Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 53

Ndiyo nimewahi kuiona
mara moja" akasema Winnie na
Seve akaileta bastora ya Vicky
"Hii si bastora ya
dada.Niliyomuona nayo haikuwa
kubwa hivi.Yenyewe ilikuwa
ndogo"
"Bastora hii ndiyo aliyoitumia
kutoa uhai wa mtu"
"Bado siamini kama dada
yangu amefikia hatua ya kutoa
uhai wa mtu.Yawezekana labda
mtu huyo alikuwa na lengo baya la
kutaka kumdhuru.Kwani ninyi ni
akina nani? Ni polisi?"
"Sisi ni watu tunaosughulika
na usalama wa nchi na mtu
ambaye dada yako amemuua
alikuwa na taarifa muhimu sana
kwa usalama wa nchi"Kwa hiyo nini mtamfanya
dada yangu?Mtampeleka
mahakamani?
"Itategemea na ushirikiano
wake kwetu.Kama akiendelea
kuwa na kiburi itatulazimu
kumkabidhi katika vyombo husika
na atapelekwa mahakamani
ambako atashtakiwa kwa makosa
ya mauaji ya kuhatarisha usalama
wa nchi.Kama jambo hili likifika
huko basi dada yako hutamuona
tena"
"Tafadhali nawaomba
msimfikishe dada yangu
huko.Tafadhalini nawaomba
mnisaidie mimi kwani
ninamtegemea yeye kwa kila
kitu.Wazazi wetu wote wamekwisha fariki na yeye ndiye
baba na mama yangu kwa sasa."
"Winnie tutakusaidia endapo
tu utakuwa tayari kwenda
kuzungumza na dada yao na
kumshawishi atueleze kile
tunachokitaka.Ukifanikiwa
kumshawishi,suala hili
litamalizika na dada yako atakuwa
salama.Can you do that?
"Ndiyo ninaweza
kufanya.Nipeni dakika kadhaa
nizungumze naye"
"Tunakupa dakika tano
zitumie vyema .Jitahdi ndani ya
muda huo umshawishi akubali
kutueleza kile
tunachokihitaji.Kama akiendelea
kuwa kiburi basi tutachukua
hatua nyingine"akasema Elvis na kumpeleka Winnie chumbani
alimo Vicky akamfungulia mlango
na kuwaacha wazungumze .
"Dada nimepewa dakika
chache sana za kuzungumza
nawe.Nina dakika tano hivyo
naomba tujielekeze katika
masuala ya msingi."akasema
Winnie na Vicky akashangaa
"Wamekueleza nini hawa
jamaa? akauliza Vicky kwa wasi
wasi
"Everything.Wamenieleza kila
kitu kilichotokea usiku wa leo.Je ni
kweli umeua mtu? akauliza
Winnie
"Winnie listen to me.You dont
have to trust these people.Right
now you have to help me get ot of here.Dont believe them" akasema
Vicky
"There is no way you are
going to get out of here.Just
answer me is it true or not that
you killed someone?
"Winnie I'm your sister and
you should be on my side and
believe me not them"
"Dada ninachohitaji kusikia
kutoka kwako ni jibu la ndiyo au
hapana.I want to help you so tell
me the truth."
Vicky akamtazama mdogo
wake kwa hasira
"Wamekufanya nini hadi
unashindwa kuniamini mimi dada
yako na badala yake unachagua
kuwasikia hao mashetani? "Dada watu hawa wako kazini
kwa hiyo wajibu
wanachokuuliza.Kwa nini
umemuua huyo mtu?
"Winnie I love you so much
but today you've dissaponited
me.How come you dont trust me?
"Dada unalifanya jambo hili
liwe gumu hata kwangu pia.Wewe
ndiye baba na mama yangu hivyo
nakuomba usilifanye suala hili
likachukua sura mpya.Bado
nakuhitaji sana.Limalize suala hili
hapa hapa lisifike mbali
zaidi.Wajibu kwa nini umemuua
huyo mtu na hicho ndicho
wanachotaka kukisikia.Kama
huwezi kufanya hivyo kwa ajili
yako do it for me.I still need you" "Get out of here now!!
akafoka Vicky
"dada please!!!
"Nimesema toka nje!!
akasema Vicky kwa ukali na
Winnie hakuwa na njia nyingine
zaidi ya kuufungua mlango
akatoka na kuwakuta Steve na
Elvis nje ya mlango
"Tafadh...................." akataka
kusema kitu Winnie Elvis
akamzuia
"Tumesikia kila kitu.Ahsante
kwa kujaribu" akasema Elvis na
kuingia chumbani
"Muda wa kucheza
umekwisha sasa ni wakati wa
kazi.Tumekupa muda wa kutosha
lakini umeupoteza na hatuna tena
muda mwingine wa kupoteza" akasema Elvis na kumtaka Steve
amfunge kamba Winnie
"Dont touch her!! akafoka
Vicky lakini Steve kwa kutumia
mikono yake yenye nguvu
akamfunga Winnie katika kitu
halafu akamfunga kitu fulani
mdomoni cha kumzuia kutoa
sauti.Macho yalijaa machozi.Steve
akamwamgia ndoo ya maji na
Elvis akakichomeka kifaa fulani
katika umeme na kugusanisha
ncha, cheche zikatoka.Vicky
akapiga ukelele na kutaka kutoka
pale kitandani lakini mkono
mmoja na miguu vilikuwa
vimefungwa kwa pingu na
hakuwa na uwezo wa kufanya
chochote zaidi ya kupiga kelele akiwataka akina Elvis wasimtese
Winnie
"You have ten seconds to help
her!! Elvis akamwambia lakini
bado Vicky alikuwa mbishi
akiendelea kutukana
"I dont have a choice"
akasema Elvis na kumgusisha
Winnie zile waya za umeme na
kumtetemesha.Vicky akafumba
macho asikione kitendo kile
namna mdogo wake alivyokuwa
anateswa.
"Help her tell us the trusth!!
akasema Elvis lakini Vicky
alikuwa analia tu na kuomba
mdogo wake asiendelee kuteswa.
"One more time!! akasema
Elvis na kumchoma tena Winnie
kwa umeme.Hakuweza kutoa kelele kutokana na kile kitu
alichokuwa amefungwa mdomoni
ila alipata mateso makali sana.
"Unaturuhusu tuendelee?
Elvis akamuuliza Vicky ambaye
hakujibu kitu machozi yakimtoka
"This is not working"
akasema Elvis na kumtaka Steven
amfungue Winnie halafu
akachukua kifaa kidogo kinaitwa
koleo na kisu kidogo
"Unataka kufanya nini?
akauliza Vicky
"Ninamuondoa kucha zake
zote bila ganzi nikianzia na kucha
za mikononi na baadae
mguuni.Kama utakuwa mbishi
nitaondoa pia jino moja baada ya
lingine na sina hakika kama
mpaka wakati huo mdogo wako atakuwa bado mzima kwani
maumvu atakayoyapata ni
makubwa mno."
"stop.Please stop !akasema
Vicky
"Are you ready now? akauliza
Elvis
"Nitawaeleza kila kitu
mnachokitaka lakini msiendelee
kumtesa mdogo wangu" akasema
Vicky
"Tell us" akasema Elvis.Vicky
akavuta pumzi ndefu na kusema
"Sina ujanja i have to tell you”
akasema huku akihema kwa kasi
“I'm a deep undercover
agent" akasema Vicky na Elvis na
Steve wakatazama
"Undercover agent? Elvis
akauliza "Ndiyo.Please take Winnie
out of here first" akasema Vicky
na Steve akamchukua Winnie
akampeleka chumbani kwa Graca
"Now we can talk.Tufafa nulie
wewe ni nani na kazi zako ni zipi?
"Naitwa Vicky.Mimi ni
mfanya biashara maarufu hapa
jijini lakini pia ninajishuhulisha na
kazi ya ukahaba ambayo
imenifanya nijulikane sana lakini
ukahaba wangu mimi si wa
kujipanga barabarani na kusubiri
wateja bali ni kwa sababui
maalum.Ninao wateja wangu
maalum na wengi wao ni viongozi
wakubwa serikalini watu maarufu
matajiri na kiwango changu
ninachowatoza ni kikubwa
sana.Ninawatoza kuanzia milioni tano nakuendelea kwa usiku
mmoja. Kazi hii ya ukahaba
ninaifanya lakini nikiwa na kazi
nyingine nyuma yake”
“Vicky hatutaki kusikia
kuhusu kazi yako ya
ukahaba.Tueleze kile tunachotaka
kukisikia”akafoka Elvis
“Mimi ni jasusi wa siri sana
ambaye ninafanya kazi maalum na
kuripoti moja kwa moja kwa
rais.Nilichukuliwa na rais na
kupelekwa katika mafunzo nchi
mbali mbali kwa siri na kuhitimu
halafu nikaja kuanza kufanya kazi
aliyotaka niifanye." KAZI GANI VICKY AMEPEWA
NA RAIS AIFANYE?
KWA NINI KAMUUA PASCAL?
MPENZI MSOMAJI
TUKUTANE KATIKA SEHEMU YA
SIMULIZI HII

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ambao mlishaangalia series ya #StrikeBack kuna jamaa huwa anadanganya kuwa yeye ni CIA kumbe ni gaidi wa kutupwa, ndo namfananisha na huyu Vicky.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…