimu kama hii ya leo. Patricia, najua una wasiwasi sana na nimeona katika orodha ya watoto ambao utaambatana nao leo bungeni, wote ni kutoka katika familia zenye uwezo mkubwa. Usijali, you have a huge support,” akasema Juliana na kumshika mkono Patricia wakaingia garini, akafungua mkebe mkubwa wa poda na kuanza kumremba, halafu akavua heleni zake nzuri za dhahabu na kumvisha. Akamuangalia na kutabasamu. “Now you look like a princess. Go now. Tutaonana baadaye,” akasema Juliana. Patricia akakimbia kwenda kuungana na wenzake. Uso wake ulikuwa na tabasamu zito. Baada ya Patricia kuondoka, Juliana akaagana na Bi Doroth kwa ahadi ya kuonana jioni ya siku hiyo katika sherehe ya kuwapongeza kina Patricia.
“Juliana, nakushukuru sana kwa msaada wako mkubwa. Umeweza kunifuta aibu kubwa siku ya leo. Bila wewe sijui Patricia angeonekanaje leo. Lakini kwa sababu yako leo Patricia ameng’aa na kupendeza kuliko wenzake wote,” akasema Bi Doroth. “Mama, hupaswi kunishukuru. Patricia ni kama mdogo wangu. Mimi ni mmoja wa watu walioguswa sana na matokeo yake mazuri. Ninathamini sana elimu hasa kwa mtoto wa kike na ndiyo maana nimeamua kwa moyo wangu kujitolea kumsaidia Patricia ili aweze kutimiza malengo yake. Bado ana safari ndefu sana na ili afikie malengo yake anahitaji sana sapoti yetu sisi sote,” akasema Juliana halafu akaagana na Bi Doroth na kuondoka kwa ahadi ya kukutana jioni.
***************
Kipindi cha maswali na majibu kilimalizika, Spika wa bunge akasoma baadhi ya matangazo ikiwa ni pamoja na kuwatambulisha wageni waliofika hapo bungeni kwa mafunzo halafu akamuita katibu ili aweze kusema ni kitu gani kilichokuwa kinaendelea. Katibu akasimama na kulitaarifu bunge kwamba ni wakati wa kuwaruhusu wanafunzi waliofanya vizuri waingie bungeni wakabidhiwe vyeti na waziri mkuu. Spika wa bunge akasimama na kusema, “Waheshimiwa wabunge, jana tulitengua kanuni ya bunge ili kuwaruhusu watu ambao si wabunge kuingia ndani ya ukumbi wetu huu. Wageni tuliowaalika ni wanafunzi ishirini bora katika mtihani wa kidato cha nne. Naombeni wakati vijana wetu wakiingia humu ukumbini, muwashangilie kwa makofi kwani wamefanya kazi kubwa sana,” akasema Spika na kumuamuru askari wa bunge awaongoze wanafunzi kungia ukumbini. Lango kuu likafunguliwa na wanafunzi wakaingia wakiwa katika mistari miwili, mmoja wa wanaume na mwingine wa wanawake. Makofi mengi, vigeregere pamoja na meza kugongwa vikasikika. Kilikuwa kipindi cha furaha sana kwa wabunge kuwashuhudia wanafunzi wale ishirini bora. Spika wa bunge akaomba utulivu halafu akamkaribisha waziri mkuu ili aweze kusema machache kabla ya kuwakabidhi vyeti. Waziri mkuu wa Tanzania mheshimiwa Thobias Kangeba kengaiza akasogea mbele na kusema:
“Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana kwa kunipa nafasi hii niweze kusema machache kuhusiana na tukio hili. Napenda nikushukuru wewe na bunge lako kwa kukubali kutengua kanuni ili wanafunzi hawa waweze kukaribishwa bungeni na kupongezwa. Binafsi ninafuraha kubwa sana kuwaona wanafunzi hawa ingawa ningefurahi zaidi kama kungekuwa na uwiano sawa baina ya wavulana na wasichana kwa sababu naona kati ya wanafunzi bora ishirini wasichana ni nane tu na kumi na mbili ni wavulana. Kuna haja ya kuendelea kuwekeza zaidi katika elimu ya mtoto wa kike ili kuwe na uwiano sawa wa ufaulu. Pamoja na hayo, kwa niaba ya serikali napenda kutoa pongezi zangu nyingi kwenu wanafunzi kwa ufaulu huu mzuri. Haikuwa kazi rahisi. Yalikuwa ni mapambano na leo hii mmeibuka vinara. Nawapongeza pia walimu na wazazi wenu kwa ushirikiano wao wa kuwasaidia kuwafikisha hapa mlipofika.”
“Mheshimiwa Spika, mfumo wetu wa elimu bado unakabiliwa na changamoto nyingi kama vile uhaba wa walimu, vitabu, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, lakini serikali imekuwa ikijitahidi kutatua changamoto hizi na leo hii tunashuhudia mwanafunzi wa kwanza Tanzania ametoka katika shule ambazo zimejizolea umaarufu kama shule za kata ambazo zimekuwa na changamoto nyingi.” Makofi mengi yakapigwa halafu waziri mkuu akaendelea:
“Mheshimiwa Spika, ninaomba niseme kwamba hata kama tukifanikiwa kutatua changamoto zote zinazoikabili sekta ya elimu hapa nchini lakini bila juhudi binafsi za wanafunzi wenyewe kamwe hakutakuwa na ufaulu mzuri. Kuna shule zenye walimu wa kutosha na vifaa vya kufundishia na kujifunzia lakini hazikufanya vizuri. Kwa hiyo basi naomba niwaase wanafunzi waongeze kasi ya kujisomea. Mwalimu ana nafasi yake lakini mwanafunzi pia ana nafasi yake. Ni vyema kila mmoja akaitumia vyema nafasi yake.”
“Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwa kutoa pongezi zangu nyingi kwa niaba ya serikali na kuwatakia kila la heri wanafunzi hawa katika safari yao ndefu. Someni kwa bidii na taifa linawasubiri mje kulitumikia. Hongereni sana,” akamalizia nasaha zake mheshimiwa waziri mkuu, wabunge wakamshangilia kwa kugonga meza halafu Spika wa bunge akasimama:
“Tunakushukuru sana mheshimiwa waziri mkuu kwa nasaha zako. Natumai wanafunzi wote wamekusikia na watayafanyia kazi yale uliyowaasa. Waheshimiwa wabunge, kinachofuata sasa ni mheshimiwa waziri mkuu kuwakabidhi vyeti vijana wote ishirini,” akasema Spika na zoezi la kutoa vyeti likaanza. Wa kwanza kuitwa kwenda kupokea cheti alikuwa Patrcia. Ukumbi wote wa bunge ukalipuka kwa makofi na kushangilia wakimpongeza msichana huyu kwa kushika namba moja. Zoezi lilipomalizika baadhi ya wabunge walipata nafasi ya kusema machache na kuwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii. Kila aliyesimama hakuacha kumpongeza na kumtolea mfano.